HABARI ZIMEINGIA SASA HIVI KWAMBA NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MH. SALOME JOSEPH MBATIA (55) AMEFARIKI DUNIA JIONI HII SAA KUMI NA MOJA UNUSU ENEO LA KIBENA KWENYE MASHAMBA YA CHAI KABLA YA KUFIKA NJOMBE UKITOKEA MAKAMBAKO KWA AJALI YA GARI.
KWA MUJIBU WA TAARIFA ZA AWALI DEREVA WA MH. MBATIA NAYE ALIFARIKI HAPO HAPO AJALINI BAADA YA GARI LAO DOGO WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUGONGANA USO KWA USO NA LORI AINA YA FUSO AMBAPO DEREVA WA LORI HILO PIA INASEMEKANA AMEKUFA
WASIFU WA HAYATI SALOME MBATIA KWA MUJIBU WA TOVUTI YA BUNGE BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Mbona inatisha sana bongo. Hizo ajali ni nini? Ni barabara mbovu, matairi mabovu,hamna speed control au ni sheria za barabarani watu hawazifuati? Inatisha sana

    RIP

    Poleni wafiwa

    ReplyDelete
  2. Jamani jamani jamani bongo kunani tenaa!! yaani nimeona tu breaking news waziri nikahisi ni ajali tu!!!
    Wafiwa poleni sana.

    ReplyDelete
  3. RIP Mheshimiwa na wale woote waliofariki katika ajali hiyo.
    Pia nawatakia kupona haraka kwa majeruhi

    ReplyDelete
  4. RIP, alikuwa dada wa shule wa mama yangu walivyokuwa Boarding school, Korogwe.

    ReplyDelete
  5. Rest In Peace..mama Mbatia, Hakika Umetuachia pengo kubwa sana.

    ReplyDelete
  6. Jamani, jamani, mbona bongo inakatisha tamaa na hizo ajali? kweli ajali ni popote pale, mungu anapoandika, lakini sasa hivi ajali bongo zimezidi jamani, hebu serikali iwachukulie hatua kali madereva wazembe!! any way, ajali haina kinga, na kazi ya mungu haina makosa. POLENI SANA WAFIWA, M'MUNGU AWAPE MIOYO YA SUBIRA, INSHAALLAH. MUNGU AZIWEKE PEMA PEMONI ROHO ZA MAREHEMU, NA AWAJAALIYE MAJERUHI WAPONE HARAKA. AMIN.
    Nu.

    ReplyDelete
  7. Mungu zilaze mahali pema peponi roho za marehemu hao

    ReplyDelete
  8. Poleni sana familia,ndugu jamaa na marafiki kwa msiba huu.

    Mwenyezi Mungu azipumzishe roho za marehemu wote waliohusika kwenye ajali hiyo mahali pema peponi.Amina

    ReplyDelete
  9. hizo ajali zimezidi tunajua hazina kinga lakini hizi zinawaandama hadi vigogo,na vibara bara vye mbamba sana na magari yamekuwa mengi.

    ReplyDelete
  10. Kwa kweli hili ni pengo kubwa, she was a strong woman and a good role model.Rest In Peace.
    Lakini jamani barabara za Tanzania zinatisha!Sijui what happened in this case lakini kwa ujumla dereva wa serikali na dereva wa fuso na mabasi ya abiria ni HATARI !!!!!!Tunaomba serikali iangalie issue hii kwa umakini.Road Safety ni nadharia tu Bongo.Leseni ziwe za kweli, correct road safety measures ziwepo.
    Mungu awalaze marehemu wote peponi.

    ReplyDelete
  11. Hii kweli inatisha. Mungu azilaze pema nyoyo za wote walohusika kwenye ajali hii. Lakini ni nini kifanyike jamani? Hii ni sababu ya kuwepo kwa rushwa everywhere Tanzania! Kwenye kutoa leseni na kila mahali. Haya....watu wanaendesha magari makubwa bila kuwa na ujuzi au elimu ya usalama barabarani ya kutosha!

