Tukio la kukumbukwa lilitokea siku ya Jumapili mjini New York katika hoteli ya Grand Hyatt ambapo Rais Jakaya Kikwete (kulia), alikutana naWatanzania nane kuzungumzia uundwaji wa chombo kitakachowaunganisha Watanzania wote walioko Marekani na baadaye duniani kote katika juhudi za kupigania maslahi ya Tanzania.
Kutoka kushoto ni Mary Mitchell, Mobhare Matinyi, Deogratius Rutabana,Namtasha Ikaweba, Shaaban Mseba, Augustino Malinda na Yasin Njayagha.Aliyekingwa na Rais ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano waKimataifa, Bernard Membe. Mtanzania mwingine, Miraji Malewa kwa bahati alikingwa na mwenzake aliye kushoto kabisa mwa picha.
Kufuatia wito huo wa Rais Kikwete tangu mwaka jana, ndoto ya siku nyingi ya Watanzania hao ilipata msukumo na hatimaye kuundwa uongozi wa muda wa Tanzanians in Diaspora na kupata baraka zote za serikali ya Jamhuri wa Muungano waTanzania.
Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zenye wananchi wake wenginchini Marekani ambapo kwa takwimu zisizo rasmi, imepitwa na nchi nnetu za Nigeria, Ethiopia, Ghana na Kenya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 43 mpaka sasa

  1. MICHUZI NASIKIA WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA MH.JUMA KUPUYA.

    NASIKIA PIA MLINZI WAKE YUPO HOI NA MH KATUMIWA NDEGE IMPELEKE DAR.NAKUAMINI WEWE NI MZEE WA BREAKING NEWS PLZ TUPATIE TAARIFA ZAIDI

    ReplyDelete
  2. nina wasi wasi na muundo wa uanzishwaji wa chombo hiki, yaani kwa sasa wanazungumzia tu wameshakwenda kumuona rais!!

    ilitakiwa kuwe na mipango makini kisha iuzwe kwa wadau lakini ndio hivyo wao wanaona rais wa nchi ni kila kitu...

    Ila overall ni wazo zuri sana kuwaunganisha watanzania wote duniani katika chombo kimoja, tutakuwa na sauti kubwa na tutaweza kuilloby serikali vizuri.

    well done mobhare matinyi and others!

    ReplyDelete
  3. Wabongo wengi walioko USA wanalalamika JK kutowahusisha au kutoonana nao, unafikiri hawa watz watalipokea vipi hili wazo ingawa ni zuri lakini mazingira linakoanzia ................

    ReplyDelete
  4. Tunaipongea nia na juhudi hii iliyoanzishwa na hao jamaa wa US na kuungwa mkono na Serikali.

    HILI SUALA NI NYETI SANA, LINAHITAJI KUFANYIKA KITAALAMU NA KWA UMAKINI SANA. MAANA IMPACT YAKE NI KUBWA VYOVYOTE (HASI AU CHANYA) KUTEGEMEANA NA JINSI CHOMBO HIKI KITAKAVYOANDALIWA NA KUENDESHWA!

    Kama kweli kinatakiwa kuwa chombo cha Kitaifa kinachounganisha Watanzania wote ughaibuni na chenye uhalali na nguvu ya pamoja kwa nini tuseme kuwa kwanza muundo uanzie US na kisha ndio uenee as if walioko nchi nyingine ama ni wachovu au bado ni wachanga au si muhimu sana au ni watu wa kuomba uanachama polepole na unaweza shangaa yakaanza masharti kama vile wapewavyo nchi ziliomba kujiunga na EU!
    Mapendekezo yangu;

    1.Ok, walioanza waendelee kama Kamati ya maandalizi(Steering Committee)=SC.

    2. Waandae rasimu ya Katiba na muundo wa umoja huu na ndani ya miezi sita iwe imekamilika maana mpaka kufikia kumwona rais tayari walikuwa na some sort of a skeleton plan. WAFUNGUE TOVUTI TUMEGEANE hekima, uzoefu na uchawi wa nondos.

    3. Kwa ajili ya urahisi wa kujioganaizi, nchi nyingine zilipo Ofisi za ubalozi au Ofisi ndogo za ubalozi, Watanzania wapelekewe hiyo rasimu na waijadili kwa kadili ya utaratibu wao na ndani ya miezi mitatu waweze kutuma mapendekezo yao kwenye hiyo SC.

    4. Baadaye kuwepo Mkutano wa pamoja wa hii SC pamoja na angalau Mwakilishi mmoja mmoja kutoka kila ulipo ubalozi/Ofisi ndogo ya ubalozi (Kutoka miongoni mwa Watanzania na asiwe mtumishi wa ubalozini)kwa ajili ya kuijadili na kuipitisha rasimu hiyo. Gharama za safari na kijikimu tunagawana pasu pasu yaani (Serikali ya JMT 50% na Mwakilishi wenyewe au mchango toka katika umoja wa nchi atokako 50%).
    MKUTANO HUU UFANYIKE DODOMA NA SIO US NA MWENYEKITI WAKE WA MUDA AWE WAZIRI WA MAMBO YA NCHI ZA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA AU MSAIDIZI WAKE!

    5. Pamoja na mambo mengine Mkutano huo pia wa na.4. ndio uunde Tume ya Uchaguzi kwa ajili ya kuandaa uchaguzi wa viongozi wa huo Umoja. UCHAGUZI UWE HURU NA WA WAZI. Wanaotaka kugombea nafasi (kwa usawa wa jinsia) wajaze fomu na kuweka sifa zao waziwazi na siku ya uchaguzi kila Mtanzania aliyeko ughaibuni afike ofisi ya ubalozi au patakapoandaliwa katika kila nchi au mtandaoni ili wapige kura ya siri. Hakika tume inaweza kulahisisha mambo kwa kuwawezesha Watanzania kupiga kura kwa urahisi bila kuhitaji watu kusafiri sana kwa kutumia teknolojia ya tarakirishi mtandaoni na kwa kufanya kazi kupitia balozi au ofisi ndogo za ubalozi kwa ajili ya kuhakikiksha kuwa wapiga kura kweli ni Watanzania.

    6. Kwa ajili ya maandalizi bora yapaswayo na uandaaji wa bajeti kwa ajili ya Ofisi ya Mratibu Mkuu au Katibu Mkuu au Mfawidhi wa Umoja huu (Ofisi inaweza kuwa katika mfumo wa mzunguko), ninapendekeza kuwa UMOJA huo uchukuwe yapata miaka miwili kutoka sasa kabla ya kuanza rasmi!

    Napenda kutoa hoja.

    wa-Chirangi

    ReplyDelete
  5. Si kuna chomba tayari kinachowaunganisha watz dunia nzima? Kinaitwa www.tanzanet.org na misheni statement yake ni hii hapa

    "TANZANET is an organization of regionally and globally separated people, organized through electronic media. The TANZANET organization shall act as a platform for communication, discussion, social, advertising and other undertakings for the economic, scientific and educational advancement of The United Republic of Tanzania and its people."

