naibu waziri wa mambo ya ndani mh. lawrence masha akikata utepe kuzindua duka la nguo za lebo ya kp akishuhudiwa na mmiliki wa duka hilo lililopo ndani ya millenium towers kijitonyama-makumbusho, dar, usiku huu katika sherehe iliyohudhuriwa na wadau kibao wa fani mbalimbali

mh. lawrence masha akihutubia kwenye uzunduzi wa duka na lebo ya kp huku masudi ali kipanya akiwa pembeni yake

mmiliki wa duka na lebo ya kp masudi ali kipanya akijitafunatafuna

full kujiamini....

wageni toka kila pembe walifurika kwenye uzinduzi wa duka na lebo ya kp usiku huu

masudi ali kipanya akiwaonesha wadau na mgeni rasmi baadhi ya vitu vyake orijino. anasema kwa maelezo zaidi mwandikie sms kupitia +255 754 291 193




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Hii ndo kila siku nilikuwa nazungumzia na kupigia kelele! Tanzania haitaendelea, na watanzania wasitegemee maisha bora kama hawatakaa chini na kupanga vitu jinsi ya kuwa wajasiria-mali! blog hii ni mfano wa kuigwa, kp na ubunifu wake ni mfano wa kuigwa pia!

    Tuache kelele na kukaa vijiweni huku tukitegemea maisha bora yatatukuta vijiweni, na nyie mlio ughaibuni, leteni elimu yenu tanzania, tukaipeleke tanzania kwenye stage nyingine, acha kug'ang'ania kazi za wazee, kufanya ulinzi, kupiga unesi, kula mabox n.k!

    Hata Roma haikujengwa kwa siku moja! ipo siku na bongo itakaribia maisha ya wa-ghaibuni..
    ALUTA CONTINUA KIPANYA na wadau wengine wenye ka kuja na fikra mpya katika kutafuta maisha bora..

    ReplyDelete
  2. Safi sana kuwa na original label za asili...Please mwambie copy right muhimu. Kesho tutaziona china town wanatajirika wengine.

    I like that...mpaka jeans bwana wangu!!! Halafu cotton yetu nzuri kweli tu hawaifagilii...

    mwambie kumarket muhimu kuna suruali zilitoka sweden wala hazina cha zaidi basi tu hilo jina...silikwenda kwa $175 a pair. nadhani mwezetu kasha kuwa millionea.

    Kipanya Big up ....hongera sana. Mfano wa kuigwa kwa wote. Mwishowe tutaexport more badala ya kuimport uchafu

    ReplyDelete
  3. awamu ya 4 kweli kiboko,waziri anapiga PARA!!!
    ubitozi mwingi wanachofanya hakionekani
    mwee!

    ReplyDelete
  4. hongera sana bwana kipanya,lakini hizo nguo bado ni made in china tunaitaji mtu mwengene ambae anafikiri za kutengeneza nguo kutoka tz kwanzi wachina wananini zaidi kuliko sisi

    ReplyDelete
  5. jamaa wa kwanza umeongea point, ila tu linapokuja suala la kurudi Tanzania eti kwa kisingizio cha kuendeleza taifa hiyo nakataa .

    Wasomi waliopo hawalipwi vizuri na wengi wao hawatumiki vizuri . Ndo maana tunakimbilia nchi kama Botswana, ushelisheli n.k .

    tusidanganyane,...

    ReplyDelete
  6. Nampongeza Kipanya and Co, kwa juhudi zao katika ubunifu, uendeshaji wa ujarisiamali ndani ya TZ.

    maoni yangu kwako KIPANYA...

    Never Never Never, compromise QUALITY, hapo pekee ndio utafanikiwa...

    ReplyDelete
  7. ..thats what i'm talking about...big up kipanya!

    ReplyDelete
  8. Nguvu ya soda tu hiyo!
    Kwa jinsi watanzania ninvyowafahamu mimi, hilo duku litakufa muda si mrefu.
    subirini tu!

    ReplyDelete
  9. Unajua mambo ya Mkukuta mara Mkurabita ni kupoteza pesa tuu ni kuosha mawazo ya vijana ili wao ndio wawe wajasiriamali na kuukataa umasikini, Hongera KP unaonyesha njia kwa vijana kwa kutumia kila njia unayoweza. Mjasiriamali wa kweli.
    Pius

    ReplyDelete
  10. Safi sana Kipanya..... umpiga hatua mdheee!!
    lkn naomba nikuulize hizo nyewele ni unataka fuga rathta ama ulisahau kuchana tehe tehe!!!
    JAMANI SIJAELEWA MIE... KWANI LEBO NDO MANAKE NINI? NDO ANAKIWANDA CHAKUTENGEZA NGUO HEE??
    KA MISTUU NA WADAU WENGINE NIHELPUNI.

