juzi usiku katika hoteli ya golden tulip wasanii mbalimbali walikusanyika kwenye mkia wa jogoo maalumu ulioandaliwa na unesco pamoja na music mayday kuhitimisha semina kuhusu hakimiliki na kupanga mikakati ya kupambana na maharamia wa kazi za wasanii. pichani juu ni toka shoto simba, carolla kinasha, bibie, paul ndunguru na jfk

baba yake dully syskes (shoto) na supa minofu wakiwa na mdau wa kijapani kwenye hafla hiyo

mzee syskes ambaye ni mpiga gitaa na mwimbaji mahiri alijichanganya vilivyo na wasanii wengine

rasi inno nganyagwa (shoto) na supa minofu wakiwakilisha

mwinjuma muumini (kulia) na wasanii wenzie wa tot walikuwepo pia.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Namwona Classmate wangu Carolla hapo! Safi sana...wasanii wote wanaonekana kuwa na furaha.

    ReplyDelete
  2. Muumin Mwinyijuma,
    Namfagilia maana sauti yake hakuna mfano ndani ya Wabongo isipokuwa watu kama Sonyo na Banza. Yeye na wenzake wana mashairi yenye hisia kali sana. Sikiliza nyimbo kama vile Juli, Cheupe Sandra n.k usikie mwenyewe na vikolezo vya rapa wake.

    Mdau na rafikiye wa Uholanzi

    ReplyDelete
  3. Sasa braza Michu! Huyo jamaa katika picha na mzee wa duli saiksi, mwenye kapelo ya chikago kabsi(njekundu) anaonyesha alama(sign) gani? Aache kuiga!

    ReplyDelete
  4. michuzi,JFK tunayemjua sisi ni kennedy,hawa wengine tunaomba uandike majina yao kwa kirefu maana unatuchanganya

    ReplyDelete
  5. Hatua muhimu iliyocheleweshwa miaka mingi na kufanya wasanii wengi kukosa mafao yao muhimu,waliohusika na kikao hicho tafadhalini fanyeni juu chini Familia ya Mzee TingaTinga(r.i.p) inufaike na maamuzi yenu. maana mpaka waleo kazi na ubunifu wake unanufaisha wengi pasipo malipo kwa familia ya originator wa kazi.

    ReplyDelete
  6. Kwenye semina na mwarsha kama hizo mbona wale WADOSI wa Kariakoo wezi wa kazi za wasanii huwa hawaudhurii?

    Kuna kipindi mtangazaji wa kipindi cha 5LIVE cha EATV Boby alishawai kuandaa mazungumzo kuongelea masuala ya wizi za kazi za wasanii na tatizo la usambazji lakini wadosi waligoma kabisa kutokea.Hii ni dharau kubwa.


    Kaka michu ukipata muda nenda KARIAKOO ukapige picha kale kaofisi ka mamu.Yaani uchochoroni hakuna hata ukarabati wa maana wanachojari wao ni kutia pesa ndani tu.

    Wasanii unganeni inawezekana kufanya mapinduzi ya sanaa bila hao Mamu.

    ReplyDelete
  7. Kila mtu anaonyesha furaha isipokuwa huyo sijui Raper (kutokanana sign yake), Mwin-juma inaonyesha akili/mawazo yalikuwa kwingine kabisa, Rasi Inno umekuwa jibaba sasa hehehhehe nakumbuka enzi zile ukiruka-ruka na jeans yako mwenyewe ulikuwa kipotaboo(nipenda shati yako), Baba'ke mzee misifa gray hiyo imekutoa vema.

    Kila la kheri katka shughuli zenu.

    ReplyDelete
  8. Kweli hii ni bonge ya koki tail LOL

    ReplyDelete
  9. JFK stands for John Francis Kitime, Njenje kwa sana! Aminia babake. Ras Inno unakumbuka kikombe cha uji studio? Umetoka bomba mzee!!
    Much love!

    ReplyDelete
  10. Huyo binti aliye katika crew la babake misifa ametoka pina..black is beauty kwa kweli!

    Naye ni msanii au?

    ReplyDelete
  11. Huyo kaka aliyesimama nyuma ya Carolla sio mumewe kweli,Athanasis?Mbona yeye hakuandikwa hapo juu na ni mwanamuziki mzuri.

    ReplyDelete
  12. SAFI SANA DULY NAONA UMEKOPY TOKA KWA MZEE UHITAJI D.N.A.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...