Serikali yafafanua fidia kwa kituo cha mafuta Mwanza
Serikali imetoa ufafanuzi wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni juu ya fidia ambayo mahakama kuu iliagiza kulipwa kama fidia kwa kituo cha mafuta huko Mwanza yenye kichwa cha habari ‘Serikali yapigwa faini ya Sh15 bn’.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, jumla ya fidia iliyoamriwa na Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza ni Sh1.2 bilioni na siyo Sh15 bilioni kama iliyoripotiwa.
Ufafanuzi huo unaeleza kuwa katika hukumu yake ya Agosti 30, Mhe. Jaji Lawrence Mchome aliamuru kuwa mlalamikaji, kampuni ya Mansoor Industries Ltd, alipwe Sh490 milioni kama gharama ya jengo lililobomolewa (special damages) na Sh730 milioni kama hasara ya jumla (general damages). Aidha, Mahakama Kuu iliamuru kuwa malipo hayo yalipwe pamoja na riba ya asilimia 17 kwa mwaka tangu ubomoaji ulipofanyika.
Hata hivyo, Mahakama Kuu ilitupilia mbali ombi la mlalamikaji la kutaka alipwe Sh13.4 bilioni kama hasara ya biashara (loss of business) aliyotegemea kupata katika kipindi cha miaka 33 ya umiliki wa kiwanja na 178, kitalu ‘A’ kilichopo eneo la Kirumba jijini Mwanza ambapo mali iliyobomolewa ilijengwa.
Pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wengine waliokuwa wakilalamikiwa katika kesi hiyo ni Waziri wa Ujenzi, Waziri wa Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa na Halmashauri ya Jiji, Mwanza.
“Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inapenda kueleza kuwa imesikitishwa na upotoshwaji uliotokea. Tunatoa wito kwa wanahabari kuwa makini wakati wanapotimiza majukumu yao na hasa wanaporipoti maamuzi ya chombo nyeti kama mahakama,” imesema sehemu ya taarifa kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Ofisi ya AG MNACHEKESHA!!! YAANI KESI MMEPIGWA CHINI HARAFU ETI MNATOA CLARIFICATIONS! Aise poor souls. Yaani ni kwamba hata kama ingekuwa mia mbili ni kwamba Serikali ilishindwa kesi na tangu lini Ofisi ya AG ikatoa tamko ku-clarify uamuzi wa mahakama? Au mmeshtuka baada ya kuona ni hela nyingi na mnaweza fukuzwa kazi? Poleni ila hii ni minimalist approach kabisa!
ReplyDeleteJust admit kama mlikuwa incompetent mkapigwa chini basi! Acheni longo longo za kiana.
Huyo kiongozi wa serikali aliyeamuru hicho kituo kivunjwe hajui ni hasara kiasi gani kiliingizia taifa?Kwa nini asilipe hizi gharama yeye?Je atawajishwa baada ya hizi gharama kulipwa?
ReplyDeleteKweli bongo safari ni ndefu.
Sasa huyu kiongozi aliyamuru kituo kivunjwe alikuwa hajui kama nchi inaenda kwa mujubu wa sheria ?
ReplyDeleteHizi jazba zake za kusifiwa zinaishia kuiingizia serikali hasara.
Heko mahakama kufanya kazi bil kuyumbishwa
huu ni mwanzo tu mwa maamuzi yasiyozingatia akili na sheria, subirini ya city water ndio mtakimbia, hivi mnajua serikali mpaka sasa imewalipa shiling ngapi akina mkono kutuwakilisha, mkijua mtasaga meno. nilijua tu maamuzi aliyoyatoa magufuri kule mwanza yatasababisha kubebeshwa mzigo, alijifanya kujua sana, ingekuwa nchi za wenye akili sasa hivi angekuwa segerea. mnawalaumu bure hao watu wa AG kutokana na kiburi cha magufuri yawezekana walimshauri lakini akaleta kiburi tu. hakika nyerere angekuwa raisi kipindi hiki zaidi ya 99% ya viongozi waliopo wangekuwa wanauza mchicha kariakoo, uwezo wao ni mdogo sana halafu wanajifanya wajuaji.
ReplyDeletesijaona hicho walichofafanua.
ReplyDeletelabda sasa mawaziri wazunguke nchi nzima kuifafanua hukumu kama wanavyofanya kwa bajeti.
tumeingia hasara kwa maamuzi ya kibabe ya John Pombe Magufuli kwa baraka za Ben Mkapa.
anonumous @ 7:22 am,
hata katika utawala wa Nyerere kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria na haki za binadamu uliokuwa ukifanywa na viongozi.
umesahau harakati za wahujumu uchumi? huo ni mfano mmoja tu. sheria iliandikwa baada ya watu kuwekwa kizuizini.