    Sasa kama hawa jamaa wanataka kuunda kitu ingine mie naona wanataka ku "re-invent the wheel" kama kuna mapungufu kwenye Tanzanet basi nafikiri itakuwa jambo la busara kukerebisha mapungufu hayo, kama waheshimiwa walikuwa hawaijui Tanzanet basi inaonesha hawako makini na hawajafanya risechi yoyote, kwa maneno mangine "wamekurupuka"

    kitu ingine kila state kule USA ina chama cha wabongo sasa kwanini wasiwasiliane na viongozi wa vyama hivyo ili kuunda umoja wa vyama vya state zote????

    ReplyDelete
  6. Unasema tanzania inapitwa na Nigeria, Ethiopia, Ghana na Kenya kwa idadi wa wananchi ake waishio Amerika.

    Takwimu hizi umezipata wapi?

    ReplyDelete
  7. Subirini CCM -USA

    ReplyDelete
  8. Hao mashushushu tu, ndiyo maana mambo yameharakishwa ki-siri siri. Kikwete hawezi kukutana na Watanzania wote kujibu maswali. Mambo ya Kabwe pamoja na promises alizozitoa nyingi tu ambazo hazijatimizwa.

    ReplyDelete
  9. Jamani tumechoka na negativity za watu....mmeshaanza Utanzania ASILI sasa! Hivi wewe Anonymous wa September 25, 2007 12:10:00 PM EAT unayosema una maana gani? Mie sio mmoja wa hao waheshimiwa waloanzisha hicho chama, but I feel very positive about it because it's a good thing for all Tanzanians. Wewe ulitaka JK aje nyumbani kwako ale ugali ndio ufurahi kwamba chama kimeanzishwa? Si M-Bongo mwingine pia angelalama hivyo hivyo? Remember that this is the president of our country na yeye kama president ana protocol. Hawezi tu kuamka akasema anaenda kuwaona watanzania kwenye cook-out au unywaji! Kama watanzania wengine mnaona vibaya basi mngetafuta mwaliko kwenda huko New York... or something!

    On the other hand, nimependa mchango wa "wa-Chirangi". Keep it up bro! We need more people like you.

    Last but not least...Maricha..we all know that The Tanzanet is bogus! With all it's fine mission statement and all. same ol' same ol'. I think it's time for something new, don't you????

    Lastly...Congratulations Mobhare Matinyi and Others. keep it up!

    ReplyDelete
  10. Takwimu, wakati wakubishana ulishapita, kama una data zitoe badala ya kuanza mabishano, chukua mwelekeo chanya kidogo.

    ReplyDelete
  11. MBONA AMEWAKIMBIA WAANDISHI WA HABARI??????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????

    ReplyDelete
  12. Nyie Wabongo mlioko tanzania mtaacha wivu lini ? sisi tunajiimarisha huku huku TUNAMPANGO WA KUANZISHA UMOJA/MASOKO/KUTAMGAZA NA KUUZA BIDHAA ZA TANZANIA MAREKANI, UK N.K. JE BIDHAA MNAZO/MNATENGENEZA AU MNAPATA KUTOKA CHINA NA INDIA.HAKIKISHENI MNAKUWA NA MADE IN TANZANIA ORIGINO SIO LEBO FEKI.

    ReplyDelete
  13. Wa-Chirangi uko fiti. Kuna haja ya kuwa na kitu cha kitaalam kitakachotusaidia kwenda mbele. Watanzania tumeachwa na watu wengi mno duniani, hata Waafrika wenzetu wametuacha mno, imefika sasa wakati wa kujikomboa. Wazo la Rais ni bomba, na hatua iliyoanza ya Watanzania hawa nane ni safi sana. Lazima kitu kianzie mahali fulani, huwezi kutegemea eti Rais wa Nchi akutane na wewe ambaye hujulikani uko. Ni upuuzi kuwalaumu watu waliopiga hatua moja mbele ambayo wengi wetu hatukuifikiria. Hawa jamaa wameona mbali na hakuna sababu ya kuwabeza, mliopigwa bao shauri yenu. Na haiwezekani kitu kianzie mahali pengi kwa wakati mmoja, lazima kuwe na chemichemi halafu ndio wengine wafuatie. Sasa ulitaka Rais azungumze na kila Mtanzania aliye nje siku hiyo? Tuacheni ulofa wa mawazo, hatuna mjomba wa kututetea duniani. Na hasa nyie mlioko nje inabidi muwe wa kwanza kuamka siyo mnapondana.

    ReplyDelete
  14. We Maricha weka akili kichwani, huo muda wa kuwatafuta viongozi wa state nyingine ungetoka wapi ghafla hivyo? Kwani haiwezekani kuwaita sasa na kuunda kitu? Watanzania tuache kuleta hizo, hapo tatizo watu tunaona wivu jamaa wamekaa na Rais wakati wengine hatuna ubavu hata wa kukaa na Mbunge. Hiyo jumuiya ya kwenye mtandao uliyoisema imefanya nini mpaka sasa? Kwa nini haikutokea ikaongea na Rais? Mimi ninavyoelewa hiyo ni klabu ya wasema hovyo.

    ReplyDelete
  15. Hizo takwimu hazimo rasmi kabisa. Huyo kaengeza chumvi sana Niambie ni community ngapi za watanzania zipo? Ukienda TX, MD, OH, NY, KS, MN na MI state ndio kuna hata watanzania wengi lakini state nyingine watanzania sio wengi kabisa. Kuna wasomalia, waseralione,wasenegal wengi sana kuliko watanzania. Watanzania hatushiki number yeyote kabisa.. Kama unaenda kwenye state tofauti utaona hizi community za hawa watu kama nigeria, kenya, Ghana, ethiopia, somalia, senegalies, seralione karibu kila state..

    ReplyDelete
  16. Wazo la kuunda chombo cha kujumuisha waTanzania wote nje ni muhimu na ni zuri sana.
    Sio USA na UK hata nchi zingine za Ulaya.

    ReplyDelete
  17. Hivi kazi za ofisi zetu za kibalozi ni nini?
    Hawa wanataka ulaji wa dezo kwikwikwi. Upuuzi mtupu eti muungano wa watz walio nje. Tukiomba waruhusu uraia wa nchi mbili hawataki.

    ReplyDelete
  18. we Anonymous wa September 25, 2007 11:57:00 PM EAT...WHAT THE H--- IS YOUR POINT EXACTLY??

    THE ORIGINAL POSTING SAID (AND I QUITE) "...kwa takwimu zisizo rasmi...", SO WHY THE QUESTION? TRUE, WE MAY NEED TO FIND OUT THE EXACT NUMBER OF TZ IN THE US, BUT REALLY...WHO CARES ABOUT THE EXACT NUMBERS OF TANZANIANS IN THE US, OR WHEREVER IN THIS WORLD? THE MAIN OBJECTIVE HERE IS TO UNITE ALL TANZANIANS WHO ARE OUTSIDE OF TZ!

