Home
Unlabelled
enzi hizo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
vipi michuzi hao jamaa wenye vitambi kama walevi wa komoni ambao wamemzunguka mzee ruksa ndio walioleta hilo kombe au.. kujipa misifa tu!! kazi afanye mwingine sifa ajimwagie kitambi! masikini tanzania!
ReplyDeleteKaka Michu,
ReplyDeleteEbu saidia majina.
Huyo aliyekamata kombe ni Mzee Ruksa enzi zake? Kushoto kwake huyo jamaa ana sura kama ya waziri Kapuya ni yeye?
Kweli hawa mabwana kabla hawajawa mafisadi walikuwa watu wa kawaida tu.
Naomba orodha ya majina ya hawa waheshimiwa.
Ahsante.
wafupi ile mbaya!
ReplyDeleteMichuzi kombe la chalenji sio lolote. Hatuko juu kisoka, tunataka kombe la Afrika.
ReplyDeleteTanzania hatujawahi kuwa juu kisoka. Tunabahatisha bahatisha tu kutegemea na timu tunayocheza. Tatizo ni kwamba kitu kikiwa cha zamani kila mtu anataka kudai kilikuwa bora. Ila ukweli ni kwamba watanzania soka sio jadi yetu. Ushauri wa bure, tungeelekeza juhudi kwenye michezo ya ngumi, riadha, na vitu vingine vichache ambavyo tumewahi kuwa na mafanikio ya kuridhisha. Lakini soka ningeomba watu wa habari watuongezee satellite systems tuangalie Brazil, Ufaransa, Italia, Ujerumani, Argentina, Uingereza, n.k
ReplyDeleteKuvaa tu nguo za bendera ya Tanzania uwanja mzima haisaidii kitu kama wachezaji wenyewe hawana uwezo, halafu wana matatizo kibao ya kijamii, kisaikolojia, na lishe. Niliwahi kuona timu za taifa Bongo na Senegal wamejipanga kabla ya mechi. Ukiangalia upande wa Senegal unaona maumbile ya wachezaji kweli na wenye misuli ya kiuchezaji. Ukitazama Tanzania, kama mtu akifunika picha kuanzaia kiunoni kwenda juu ukitazama miguu na misuli yao ni kama washiriki wa Miss Temeke wamejipanga.
Kupiga kelele sana hakiunui soka. Tunatakiwa kujua uwezo wetu uko wapi na kuandaa program za kuwezesha kufanya vizuri. Nchi nyingi sana hazichezi soka lakini zinafanya vizuri kwenye maeneo mengine. Sio lazima kila mtu acheze soka