Ijumaa ijayo msanii AY atazindua kazi zake 3 kwa mpigo.
Atazindua documentary “UNDANI WANGU” ambapo ameamua kuweka wazi mambo yake mengi ya maisha binafsi & kimuziki pia ndani humu ataelezea uhusiano wake kati yake na ampendaye je ni kweli yule mashabiki wa AY wanaomuhisi siku hiyo ya ijumaa wasikose kufika hapo Club Maisha tarehe 16/11/2007 siku ya ijumaa.

Pia ataachia Clothing line ambapo AY ataingiza sokoni nguo za kiume pamoja na kina dada zenye jina la “Commercial Wear” na angependa mashabiki wake siku hiyo wazivae na kujumuika naye katika siku maalum kabisa kwake ya UNDANI WANGU.Nguo zinapatikana Zizzou Fashion-Sinza na Dream Wear ghorofa ya kwanza Millenium Tower

Hatimaye atazindua rasmi tovuti yake ya
www.ay.co.tz ikiwa ni maalum kwa wale mashabiki wake waliopo mbali na kutaka kuwasiliana naye kupitia mtandao wake. humo kutakuwa na vitu mbalimbali mfano habari zake, tarehe za show zake, picha,video na nk.

Hatokuwa peke yake. Wasanii kibao watampa tafu. Nao ni JUACALI kutoka Kenya & MICHAEL ROSS kutoka Uganda hali kadhalika BESTA &JUMA NATURE kutoka Bongo
Sponsor wa uzinduzi huo ni Straight muzik na show imeandaliwa na Lips Entertainment.


mp

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kama kuna watu nawakubali.. AY mmoja wao.. yaani jamaa sio siri anakomaa mbaya na maisha .. AISEE vijana wote wa bongo mngekuwa kama AY sijui Ingekuwaje.. naona mizinga ya Mia mia barabarani isingekuwepo.. Tunajua kabisa kama Kiwanja hicho tight.. lakini kuona watu wanakomaa nacho.. Inatia moyo sana..Juzi kipanya kafungua nGuo.. leo Ay kafata na documentary.. Jamani Mkiamka Mnatustua sana.. Ndio kabisaaa.. Nazidi kuwa na matumaini na vijana wetu huko.. Big Up.. Ambwene.. Much respect.

    Wenu Mkandamizaji Mwandamizi.

    ReplyDelete
  2. Nafurahi sana ninaposoma kuwa hiki kizazi kipya cha wasanii huko Tanzania kipo mbele katika suala ya ujasilimali kwa kwatumia brand za majina yao kama Mr KP, na sasa Ay.

    Fanya vitu vijana kwani tunahitaji kizazi cha kina Jay-Z(Jigga Man),Puff Daddy(P.Diddy---Diddy),Usher, Jermine Dupri(JD) na Nelly ambao wote wanatengeza mahela kwa kutumia majina yao bila ya kumsahau Eminem na 50 Cent(Mr Fitty Cent).

    Hey, Ay and Kp, thats what's up.

    "Get money"--Biggie Smalls , my man and Lil Kim.

    "Go get your money lil Duffle bag boy"---Lil Wayne and Playas circle.


    Atl-US.

    ReplyDelete
  3. Ndo tatizo la Wabongo hilo.
    Mtu akianzisha kitu tu basi watu wote nao hukohuko. As if hakuna vitu vingine vya kutoka navyo.
    Mtu akianzisha YADI ya kuuza Magari, basi mtaa mzima watavunja nyumba zao na kugeuza yadi za magari.
    Akianzisha SALUNI, vivyo hivyo mtaa mzima.
    Hivi kwani hakuna ubunifu mwingine?
    Come on!

    ReplyDelete
  4. Perez hapo juu acha unafiki unadhani ingekua kuiga ingekua haraka ivyo,kila m2 na mawazo yake acha vijana wafanye kazi jamani.Kuweni na moyo wa kukubali kazi za wenzenu.
    Gooooooooo Ambwene MUNGU akutangilie

    ReplyDelete
  5. Hivi huyu mwanadada bado anang'aa ng'aa macho hapo bongo. Nenda Parisi au NY City kabla CV yako haijachoka...Changamka umeshatangaza jina la nchi sasa ni kujipatia chako kidogo kidogo. Ukizubaa watu watakusahau...ninda na portfolio yako haraka.....oh hooooo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...