    SASA UNATUHUBIRIA MAMBO YA WA"SENEGALESE", ETC ILI IWEJE? WEWE UNATAKAJE SASA?

    WABONGO BWANA...SO NEGATIVE! NO WONDER HATUENDELEI!

    ReplyDelete
  19. Jamani ndugu zangu,kila jambo ni lazima lianze mahali fulani.mimi ni mmoja wa waanzilishi wa hiki chombo ambacho masilahi yake ni kwetu sote.Cha msingi tuangalie mikakati kamili ya kuwa na uongozi bora wenye kujali maslahi ya umma.mipango mbalimbali inafanywa ili kila mtanzania nje ya nchi aweze kuhusichwa katika nyanja kama za uongozi na mipango."Ukishikwa shikamana"

    ReplyDelete
  20. Baadhi wa watanzania ni mambumbumbu, hawapendi kujishughulisha na hata kushugulisha akili zao.
    Hebu fikiria watu wachache wamekaa chini na kubuni jambo kwa manufaa ya wengi wanatokea wajinga wachache wanaona hilo ni jambo la kipuuzi, haingii akili hata kidogo. kilichotakiwa ni kutoa mawazo yako lakini bila ya kusahau jitihada binafsi zilizokwisha chukuliwa. Tuwe waungwana sio unaamka unakuja kusukutua kinywa chako hapa.
    Hiyo group ya watu 8 ingeweza kukutana na Rais bila ya kuripotiwa ungesema nini? Wameonyesaha wana nia ya kuwaunganisha watanzania, kama hutaki kaa kimya, hulazimishwi.
    Kwa dhati kabisa nakupongeza Mobare na wenzako kwa hatua mliyochukua hii inadhihirisha kuwa mko makini na mnajua nini hasa watanzania wenzenu wanahitaji 'UMOJA na MAPENZI YA KWELI KWA NCHI YAO YA TANZANIA'

    Mdau Houston

    ReplyDelete
  21. Hivi huyu Matinyi ndiye mwenyekiti wa hiki chama? Nimemsikia kwenye pipeline muda mrefu alipokuwa TZ lakini, na alikuwa anasimamia vitu vinaonekana.

    Labda this time chama hiki kitakuwa tofauti na vyama vingi vilivyokwisha anzishwa bila maendeleo yoyote. Je kuna uchaguzi wa viongozi? Je waTZ tutakuwa na uwezo wa kuchagua viongozi wa chama hiki au ni wa kuteuliwa? Jamani tuachane na yale mambo ya CCM...kiongozi anang'ang'ania tu madaraka bila kuonekana kitu chochote cha maendeleo. Nafahamu baadhi ya waliotajwa hapo...ni viongozi wa vyama fulani hapa lakini hakuna lolote!!

    ReplyDelete
  22. Mimi Takwimu niliwataka kuonyesha takwimu za kweli.

    Kamwe, Watanzania sio wengi kama tulivyoelezwa!

    Ndi kuna Wasenegali (shauri ya ukavu wa Sahel - uliathiri ulimaji wa karanga na pamba) wengi Amerika kuliko Watanzania.

    Kuna Wasomali wengi walio Rhode Island na Arkansas kuliko jumla yote ya Watanzania Amerika.

    Kuna Wasudani wengi huko Minnesota pengine kuliko Watanzania wote waliko Amerika.

    Juzi Amerika imewapokea Warundi kama 35,000! Warundi hao ni wengi zaidi ta Watanzania!

    Fanyeni "homework" zenu vizuri kabla ya kutangaza uwongo!

    ReplyDelete
  23. Takwimu, what is your exact argument? Hivi kama kuna watanzania 10 au 10,000 all over US, will it make a difference kuhusu kuanzishwa au kutokuanzishwa kwa hiki chama?

    Maybe YOU should do your homework. The posting said "takwimu zisizo rasmi", sasa kama ikihitajika idadi ya watanzania US, au popote pale duniani, itapatikana tu.

    Na cha msingi sio kulinganisha idadi ya wasenegali au wasomali (whether wako US kwa ajili ya uhaba wa karanga, pamba au whatever!).

    Hiki chama, kama sijakosea - kina lengo la kuunganisha watanzania WOTE popote duniani, waliopo nje ya Tanzania!

    So stop writing CRAP!

    ReplyDelete
  24. Kwanza naomba kumshukuru bwana Michuzi kwani angalau tumepata pa kutoa mawazo yetu hasa kwa sasa ambapo mtandao wake umetuweka pamoja maelfu ya watanzania;
    Lakini la muhimu nawaomba ndugu zangu tuwe na mwamko wa kisasa,hivi kweli mtu anang'ang'ania kuwa katolewa idadi potofu ya watanzania waliopo USA, UK,Japan, itatusaidia nini?
    Chamsingi ndugu zangu naomba tuelewe kuwa hiki ni chombo ambacho malengo yake ni kumunganisha mtanzania popote alipo nje ya nchi yetu na mtanzania aliyepo nchini Tanzania katika nyanja za uchumi,utamaduni na maendeleo;
    Ikumbukwe maendeleo si lelemama,na maendeleo ni nafsi yako,kwani wengi wetu tumeone ni jinsi gani unaweza kujaribu kumsaidia nduguyo katika maendeleo yake na bado hatokuelewa!
    Wenzetu sas katika nchi zilizo endelea wanatumia zaidi DIASPORA katika kuleta maendeleo ndani ya nchi zao.
    Nawaomba tena ndugu zangu tuwe na mwamko kwani chombo hiki ni kwa manufaa yetu na taifa letu.
    Nawaomba pia tuwe wavumilivu kidogo kwani karibuni tutaizindua web ya DIASPORA ili tuweze kuchanua mambo humo.Lakini pia kama una jambo la haraka katika kufanikisha naomba wasiliana na 1 301 379 0693.
    Utaratibu unafanywa ili kuwa na mtandao ambao utatoa mwenendo mzima wa Tanzanian Diaspora.
    "UKISHIKWA SHIKAMANA"

    ReplyDelete
  25. Takwimu nadhani hukusoma ukaelewa, japo watu wamerudia kukufahamisha bado inaonekana hujaelewa. Unaelewa nini juu ya sentensi hii ifuatayo '...takwimu zisizo rasmi zinasema watanzania hapa US wapo 5,000,000...' Kwa kifupi taarifa yako hiyo idadi inawezekana ni kweli au siyo kweli. So don't derail people from the main mada ndugu yangu.
    Toa mawazo yako kuboresha hoja ya kuundwa kwa umoja wa watz nje ya Tanzania. Usiangalie USA wabongowapo hata Fiji, Nairobi, Baghdad nk

    ReplyDelete
  26. Jamani hilo la Watanzania kuwa wengi au wachache halina maana, wanaotaka Watanzania wawe wachache basi wameshinda. Ilisemwa takwimu zisizo rasmi sasa mcheche wa nini?