    ReplyDelete
  12. RIP mama.

    ReplyDelete
  13. WANA BLOG WENZANGU......

    HASA WEWE ANOY OCT. 24 8:13:00 MBONA UNAONGEA KAMA PUMBUONE, UNASEMA AJARI NI POPOTE KAMA MUNGU ANAPOANDIKA.SASA ULITEGEMEA VIPI HUYU BINTI/MAMA ANGEPONA? UMESAHAU MSEMO WA KWENYE BIBLIA KWAMBA KILICHOPANGWA NA MUNGU MWANADAMU HAWEZI KUKIPANGUA? SIKU YAKE HUYU MAMA IMEFIKA NA YA KWANGU, MICHUZI NA WEWE ITAFIKA TUTAWAACHIA HII DUNIA WENGINE WAENDELEZE LIBENEKE KUMBE HAKUNA HAJA YA KUNUNG`UNIKA SUBILI ZAMU YAKO KAMA NI HOSPITALI AMA UTALAMBWA NA KIBAKA SIJUI. LILILOPO HAPA NI KUMWOMBEA HUKO ALIKO ALE GOODTIME THAT IS IT. LAKINI OOH BONGO HAKUNA LAMI MARA OOH BONGO KUNATISHA NA AJARI, SUBIRI ZAMU YAKO UTAONA NI NINI KINAKUONDOA KWENYE HII DUNIA YA RAHA ANASA NA MATESO...ASANTENI SANA MAMA TUNAKUOMBEA HUKO ULIPOTUTANGULIA MBELE YA HAKI ULE GOOD TIME SANA NA UTUPOKEE SIKU MOJA NA SISI TUKIJA. BWANA ASIFIWE MILELE AMINA.

    ReplyDelete
  14. NGOMA INATISHA JAMENI...!
    OOOH OOH JAMENI MIMI SIJUI NISEMEJE JAMENI YAANI BASI TU HUYU DADA KATUTOKA? JAMANI MBONA HAKA KAUGONJWA KA NGOMA BARABARANI KATATUMALIZA? JAMANI JAMANI TUITIKIE WITO WA MWESHIMIWA RAIS JAMANI...TANZANIA BILA NGOMA INAWEZEKANA JAMANI...MBONA NGOMA ITATUMALIZA JAMANI...KWANI HIZO DAWA ZA NGOMA HAZIWAFIKII WENZETU JAMENI..ZA KUONGEZA/KUREFUSHA MAISHA? MAMA KATUTOKA JAMENI TUMWOMBEE KWA MORA. LAKINI TANZANIA BILA NGOMA INAWEZEKANA KABISA JAMANI. HIZI NGOMA ZA AJARI ZINA TISHA SANA HASA KWA NDUGU ZETU VIGOGO WALAHI INATISHA,KIKWETE HAWA TRAFIC HAWAWEZI KUZUIA HIZI NGOMA KWELI ZA BARABARANI MWENYEZI MUNGU TUEPUSHE NA NGOMA JAMANI!!

    ReplyDelete
  15. Mungu aipokee roho yake ailaze pema peponi! sasa...jamani.. Mungu yaani ua likichanua anachuma. Basi yeye ndiye muweza wa yote tumuheshimu na kumtumikia.
    Pole zetu wafiwa!

    ReplyDelete
  16. Roho za Marehemu zipumzike kwa Amani na Pole za dhati kwa familia, ndugu na jamaa za marehemu. Pengo la Marehemu hawa alitokaa lizibike. Mola wetu awaweke pahala pema peponi na hawajalie pumziko la milele na mwanga wa milele awaangazie. Amen

    ReplyDelete
  17. Tatizo la Tanzania madereva wanandhani kuendesha gari ni haki yao that's why they don't care. Nchi zilizoendelea wanasema kuendesha gari ni Privilege, hivo ukiiabuse serikali ina haki ya kukunyang'anya leseni yako forever. Kuna watu hawaruhusiwi kuendesha gari for the rest of their lives. Lazima tuimplement centralized system itakayo track bad drivers na kuwaadhibu kabla hawajaua raia wema ambao wapo barabarani kujenga nchi. Pole ni wafiwa na serikali kusema kweli mwaka huu serikali imepoteza viongozi mashuhuri na baadhi yao kujeruhiwa vibaya hadi kupoteza viungo vyao, I think it's high time Serikali ilichukulie hili suala seriously. THIS IS AN INNOCENT AND PAINFUL NEWS TO HEAR!

