maafisa waandamizi wa kikosi cha faya na baadhi ya maofisa wa hoteli ya sea cliff wakikagua uharibifu. nyuma ni kamishna wa kikosi hicho. huyo mwenye kombati ndiye yule shujaa aliyetunukiwa nishani kwa kuweza kuuzima moto wa depo ya mafuta ya ndege pale ubungo mwaka juzi. wote hawakuwa na la kusema zaidi ya kwamba moto umethibitiwa na tamko litatoka baada ya tathmini kufanywa kutapokucha



wana faya wakipumua baada ya kugombana na moto huo kwa masaa kadhaa na kufanikiwa kuuzima



naona bendera zimesevu...


gari la faya la halmashauri ya jiji likiingia sea cliff hotel kumalizia kazi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kaka Michu! Huyo shujaa wa faya ambaye alitunikiwa nishani, mbona kavaa gamu boti za kukatia majani...? Hazishiki moto?

    ReplyDelete
  2. Iliungua ikulu tuliambiwa chumbani kwa rais, ikaungua bahari beach, ikaungua benki kuu, ikaungua waterfront, ikaungua WIZARA YA MAMBO YA NDANI...waTZ tunaangalia tu wondering...ikaungua tiper, sasa seacliff...tunaangalia tena...

    ReplyDelete
  3. Inasemekana chanzo cha moto huo ni gas iliyolipuka huko jikoni.na inasemekana wageni wote wanaolala pale wamehamishiwa whitesand.
    Poleni sana wandugu.

    ReplyDelete
  4. thanx a lot Bro Michu for them Photos its sad couse I use to work there, again thank God no one was hurt, I wish I could see the face of Subash Patel(M.D) and Kelvin Stander(G.M), ta-ra for now

    ReplyDelete
  5. HIVI OWNER WA SEA CLIF NI NANI?

    ReplyDelete
  6. Jamani hii ni hasara kubwa, hoteli ilikuwa nzuri sana. Hasa maswala ya mlo na service kwa ujumla jamaa wamebobea. Basi Insurance ifanye kazi yake.

    ReplyDelete
  7. Poleni sana jamani.
    Du afadhali moto huu haukufika jirani kwa wakali wangu wa piza kubwa za jibini na ribs (Alezanda Fobesii!!)maana wakati napanga ratiba yangu ya kurejea nyumbani nilianza kuwaza ile meza ya kwenye kona ambayo nimeizoea.
    Bado kitambo kidogo.......

    Nyakatakule unyilisya echalo

    ReplyDelete
  8. Labda insurance ilishafanya kazi yake kabla haijaungua...who knows..!! Wabongo walivyo hawa..huoni hayo yaliyotajwa hapo juu..yalivyoungua..ulisikia chanzo, nani kakamatwa na nani kala nini..na insurance imelipa nini na kwa nani? Mjini hapa..!!

    ReplyDelete
  9. nakubaliana na anon wa 6.51.....hakya mungu na mtume tena hili ni chongo i mean bonge la mchongo jinsi gani mibepari ionavyo mbali imeuwasha ili wakazoe comprehensive insurance zao...hapa valuer anakula,wachunguzi wanakula,sirikalini walishavutaga chao long t...ebwana hata mie ingenipiti ningelamba kitu gani bwana.....

    ReplyDelete
  10. SEA CLIFF SIO MOTO WA KWANZA, KUNANI HUKU KWA VIONGOZI WOTE KUTEMBELEA???????????!!!!!!!!!NINA MASHAKA MWENZENU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...