jk na mama wa kwanza salma kikwete wakipozi na Papa Benedict wa 16 huko vatican jana.

kiongozi huyo wa kanisa katoliki jana hiyo hiyo aliteua makadinali wapya 23 na kwa habari hiyo kamili bofya hapa . Papa amekubali kuzuru bongo karibuni na kwa habari hiyo ya ziara ya jk huko vatican bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Kwa kweli mama yetu wa kwanza anajula kupigilia pamba ona alivyotoka kidiplomat

    ReplyDelete
  2. jamani kutokana na enzi za uwazi na ukweli mi leo nasema manake kila siku kinakera nafsi yangu mnaonaje first lady tumshauri afanye diet?. au waafrika utamaduni wetu ni unene?. lakini unene unaleta maradhi jamani

    ReplyDelete
  3. Namshukuru sana mheshimiwa rais kwa ombi lake la kuomba ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki duniani aje kuitembelea Tanzania.Itakua faraja kubwa kwetu pia nahisi matatizo ya kanisa katoliki yatapungua. Na mahusiano na madhehebu mengine pia dini nyingine yataimarika zaidi

    ReplyDelete
  4. Bro Michuzi,
    Kuna maoni nimepost juu ya kivazi cha mama wa kwanza umeyabania!!! basi ningeomba uyaweke maana this is a free society na tuna haki ya kuexpress mawazo yetu. If they dont mean anything;they can still be posted anyway...what do u think.

    Mdau.

    ReplyDelete
  5. First lady looks eminent and superb which reveals the aunthentic african figure....I like it so long as her table is not loaded with Genetically Modified Food to imperil her health!

    Kimori Seniour

    ReplyDelete
  6. Ash,

    Usione ajabu bi mkubwa kunenepa, unene ni dalili ya maisha mazuri afrika. Angalia waafrika wengi duniani ni wanene kweli lakini ki afra ni hatari sana.

    ReplyDelete
  7. Mmh!wasuuza vinywa tulieni hata hapa mnataka kutia mdomo?First Lady katulia hana kasoro yoyote umbo la mama wa kiafrika je mnataka atoke vifupa kama ma miss wenu? Hana magonjwa kila mara anafanyiwa chech up na afya yake hata Dr hana wasiwasi nayo.

    ReplyDelete
  8. Duuuh Rais wetu na mama yetu wa kwanza wametoka mchicha sana.
    Mnawakumbuka BWM na mama wa kiraracha walivyokuwaga ilikuwa vichekesho walikuwa wanaonekana kamamabeano.Big up JK we like you all.

    ReplyDelete
  9. Apunguze kuvaa madhahabu yaho ya mabangili, miwani, mapete, na mavidani!

    Huu ni wakati mbaya wa dhahabu yetu kunyakuliwa na wawekezaji wa nchi na mafisadi wazawa!

    Kuna wakati Bush Mzee alipokuwa Rais, mmoja wa mawaziri wake, Allen, aliyeshutumiwa kwa kuhongwa na Wajapani, waandishi wa habari walikuwa wamejitega hapo nyumbani kwake kutaka kumwuliza uliza.

    Siku moja asubuhi, mmoja wa waansidhi wa habari alimwuliza Waziri Allen, "What tine is it, sir?

    Waziri Allen alivuta mkono wa suti yake kuangalia saa...akakumbuka kuwa mojawapo ya tuhumu hizo ilikuwa kahomgwa saa ya gharama ya Seiko!

    Alipotanabahi, alikimbia bila kujibu swali hilo!

    Kuna siku watu wataanza kumwuliza au kupiga kelele, "Ni saa ngapi sasa, Mama Kikwete?"

    CHEKENI SAAAANA!

    ReplyDelete
  10. mjomba jk nimefurahi kusikia umekuja kwa poppe,sema sisi walala hoi hapa passpoti ya kurudi nyumbani tunaekewa mizengwe lakini wadosi wanazo tufanye nini mjomba?nataka kurudi gezaulole bwana.

    ReplyDelete
  11. Kwenye hii picha Mama Kikwete kamsogelea mno papa.Halafu na papa naye naona anamtazama mama Kikwete kwa Jicho la .............ngoja niwahi sala St.JOSEPH nisije chomwa motoni bure.

    ReplyDelete
  12. hivi huyu Mkwere(JMK)bado anajitambulisha tu!mpaka amalize dunia nadhani itakuwa ni mwaka 2010 na hapo inabidi aanze kuaga hadi mwaka 2015.
    Nchi maskini bwana kazi kwelikweli!hata viongozi wake wanakuwa na akili maskini.

    ReplyDelete
  13. woote mliotoa maoni hapo mngekuwa mnamjua papA ni nani na ana mpango gani na Dunia yetu MNGETOA MAONI TOFAUTI. Mjitahidi basi mjue hata JESUITS yatosha kubadili mawazo yenu!!!

    ReplyDelete
  14. bro michuzi kuna maoni nimetoa jana kuhusiana ha hoja hii ya JMK ila haujaitoa hewani..
    USINIBANIE KAKA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...