Mdau,
Natumaini kheri ipo pamoja nawe na kwamba umeiona siku hii salama na ndio maana umepata japo upenyo kidogo katika ratiba yako ngumu ya siku ili kusoma kutoka kwangu.
Kwa mujibu wa kalenda niliyonayo hapa ukutani kwangu leo ni tarehe 18 Novemba, 2007. Kwa maana hiyo, kamaulihifadhi vizuri kumbukumbu zako, leo ni Tanzania Blog Day kwa mujibu wa mkutano wa kihistoria tulioufanya mwaka jana siku kama hii.
Tumefikisha mwaka mmoja jamani!
Pamoja na hayo nadhani kwa kiasi fulani tumeisahau siku hii,uongo?Mimi nadhani jibu ni ndio au kweli. Basi kuzingatia hilo mdau Jeff Msangi ameandika kidogo kuhusu siku hii muhimu kwetu wanablogu wa kitanzania. Ametuandikia ujumbe huu uungane naye katika kujadili mawili matatu kuhusiana na siku hii.
Nakutakia kila la kheri katika siku hii.
Ni kweli kabisa, juma lililopita nilijikumbusha kwenye shajara yangu nikaona hiyo tarehe, lakini nimesahau kabisa kaka. Hongera kwa wanablogu wote, hongera kwa jumuia ya wanablogu tanzania, hongera kwa blogu mpya zenye mambo mapya mapya.
ReplyDeletehappy b'day siku ya blogu tanzania.