spika wa bunge la jamhuri mh. samwel sitta akielezea ajali iliyomkuta waziri wa ulinzi na jkt mh. profesa juma kapuya mara baada ya majeruhi kuwasili jioni hii kwenye uwanja wa ndege wa jeshi airwing.
amesema tairi la mbele la gari la mh. kapuya lilipasuka na gari likabiringika mara tatu na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi abirtia wengine wanne akiwemo mh. waziri ambaye alisema amepata jeraha kifuani na kwenye paji la uso ambalo liligota kwenye kioo na vipande vyake kubakia kichwani, kilichomsaidi mh. waziri, alisema, ni kuwa alikuwa amefunga mkanda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya mh.Diwani mahali pema peponi.Amina.



    Pia tunawaombea majeruhi wengine pamoja na mh.Kapuya waweze kupona haraka na kurejea katika ujenzi wa taifa.
    Ameni

    ReplyDelete
  2. Aaah! Ajali hizi mbona zimekuwa nyingi sana mwaka huu? Mungu ampumzishe marehemu na wajaalie majeruhi wapone haraka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...