
Ndugu Issa, kwa niaba ya wadau wa blogu yako wa hapa Michigan napenda kutoa pongezi za dhati kwa blogu yako kwa kuwa chombo cha haraka cha kutupasha habari toka nyumbani.
Picha zako zinakuwa na maneno mengi ambayo mara nyingi huzidi maneno ya kwenye magazeti. Uwepo wako kwenye mtandao umekufanya uwe mfungua njia (trail blazer) na kutufungulia na sisi wengine ambao ndio tumeingia kwenye fani.
Kwetu sisi wa Michigan zaidi ya pongezi tunatoa shukrani za dhati kwa ushirikiano wako mkubwa hasa pale ambapo tulipatwa na msiba mkubwa karibu mwaka mmoja kamili uliopita na wewe kututumia ripoti yako kwenye KLH News kutoka msibani nyumbani Dar. Utayari wako wa kuweza kushirikiana na wadau wengine mahali mbalimbali licha ya tofauti ya itikadi, mitazamo, au umbali unakufanya uitwe Gwiji wa Mtandao na Kinara wa Bulogu!
Miaka miwili iliyopita ni kiduchu tu ukilinganisha na ile ya mbeleni. Ni matumaini yetu na dua zetu kuwa utanendelea kutuletea picha motomoto na habari kemkem na hivyo kutufanya sisi sote ni sehemu halisi ya Blogu yako. Tunakutakia maisha mema, afya ya mwili, fanaka ya pochi, baraka nyingi kwako na kwa wale wote ambao wanashirikiana nawe, na hasa kwa my waifu wako ambaye bila ya shaka kuna wakati anakaribia kukuzaba kibao kwa kukaa kwenye mtandao muda mrefu! Heppy besidei tu yuuuu!!! endi meni meni moa!!
Mwenyeji - KLH News
Sauti ya Watanzania kwenye Mtandao!
Hatulali - Daima tuko Macho!!
http://mwanakijiji.podomatic.comSauti ya Watanzania kwenye Mtandao!
Hatulali - Daima tuko Macho!!
Asant sana KLH news. Wewe pia ni hero wetu bethidei yako lini??? HUUUU NI WAKATI WETU!! I can not say more...
ReplyDelete