WADAU LEO NI SIKU YA KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE. NINA HESHIMA YA KUITAMBUA SIKU HII MUHIMU KATIKA HISTORIA YA NCHI YETU KWA KUBANDIKA BAADHI YA PICHA KUADHIMISH SIKU HII ADHIMU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Michuzi, kulingana na habari za magazetini, inasemekana kuwa kibanda hicho hakijulikani kiko wapi!

    Je, ni kweli?

    ReplyDelete
  2. Hakika pengo lako tunaliona.Kimwili tunaamini hatuko nawe lakini kiroho upo nasi basi tunaomba utuombe kwa mungu hawa mafisadi wote kwa mujibu wa umoja wa kisiasa kupitia kwa Dr.Slaa,watokomee. Tuombee pia ili rais wetu aweze kushaurika na pande zote bila kuegemea itikadi za kisiasa kama ilivyo sasa. Tuombe pia ili tuepukane na jinamizi hili la viongozi wetu wa nchi kulimbukia utajiri wa kidunia na kuliangamiza taifa lao wenyewe kwa kukosa uzalendo. Taifa hili tajiri kwa maliasili linaangamia kwa kukosa uzalendo,mwalimu tuombee ili tuweze kujua nini maana ya uzalendo maana viongozi wetu hawajui maana ya uzalendo,pengine wanafikiri mzalendo ni gazeti ! Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  3. Michuzi unampamba sana Mwalimu kitu alicholeta Tanzania ni UHURU tuu. Huyu mtu alikuwa msoshalisti, mkandamizaji wa alikiuka haki za binadamu. Mimi simuenzi mtu mnafiki na rafiki wa Jimmy Carter na Castro. Pamoja na makosa mengi Mwinyi alikuwa Bora kuliko Nyerere...nipe hoja

    ReplyDelete
  4. Unajua kuna vitu vya kupotea sasajamani kibanda kikubwa kama hiki kinapoteaje? maana hii debate ya wapi kilipo imeanza kitambo na wusika wamekaa kimya tuu... mnatucezea siku tutachapana viboko.

    ReplyDelete
  5. Ni kweli aliuwa na kasoro zake ambazo kila mwanadamu anazo, Nyerere alikuwa kama nabii amaye alikuwa na uwezo wa kusema na kusikilizwa na kila mtu. kwani hata maisha ya Yesu ni miaka mitatu tuu ndiyo tunayoisoma kwenye maandiko sembuse miaka 30 ya maisha ya mtu wa kawaida kama Nyerere?

    ReplyDelete
  6. Hakuna hata kimoja cha maana alichokileta chenye manufaa kwa nchi, zaidi ya ukiritimba wa Siasa za Ujima, mwelekeo wake haukuwa na msingi wowote.

    Tumenyanyasika kiuchumi, kielimu na kila sekta muhimu munayoifahamu.

    Tumekula Yanga chungu, maduka ya UShirika, Azimio la Arusha(Squandering of peoples wealth).. Sasa tunaanza upya kwa jamii ambayo kizazi baada ya kizazi still inaathirika na fikra zake.

    Hakika kama angekua madarakani, nisingeweza kufikia hapa nilipo mimi mwenyewe binafsi.

    Kutokana na elimu ndogo na ujinga mkubwa uliyoikumbuka TAnzania, hususan viongozi wetu wa leo, ndio maana hatufikii popote, fikra zetu zimefungwa kutokana na kasumba na Siasa mbovu za JK Nyerere.

    Yapi na mazuri munayojua nyinyi, Hakuna hata moja, mtu kumiliki passport ilikua marufuku katika kipindi chake, TV alikua anaangalia yeye tu.

    Alikua ni mjinga wa fikra na mawazo. Leo hii vijana wenye fikra mpya na mawazo mapya ndio wanaiongoza Rwanda, na katu kwa siasa hizi wazee wa zamani kushikilia nchi katu hatutoweza kufika popote pale.

    Zaidi kunyanyasika kifikra, kimawazo na kielimu kama tunavyonyanyasika sasa.. Waekezaji wanasquander mali zetu kutokana na kutokuwa na viongozi imara wenye mwelekeo ulio bora wa nchi, kwa sababu gani ?? You tell me, kwa sababu ya kushikana na fikra za JK.. Someone has to break loose turidu pale mwanzo baada ya kupata UHURU.. Maondeleo yalikuwepo..Huyu JK kakiwasha tu .. Hamna lolote la maana alilotuletea, na athari kubwa kama mkizidi kung'ang'ania fikra zake ndio zituelekeza pa zuri..

    LAzima mutakuwa day dreaming.

    FIKIRI! FIKIRI!

    ReplyDelete
  7. acheni kumkashifu nyerere,nyie mlio majuu wengi wenu mmesoma bure enzi zake harafu leo mnajifanya kumkashif, eti alikuwa mkandamizaji? sasa hawa viongozi wenu wa leo ndio? fisadi? wala rushwa? au?
    go east and west but nyerere will remain the best...

    ReplyDelete
  8. Nyerere,alikuwepo,amepita,hata sisi,tutapita,cha kuiuliza wewe na mimi hat kama haturidhiki na alichofanya wewe na mimi tumefamnya nini kwa Taifa letu,na tuna waachia nini watoto wetu cha kuendeleza?
    nafikiri tuache manung'uniko,haa tusaidii kama kuna mwenye mwelekeo ajitokeze na awe mvuto wa marehemu.sasa amelala milele hasidii kumbeza.jiweke tayari nawe au mimi kwa hatua za kesho....Mambo yake mazuri bado yanatufaa..

    ReplyDelete
  9. Wanasema eti bahati huja mara moja katika maisha ya mtu basi yetu ya kumpata kiongozi kama Baba Nyerere imepita. Maskini watanzania! Nyerere utamkumbukwa daima, na mapungufu yake alitupenda watanzania wote sawa maskini/matariji, makabila yote wahindi/wathungu/waafrika..., waathirika/wasio/ nk mtu asibishe hapa

    rip Baba yetu wa taifa

    ReplyDelete
  10. Wewe wa October 14, 2007 12:03:00 PM EATRwanda, Rwanda, nenda kaishi huko!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...