
hayati mwivano. chini ni picha ambazo msanii wa polisi alichora baada ya maiti yake kugundulika. picha hizi za kuchorwa ziliwezesha utambuzi wa marehemu na kupatikana na muuaji wake

Da'chemi juzi aliangalia documentary kuhusu jinsi wataalam wa forensics walivyo gundua kuwa vipande vya maiti yaliotupwa kwanye mto huko Wisconsin yalikuwa ya marehemu mwivano mwambashi kupaza. anadhani baadhi yenu mnakumbuka pilipilika za wakati ule miaka ya 1999/2000. Kwa wasiojua anawasimulia kwa kifupi mambo yalivyokuwa kupitia http://swahilitime.blogspot.com/ ambacho ni kisa cha kusisimua na kusikitisha.
Maskini Mwivano! RIP,
ReplyDeleteHuyo Peter Kupaza nae angenyongwa tuu,, naona kama kifungo cha maisha hakimtoshi. Ila wenzetu jamani! bongo hii kesi ingeishia hewani
Maskini Mwivano Kupaza! RIP sister, Ni kisa cha kusikitisha sana! kuna watu wakatili jamani! Nimesikitika sana ila Huyo Peter Kupaza nae angenyongwa tuu,, naona kama kifungo cha maisha hakimtoshi. Sijui nisemeje,tena jela zenyewe za ulaya! anakula na kulala.. na kuangalia movie.. au ikoje jamani mlio huko?afadhali angeletwa segerea au wangemnyonga tu!
ReplyDeleteIla wenzetu jamani kweli wameendelea ! bongo hii kesi ingeishia hewani kimya kimya..
Ekhe! hivi huyu muuwaji ndiye yule Kupaza mpole mwimbaji na mchezaji tuliyesoma naye Lutheran Junior Morogoro?
ReplyDeleteLabda siye maana LJS, Msemembo, Mzungu, Mwambashi na Melisari hawajawi kutoa product kibonzo let alone Muuaji mbaya wa historia ya Tanzania nchini marekani kama huyu.
Inatia kichefuchefu!
Peter Kupaza alikuwa Profesa hapo wisconsin. Aliwahi kuowa mzungu..Kuhusu kunyongwa au maisha inategemea na sheria za Jimbo(State) zikoje..Kuna majimbo mengine America hayanyongi..Unaweza kupata habari kwenye mtandao wa FBI..
ReplyDeleteSo so sad, i never thought any Tanzanian was capable of doing anything near this! Sijui kama wazee wa ngunguri wanavisit umu? Karne hii bado wanatumia msuli kupata evidence, utapewa mkong'oto,utapigwa shocks za umeme,etc ili tu ukubali hata kama sio wewe.Kazi kwelikweli.....
ReplyDeleteMaskini msambaa wa watu R.I.P mtani
ReplyDeletemungu amemlipia marehemu mwivano kupaza maana alizulumiwa maisha yake na mshenzi huyu peter kupaza, mola amlaze pema peponi amina.
ReplyDeletesasa mnaona watu tulivyokosa imani na tulikuwa tunasema watanzania ni watu wa imani na upendo, jamani wote we are flesh and blood, na duniani kuwa wabaya na wazuri tusidanganyane bure kwamba watanzania ni watu wa imani na upendo.
RIP Mwivano
ReplyDeleteSamahani natoka nje ya topic kidogo jamani ni mwaka mmoja nadhani toka Walter Mazula na Vonetha Nkya wauawe...kuna habari zozote kuhusu uchunguzi wa mauaji haya?
Mtanzania?!!!!! on Court Tv Forensic files. I thought this was for crazy wazunguz. maaaaaaaaann I am shocked
ReplyDeleteTuangalie kwa upande wa pili,X-Wife wa Kupaza(Mzungu)ana backgroud ya kazi ya unesi ktk Hospitali,Mwivano alichinjwa na mtu mtaalamu sana kama anayefanya kazi ya surgery ktk Hospitali kwani hata mfupa haukuvunjwa,hakuna mtu aliyeweza kuprove mahakamani kuwa Peter aliwahi fanya kazi za Bucha,walisikia hiyo ni kazi common kwa vijana wa ki TZ,hata mamae aliwahi toa ushaidi kuwa Peter alikuwa akiogopa kuchinja hata kuku,kwanini X-Wife mzungu asihusiswe ikichukuliwa aliachana na Kupaza sababu ya Mwivano na kuwa yeye aliua kwa kulipiza kisasi kwa kuhisi Kupaza alimtumia kupata uraia wa US na si kwa mapenzi,na baada ya kuua alimpakazia ushahidi wote nyumbani kwa Kupaza tukichukulia yeye ndo alikuwa wa kwanza kutoa ushahidi polisi na alikomalia kesi kuhakikisha peter anafungwa,kwani hatujui wa-US walivyo capable of doing anyting?Ni kweli Mwivano alikosa kabisa mtu wa kumfinance kurudi TZ zaidi ya Peter?Ni kweli mtu anaua sababu tu hawezi kumtunza mwenziwe?Ni kweli US ni kugumu kutengeneza $1'500 kiasi hicho?Kuna mchezo unaendelea hapa katu tusichukulie kijuu juu jamani?