    Jamani viongozi wa umoja wetu huko majuu tunaomba mtaje nani ni viongozi, tuna hamu ya kufahamu kwa sababu wengine hapo ni wababaishaji na wengine ni babu kubwa.

    Mimi namfahamu Matinyi, huyu jamaa mtu wa kazi. Tulikuwa naye India long time alikuwa si mchezo kwenye kuongoza, hata muwe wazembe vipi, jamaa atajua jinsi ya kusogeza mambo mbele na kila mtu anaridhika.

    Nakumbuka Tanzania jamaa akiwa yanki mdogo kabisa alipewa kuongoza gazeti lililokuwa kali kushinda yote Tanzania wakati huo, na sasa limekwisha. Jamaa yuko mzima, kama yeye ndiye Mwenyekiti, basi kuna jambo linakuja. Halafu mshikaji mtu wa mjini, hana upuuzi.

    ReplyDelete
  27. Dk. Slaa azidi kukabwa koo

    2007-09-28 09:07:16
    Na Mwandishi wetu


    Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa anazidi kukabwa koo na vigogo aliowataja kuhusika na ufisadi ambapo jana Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Bw. Patrick Rutabanzibwa naye ametangaza kuchukua hatua za kisheria dhidi mbunge huyo na wenzake.

    Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

    Bw. Rutabanzibwa alisema madai aliyoyatoa Dk. Slaa na wenzake Septemba 15, mwaka huu kwenye mkutano wa hadhara wa kisiasa uliofanyika katika viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini si ya kweli na yamemharibia heshima yake mbele ya Watanzania.

    Alisema katika mkutano huo walimtaja kuwa yeye (Rutabanzibwa) ni fisadi na kwamba hata katika toleo la Septemba 19, mwaka huu la gazeti la Mwanahalisi lilichapisha madai hayo.

    `Matamshi ya Dk. Slaa na wenzake yamenishangaza, yamenisikitisha na yamenihuzunisha sana,` alisema.

    Alisema madai hayo ya Dk. Slaa na wenzake dhidi yake ni uzushi mtupu na kwamba anakanusha vikali tuhuma hizo za kumhusisha na vitendo vya kutumia wadhifa wake kama mtumishi wa umma vibaya au kwa maslahi yake binafsi.

    Aliongeza kuwa madai hayo, yanalenga kumchafulia jina na kumshushia heshima mbele ya watumishi wenzake na jamii ya watanzania kwa ujumla.

    `Ili nitendewe haki na kwa lengo la kulinda heshima yangu inayotokana na kuutumikia umma wa watanzania kwa uadilifu kwa miaka 28 hadi sasa, sina budi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Dk. Slaa na wenzake,` alisema.

    Kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Maji, Bw. Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

    Wa kwanza kukanusha tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa ni Mbunge wa Musoma Vijijini na Mwanasheria maarufu, Bw. Nimrodi Mkono ambaye alisema tuhuma zake ni za uongo zenye lengo la kumchafulia jina lake.

    Hata hivyo, Bw. Mkono anatofautiana na watuhumiwa wenzake
    baada ya kusema kwamba hana nia ya kumshitaki Dk. Slaa kwa kuwa hana fedha za kumlipa.

    Aliyefuata ni Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi ambaye aliwaambia waandishi wa habari mwanzoni mwa wiki kuwa atamshtaki Dk. Slaa kwa kuwa tuhuma alizozitoa dhidi yake hazina ukweli wowote.

    Juzi, Katibu Mkuu Kiongozi wa Wizara ya Fedha, Bw. Grey Mgonja naye alitangaza kuwa atamshtaki Dk. Slaa kuwa kumtaja kwa ni mfisadi.

    ReplyDelete
  28. TUNAUNGA MKONO UMOJA HUO, LAKINI HTUUNGI MKONO UPANDIKIZWAJI WA " MAKACHERO/MASHUSHU " WA SERIKALI YA TANZANIA NDANI YA UMOJA HUO.

    ReplyDelete
  29. Haya mengine haya ya upuuzi!....wewe Anonymous wa September 28, 2007 2:50:00 PM EAT, you MUST be shushushu! Who cares kama kuna shushushu humo? Hiyo ndiyo kazi ya serikali bwana, kama wewe ni shushushu na ulitaka upandikizwe wewe humo basi pole - mwingine keshawekwa!

    My fellow Tanzanians, You must understand that LAZIMA kuwepo na hao watu anywhere ili kulinda maslahi ya Tanzania! Kwa mfano sasa kama chama hiki kikianzishwa halafu kikapoteza dita na kikawa na mahusiano na magaidi au mambo mengine ambayo ni kinyume na Utanzania kwa namna fulani, don't you think kuwepo kwa shushushu kutasaidia kuweka chama kwenye mstari? Again, I am saying....STOP WRITING CRAP YOU TRAITORS!!!!

    ReplyDelete
  30. Hivi nyie mnaodai sijui mashushushu mnaishi duniani gani? Sasa Watanzania kuunda Umoja wetu huku Majuu mashushushu wa nini? Yaani wewe kusaidiwa kupata habari za kuwekeza nyumbani au kumsaidia Mtanzania anayetaka kufanya biashara na Majuu, shushushu atafanya nini hapo? Acheni upuuzi Wabongo, duniani kote wanashirikiana kujenga nchi zao sisi tumelala. Yaani jamaa kumuona Rais basi kiwewe kinatushika, mbona ni jambo rahisi. Kama Rais mwenyewe anataka mambo yafanyike hivyo ni lazima akisikia watu wanataka kufanya kitu atapenda kuwapa mawazo yake. Msiwaze siasa tu, ni ushamba kupigia watu kelele na hofu ya makachero. Wewe ukifiwa hapa Majuu ukahitaji msaada, umeambiwa shushushu atazuia usichangikiwe? Halafu shushushu atakaa Marekani ahangaike na kazi kibao wakati Tanzania kuna ishu kibao za kufuatilia? Watu wengine sijui hamkosoma shule?

    ReplyDelete
  31. MICHUZI KAMA UNA CONTACTS ZA HAWA JAMAA WALIOKUTANA NA JK, TUNAOMBA UWAAMBIE WATOE STATEMENT ILI WATU TUANZE KUCHANGAMKIA CHAMA HICHO. HILI WAZO NI ZURI MNO SIJAWAHI KUONA, TAFADHALI WAAMBIE. HUYO MMOJA WAO NI MHARIRI WA SIKU NYINGI, AWASAIDIE WENZAKE KUANDIKA ILI TUJUE KINAENDELEA NINI. NASHUMKURU MMOJA WAO KWA KUTUPA SIMU. HII NDIYO TUNATAKA SIYO HUYO TAAHIRA ANAYESEMA ETI KUNA MASHUSHUSHU, SAWA KAMA WAPO WATATUZUIA KUENDELEA MBELE AU WATATUSAIDIA?

