naibu waziri wa miundombinu mh. dk. maua daftari na mbunge wa mbinga mh. john komba wakimpa pole mbunge wa mchinga mh. mudhihir mohamed mudhihir kitandani pake muhimbili sasa hivi ambako amesema hali yake inaendelea vyema baada ya kukatwa mkono wa kuume juzi kufuatia ajali ya gari huko lindi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Natamani watu wote hasa wale wasio na ndugu zao vigogo wangekuwa wanatembelewa hivi hape MOI!...Matawi ya juu jamani!

    ReplyDelete
  2. Michuzi mimi napenda kuwakilisha ombi hili la wazo,Hivi kwa nini ni viongozi tu wanaopelekwa nje kwa matibabu kwa pesa za wananchi wakati hao walipa kodi wenyewe wanapoumwa hawapelekwi kokote,na hivi mradi mmoja wa mgodi hauwezi kujenga Hospitali kubwa yenye hadhi ya nje ili wakubwa wasipelekwe nje kama South AFRICA,Hivi raisi yeyote wa nje anaweza kuletwa kutibiwa MUHIMBILI.Naomba kuwakilisha.

    ReplyDelete
  3. mungu bwana...sijui nisemeje...yaani akaukata ule mkono wa kutia saini....machozi ya wanyonge bwana kaa nayo mbali....nani anasema kuna hell??? mi naona payback hapa hapa duniani

    ReplyDelete
  4. Pole sana kaka yangu Mudhihir. Ila siku zoote nilikuwa sikufuatilii kwa undani, baada ya kukuona Bungeni ukimwaga Pumba kuhusu Zitto, ndipo nilipoanza kukuchukia Ghafla.
    USIPONE, ENDELEA NA MAUMIVU TU. kama sisi walala hoi tunavyoteseka kila siku. Ningeweza ningekuroga, lakini uchawi wala ulozi siujui. MHALIFU WA TAIFA WEWE.

    ReplyDelete
  5. Mtu akikupiga shavu la kushoto mgeuzie na la kulia, Bwana zito tunaomba utoe salamu za pole kwa mbunge mwenzako. Usilipe baya kwa baya na Mungu atakuongoza.

    ReplyDelete
  6. Acheni uchonganishi na mawazo ya kizamani ajali niajali hii haiusiani na mawswala ya ZITTO NA MUDHIHIL bungeni je angepata ajali ZTO NDO MNGESEMAJE wa TZ TUJITAHIDI KUBADILIKA KIMITAZAMO

    ReplyDelete
  7. jamani kaka michuzi mbona kikwete hajenda kumpa pole rafiki yake????

    ReplyDelete
  8. HUYU BWANA AMESABABISHA NIFUKUZWE BUNGENI SASA SINA HATA CHAPA YA KULIPIA LAND CRUSER LANGU NINASAIDIWA NA MBOWE, NADHANI NEXT TIME ATAJIFUNZA KU DEAL NA WATOTO WA UJIJI KWANZA NIMEMUHURUMIA NINGEKULA MIKONO YOTE MIWILI NA MGUU MMOJA. BADO HUYO SITA DAWA YAKE INAKUJA NAENDA NA HELKOPTA KIBONDO MWEZI KESHO DAWA IKO CHOONI INAIVA.

    ReplyDelete
  9. Hivi Mheshimiwa hukujua mambo ya Mungu yako computerized? Ubaya au fitina ulomfanyia Zitto, Mungu hakuhitaji kuitisha kikao au kuunda tume juu yako.Hiyo iko programmed kwenye kompyuta za Mungu kwamba ukatwe mkono. Na hapo tunashukuru kwamba unabaki ili ukatubu mbele ya Watanzania kama ulitumiwa na wenzako kwenye Bunge.Pole sana!!

