mdau tusa njwaba (kati) aliyejizolea nondozzz katika sheria za kimataifa na haki za binadamu huko chuo kikuu cha ultrecht university cha uholanzi. tusa pia ni mwanaharakati wa kutegemewa katika kutetea haki za wanawake na watoto. huko uholanzi tunaambiwa vyuo vingi sasa hawatumii majoho wakati wa kula nondozz na ndio maana mdau tusa hajavaa joho.



mdau twisa (pili kulia) akifurahia na wadau wengine baada ya mahafali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Vyuo vingi Uholanzi hawatumii majoho,na hicho hapo juu vipi?Au the Hague sio Uholanzi?Tuache kudanganyana huyu hapa hajachukua nondoz wala nini,anapenda aonekane tu hapa...

    ReplyDelete
  2. Kweli nimeamini watanzania tunapenda kuchonga pasipo sababu. Amesema vyuo 'vingi' na siyo 'vyote'. Kwa ufafanuzi zaidi maana naona ujumbe wa mwanzo kidogo una utata, vyuo vingi vya Netherlands vinavyofuata utamaduni wa kidutch hawatumii majoho kwenye mahafali. Hilo ni kweli nimeshuhudia mwenyewe so msianze mnanga dada wa watu. Sasa huenda ikawa chuo alichograduate dada Mbagga hapo juu ama hawafuati utamaduni wa kidutch au ni kati vile vichache vinavyofuata utamaduni wa kidutch kwa mapungufu. Nikisema kwa mapungufu namaanisha kuna baadhi ya mambo wamelegeza kama haya ya kutumia majoho kwenye mahafali

    ReplyDelete
  3. Wewe hapo juu umeishi uholanzi na umesona vyuoni? nni kweli kabisa hawavai majoho na kama wakivaa ujue ni aina tofauti ya shule vitongoji vyake vitakwua UK au USA. Ila wka wadutch suti na kwua smart tu inatosha kupokea nondo tena anaweza vaa mtu tshirt tu na akapewa nondo yake hawaoni umuhimu wa kuvaa joto maana hadi chekecheka wanavaa tz no dhamani kabisa muhimu cheti kwisha.Sie tumeiga machumbuko ya british colonial basi tunyamaze.

    ReplyDelete
  4. Hongera sana Tusa.

    ReplyDelete
  5. Toka nizaliwe sijawahi ona chuo kikuu wanacho-graduate bila joho.

    Nimezoea kuona vyuo vya VETA ndio hu-graduate bila majoho.

    Hicho nacho nilidhani pia ni chuo cha VETA hata nilipoangalia hii picha kinafanana kama Chuo Cha VETA.Kumbe nimeona vibaya samahani.

    ReplyDelete
  6. Michuzi unatuchanganya, hapo juu umeweka mdau kala nondoz toka uholanzi amepiga johozz. Huyu hapa hana kitu kweli kala nondozz? Please verify

    ReplyDelete
  7. Tusa, Hongera sana. Naomba contacts zako tafadhali kwa ajili ya mambo ya shule. Nami natamani kukamata nondo.

    ReplyDelete
  8. ANONS WA 19 SEPT 4:50:00 NA 2:16:00 KAMA HAMJUI KITU HAINA MAANA HAKIPO!!!UNASEMA VETA....MWINGINE ANATAKA UFAFANUZI, TEMBEENI MFUNGUE MACHO..UNAJUA BWANA EXPOSURE NI KITU MUHIMU SANA...TASWIRA YENU YA DUNIA NI NDOGO SANA! KWASABABU TUMETAWALIWA NA WAKOLONI WA UINGEREZA NA TUNAFANYA KILA KITU KAMA WAINGEREZA HAÍNA MAANA WAJERUMANI NA WAHISPANIA NA WASWEDE NAO WANAFANYA HIVYO HIVYO..., WAO HAWAKUTAWALIWA!

    ReplyDelete
  9. kupata nondo sio lazima joho!sio huko tu hata algeria hawavai joho na wameiga mfaransa aliyewatawala!wewe ambaye hujawahi ona tembea uone!!

    ReplyDelete
  10. Kinehe Matondo, ndikubona namhala

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...