    ReplyDelete
  32. NA BADO.MTABISHANA MPAKA MKIJA TAHARUKI MUDA UMEKWISHA, JK AMEMALIZA MUDA WAKE NA HAKUNA LILILOTENDEKA. NDO KAZI YA WABONGO...WAMEJAALIWA DOMO

    ReplyDelete
  33. Chonde JK rudi home!

    2007-09-28 18:46:27
    Na Mwandishi Wetu, Jijini


    Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Jakaya Kikwete akiendelea na ziara ya kikazi huko nchini Marekani, baadhi ya wananchi waliojitambulisha kama wakereketwa wa maendeleo, wamemlilia kiongozi huyo wa nchi wakitaka arudi nyumbani haraka kuokoa jahazi.

    Wamesema jahazi linaelekea kuzama kutokana na baadhi ya watendaji wake muhimu kuzidi kuumbuliwa laivu na wananchi kila wanapokwenda kwenye ziara vijijini, kitu kinachoonyesha wamechoshwa na utendaji wao.

    Kwa mujibu wa wakereketwa hao, kurudi kwa JK, kwa upande mmoja kutasaidia kwani atawakumbusha tena watendaji wake hao juu ya kile alichowafundisha katika semina elekezi kadhaa alizowahi kuwaandalia na hivyo kuwaepusha na aibu zaidi.

    Aidha, wananchi hao wamedai kuwa kwa kufanya hivyo, vigogo hao wa ngazi mbalimbali mikoani, wataweza kujirekebisha na hatimaye kuacha kuumbuka kutokana na zomea-zomea wanayokumbana nayo kila kukicha.

    ``Hali siyo nzuri kwakweli? aibu wanazopata baadhi ya vigogo wa mikoa katika ziara ya Waziri Mkuu Lowassa ni ushahidi kuwa baadhi yao wanastahili msasa zaidi kama si kuondolewa,``amesema mmoja wa wakereketwa hao, Mzee Dickson Kunambi, mkazi wa Ubungo Jijini.

    ``Licha ya umuhimu wa ziara anayofanya sasa kwa taifa, bado kuna haja ya kumtaka Rais Kikwete arejee ili kurekebisha mambo? wapo watendaji ambao wanamuangusha wazi na wakiendelea kuachwa, kasi mpya na nguvu mpya ya kusaka maendeleo itaendelea kukutana na vikwazo,`` akasema mkereketwa mwingine, aliyejitambulisha kwa jina la Mama Mary.

    Matukio yanayotajwa na wananchi hao kuwa ni mfano wa kuumbuka kwa vigogo ni pamoja na yale yaliyojiri mkoani Mwanza.

    Mbunge wa Geita, Mhe. Ernest Mabina, CCM, ni miongoni mwa waliokumbwa na kibano cha wananchi.

    Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, ni kwamba mbunge huyo alizomewa Septemba 23 mwaka huu, mbele ya Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa alipokuwa ziarani wilayani humo.

    Kigogo mwingine aliyekutana na adha hiyo ni Waziri wa Miuondombinu, Bw. Andrew Chenge, ambaye alitolewa nishai na wananchi wa Ukerewe, huku wakiungwa mkono na Mbunge wao, Bi. Getrude Mongela, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Wilayani Ukerewe.

    Waziri Chenge alijikuta akiumbuka baada ya kujaribu kukanusha malalamiko ya wananchi waliyoyatoa kwa Waziri Mkuu Lowassa kuwa kivuko cha Kisorya kinachounganisha wilaya hiyo na mkoa wa Mara ni kibovu.

    Mwingine anayetajwa katika orodha ya vigogo walioumbuka hivi karibuni kwa kuzomewa na wananchi ni Afisa Kilimo wa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Bw. Marco Nkilila.

    Afisa huyo alizomewa baada ya kudaiwa kutoa taarifa za uongo kwa Waziri Mkuu kuhusiana na mfereji unaopeleka maji kwenye mashamba ya mpunga ambao wananchi waliulalamikia kuwa umeziba.

    ReplyDelete
  34. TUNASHUKURU SAANA KWA MAONI YAKO ".SHANGAZI." "MKEREKETWA" September 28, 2007 4:23:00 PM EAT.UNAJUHUDI SANA WEWE, ENDELEA KUWA KIBARAKA, VYAMA VYETU USA HAVIKUUNDWA KWA SIASA (CCM)TUNAJUMUIKA PAMOJA KWENYE KILA JAMBO, WABONGO KWA KUTAFUTA ULAJI ? TUMIENI MASHUSHU KUZUIA UJAMBAZI TANZANIA NA KUKOMESHA BIDHAA FEKI/TAKATAKA ZINAZOMWAGWA TANZANIA. HILO HAMJALIWEZA BADO. HILI SIO KOSA LAKO NA NINAJISIKIA VIBAYA KUINGILIA NDOA YAKO NA MUMEO.NAOMBA SAMAHANI/KUMRADHI TENA MBELE YA WADAU.

    ReplyDelete
  35. DC ampinga Lowassa hadharani
    na Sitta Tumma, Mwanza

    KATIKA hali isiyo ya kawaida, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza, Kanali Peter Madaha, ameonyesha jeuri ya kumpinga waziwazi Waziri Mkuu, Edward Lowassa, baada ya kuikataa taarifa ya wilaya hiyo.

    Mkuu huyo wa wilaya alilazimika kumjibu Lowassa hadharani na papo hapo, baada ya kuikataa taarifa hiyo ya wilaya na kisha akamweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa uongozi wake ni dhaifu.

    Malumbano hayo yaliyozua gumzo kwa viongozi na watendaji wa serikali yalitokea jana, saa 3:45 asubuhi, Ikulu ndogo jijini hapa wakati mkuu huyo wa wilaya akitoa taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo.

    Katika taarifa hiyo, Lowassa alionekana kutoridhishwa nayo hususan katika sekta ya elimu na kilimo, ambayo ilielezwa kuwa na udanganyifu mkubwa hata waziri mkuu kulazimika kuikataa na kusema mkuu huyo wa wilaya hana uongozi thabiti katika wilaya yake.

    “Huwezi ukaniambia mimi sina uongozi imara...mimi ni kiongozi na nina miaka 24 nikiwa kama kiongozi wa Serikali ya Tanzania. Mimi ni kiongozi, tena mzuri sana,” alisema DC huyo kwa kujiamini na kwa sauti ya juu.

    Katika hali hiyo, Lowassa hakuweza kubishana naye wala kumjibu lolote, isipokuwa alisisitiza kuikataa taarifa hiyo ya wilaya na kuonyesha kusikitishwa na kushangazwa na kauli ya DC huyo.

    Mbali na hilo, wakati DC huyo akisoma taarifa hiyo walitoleana maneno makali na Ofisa Kilimo wa Wilaya hiyo, Justus Kulwijila, mbele ya waziri mkuu kwa madai kuwa ofisa huyo wa kilimo alikuwa ametoa taarifa ya uongo kuhusu kilimo cha pamba.

