Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Waziri wa utalii sasahivi ni kiboko,leo U.S.A pacific time nimeona tangazo kwenye CNN baada ya mdahalo wa Rais wa Iran columbia University maaara THE LAND OF KILIMANJARO AND ZANZIBAR.Damnn ilikua ni kiboko ile mbaya kweli tunaamka pole pole.Wakenya kama walikua wakitudhulumu tutawapita we ngoja tu.

    ReplyDelete
  2. Aaah! huyu jamaa bwana. Maisha bora hatuyaoni, yeye kakazania kupima ukimwi tu. Kwani kupima ukimwi ni ilani ya CCM anayotekeleza au anazuga kupoteza muda?. Hupati maisha bora hadi uwe Waziri ukasaini mikataba mahotelini nje huko. Sisi tnaungua jua kwa kunapanga foleni za kupima ukimwi, wenzetu wapo hukoooooo wanakula nchi.

    ReplyDelete
  3. Ahh, sijui tunakwenda wapi na msanii wetu huyu! Namsikitikia sana kwa kweli.

    ReplyDelete
  4. Sasa wewe mdau wazo ulilotoa hapo juu linahusianaje na hiyo topic hapo juu au umeamua kuandika tu kama unavyojisikia? Hata kama huo utalii utatangazwa tukapata pesa we utafaidikaje na hizo pesa? Hapa sisi tunaongelea ukimwi halafu wewe unaleta story zako za ajabuajabu.

    NARUDI KWENYE MADA
    Hii issue ya ukimwi ni miradi ya wakubwa sisi wananchi tunatumiwa kama chambo tu. Si unaona chombo chenyewe kinachohusika na ukimwi jinsi kinavyofuja pesa na kisha inaundwa tume ya kuchunguza halafu majibu hatupati?

    Ikiwa madarasa yanajengwa kwa maagizo na huo ukimwi basi utibu kwa maagizo. Eti juzi naye mkuu wa mkoa wa darisalama akawaagiza waajiri wawakate mishahara wafanya kazi kwa ajili ya kujengea madarasa! Ina maana ile income tax wanayolipa wafanyakazi tuiweke kundi gani? au hiyo tax ni kwa ajili ya wakubwa kunywea pombe na kuhongea nyumba ndogo na kujengea mahekalu? Na hao wamiliki daladala kwani hawalipi kodi na maushuru mengine kibao mpaka walipishwe pesa kwa lazima? Na hao mabepari wa mafuta wanaotukaanga kwa ugumu wa maisha mbona hawaguswi? Au hii ni miradi ya wakubwa?

    Baada ya kuona amechemsha ndio sasa anajikosha...."walah mungu mmoja mie sikusema hivyo wameninukuuu vibaya" Nchi hii ina makasuku wengi kweli! Sijui kama tutafika.

    ReplyDelete
  5. Nimeliona lile tangazo lililotokea mara baada ya hotuba ya Rais wa Iran.
    Ni tangazo zuri sana na liliweka at a very right time kwani kwa wakati ule kulikuwa na watazamaji wengi sana (huenda kuliko TV station yeyote).
    Hii ndiyo inayotakiwa kuitangaza nchi yetu katika anga muhimu.
    Nadhani sasa lile tangazo lipelekwe na China, S.Korea, Japan na kwingineko.

    ReplyDelete
  6. Mh. Kikwete akiwa kama kiongozi wa nchi ana nafasi yake pia katika kupiga vita ukimwi.
    Kwa hiyo anonymous hapo juu hii ni kazi halali ya Rais, na asingefanya haya tungemshagaa, appreciate kazi nzuri inayofanywa.

    ReplyDelete
  7. jamani wamezidi wakubwa wanakula mno,na inasikitisha kwakeli,watu wengi wanaishi maisha duni sana,punguzeni kula,hatuzikwi navyo vyote,leteni maendeleo,kuzeni kilimo,watu wapate ajira,acheni kujilimbikizia mali,jamani,ninauchungu mimi.