    ReplyDelete
  18. May the Lord of plans and power rest the soul of mama Mbatia in peace, He is the only one who knows our fate, so please lets not continue blaming any of us so far we dont know whats going to be our fate.
    Poleni wafiwe wote, Mungu awatie nguvu na kuwapa amani.
    Bwana alitoa, na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe. Amen

    ReplyDelete
  19. Masiktiko makubwa kupoteza mama huyu mtendaji mahiri.
    Faraja kubwa ziwe na zamilia yake, wapiga kura wake, na watanzania kwa ujumla. Kaka michu ukiweza tuwekee picha za tukio la ajali

    ReplyDelete
  20. Rest in Peace mama Mbatia. Mungu awafariji wafiwa wote - familia, ndugu na marafiki. Tuko Pamoja mpaka mwisho

    Kwa taarifa ya wasiofahamu - barabara hiyo ni lami safi kabisa hadi mbeya so ishu sio barabara. nahisi ni dereva wa fuso maana wamezidi kutumaliza.
    Picha zipo kwenye magazeti ya leo asubuhi- zinatisha sana. I believe kaka michuzi utazi upload wote wazione.

    ReplyDelete
  21. RIP Mama. Kwa kifupi mama alikuwa na busara sana. Basi hatunae tena. Nawatakia wanafamilia nguvu kuikabili hali hii

    ReplyDelete
  22. Tatizo la hili naona. Serikali iweke mkazo kwa kupitia vyeti vya madereva wote wa viongozi na wa mabasi makubwa

    ReplyDelete
  23. jambo muhimu ni kwamba hata zitto kabwe ametoa salamu za rambi rambi. hii ni jambo jema sana siasa za nchi kujaliana wakati wa shida

    ReplyDelete
  24. Maskini Salome, dada yetu wa Korogwe girls na akina Mwanaidi Sinare, Regina Mumba(Lowassa), na wengine jamani wa Korogwe High school mpo?

    Moyo unaniuma sana! RIP dada

    ReplyDelete
  25. Jamani miundo mbinu isipotengenezwa itamaliza hawa mawaziri. Kwa sababu sasa hivi wanatakiwa kwenda kila mkoa kuelezea bajeti ya JK, na barabara ni mbaya ajali ngapi tunangojea? JK kuwa mwanaume tenga mabilioni uunganishe mikoa yote ya Tanzania uone uchumi utakavyokua. Hakutakua na haja watu kukimbilia Dar tu. Mtu atatoka Mwanza uza mazao yake asubuhi Kariakoo jioni yupo Mwanza tena. Miundo MBINU JAMAAA itaua Mawaziri wote tusipoangalia!!!!

    ReplyDelete
  26. Jamani tatizo sio madereva, ingawa na wao pia wanatakiwa kulaumiwa. Ila hii ni miundo mbinu. Barabara ni mbovu, hii imegongana uso kwa uso kwa ajli ya kukwepa mashimo na kadhalika. Yaani tusipoangalia miundo mbinu, hawa mawaziri wataisha kwa ajili siku hizi wanatakiwa kwenda mikoani kutetea bajeti ndio maana katika miezi miwili tumeshuhudia ajali kama tano za mawaziri. Wote walikuwa mikoani kuelezea bajeti. Barabara zitengenezwe jamani. Watu wataanza kukataa wakiteuliwa kuwa Mawaziri.

    ReplyDelete
  27. i cant imagine such accident.i believe there is a certen hand over CCM.why was Kabwe Zito behind on his car.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...