    “Waziri Mkuu nikiwa kama mkuu wa wilaya, wilaya yangu hailimi zao la pamba na leo hapa nashangaa umepewa taarifa ya kilimo cha pamba,” alisema mkuu huyo wa wilaya.

    DC huyo alikwenda mbali zaidi kwa kumweleza Lowassa kuwa, taarifa ya kilimo cha pamba ndiyo aliyopewa Rais Jakaya Kikwete alipokuwa na ziara ya kikazi mkoani hapa miezi kadhaa iliyopita na kusisitiza kuwa taarifa hiyo ni ya uongo mtupu.

    Wakati mkuu wa wilaya akiendelea kumweleza waziri mkuu kuhusiana na suala hilo, ghafla ofisa kilimo huyo alisimama na kukanusha kauli hiyo.

    “Mheshimiwa waziri mkuu si kweli kwamba wilaya yetu hailimi pamba…..pamba inalimwa sana na ndiyo maana nimetoa taarifa hiyo ya kilimo,” alisema Kulwijila.

    Kutokana na mvutano huo, waziri mkuu alieleza kusikitishwa kwake na utendaji mbovu wa wilaya hiyo ya Nyamagana, na kwamba serikali haitaendelea kuona viongozi wabovu na wasiofaa katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete.

    Source: Tanzania Daima

    ReplyDelete
  36. Naam naona sasa tunaelekea kwenye njia nyoofu."ka kifupi ni kwamba,jitihada za kuwa na chombo hiki zimeanza siku nyiingi,na hatimaye sasa zinakamilika.Nawaombeni sana ndugu zangu tuendelee kupata mawazoya hapa na pale wakati tukijiandaa kuzindua uwanja wa majadiliano katika mtandao wetu wa TADI(Tanzanian Diaspora).
    Kwasasa uongozi wa muda unashikiliwa na;Bwana Yassin Njayagha kama Mwenyekiti nae ndiyo kwa sasa anaweza kujibu maswali yetu hadi hapo mipango yoote itakapao kamilika pamoja na Uchaguzi kamili.
    Kwa upande wa serikali mambo yoote yameachwa kwa Mh.Membe,Waziri Mambo Ya Nchi za Nje.Uongozi wa muda umepata baraka za Mh.Rais na unaomba ushirikiano wetu sote kwani chombo hiki ni chetu na kwa manufaa yetu.
    Tunatarajia kuwa na Contact benches karibu kila Balozi zet pindi mambo yatakapo kuwa sawa(in a month's time)."TAFADHALI KAMA UNAONA UNAMCHANGO WA KUBORESHA CHOMBO HIKI TAFADHALI WASILIANA NA BW.Yassin Njayagha,1 301 379 0693.
    Ili mawazo yako yawe ni moja ya misingi ya chombo hiki.
    "UKISHIKWA SHIKAMANA"

    ReplyDelete
  37. WAFADHILI WATAKA UFAFANUZI WA TUHUMA ZA UFISADI KWA WAANDISHI WANAOTOA HABARI JUU YA RUSHWA ZINAZOENDELEA.

    SAKATA la tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi wa serikali na wafanyabiasha nchini linaendelea kutimua vumbi baada ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) kutaka serikali itoe ufafanuzi wa kina ili kurejesha imani kwa wafadhili na wananchi.

    Katika mahojiano Maalum na Mwananchi, Mkuu wa Mabalozi wa EU walioko nchini, Maddens Peter, alisema hadi sasa tuhuma za rushwa dhidi ya baadhi ya viongozi hazijakanushwa na akaonya kama serikali itaendelea kukaa kimya basi huenda watu na nchi wafadhili wakadhani kuwa tuhuma hizo ni za kweli.

    "Tuhuma zinaonekana bado hazijakanushwa. Serikali inatakiwa kueleza vema kazi, sera na hata mafananikio yake. Mawasiliano ni jambo muhimu sana kwa nchi wafadhili, hivyo ndivyo demokrasia na utawala bora inavyotaka," alisema.

    Peter alisema ni kazi ya serikali kutoa ufafanuzi wa tuhuma hizo ili nchi wafadhili ziweze kuwaeleza wananchi wao.

    "Nchi wafadhili wanatakiwa kuwaelezea walipakodi wao jinsi fedha zao zinavyotumika katika nchi hii hivyo tunatakiwa kuwa na ripoti sahihi na ya uhakika ili tuendeleze ushirikiano tuliokubaliana," alisema.

    Kuhusiana na ukaguzi unaoendelea Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Peter alisema nchi wafadhili wana wawakilishi nchini Tanzania wangependa kuona uchunguzi wa kina unafanyika na wakaguzi walioteuliwa.

    "Serikali iliwaahidi walipakodi kwamba uchunguzi makini utafanyika na sisi tunasema, si kuwa na ripoti ya ukaguzi tu, lakini pia kuona utekelezaji wa mapendekezo ambayo yatatolewa," alisema.

    Kampuni ya Ernest and Young ambayo imepewa kazi hiyo, ilianza kufanya ukaguzi wa mahesabu BoT Septemba 10, mwaka huu na inatarajia kumaliza kazi hiyo baada ya siku 60.

    Wakati huo huo; Balozi Msaidizi wa Ujerumani nchini Tanzania, Ingo Herbert, aliishauri serikali ya Tanzania kujibu shutuma zote za rushwa zinazotolewa dhidi ya baadhi ya viongozi wake kwa sababu nchi wafadhili zinafuatilia kwa karibu malumbano yanayoendelea na kwamba zingependa kufahamu ukweli.

    Tuhuma zinazotolewa kuhusu ufisadi ni nzito, nasi tungependa serikali ikatoa tamko lake mapema iwezekanavyo kuhusu tuhuma zilizotolewa na vyama vya upinzani dhidi ya baadhi ya viongozi,� alisema.

    Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo, jijini Dar es Salaam jana, Herbert alisema ni vizuri serikali ikazingatia misingi ya utawala bora ambayo dhana yake ni uwazi, ukweli na uwajibikaji.

    Alisema Ujerumani ni mshiriki mkubwa wa maendeleo ya Tanzania, kwani katika miongo minne iliyopita imetumia kiasi cha Euro bilioni 1.8 kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo hivyo hata walipa kodi wa Ujerumani nao wangependa kufahamu kuwa kodi zao zinatumiwa vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa.

    Herbert alikuwa akieleza kuhusu wiki ya Ujerumani iliyoanza jana, ambayo lengo lake ni kuwatambulisha Watanzania kuwa Ujerumani ni miongozi mwa washirika wakubwa wa maendeleo nchini, hivyo Ubalozi wa nchi hiyo umeandaa maonyesho ya shughuli zake inazofanya Tanzania chini ya taasisi zake za maendeleo ambazo ni Partner for the Future Worldwide (Gtz), Hanns Seidel Foundation (Hsf), Konrad Adenauer-Stiftung (Kas), Friedrich Ebert Stiftung (Fes), Deutsche Welle na Germany Capacity Building International (Inwent).

