pamoja na mambo mengi mengine, baba wa taifa atakumbukwa daima kwa kuwa mtu simpo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Jamani ebu angalieni kweli mzee wetu alikuwa simpo na aliipenda nchi yake kweli2!utadhani alistaafu akiwa Katibu Tarafa kumbe President!Hivi BWM analijua hili manake kupitia utawala wake ndo katuachia msululu wa kila aina ya Ufisadi!Leo kuwa kiongozi manake ni deal kubwa sana thats why pale Kizota walikuwa wakisuguana misuli kuingia kwenye chungu kitamu!Mwenyezi Mungu ailaze roho yake peponi Amen.

    ReplyDelete
  2. Ninanukuu - "Nchini Cuba watoto wa shule wana kiapo chao : Seremos como Che: Tutakuwa kama Che (Guevara). Haieleweki kwa nini watoto wa Tanzania wasifundishwe kuapa, “Tutakuwa kama Kambarage.” Mwisho wa Kunukuu. ......... (dRU)

    ReplyDelete
  3. " maskini na mwanae tajiri na mali yake "

    Kambarage alikuwa na watoto wake na waliopo sasa nao wana mali zao !

    Mzushi

    ReplyDelete
  4. Wabongo bwana!!
    kiongozi akipiga picha kavaa sandoz tayari eti alikua simpo!!wapi.
    mbona ni sifa ya watu wengi hiyo kuvaa sandoz na kutoka mkanda nje na hawaambiwi kuwa wako simpo?
    jamaa alijitahidi kupinga ukabila na sera mbaya tu za kiuchumi!
    isitoshe aliponikera zaidi ni pale alipoleta muungano wa Tanganyika na Zanzibar.hii ndio ile uwamuzi wa mtu mmoja unaeffect millions of people in the years to come!
    Yote kwa yote hongera ni zake kwa kupigania uhuru wa Tanganyika japo hata kama asingepigania by now Tanganyika ingekuwa huru tu.
    Amani kwake yeye Julius Kambarage Nyerere!

    ReplyDelete
  5. Dar kweli hapa! Babu nae, mbona kavaa Jacket kwenye joto,hata kama si jacket mbona mashati mawili, ya nini? mmmhhh mmmhhh mmhhh, kwikwikwi, youweeeeeee, aaaa aaaa we acha tu! Lakini kapendeza, poa!

    ReplyDelete
  6. Ehe bhamula namwichuka Omutangasya weswe ali ewae Bhutiama amasiga ga gela!!

    Nyakatakule Unyilisya echalo

    ReplyDelete
  7. Mwalimu was not an ord. human being,alikua Mkombozi,kama Kristo alikuja kwa ajili ya ukombozi, aliletwa na Mungu kwa sababu maalum ilipokwisha akamchukua.Sasa ni wakati wa mafisadi,manyang'au,walafi na wote wana-alama kama utawangalia vizuri katika mapaji ya nyuso zao.An evil star!!Mungu epusha balaa na nchi yetu.Senyandumi,USA

    ReplyDelete
  8. Hapo yupo kwake Mwitongo. Wakati wa jioni na majira ya mvua mvua huwa kuna kibaridi. Na uzee ukiingia, ni sharti wakati mwingine uvalie kutunza joto mwilini.

    Anyway, moja, Nyerere alilelewa katika ujamaa wa Kiafrika (maisha ya "indigenity and existentialism", kama ilivyotekelezwa na wa-Zanaki, kwa mfano). Mbili, kafundishwa u-Uristo wa Katoliki. Tatu, kasomea u-Magharibi wenye itikadi za aina mbili kubwa: ubepari na ubepari/ujamaa wa “liberalism” - sana sana wa ki-Fabianism. Nne, kawa "nationalist" wa kujenga taifa jipya la Tanganyika (hapo baadaye Tanzania).

    Katika hali halisi iliyojitokeza wakati huo, Nyerere alioanisha pamoja yafuatayo:

    Ujamaa wa Kiafrika. Ujamaa mseto wa kisasa wa Fabianism (Ulaya Magharibi). Ujamaa wa Kibbutzim (Israel) - Makazi Mapya (new Village Settlements) na mambo ya Biashara ya Cosata. Siasa ya Kujitegemea (Juche) ya Korea Kasikazini). Vijiji vya Ujamaa mithili ya Urusi/Uchina.

    Nyerere alikataaa kuitwa "m-Komunisti" kwa sababu moja kubwa, kama alivyokiri alipoulizwa siku moja na mwandishi wa habari wa gazeti la wiki la Newsweek, “Hakuna m-Komunisti anayemwamini Mungu. Mimi ni m-Kristo.”

    Baadaye,Nyerere alivutwa na mwamko wa (Liberation Theology) wa viongozi wa ki-Katoliki (mapadre) wa huko Amerika Kusini. Mapadre hao waliongozwa na maandishi ya Padre Paulo Freire wa Brazil (aliyeandika kitabu cha Pedagogy of the Oppressed) kutaka kuwakomboa walalahoi wa huko kutokana na unyonyaji kwenye mashamba makubwa (haciendas) na migodi na umasikini uliojikita ndani yake.

    Wengine tunamkumbuka Nyerere kwenye hotuba yake ya kutangaza Azimio la Arusha hapo Mnazi Mmoja. Katika hotuba hiyo, aliasa wananchi waachane na maisha ya kukogana:

    “Eti wengine wanalilia masuti na viatu vya Kitaliano. Viatu vya mchongoko na wengine viatu vya mchuchumio! Viatu vya mchuchumio na mchongoko! Unataka kumkoga nani? Mimi nina masuti mengi. Ninaweza kuyavaa na kubadilisha kila siku ya juma bila ya kuyamaliza! ”

    Wengi tulilelewa katika mazingira ya Nyerere. Yeye kapenda kuitwa "Mwalimu" kuliko kuitwa
    "Mheshimiwa". Alitamka "Mheshimiwa ni Mungu peke yake."

