mshambuliaji mwiba wa simba ulimboka mwakingwe akikata mbuga kwenda kuwaumiza yanga baada ya kumtoka mlinzi wa jangwani leo uwanja wa jamhuri morogoro ambako msimbazi wameibuka kidedea kwa mara ingine kwa ushindi wa goli 1-0.
beki wa simba nurdin bakari ambaye ndiye aliyetoa pasi hii iliyozaa goli alizimia baada ya mechi. mchezaji huyo ana historia ya kuwa na matatizo ya moyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Yanga kwa Simba ni kama mbwa kwa chatu au katika simi za siku hizi ni kama kumsukuma mlevi. kwa heri.

    ReplyDelete
  2. That's what I'm talking about. Siiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiimbaaaaaaaaaaaaaa! Yap, acha bakora zitembeee Jangz!!!

    ReplyDelete
  3. Kweli mshambuliaji anachanja mbuga..Uwanja huo no mbuga kweli kweli vumbu tu kama vile umeona kundi la nyumbu mbugani..
    Na huyo beki wa simba anayezimikazimika inabidi awaone wataalamu, yasije yakatokea kama ya marehemu Marc Vivian Foe!

    ReplyDelete
  4. Waswahili husema "kuku ni kuku tu jogoo no jina" ndivyo ilivyokuwa kwa Yanga hata baada ya kupewa shs 50M kuimaliza Simba bado wamepigwa. Fedha haziwezi kuwa kila kitu!!!! Lakini Michu, mbona ya bwawa la maini huyasemi?

    ReplyDelete
  5. YANGA MDEBWEDO, BONYEEEEE!!!

    ReplyDelete
  6. Bro Michu, Bwawa la maini aibuuuuu tu! Pointi mmoja kati ya mechi tatu championi ligi?? Pole sana!

    ReplyDelete
  7. Naomba chama cha mpira kiingilie kati kuhusu huyo mchezaji wa simba anayeumwa ugonjwa wa moyo kwasababu hawezi kuendelea kucheza mpira huku anaumwa matokeo yake ipo siku atapoteza maisha kama wachezaji wengine waliokuwa na ugonjwa kama huo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...