ReplyDeleteHuyu Peter wala wasimnyonge,watakua wanampunguzia machungu.Akae huko jela milele atapata wababe watamweka kinyumba mpaka mwisho wa maisha yake! Kitendo alichofanya ni cha kutisha na kuchafua roho.
ReplyDeleteMungu amlaze pema peponi marehemu Mwivano.
Ni habari ya kusikitisha na kuumiza sana.
ReplyDeleteNimejitahidi kusoma kwenye link tofauti kuhusu hiyo case.
Naamini Mwivano alikufa kifo cha maumivu makali sana.Pole kwa ndugu zake,jamaa na marafiki,naamini walishindwa hata kuiona sura ya kipenzi chao wakati wa mwisho.
Mwenyezi mungu iweke roho ya marehemu MWIVANO mahali pema peponi .Amina
Kwanza huyo baba asivyo na aibu juzi juzi aliappeal...kuna mwana dada aliyekua anatumia search dogs (ambao mbwa wake na yeye walitumiwa pia kwenye kesi hii) huyo mwanana dada alikua anatumia plant evidences ( kila akisearch yeye ni lazima kitu kinapatikana.) Sasa naye yuko jela kwa mashitaka hayo hiyo watu wote walio fungwa ambazo kesi zake huyo dada alizisearch waliappeal na zikarudiwa kuangaliwa kwa upya...wengine waliachiwa na Na huyu baba aliappeal akizania atashinda ...alishinda wapi...walimwambia evidence zake zilikua nyingi sana hata huyo dada na mbwa wake haikuchangia sana... walimrudisha gerezani muuaji mkubwa...alivyomtesa cousin wake akiwa hai haikutosha mpaka akamuua na kumkatakata hivyo...
ReplyDeleteJapo miaka imeshapita mingi lakini bado tunakuomba eeh mwenyezi mungu ipumzishe pema peponi roho ya marehemu Mwivano.
ReplyDeleteAnon wawili mlioandika 1.kuhusu mdada mwenye hao search dogs 2. kuhusu huenda ex-wife wa Peter amehusika,,mi nasema hivi, hizi kesi kubwa kubwa zinaweza chukua hata miaka 20 zikamilike, kwa hiyo bado iko nafasi ya kutoa mawazo yenu na kuifurumua kesi zaidi. Mi naona kama kuna watu mlioishi jirani na Peter, Wisconsin au mahala pengine,mliofanya naye kazi au kuwa naye katika associations/gatherings flaniflani,, mliomuona na kumjua Mwivano, aliowahi kuwabonyeza kuwa anateswa na mjomba au na mke wa mjomba...mkiwa kama watanzania na wenye uchungu na Mwivano, hemu kaeni chini mfikirie, muweke hata vikao muendelee kuichimbua hii kesi mkiwainvolve na polisi,,TUSIKUBALI MTU MMOJA AU WAWILI WAKALICHAFUA JINA LA TANZANIA NAMNA HII,,ndo tunashangaa ndugu zetu wamenyimwa visa kuja kusoma au kutembea, au tunanyimwa nafasi za shule,kazi etc ni UNYAMA kama huu unawekwa kwenye historia za nchi za watu na UNATUCHAFULIA SANA,, msikubali AMKENI,,tena waandishi wa kibongo mngeliwatafuta waanze kuchakarika na hii kitu, watafute data, kije kiandikwe kitabu, tukizubaa kesi itaishia juu juu, wabongo tutachukiwa kijumlajumla na atazuka mzungu ataandika kitabu(kama bado hawajaanza kuandika).
Hata kama hakumtesa au hakumuua lakini alikua guilty of something kitendo cha kuwaambia ndugu za mwivano bongo kuwa huyo msichana yuko busy sana na masomo ndio maana hawasiliani nao, na US kuwaambia kuwa ameamua kurudi nyumbani..basi alikua anajua jambo ndio maana akawa middle man na pia kama kweli huyo msichana alitoa mimba yake basi he is guilty ...first cousin kutembea naye it is not right.
ReplyDeleteKuna watu wara roho mbaya na wala haijali kuwa unatoka nchi gani. Na sio kuwa kesi yake inawafanya watu wawaogope watanzania kwa vile hii kesi waliionyesha kwenye Court TV ambayo ni cable channel. Na sio wengi walikua wamesismka kwa ajili ya watu walikua wataifa bali kilichosisimua ni kuwa alikata mwili na viungo akatupa sehemu tofauti lakini bado artist guy aliweza kutengeneza sura ya mtu kutoka kwenye skull tu na kufanana na mtu hai kamala hata hajamuona.
Sasa hapa ndio unaambiwa kweli ubaya hauna rangi wala dini,Maanake kuna kasumba sana katika jamii ya watu weusi kuwa watu weusi sio wauwaji kwa kikatili, lakini ona yaliyomfika huyu dada wa watu. na huyo bwana mwenyewe si ndio alikuwa ameoa mzungu basi sijui akifikiria atageuka kuwa mzungu siku moja.
ReplyDeleteMungu ailaze roho yake mahali pema peponi. AMINA
Ni habari ya kusikitisha sana .
ReplyDeletePole nyingi kwa wazazi na ndugu wa marehemu Mwivano.
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.
Kama Peter hana hatia kwa nini aliwaambia polisi kuwa hamjui Mwivano?
ReplyDelete