Amina Waziri, mjukuu wa gwiji wa Kiswahili, Shaaban Robert, Mtanzania anayejituma na kusukama utamaduni wetu London. Madarasa ya Kiswahili yatakuwa bure kwa mwezi mzima kama majaribio. Jana jumamosi, siku ya kwanza walishajiandikisha wanafunzi 20. (Picha na Freddy Macha)
Amina akiwa nami, Freddy Macha, baada ya kunieleza mipango yake hii ya kukikuuza Kiswahili kama babu yake maarufu, Shaaban Robert.(Picha na Fawz )
Amina Waziri akiwa na mwanae kitinda mamba, Fawz, nje ya nyumba yao mjini London. Masomo ya Kiswahili yatafundishwa si mbali na hapa.
(Picha na Freddy Macha)
MJUKUU WA SHAABAN ROBERT AFUNGUA MADARASA YA KISWAHILI LONDON
Na Freddy Macha
Kiswahili chetu kinazidi kukua duniani na miaka ijayo huenda kikawa moja ya rasilmali zetu kuu za kiuuchumi na kitamaduni, kimataifa. Kauli hii imeonekana rasmi kutokana na ari ya Mtanzania mkazi wa hapa London.
Amina Waziri Richards, kafungua rasmi madarasa ya Kiswahili kwa wenyeji wa hapa yatakayoanza juma hili kila siku asubuhi na saa za jioni. Madarasa hayo yatakuwa bure lakini baadaye itabidi wanafunzi ambao wengi ni Waafrika waliozaliwa nje ya bara, walipie.
Akizungumza nami Jumamosi usiku Amina alisema mradi huu umekuwa ukipikwa muda mrefu na unafadhiliwa na Kituo cha Waafrika cha kitongoji cha New Cross (African Community Partneship) kusini ya London anapoishi miaka mingi.
Dada Amina alisema wakati wa ufunguzi wa madarasa haya Jumamosi mchana tayari walijiandikisha wanafunzi ishirini kutoka hususan visiwa vya Karibi: Jamaika, St. Kitts, Cuba, Grenada, Cuba, Guyana, Trinidad na Tobago, vile vile wachache kutoka nchi nyingine za Kiafrika. Wengine wana mipango ya kuja kufanya kazi za kitaalamu Tanzania.
“Naipenda sana kazi hii maana inanipa amani na kuona kwamba ninaweza kutoa mchango wangu kwa wengi, hasa,Wakaribi ambao wana kiu cha kutaka kujua lugha ya asili ya mtu mweusi. Suala la utumwa limewatia pengo, wanaona wameibiwa silaha ya lugha, kwani lugha ni amana kubwa,” alisema.
Amina ambaye ni mjukuu wa mwandishi maarufu wa Kiswahili, Shaaban Robert keshaishi karribu kila sehemu Tanzania hasa akiwa zamani mfanyakazi-mhudumizi wa shirika la ndege la Air Tanzania. Keshasafiri na kuishi pia sehemu kadhaa duniani ikiwepo China na Sudan. Mwaka jana alichapisha kitabu chake cha kwanza kwa lugha ya Kiingereza kiitwacho, “Oneness.” Kinaelezea maisha magumu na katili ya mwanamke wa Kiafrika anavyojitahidi kupambana na na maisha.
Lengo lake anasema maishani ni kukuuza Kiswahili, kuinua nchi na bara la Afrika. Kapitia mengi. Amezaa watoto tisa, kati yao waliofariki wanne, walio hai watano na anao wajukuu wawili.
Ukitaka kuwasiliana naye mwandikie barua pepe:
waziri_amina@yahoo.co.uk.
Simu +44-7504112344.
Soma mahojiano marefu na Amina katika blogu ifuatayo:
http://kitoto.wordpress.com
Simu +44-7504112344.
Soma mahojiano marefu na Amina katika blogu ifuatayo:
http://kitoto.wordpress.com


Mi binafsi naona ni wazo zuri sana kwani kuna hata watoto wa watanzania hawajui kiswahili achilia mbali wataalamu kuja kufanya kazi nchini.Ila kuna baadhi ya watu aidha kwa ulimbukeni au ujinga HUWAKATAZA WATOTO WAO KUONGEA KISWAHILI MBELE ZA WATU,hii niliishuhudia mwaka jana nilipoenda london kwa matembezi mafupi.ILA WAZO la Wajamaica au wa CARIBIAN KUTAKA KUJIFUNZA LUGHA ya kiswahili NADHANI SIO ZURI kabisa KWANI NAHAKIKA WANATAKA KUANZA KUUZA UNGA(UDAGA) BONGO.Hawa sio wataalamu, kwani shule hawapendi zaidi ya unga na saloon.
ReplyDeleteAksanteni.
Big up sista endeleza lugha yetu ughaibuni achana na hawa wanao abudu lugha za mazeruzeru
ReplyDelete