    Alisema serikali ya Ujerumani imeshiriki katika sekta tatu muhimu za maendeleo nchini Tanzania ambazo ni huduma za afya, miradi ya maji safi na salama na uimarishaji wa serikali za mitaa.

    Alisema miradi yote hiyo inaendeshwa chini ya mpango wa mashirikiano baina ya Ujerumani na Tanzania ambao lengo lake ni kutekeleza sera ya maendeleo ya Ujerumani ambayo ni kusaidia kunyanyua kiwango cha maisha cha watu wa nchi zinazoendelea.

    Herbert alisema katika makubaliano ya ushirikiano baina ya Ujerumani na Tanzania, kipaumbele zaidi kimewekwa katika mpango wa serikali ya Tanzania wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini (Mkukuta), ili kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia ambapo nchi hiyo inaisaidia katika nyanja tatu ambazo ni kukuza uchumi na kupunguza umasikini wa kipato, kuboresha kiwango cha maisha ya watu na huduma za jamii na kukuza utawala bora na uwajibikaji.

    Kuhusu suala la utawala bora na uwajibikaji, Herbert alisema wanafuatilia kwa karibu siasa za Tanzania na Ujerumani imeguswa na malumbano yanayoendelea ambayo yanawahusisha viongozi wa serikali ya na tuhuma za rushwa.

    Huyu ni balozi wa tatu wa nchi wahisani wa Tanzania kutoa maoni yake kuhusu tuhuma za rushwa na ufisadi zilizotolewa na Dk Wilbroad Slaa dhidi ya viongozi mbalimbali zinazohusisha ufujaji na upotevu wa rasilimali za umma.

    Mwishoni mwa wiki iliyopita, Balozi wa Uholanzi Karel van Kesteren, alielezea kukerwa kwake na tuhuma hizo dhidi ya viongozi waandamizi wa serikali na kutaka serikali itoe tamko lake haraka iwezekanavyo.

    ReplyDelete
  38. WAPINZANI WAMJIBU WARIOBA

    2007-09-29 08:40:57
    Na Restuta James


    Umoja wa vyama vya upinzani umejiingiza katika malumbano na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba kwa kudai kuwa hautishwi na utetezi uliotolewa na kiongozi huyo na kwamba wakigundua kuna ubadhirifu aliowahi kuufanya wakati akiwa kiongozi wa ngazi za juu serikalini watamshughulikia.

    Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Jaji Warioba kuzungumzia tuhuma zilizotolewa na wapinzani za kuwataja hadharani viongozi wa serikali na kuwahusisha na ubadhirifu wa mali za umma.

    Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za makuu ya CHADEMA, jijini Dar es Salaam, viongozi hao kutoka vyama vya TLP, NCCR-Mageuzi, CHADEMA na CUF, walisema wanashangazwa na kauli zinazoendelea kutolewa na watu waliowatuhumu pamoja na ile ya jaji Warioba na kueleza kuwa hawatambui Jaji Warioba alizungumza kwa kutumia utaratibu gani kwa kuwa hivi sasa hashikilii wadhifa wowote.

    Viongozi hao wa vyama walisema Jaji Warioba alipaswa kueleza juhudi zake za kupambana na ufisadi na kwamba baadhi ya majina ya watu wanaowatuhumu si mageni badala ya kukaa kimya na kuwashangaa wapinzani ambao wana nia ya dhati ya kutaka ukweli juu ya matumizi ya rasilimali za umma na fedha za walipakodi.

    `Sisi tunaamini kuwa Jaji Warioba ni miongoni mwa viongozi waadilifu lakini kauli yake ya juzi inatupa utata sana maana alitakiwa kuwashauri viongozi wa serikali juu ya kutoa tamko kuhusiana na tuhuma hizi kuliko ambavyo viongozi hao wanaanzisha malumbano kwenye vyombo vya habari hivi sasa,` alisema Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuza Taifa Bw. Sam Ruhuza.

    Katika hatua nyingine viongozi hao walisema wameahirisha kulipua `mabomu mengine kwa kuwa bado wanafanya uhakiki na uchunguzi zaidi wa `mabomu` wanayokusudia kuyalipua.

    Walifafanua kuwa kwa sasa wanashirikiana na wataalamu mbalimbali kukamilisha uhakiki wa jambo wanalotaka kuwaeleza wananchi.

    Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bw. Victor Kimesera alisema bomu lililopangwa kulipuliwa ni jipya na kwamba halihusiani na yaliyotangulia akitaja Buzwagi na viongozi waliotuhumiwa kujihusika na ufisadi.

    `Hili jambo ni jipya hatutazungumzia uamuzi uliofikiwa na watuhumiwa wa kutaka kutuburuza mahakamani maana hilo litatatuliwa kimahakama kama ambavyo wanadai,` alisema.

    Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema viongozi wa vyama hivyo wanashirikiana na jopo la wataalam wa kada mbalimbali kujadili suala hilo kwa kina na kwamba siku chache zijazo watawaeleza wananchi.

    Naibu Katibu Mkuu wa CUF ? Zanzibar Bw. Juma Duni Haji , kwa upande wake alisema anashangazwa na watuhumiwa waliotajwa kutokwenda mahakamani hadi sasa, badala yake kuendelea kusema kuwa wamechafuliwa majina na kukashifiwa.

    `Wanajifanya kuwa wamechafuliwa majina lakini hawataki kwenda mahakamani. Hiyo janja yao ya kutaka kuwaathiri wananchi kisaikolojia tumeigundua hivyo tunawaomba wananchi wawe makini kwa kufuatilia mambo haya bila kukata tamaa hadi hapo ukweli utakapojulikana` alisisitiza Bw. Haji.

    Mjumbe wa Halmashauri Kuu NCCR-Mageuzi Taifa Bw. Ruhuza aliongeza kuwa wanasuburi kuburuzwa mahakamani ili watoe mambo yaliyotakiwa kuzungumzwa bungeni na viongozi waliotaka kuwasilisha hoja binafsi.

    Mkutano huo ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa TLP Bw. Mrema, Bw. Ruhuza wa NCCR-Mageuzi, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Bw. Haji pamoja na viongozi mbalimbali waandamizi wa vyama hivyo kutoka bara na visiwani.

    Aidha viongozi hao walisema wataitisha mkutano mapema pale kazi ya uhakiki wa nyaraka za `bomu` wanalotaka kuwaeleza wananchi itakapokamilika.

    ReplyDelete
  39. Jamani haya mambo tunajadiliana hapa kwenye blog ili kupeana mawazo...lakini naona wengine wanachukulia kama personal attack! Sasa nakwambia wewe Anonymous wa September 29, 2007 2:34:00 AM EAT kama huna la kusema bora usiandike kitu...kwani ni lazima uandike jamani?