    ReplyDelete
  11. KIPANYA HONGERA SANA IT L@@K$ @K, HALAFFU WEWE "..MLALAHOI.." POLE SANA KWA MAUMIVU NA MUOMBE MUUMBA AKUSAIDIE..MUUMBA NDIO MPAJI WA VYOTE..

    ReplyDelete
  12. Huyo Kipanya ni bitozi sana. Hapo Millenium towers kuna Steers, Millenium Hotel, Maofisi kadhaa na maduka kibao ya nguo. Cha ajabu hakualika jirani zake hata mmoja kwenye ufunguzi wa duka lake. Majirani walishangaa tu kuona watu kibao wanakuja kwenye ufunguzi wa duka la jirani. Sasa ndio ujasiriamali unavyotakiwa wajameni? Love thy neiba! Ukipata ajali wao ndo watakuwa wa kwanza kuja kukusaidia.

    ReplyDelete
  13. Anony wa Friday, October 19, 2007 8:48:00 AM EAT, wapi umeona a close competitor (in this case maduka ya nguo) anaalikwa kwenye ufunguzi wa new player on the block?

    Maybe they should be glad for the foot traffic in the building and maybe it will generate some more customers and especially after a hip-hop Generation X junior minister and a bunch of bongo celebs were in attendance.

    ReplyDelete
  14. cul kipanya umefanya kazi nzuri sana nakutakia mafanikio na uzidi kutoa quality bomba made in tanzania wawaaaaa

    Australia

    ReplyDelete
  15. Wewe annony wa Friday, October 19, 2007 9:28:00 AM EAT...
    NADHANI WEWE NI FINA MANGO... yaani ni wewe tu kwani icho ki-inglish duuuh na iyo reason uliyoitoa lazima ni wewe BIG UP FINA

    ReplyDelete
  16. Kaka Michuzi na Wadau wengine. Kitaalamu hiyo haiitwi "Lebo" bali huitwa TRADE MARK.
    Ili kuilinda asiiibiwe na watu wengine. anatakiwa aende pale BRELA mtaa wa Lumumba D'salaam, ili akaiandikishe na kupata legal protection.
    Hongera.

    ReplyDelete
  17. Congrat's kipanya umepiga hatua mbele walau kuonyesha cornfidence but usijiweke juu sana walau watu wa kawaida waweze kununua bidhaa zako.
    Anon wa kwanza naona umetoka nje ya mstari watu wa majuu wee achana nao waowanachangi circulation ya pesa bongo.wengi wetu ndiyo wafadhili wa miradi kibao ya ndugu zetu huko bongo.
    Hata hayo maandazi ulokunywa nayo chai leo asubuhi mtaji wake umetoka majuu kwa wapiga box. nduguyangu acha mawazo na makali ya maisha ya kijiweni.

    ReplyDelete
  18. samahani wadau, lakini sisi tanzania hatuna kiwanda cha nguo sasa hizo nguo za kipanya mnasema eti ni original tanzania? nguo za ku order china na kuja kuuza tanzania ndio original? mimi naona bado ni feki maana alichofanya kipanya ni kuweka lebo yake tu lakini nguo ni made in china!!!!!

    ReplyDelete
  19. mhh nguo made in china zimewekwa lebo tu!!!!!

    ReplyDelete
  20. Masoud, nipigie simu haraka kuna jamaa hapa London wanataka nguo hizo, ni Watasha watupu wanalonga Kiswahili ile mbaya, wamekuzimia sana, piga simu mshikaji, mwambie Michuzi akupe simu yangu kama huna, changamka, mie nina hela kibao kwa mambo ya mizaha mizaha.

    ReplyDelete
  21. wewe unayejiita mlalahoi usiseme usichokijua,usidharau ujuzi wa watu wengine.Unesi ni proffessional inayoheshimika hapa Ulaya na watu wanasoma kuanzia miaka mitatu,mitatu na nusu hadi minne kupata Bachelor degree in Nursing ,na inatakiwa usajiliwe na body ya afya ya nchi husika.Mshahara unatafutiana nchi hadi nchi ila na kazi inayolipa.Sema kitu unchokijua sio kukurupuka.