    ReplyDelete
  8. USTAADH ISSA TUNASHUKURU SANA KWA PICHA NZURI NA HARAKATI ZA KUPAMBANA NA UKIMWI.NAONA MHESHIMIWA JK ANAWAKUMBUSHA KWAMBA YUKO SAFI, DA REAL PLAYA, HUYU JK NASIKIA KABILA LAKE NI " MKWARE " kumradhi jamani kama nimekosea "MKWARE" fuska NA "MKWERE" kabila ZINATOFAUTI NDOGO KIHERUFI "A" NA "E".

    ReplyDelete
  9. KONTENA LENYE TV FEKI LADAKWA JIJINI

    2007-09-25 16:57:51
    Na Futuna Selemani, Jijini


    Kontena moja kubwa lililokuwa na seti kadhaa za bidhaa feki ikiwa ni pamoja na seti za televisheni na balbu limedakwa Jijini, imeelezwa.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi akribuni na Baraza la Taifa la Utetezi wa Watumiaji Bidhaa nchini, ni kwamba kontena hilo lenye bidhaa feki limenaswa bandarini wakati likiwa mbioni kusafirishwa na hatimaye bidhaa zake kufikishiwa kwa walaji.

    Mkurugenzi wa baraza hilo, Bw. Michael Shilla, amesema bidhaa hizo zilizodakwa hazina viwango vinavyokubalika na wala hazikuwa halisi.

    Akiuzungumzia mzigo wa bidhaa zilizokuwa kwenye kontena hilo, akasema kulikuwa na seti 50 za TV feki na balbu kibao zilizotokea nchini India.

    Bw. Shilla akasema kazi ya kuzinasa bidhaa hizo, ilifanywa na maafisa wa Baraza lao, ambao hivi sasa wanafanya kazi ya kukagua bandarini na maeneo ya mipakani ili kuzinasa biadhaa za aina hiyo.

    Bw. Shilla akasema kuwa bidhaa hizo zitateketezwa kwa vile hazifai kwa watumiaji.

    `TV, balbu na bidhaa nyingine feki zitaendelea kulamatwa na ikiwezekana kuharibiwa na mamlaka husika na hili ni zoezi litakalokuwa la kudumu na wala sio nguvu za soda,` akasema Bw. Shilla.

    ReplyDelete
  10. WABONGO BWANA,
    MKIDOKEZEWA MAMBO YA UKIMWI NA MADA MNABADILISHA.TUTAZIDI KUZIKA SANA NA TABIA ZETU ZA KUWA KAMA INZI.MPAKA SASA HATUAMINI KAMA KUNA UKIMWI.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  11. Point anon hapo juu. Tuchangie kufuatana na mada. Ukimwi ni issue kubwa inayo kabiri jamii na Tz bado tuko nyuma sana kwa mengi kuhusu ukimwi.Hapa pia ni mahali pa kujadili hilo lkn helas! watu wanakwepa tutafika kweli?

    Big up baba wa taifa lkn maoni yangu sio ukipima tu kwanza watu waelimishwe ili wawe na positive approach, one has to accept, consider it as any other desease, then watu hawatajificha, jamii haitabagua, etc.. etc..
    serikali pia iwe wazi nahuduma inayotoa kwa waathirika....na zitekelezwe kikwel....let us start from there.

    ReplyDelete
  12. Huyu rais anajitahidi kwa kazi kwakweli hebu mpeni credit.
    Na anatetea sana haki za wanyonge lakini si mnajua hata daraja huwezi kujenga kwa siku moja baada ya mda kidogo nchi yetu itakuwa mbali na huyu akimaliza mda ataacha legendary yaani atakuwa extremely well known na atakumbukwa huyu kuliko nyerere mtakuja kuona tu.