    You need to understand this:

    1. Mimi ni mkereketwa, lakini sio kibaraka.
    2. Sijaolewa bado,...Hivyo koma kabisa! Kama unaingilia ndoa basi ni ya mtu mwingine.Stop writing crap!
    3. Hivi wewe unaelewa unachoongea? Sasa mashushushu waende kamata majambazi, na kazi ya polisi ni nini?
    4. Kama unatafuta ulaji kupitia hiko chama basi pole...wewe nenda tafuta kazi ya pili, ya tatu au hata ya nne! maana hayo ndiyo maisha yenu ya huko marekani! Rudini khapa nyumbani mkafa mjkutengeneza pesa!...sio kubeba maboksi tu na kutunza viajuza huko! Upuuzi mtupu!

    ReplyDelete
  40. Nyie mnaotusema eti tunabeba mabox tafuteni info zaidi. Angalia hii e-mail mke wa Obama anamuomba mwanamke wa Kibongo pesa za kampeni za mumewe. Unadhani angekuwa na kazi ya kibabaishaji angeombwa hizi pesa. Someni hapo.


    From : Michelle Obama
    Sent : Saturday, September 29, 2007 8:10 PM
    Subject : RE: Hey

    I don't write often, but I wanted to emphasize how important tomorrow's deadline is.
    When Barack and I discussed this campaign and what it would mean for our family, we agreed it would only be worth doing if we left the political process better off than how we found it -- not just for our family, but for the country and for folks around the world.
    Hitting our goal of 350,000 donors by tomorrow at midnight will be an unmistakable sign that people can take back the process. I'm so passionate about this campaign because we're not here to just change the players -- we're here to fundamentally change the game.
    Please, make a donation and get us there:
    https://donate.barackobama.com/match
    In the next 36 hours we can transform politics.
    Thank you,
    Michelle

    ReplyDelete
  41. Bwana Issa Michuzi mie naomba nitoe dukuduku langu kama nitajaaliwa kuwepo humu ndani. Kwanza naomba Huyo Shushu na Shangazi Mkereketwa wawe na subira na subira yavuuta heri. Shangazi utaolewa Mwenyenzi Mungu akipenda, ni kazi yamungu, kumradhi lakini kama nitakuwa nimekuudhi moyoni. Na shushu huo umoja bado haujaanza hatujui A wala Z, kumradhi lakini kama maneno yangu sio busara.

    Mie naelewa kwamba watu huku Tanzania tunamazuri na mabaya yetu, Kilicho nisibu mie katika maongezi yao ni huyu Shangazi kusema kwa dharau na moyo wa husda, kwamba watu wa huko USA walea ajuza na kubeba maboksi, mswalie mtume shangazi mkereketwa, kumradhi kama sio dini yako, mwezi wa toba huu.

    Mimi nina wanangu huko na msituharibie watoto kwa lugha zisizo kuwa na adabu,zilizo jaa dhihaka, kwamaana gani natumia wakati wangu kusema maneno haya. Mwanangu alivyokuwa hapa kwangu ilikuwa sakomoko humu ndani, yeye alikuwa akiingia, kula nakutoka hafanyi kazi hajishughulishi. Kwasababu mnyaanzi Mungu hamtupi mjawake, yeye akaenda huko, akafanya kazi hizo hizo akapata digiree yake na kipindi hicho hicho aliweza ezeka nyumba yetu ya pango kwa kigaye chekundu. Vivyo hivyo kwenye banda la uani akatekeleza kwa kuezeka kigaye chekundu.

    Sasa maneno yako Shangazi mkereketwa yanifanya mie niuguze roho yangu, sijui hao wengine walioko USA wana jisikiaje, na wanahitajika kwenye umoja huu na umoja ni nguvu jamani wanangu.Mimi sikujua kama nitaishi kwenye nyumba ya kigae chekundu maishani mwangu, lakini hizo kazi zimesaidia sana. Na huyo mwanangu akamuita mwenzie akaenda uko punde tu nikatumiwa Toyota, bibie shangazi mkereketwa raha ilioje, na kazi ni hizo hizo unazo zitaja wewe.

    Sasa huyu mdogo wao wa mwisho hana kazi wala kibarua chochote, ila ananifaa mie ananiendesha nahii gari iliyoletwa, kwasababu mie mtumzima sasa, mikono yangu hainaguvu inanizizima. Anaosha gari anaanglia TV, hii TV na huu muziki vimenunuliwa na hizo kazi unazozisema wewe.

    Hayo ni machache tu lakini nilipata ruksa ya kwenda huko kwenye Mahafali yake nikajaaliwa tembelea sehemu nyingi tu nilizokuwa nikiona kwenye TV. Maisha yake si haba, kunagari mbili pale kwao tena nzuri sana jokofu limejaa baraka, vitoweo vya aina mbalimbali na ninamkumbusha kila siku atumie (kitoweo halali), na yule mwanangu aliye pata cheti sasa anakazi bora zaidi ya ile unayo isema shangazi mkereketwa.

    Mimi najivunia wanangu kwamba sikumoja watarudi na mambo mazuri tu, huyo mkubwa nishamtafutia shamba hukoo, kwahiyo shangazi mkereketwa na shushu msituharibie watoto kwa lugha potofu jamani, naelewa kwamba watoto wangu ni watu wazima sasa hivi lakini hawa ni binaadamu na wenzi wao waishio huko vilevile. Nawataka radhi jamani kama nime utia maradhi moyo wa mtu yoyote humundani.

    Naomba uniwekee hii mwanangu lakini hizo salamu nyingine nizako na mwenzio, labda Issa ataianika kwenye mtandao, kaaimara huko uliko.

    ReplyDelete
  42. Mimi ninaomba radhi kwa wadau nilowaudhi (haswa mzazi hapo juu..samahani) kwa statement yangu ya "kubeba maboksi na kuangalia viajuza". Ila mie mashambulizi haya nilikuwa nimeyaelekeza kwa anonymous alosema kwamba mie ni kibaraka.

    Mimi nina ndugu na marafiki huko US, na wanaendesha maisha yao vizuri tu, na kufanya mambo mazuri hapa nyumbani, kama watoto wa huyo mzazi hapo juu.

    Jambo la muhimu kwa hiki chama ni kuacha kuonyeshana vidole kwa wale wanaotoa mawazo, ila kuyachukua na kuyatafakari wakachukua yale yanayowasaidia na kuyaacha yasokuwa na maana.

    Hofu ya baadhi ya wadau kwamba kuna mashushushu kwenye hicho chama (sijui wamejuaje???) nadhani ni hofu zisizokuwa na msingi.

    Mie ni mkereketwa wa Taifa la Tanzania. Asante na kumradhi tena.

    ReplyDelete
  43. wee michuzi weee mbona unanifanyia roho stoki hujaniwekea comment yangu humu, kwamba nampenda na ninamzimia sana YASSIN NJAYANGA..jamani niwekee nakufa juu ya kijana huyu silali usiku kucha na mchana kucha sili si vai namuwaza yeye na karibuni nitajiuwa juu yake yeye. mwambiyeni ajue jambo hili naona ananidengulia sana tuu.

    kaka michuzi tafadhali weka comment yangu hii.
    salaam zinatoka Los Angeles

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...