

ndo natoka sea cliff hotel sasa hivi na moto umeshazimwa karibu wote na hao wana faya wanamaliziamalizia. habari nilizopata ni kwamba iliyoathirika ni ghorofa ya juu na huenda vyumba vimesevu, lakini habari kamili ya hasara iliyopatikana tutapata baadaye maana hapo umeme hamna na ni vigumu kusema kwa kuona tu. ila sehemu ya baa ya ufukweni pamoja na casino na pale pa kuchezea bowling paa zake nimeziona hazijaathirika. lakini kama nilivyosema ngoja kukuche ndo tutajua kwa uhakika. ila inaonesha vyumba vimesalimika kama muonavyo pichani...
HONGERA ZIMAMOTO TZ.
ReplyDeleteMh bongo jamni, kesi ya kuku, kuua ng'mbe. Heeh mbona mambo
ReplyDeleteHuku Moshi na Arusha mambo ya kuezeka na makuti walishakataza siku nyingi. Nashangaa huko Dar bado mnaendelea, kutumia vitu asili ni muhimu ila kama hatuna Fire brigades za uhakika bora tusiezeke. Poleni sana menejiment ya Sea Cliff
ReplyDeleteMiaka ya 80's ile hall kubwa ya hoteli ya Bahari Beach iliungua moto baada ya mgeni (Mtoto wa kizungu) kuliunguza kwa kucheza kibiriti. (ilikuwa imeezekwa na nyasi)
ReplyDeleteHuko Bagamoyo Chuo cha Usanii ukumbi wao na vifaa muhimu viliungua! Jengo ilikuwa imeezekwa na nyasi!
Jamani hizo nyasi zinapendeza na zinavutia wageni lakini jamani, mweke fireproof roofing chini.
Poleni wafanyakazi na wageni wa Sea Cliff Hotel.
makuti na joto wapi na wapi? Kweli hata insurance watalipa hapo?
ReplyDelete