Mtandao wa Wanataaluma na Wasomi Tanzania (Tanzania Professionals Network -TPN), unawaalika Wanataaluma, Wasomi, Wafanyabiashara, Taasisi na Makampunimbalimbali katika Hafla ya Kutunisha Mfuko wa Ujasiliamali na Uwezeshaji waKiuchumi.

Hafla hiyo itafanyika:
Siku:Jumapili Tarehe 18 Novemba 2007
Mahali:Viwanja vya Karimjee
Muda:Kuanzia saa 10.00 Jioni hadi Saa 4.00 Usiku.
Mgeni Rasmi:Mh. Samuel Sitta, Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano

Lengo la Hafla hii ni:
1.Kuchangia Mfuko Rasmi wa Ujasiliamali na Uwezeshaji waKiuchumi kwa Wanachama wake na Watanzania kwa Ujumla.
2.Kuelezea faida kubwa za kujiunga na Mtandao waWanataaluma
3.Kuandikisha wanachama wapya ambao watapenda kujiunga naMtandao
4.Kuwatambua na Kuwazawadia baadhi ya watu na taasisi ambaowametoa mchango mkubwa katika jamii.

Hafla hii itatangazwa moja kwa moja na Radio Mlimani FM 106.5 nawasikilizaji wanaweza kuchangia moja kwa moja kwa kupiga simu namba 0787 7777 88,

0754 833 985,
0713 334 078
kuanzia saa 3.00 Usiku.

Kutakuwa na kipindi maalumu cha mahojiano kuhusiana na TPN katikaTelevisheni ya TVT siku ya Jumapili kuanzia saa 1.00 hadi saa 2.00 Asubuhi

Kwa habari zaidi, tembelea tovuti ya TPN:

www.tpn.co.tz ama www.tpn-tz.blogspot.com

Ili Kujiunga na TPN, tuma barua pepe register@tpn.co.tz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...