    ReplyDelete
  10. alhamdilulah sasa naamini mungu yupo kweli coz sikuwa naamini.....au ndo mambo ya kigoma jamani????/no way ni mungu tu!!!!ameshindwa kuvumilia kuwaona wakinamama wa buzwagi na wavuja jasho wakimenyeka jamani kha....me mtoto wa kigogo ila ukweli hata sipendezwi sema sina pakusemea ntauwawa mie

    ReplyDelete
  11. Du! kwakweli huwa sina tabia ya kumchukia mtu ila Mudhihir nimetokea kumchukia kwani alikuwa anajipendekeza kwenye kambi ya mtandao kwa kumkana Zitto, lakini namuombea ungu apone ila afahamu sana kwamba pumba alizozitoa bungeni zitamcost.Na pia afahamu yeye ni mbunge mchemfu kwani huwa hatoi hoja zozote za maana.Tungefichua siri zake hata hao watu wa jimboni kwake wasingetaka kumuona. NYEPESI (zito) juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  12. Jamani wasiomuamini Mungu sasa wajue yupo,hakuna dhambi mbaya kama ya unafiki na kujikomba kwa wakubwa kwa lengo la kupata madaraka,huyu Mudhihiri ni mfano mbaya sana kwa viongozi wanafiki na wasaliti wa wananchi,alitumia hila kumsimamisha Zitto Kabwe kipenzi cha watanzania ubunge..naomba ajue sasa kilio cha watanzania waliomlilia Zitto Kabwe ndio kinamrudi wala asifikiri ni Zitto Kabwe amemlipizia kisasi...naomba afahamu msemo mmoja usemao kwa kilatini VOXI POPULI VOXI DEI yaani SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU,na wale wasaliti wote walioko bungeni waangalie mfano huu.

    ReplyDelete
  13. Duh wallah hadi huruma masikini... mie sifurahii ila kama wadau wanavyosema, CHOZI LA MNYONGE MALIPO KWA MUNGU BABA! Kama kweli Mheshimiwa una kona kona nyingi na haukuwa na sababu thabiti ya kumfanyia Zitto Mtimanyongo kwa kutetea haki za Wanyonge, ... yaani hiyo size yako kabisa. Ila kama haikuwa hivyo... basi ni Mungu tu alipanga, hata usingemfitini Zitto ungeukosa tu huo mkono mmoja. Ila mwanawane sasa utatia vipi signature? Duh kujifunza kuandikia mashoto nayo ni issue.

    ReplyDelete
  14. Ndugu zangu tuwe na ubinadamu! Tunaanza kuwa binadamu kabla ya kuwa wanasiasa au wachezaji au hata wabunge. Ajali aliyoipata Mh. Mudhihir haihusiani kwa namna yoyote na kikao cha bunge kilichopita. Yote ni mipango ya Mungu, ni wangapi wamepata ajali hivi karibuni na wengine hata kupoteza maisha, je walimkosea nani? Tukumbuke kwamba sisi wote ni tunaanza kuzaliwa kama binadamu, then tunakuwa watanzania na kisha wanasiasa au fani nyingine yoyote. Namtakia afya njema ndugu yetu Mudhihir, tukumbuke ule usemi wetu wa kiswahili hujafa hujaumbika!

    ReplyDelete
  15. Hiyo ndo KIGOMA TRANS LTD na mtanange unaendelea.....Bungeni lazima kunyooke. Sema maskadi yakianza kama hivyo sijui itakuwaje?

    ReplyDelete
  16. kama kukiona cha moto basi amekipata na hiyo ni trailer only full picturer inakuja.mbunge mjinga kuliko wote na toka mchonga,na miguu ingekatika hapo hesabu ingetimia kabisa mlevi mbwa huyo

    ReplyDelete
  17. Anonymous September 16, 2007 5:20:00 PM EAT
    Ninakunukuu'...Natamani watu wote hasa wale wasio na ndugu zao vigogo wangekuwa wanatembelewa hivi hape MOI!...Matawi ya juu jamani!...'

    JE, NI SIKU GANI ULIKWENDA KUWATEMBELEA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YEYOTE NA KUWAPA POLE?