    ReplyDelete
  22. safi sana, tena sana...watanzania tumuunge mkono huyu bwana masudi.

    ReplyDelete
  23. Tatizo sio label.Je zitanunuliwa??Mzee mzima umevaa kipanya! HOW?

    ReplyDelete
  24. Jamani lakini Masha bonge la handsome mimi nammind kama nini nilimuona huku DC recently. Mheshimiwa umetulia dear kwani umeoa?? Maana mi nimeolewa lakini we can work something out, au vipi?

    ReplyDelete
  25. WEWE Friday, October 19, 2007 12:15:00 AM EAT MVIVU WA KUFIKIRIA HIZO NI NGUO MADE IN CHINA NA LEBO YA KIPANYA....".HONGERA ZAKE KIPANYA.."LAKINI KUMBUKA KWAMBA WENZETU WACHINA NI VERI KRIETIVE WANAFAHAMU FIKA KWAMBA "..TUNAPENDA SHOO.." WHAT THEY DO IS VERY SIMPO PUT YOUR LEBO THATS ABAUT IT. HALAFU TUNAZIDI KUWAUZIA NGUO ZAO.."..MLALAHOI.."..UTAZIDI KUWA HOI.." NINANUKUU: POLE KWA MAUMIVU...

    ReplyDelete
  26. acheni mambo yenu, mbona hata nike inatoka china? na wanabandika tu lebo????

    ReplyDelete
  27. Anony 7:17 Acha wivu

    Anony 8:48 business haina cha love thy neighbor.

    Perez …. The term designer label refers to clothing and other personal accessory items sold under an often prestigious marquee which is commonly named and Trademark is a distinctive name, symbol, motto or emblem that identifies a product, service or firm that has been legally registered as the property of the …. . Kwa hiyo wanavyoita label hawajakosea akiregister ndio inakua trade mark yake.

    Na wengine hivi mnajua kuwa hata seven for all mankind, Prada, Citizen of humanity, bebe, True religion wote wanatengenezea nguo zao China? Sasa kwanini yeye muanze midomo juu? Hamna kiwanda cha raba wala jeans US au Uk kwa hiyo hata yeye alivyofanya sio jipya.

    Ila kipanya uwe unakwenda huko huko kutafuta na kuchagua quality ya nguo unazotaka. Na pia upeleke style zako unazocreat mwenyewe. Never compromise quality for price. Na ukeep originality utafanikiwa sana.

    ReplyDelete
  28. UMESEMA KWELI, HATA MA DESIGNER WAKUBWA WANATENGENEZA NGUO CHINA .

    TOFAUTI NI KWAMBA WAO WANA DESIGN, KISHA WANATAFUTA KIWANDA KITAKACHOCHUKUA TENDER YA UTENGENEZAJI TK KIWANGO WANACHOTAKA WAO.

    HIYO NI TOFAUTI NA KWENDA china KUNUNUA NGUO AMBAYO TAYARI WATENGEZAJI WAMEBUNI, KISHA WEWE UNAWEKA LEBO YAKO YA mbwegelembwegele .

    KITU MUHIMU NI KWAMBA KIPANYA ANAJARIBU KUJIIMARISHA KIUCHUMI . WAOSHA VIVWYA TUTAONGEA SANA BILA FAIDA KUPATA .

    KIPANYA HONGERA BANA !!

    ReplyDelete
  29. Nenda Kipanya nenda!
    Kila kitu lazima kiwe na mwanzo, tunahitaji watz wabunifu kwa vyovyote vile.
    Tanzania ya leo haitajengwa na majungu, umbeya na unafiki.
    Ukitaka ulipwe vizuri na uishi maisha mazuri ya kawaida ni vema ukajituma kwa kwenda extra miles kulikoni kulalamika bila ya majibu ya msingi.
    Nawapongeza wale wanaompa moyo KP na ushauri mzuri (Ushauri mzuri namaanisha positive na negative)

    Ninawalaani wanaodharau jitihada zake.

    Kila la heri Masoud.

    ReplyDelete
  30. U GOT 2 BE A "SHIRTLIFTER" 2 SUCCEED IN THIS KIND OF BUSINESS[CLOTHES DESIGNER] MR.KP R U 1 OF THEM???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...