    ReplyDelete
  13. Tangazo la waziri huko umoja wa mataifa "lipelekwe China"...!Loo!Mchina akija bongo haondoki,halafu ataleta wanakijiji wenzake wote na kumiliki kila atakakachoweza!(ukoloni mamboleo)
    Hawa sio wajerumani, ambao wakija kutalii wanarudi kwao na kushauri wenzao waje Bongo kutalii!
    Mchina hatakuja Bongo kufaidisha utalii yeye mwenyewe anahitaji kila kitu kuanzia ardhi nk.
    Wacheni mchezo jamani,Tanzania inahitaji wawekezaji zaidi kuliko wazamiaji.

    SOLE

    ReplyDelete
  14. MAMBO YA BAJETI YA TANZANIA (BONGO)

    http://www.ippmedia.com/ipp/bajeti/2007_2008.pdf

    KWELI WACHINA WAMEZIDI HALAFU SERIKALI INAWAANGALIA TUU. WANAKUJA NA MELI ZA MIZIGO NDANI YA KONTENA MAALUM NA WENGINE WANAJIFANYA MABAHARIA. BAADA YA MIAKA KUMI UTAONA. SHESHE.

    ReplyDelete
  15. wewe anonymous acha mawazo ya kizamani, na wewe nenda china ukajijaze huko ndiyo ulimwengu unavyokwenda.
    Utake usitake wageni lazima wataingia na kufanya biashara nk

    ReplyDelete
  16. Dk. Slaa azidi kukabwa koo

    2007-09-28 09:07:16
    Na Mwandishi wetu


    Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa anazidi kukabwa koo na vigogo aliowataja kuhusika na ufisadi ambapo jana Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Bw. Patrick Rutabanzibwa naye ametangaza kuchukua hatua za kisheria dhidi mbunge huyo na wenzake.

    Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

    Bw. Rutabanzibwa alisema madai aliyoyatoa Dk. Slaa na wenzake Septemba 15, mwaka huu kwenye mkutano wa hadhara wa kisiasa uliofanyika katika viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini si ya kweli na yamemharibia heshima yake mbele ya Watanzania.

    Alisema katika mkutano huo walimtaja kuwa yeye (Rutabanzibwa) ni fisadi na kwamba hata katika toleo la Septemba 19, mwaka huu la gazeti la Mwanahalisi lilichapisha madai hayo.

    `Matamshi ya Dk. Slaa na wenzake yamenishangaza, yamenisikitisha na yamenihuzunisha sana,` alisema.

    Alisema madai hayo ya Dk. Slaa na wenzake dhidi yake ni uzushi mtupu na kwamba anakanusha vikali tuhuma hizo za kumhusisha na vitendo vya kutumia wadhifa wake kama mtumishi wa umma vibaya au kwa maslahi yake binafsi.

    Aliongeza kuwa madai hayo, yanalenga kumchafulia jina na kumshushia heshima mbele ya watumishi wenzake na jamii ya watanzania kwa ujumla.

    `Ili nitendewe haki na kwa lengo la kulinda heshima yangu inayotokana na kuutumikia umma wa watanzania kwa uadilifu kwa miaka 28 hadi sasa, sina budi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Dk. Slaa na wenzake,` alisema.

    Kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Maji, Bw. Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

    Wa kwanza kukanusha tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa ni Mbunge wa Musoma Vijijini na Mwanasheria maarufu, Bw. Nimrodi Mkono ambaye alisema tuhuma zake ni za uongo zenye lengo la kumchafulia jina lake.

    Hata hivyo, Bw. Mkono anatofautiana na watuhumiwa wenzake
    baada ya kusema kwamba hana nia ya kumshitaki Dk. Slaa kwa kuwa hana fedha za kumlipa.

    Aliyefuata ni Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi ambaye aliwaambia waandishi wa habari mwanzoni mwa wiki kuwa atamshtaki Dk. Slaa kwa kuwa tuhuma alizozitoa dhidi yake hazina ukweli wowote.