    NADHANI UMEKUWA OVERWHELM NA HIZO PICHA ZA WANAOMTEMBELEA MH. MBUNGE.
    LAKINI KAMA UNGEKUWA NI MTU UNAYEJALI MASUALA YA KIJAMII NA SOI USHABIKI WA KISIASA NA DHANI UNGEFAHAMU KUWA KUNA MAKUNDI YA WATU MBALIMBALI YA KIJAMII HUTEMBELEA WAGONJWA KATIKA MAHOSPITALI HAPO DAR NA KWINGINEKO. UKITAKA KUJUA ZAIDI TEMBELEA OFISI ZA UHUSIANO ZA HOSPITALI YA KUBWA ILIYOKARIBU NAWE UWEZE KUPATA TAARIFA ZAIDI.
    HATA WEWE UNA NAFASI KUBWA YA KUTEMBELEA WAGONJWA NA KUWAFARIJI KAMA UNAVYOONA PICHANI.

    ReplyDelete
  18. Mdau hapa juu yangu "Mkweli" baada ya kusoma mada yako nimehamua kuandika. Huyo mdau aliongelea juu ya kutembelea hospital ni mtu mwenye Elimu ya chini sana, anaweza kuwa ni wale wanafunzi walifundindishwa wakati wa UPE, sasa yeye anaongea kama mtoto mdogo juu ya kutembelewa mbunge, sasa yeye ajui kama hao wanaomtembelea ni wabunge wenzake? ajui kama kuna vikundi mbali mbali vya dini vinatemblea wagonjwa hospital, pia watu wenye mapenzi mema, yeye angekuwa wa kwanza kutembelea wagonjwa halafu ndiyo angechonga mdomo wake, wewe nenda kula dagaa za Mwanza.
    Anthony - Boston - USA

    ReplyDelete
  19. Watu wote waliotoa maoni yao ninawaunga mkono kwa sababu kila mtu ametoa maoni yake kulingana na utashi wake ulivyomtuma hasa ikizingatiwa kuna demokrasi ya kutoa maoni,ninamshukuru sana michuzi kwa kutuletea hiki kisemeo cha wanyonge.Mimi langu tu ni kwamba kwa wale wote wanaomtakia mabalaa Mheshimiwa Mudhihir waache,kilichoko tu ni kumuombea kwa Mungu ili aweze kupona na kuendelea kuwawakilisha wananchi wa Mchinga bungeni..ni kweli aliwakosea Watanzania kwa yale aliyoyasema bungeni kwa sababu yalikuwa hayana maslahi na yanaweza tu kusemwa na mtu ambaye ana upungufu wa akili lakini tuyasahau yote hayo na tumsamehe kwa sababu Bwana Mungu alisema tusamehe sabini mara saba na ninaamini hata Zitto Kabwe aliye mhanga wa jambo hili ameshamsamehe.Tubadilike jamani

    ReplyDelete
  20. Hivi ni nani ambaye hajawahi kukosea? Si nawauliza nyie? Mbona watu mnafanya makosa katika maamuzi na maneno yenu sehemu mbalimbali iwe nyumbani,makazini nk.? Sasa kwa nini kosa la siku moja tu la Mudhihir limchafue kiasi hicho kiasi kwamba hakuna alichowahi kufanya hapa nchini?Ikumbukwe Mudhihir ameshawahi kuwa Naibu waziri na Kiongozi wa michezo hususani klabu ya Yanga kwa hiyo kwa njia hizo ameifanyia nchi mambo makubwa,kosa lake la siku moja bungeni isiwe kigezo cha kuyafuta yale mema yote aliyotenda,tuchukulie kilichotokea bungeni ni hali ya kibinadamu tu kukosea na hakuna binadamu aliye mkamilifu.Pole sana mheshimiwa

    ReplyDelete
  21. Hivi Waziri Karamagi ameshamtembelea? Sijaona picha yake akimtizama mgonjwa.

    ReplyDelete
  22. MBUNGE wa Mchinga, Mudhihir Mudhihir, amewataka Watanzania kutoihusisha ajali iliyosababisha akatwe mkono wake wa kuume na masuala ya kisiasa.

    Aidha, mbunge huyo amesema ajali hiyo iliyotokea Lindi mjini mwishoni mwa wiki iliyopita ilikuwa ni mapenzi ya Mungu na haina uhusiano wa namna yoyote na hoja aliyoitoa bungeni dhidi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zuberi Zitto.

