

gwiji la muziki zahir ally zorro anaendeleza libeneke na bendi yake ya mtu mmoja ijulikanayo kama man zorro inayotumbuiza kwenye hafla mbalimbali kwa ustadi wa hali ya juu kiasi wamemfananisha na luciano pavarotti kwa sauti isiyo na mfano kwa hapa bongo. huyu ndiye baba yake banana ambaye naye ni moto wa kuotea mbali katika muziki wa kizazi kipya.man zorro inapatikana kupitia namba +255 713 661 717
nakukubali sana hasa lile dude Cleopatra lilikuwa balaa.
ReplyDeleteTupo pamoJAH!!!
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeletePUNGAAAAAAAAAAAA
ReplyDeleteMichu,
ReplyDeleteHawa ndio wanamuziki wa kuweka ktk blog hii, wana historia ya muziki ktk nchi yetu tofauti na muziki wa kizazi kipya ambao wanarudia tungo za magwiji wa zamani. Bw. Zahir kapendeza sana hasa hizo rangi za nguo!!!!
Hao wanaomfananisha na Pavarotti(RIP) inaonekana kuwa hawajawahi kumsikiliza Pavarotti(RIP). Kwanza aina ya musiki ni tofauti. Eti Pavarotti kwikwikwi. wamfanishe na mtu mwingine lakini sio Pavarotti(RIP) kwa sababu ligi ya Zorro bado yupo kwenye chandimu kama watamfananisha na Pavarotti(RIP)
ReplyDeleteNini tafsiri ya neno kufananisha?
ReplyDeleteNadhani angetoa mtu mweupe (si mbongo) akamfananisha na Pavarotti, nina hakika wewe anaonymous hapo juu ungefagilia, anyway, twende mbele.
Sasa ndiyo nakumbuka hadith aliyonipa rafiki yangu kule Minnesota, kuwa ukiona wabongo wakimbie kwani kitu cha kwanza ukiwa nao watapakaza au watakupakazia kwa lolote, nikamuuliza kwani? akasema
- wengi wao hawajui thamani ya utaifa wao.
- ulimbukeni wa kuishi abroad
Vitu hivyo viwili vimewaathiri katika uwezo wao wa kujitambua wanatoka wapi na wanakwenda wapi.
Kwahiyo sishangai sana kuwaona wabongo wakiongea mambo ya hovyo especial kulalamikia kila kilicho cha kitanzania, angalieni mtaendelea kuwa watumwa mile na milele.
Hayo ya minnesota waachie wahuko huko. Unavyosema kuwa watu hawathamini utaifa wao ni utaifa gani huyo wa kumfananisha huyu Ali Zoro na Pavaroti? Au Pavaroti alikuwa Mtz? Kumuziki huyu jamaa hamfikii Pavaroti hata aende kuroga. Ukumbuke kuwa sijasema kuwa hajui kuimba. Ninachokataa ni kumfananisha na Pavaroti kwani wapo kwenye fani tofauti kabisaaaaaaaaa. Kwani hakuna mwanamuziki achilia TZ, Africa ambaye anaimba vizuri? Au unataka kusema ZOro ni mwanamuziki bora Africa? Kama mtu anatoa habari za kijinga nitazipinga sitojali kama ni mweupe, mweusi, mwekundu, kijani, zambarua, Udhurungi n.k. Kamwe sitoshabikia upumbavu hata kama utakuwa unasemwa na ndugu yangu. Kwa hiyo usidhani kuwa kila mtu ana akili finyu kama yako.
ReplyDeleteKama kuwa mshabiki wa Pavaroti ni kutouthamini utaifa basi hata Kikwete na watz wengi sana hawauthamini utaifa kwani wanapenda timu za soka za ulaya.
P.S.Michuzi kama utaweka poa ukiizui hii komenti poa pia.
Huwezi fananisha chungwa na nanasi. siku zote havitafanana
ReplyDelete