    Juzi, Katibu Mkuu Kiongozi wa Wizara ya Fedha, Bw. Grey Mgonja naye alitangaza kuwa atamshtaki Dk. Slaa kuwa kumtaja kwa ni mfisadi.

    ReplyDelete
  17. AAA WATU BWANA.WE ANON WA HAPO JUU HAWA WAKWERE WAMEKUFANYIA NINI?? HIVI KILA SIKU KWA NINI MNAMSHAMBULIA NAMNA HII JK..MBONA AMEJITAHIDI SANA..NAJUA MNA KA-CHUKI KENU KALE KALE MLIKOKAZOEA.MARA OOO ANA HILI...MARA EEEE MGONJWA...MNAKUMBUKA MLIMCHAFUA SANA BEFORE EVEN NEC ELECETION.BUT GOD'S GREAT AMESHINDA.KWA TAARIFA YENU HAMNA MTU CLEAN NA MUADILIFU KAMA JK TZ.HAMNA..ILA MTAONA BAADAYE MUDA UKIFIKA.REGARDS
    SAMEER-ATHENS

    ReplyDelete
  18. WEWE DADA NANIHII WA September 26, 2007 10:43:00 TUNASHUKURU KWA UHURU TULIOPEWA WA KUTOA MAWAZO YETU. MDOMO MALIYAKO, MTOTO WETU AJAMBO LAKINI.SAMAHANI NTAKUPIGIA SIMU, MWENYENZI MUNGU AKUBARIKI.AMINA.

    ReplyDelete
  19. WAHAMIAJI HARAMU 104 WAFUKUZWA NCHINI
    2007-09-28 18:44:33
    Na Mwandishi Wetu, Jijini


    Serikali ya Tanzania imetoa amri ya kuwafukuza nchini wahamiaji haramu 104 waliokamatwa na kuhukumiwa katika maeneo mbalimbali kati ya kipindi cha kuanzia Julai na Septemba mwaka huu.

    Hati za kuwafukuza wahamiaji hao zimesainiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Joseph Mungai kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu Na. 14 cha Sheria ya Uhamiaji Na. 7 ya mwaka 1995.

    Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo inasema, kati yao, wahamiaji haramu 74 wanatoka nchini Ethiopia na 30 kutoka nchini Somalia. Wahamiaji hawa haramu walikamatwa katika mikoa ya Pwani, Tanga, Shinyanga, Mtwara na Manyara.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, idadi hii inafanya jumla ya wahamiaji haramu 388 waliofukuzwa nchini kuanzia mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu ambapo 284 walifukuzwa nchini mwezi Julai.

    Aidha Serikali inaandaa vibali vya kuwafukuza nchini wahamiaji haramu wengine 52 waliokamatwa mkoani Pwani hivi karibuni.

    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Joseph Mungai ameipongeza Idara ya Uhamiaji na pia Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri wanayofanya kukabiliana na tatizo la wahamiaji haramu.

    Aidha Mhe. Mungai ametoa wito kwa viongozi wa Serikali katika ngazi za vijiji na wilaya pamoja na wananchi wote kushiriki katika zoezi hili la kukomesha vitendo vya wahamiaji haramu.

    Amesema Serikali za vijiji na wilaya pamoja na wananchi wana nafasi nzuri ya kuwabana wahamiaji haramu kwa vile wahamiaji hao wanapitia katika maeneo yao.

    Aidha amesema Serikali itaendelea kuimarisha doria katika maeneo ya miji na mipakani na akatahadharisha kuwa hatua kali zitaendelea kuchukuliwa kwa wahamiaji haramu watakaokamatwa.

    Amesema kuwa adhabu kali pia zitawahusu wananchi watakaobainika kusaidia kuwahifadhi na kuwasafirisha wahamiaji hao haramu.

    "..TUNAISHUKURU SERIKALI KWA MWENDO HUU WENGI WAO NI MAJAMBAZI NA WENGINE WANATUJAZIA TAKATAKA KUTOKA ASIA WAKIDAI NI WAFANYA BIASHARA.."

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...