    Tuliolelewa katika mazingira hayo ya ujamaa nchini mwetu, sauti ya Nyerere bado tunaisikia kana kwamba anazungumza leo hii. Na wala si mwangwi.

    Cha ajabu ni kwamba hata wale walioketi miguuni pa Nyerere, hawakuhitimu katika maadili ambayo yanawavutia wengi (wakiwemo hata wale wa vyama pinzani vya Chama cha Nyerere)!

    Of course, alikuwa na madhaifu yake, kama binadamu (wewe na mimi)! Yapo mengi sana ya kuandika juu ya Julius Kambarage Nyerere: pro and con.

    ReplyDelete
  9. Kumbe "Mchonga" nae alikuwaga anavalia suruali tumboni kama ma PE DE DJE wa siku hizi!
    Kudadadek walah!

    ReplyDelete
  10. Hakuna cha usimpo wala nini, simpo gani ana panda benzi, simpo gani ana msafara mkubwaanapo safiri popote, simpo gani amefia Ulaya tena kwenye Posh Hospital, simpo gani ana pelekwa kuchekiwa kimatibabu Ulaya,Simpo gani watoto wake walisoma nje (Cuba na Urusi)?.

    Yeye na sokoine simpo gani?, kwanza Sokoine alifia kwenyE Marcedez, usimpo gani huo?.
    hawa hawakuwa simpo walikuwa hawajui vitu vizuri ,hawakuwa na taste ya mavasi na uleo, ila waliishi comfotable kwa kila walicho taka walipata, Usafiri mzuri, (nguo sio lazima sana kwao, maana walisoma vijijini,kwa sokoine ni masai), NyererE alijifanayA simple kuvaa, kuwa zuga watu, walipata matibabu muhimu, Nyumba nzuri, kila walipo safiri ni first Class,watoto walisoma shule nzuri, na uhakika wa pension ya kueleweka ili waishi maisha mazuri muda wote.

    Tulidumazwa sana waTanzania mbaka hatujui Lugha za kimataifa , matokeo yake watu tuna struggle na wengine kutojiamini.

    Hongera kwa kutuweka wamoja na kutokomeza Ukabila, ila Ukombozi, tunge kumboka tuu hata kama asingekuwepo.

    ReplyDelete
  11. KAMA HAJAFA! MAISHA...NO...PICHA BWANA INDANGANYA KWELI.

    ReplyDelete
  12. wengi wenu mmezaliwa mwaka ya 80 na late 70's,kwahiyo nyerere mwamjua kwenye magazeti tu.waulizeni baba zenu umuhimu wa nyerere badala ya kubwabwaja tu.he is a legend..............

    ReplyDelete
  13. Hakuna cha umuhimu wala nini. Alikuwa binadamu tu kama binadamu wengine wote.
    Mwenzenu alikuwa na TV nyumbani nyie hamna, anangalia CNN huko halafu anakuja kuwahutubia nyie mnasema Mzee anajua mambo mengi kweli huyu, kumbe kayatoa kwenye TV nyie hamjaona ndo mnashangaa shangaa.
    Usitubabaishe wala nini!

    ReplyDelete
  14. Yesu aliwaambia wale wayahudi waliotaka mtwanga mawe yule mwanamke kwa kosa la kuzini kwamba ambaye hajawahi fanya hilo tendo na awe wa kwanza kuinua jiwe (hii yanifanya nijiulize sikuzote kwani hiyo njemba iliyozini na demu ilienda wapi mpk na yenyewe isitake pigwa mawe) Anyway hapa wht am trying to say ni aibu kwenu nyinyi mnaomkashifu Baba wa Taifa aliyefanya leo ujiite mtanzania, uwe na uhuru ulionao hadi wakuropoka uwezavyo hapa, aliyemtimua malkia na virago vyake la sivyo tungekuwa tunatawaliwa hadi leo halafu wamtusi, shame on you kwakweli au ndio baya moja hufuta mazuri elfu moja he was after all a human being wacheni kashfa wkt mnajua umuhimu wake mshindwe na mlegee, kwakweli i miss huyu baba angekuwepo mambo mengi yasingetendeka yanavyotendeka sasa, mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, pls pls watanzania wenzangu huyu mzee ni wakumuenzi ukienda huko kwa wenzetu wanamjua yeye ni mtu wa kujivunia si vinginevyo hamuoni wasauzi na mandela wao wajameni tujifunze, inasikitisha kwakweli baadhi ya comment hapo juu kutoka kwa watanzania wenzetu loh

    ReplyDelete
  15. MHESHIMIWA ISSA..LUGHA YA PICHA INAELEWEKA..WAZEE WA ZAMANI SIO MCHEZO MWALIMU J.K NYERERE KALA POZI NA "..MKONO MFUKONI.."..WEWE..CHONDECHODE ISSA

    ReplyDelete
  16. Kama alivyosema anon mmoja hapo juu, "wengi wenu mmezaliwa mwaka ya 80 na late 70's", pengine, ingefaa sana mtuulize sisi tulioona TANU ikizaliwa; serikali ya madaraka; na uhuru unaingia na hadi sasa roho zetu bado zinadunda na akili bado timamu!

    Mwingine kasema ya CNN!!Kwani hiyo CNN ilianza kuwa hewani mwaka gani?

    Ukitaka kujua, kwa habari za kila siku za kimataifa, Nyerere alikuwa anasikiliza BBC radio!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...