    Mudhihir, mmoja wa wabunge wacheshi na wenye uhusiano wa karibu na wanahabari, aliyasema hayo jana kitandani kwake katika wodi ya Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), alikolazwa akiendelea kuuguza majeraha aliyoyapata katika ajali hiyo ambayo ilitokea baada ya gari alilokuwa akiliendesha kupinduka katika eneo la SIDO, Lindi mjini.

    “Mungu ndiye mpangaji wa kila kitu, sipendi ajali hii ichanganywe na siasa au masuala ya Kabwe, kwani hayaingiliani kabisa na ajali niliyoipata,” alisema Mudhihir aliyeonekana akiwa amechangamka kuliko ilivyokuwa siku chache zilizopita.

    Alisema anaamini hivyo kwa sababu binadamu yeyote mwenye akili timamu hawezi hata mara moja akamwombea mwenzake akapatwa na matatizo.

    Mudhihir ndiye mbunge aliyetoa hoja ya kulitaka Bunge limuadhibu Zitto kutokana na hoja yake ya kumtuhumu Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kusaini mkataba wa mradi wa uchimbaji wa dhahabu huko Buzwagi akiwa nje ya nchi na kwa njia ya siri.

    Hoja hiyo na Mudhihir iliungwa mkono na wabunge takriban wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ndipo Bunge likapitisha azimio la kusimamisha uwakilishi wa Zitto bungeni kwa muda wa miezi mitano hadi Januari mwakani.

    Akizungumzia maendeleo yake kiafya, Mudhihir alisema kwa kiwango kikubwa maumivu makali aliyokuwa akiyapata hasa katika mkono wa kulia uliokatwa yamepungua na tayari alikuwa ameshaanza kufanya mazoezi ya viungo chini ya uangalizi wa daktari aliyemtaja kwa jina moja la Marealle.

    Mbunge huyo aliyaelezea matibabu anayoyapata hapo tangu afikishwe hospitalini kuwa ni mazuri na ya kiwango cha juu, na akatoa shukrani kwa wote waliochangia kupata kwake nafuu wakiwamo madaktari, wauguzi na viongozi wa Bunge na serikali.

    Mudhihir alisema alikuwa pia tayari wakati ukifika kuutekeleza ushauri aliopewa na watu mbalimbali akiwamo Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kwa kutaka aende nchini Ujerumani kupata matibabu zaidi, ikiwa ni pamoja na kuwekewa mkono wa bandia.

    Mbali ya hilo, mbunge huyo alisema iwapo hali yake itaendelea kuimarika anatarajia kuwa ataweza kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na kikao kijacho cha Bunge kinachotarajiwa kufanyika mwezi ujao mjini Dodoma.

    Mbunge huyo alisema wakati ukifika anatarajia pia kukamilisha ziara yake ya kutembelea kata zote zilizo katika jimbo lake baada ya kuzitembelea 10 na kubakiza tatu tu.

    Alizitaja kata ambazo alikuwa hajazitembelea kuwa ni Mbanja, Mchinga na Kilolombwa.

    Aidha, Mudhihir alisema mbali ya ajali hiyo kukwamisha ziara yake hiyo, tukio hilo limesababisha alazimike kuahirisha mitihani yake ya mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu Huria cha Dar es Salaam iliyokuwa ianze kufanyika Jumatatu wiki ijayo, Septemba 24 hadi Januari mwakani.

    Hata hivyo alisema bado alikuwa anaamini kuwa pamoja na kuahirisha huko, atafanya vizuri kama ilivyokuwa wakati alipofanya mitihani yake ya mwisho.

    Mbunge huyo aliyepata kuwa Naibu Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo katika Serikali ya Awamu ya Tatu, alitoa shukurani kwa waandishi wa habari kwa kuandika habari zinazohusu ajali yake, hivyo kuwezesha ndugu, jamaa na viongozi mbalimbali wa serikali kujua ukweli wa mambo kuhusu ajali hiyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...