jk akitoa maelekezo ya jinsi ya kuboresha maeneo yenye vivutio vikubwa vya asili katika hifadhi ya Ngorongoro hivi karibuni wakati alipokuwa katika likizo ya kikazi wilayani Ngorongoro,Mkoani Arusha.wanaomsikiliza ni Kaimu muhifadhi wa hifadhi ya Ngorongoro Bernard Murunya(wapili kushoto) na mjumbe wa bodi ya hifadhi hiyo Bwana Elvis Musiba.Rais Kikwete ambaye pia alivitembelea vivutio hivyo vinavyofikika kwa taabu kutokana na ukosefu wa barabara,alitoa maagizo hayo aliposimama kwa muda katika lango la kuingilia hifadhi ya Ngorongoro lililopo eneo la Lodoare. Habari kamili soma hapo chini...
Na Mwandishi Maalumu, Arusha
Rais Jakaya Kikwete ameitaka Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), mkoani Arusha, kujenga makumbusho yenye hadhi inayofaa na inayofanana na historia na jinsi bonde hilo lilivyojitengeneza, miaka milioni nne iliyopita.
Rais pia ameitaka Idara ya Mambo ya Kale pia kujenga makumbusho ya kuhifadhi nyayo za kwanza za binadamu katika eneo la Laetoli, ambalo ni sehemu ya NCAA. Rais ametaka ujenzi wa makumbusho hayo kuanza mara moja kwa kadri inavyowezekana.
Rais Kikwete alitoa maagizo hayo majuzi wakati alipotembelea maeneo hayo yaliyoko chini ya NCAA – Ngorongoro Conservation Area Authority, ikiwa sehemu ya likizo yake ya kikazi ya mwisho wa mwaka.
Rais alisema kuwa badala ya NCAA kuendelea kutangaza na kuingiza mapato kutokana na bidhaa moja tu – yaani Bonde pekee la Ngorogoro, ni vyema uongozi wa Mamlaka hiyo kuongeza bidhaa nyingine katika eneo hilo lenye historia ya kipekee duniani.
Alisema kuwa kujengwa kwa makumbusho – ya historia ya jinsi Bonde la Ngorongoro lilivyojitengeneza na yale ya kuhifadhi nyanyo za kwanza za binadamu – kutaongeza thamani ya eneo hilo na kuvuatia watalii kutembelea eneo hilo.
Kwa sasa historia ya Bonde la Ngorongoro inaonyeshwa katika kibanda kidogo kwenye lango kuu la Lodoare la kuingilia katika eneo hilo la NCAA, kutokea mjini Karatu, wakati nyayo za kwanza za binadamu zimehifadhiwa kwa kufunikwa na mawe katika eneo la Laetoli, magharibi mwa Bonde la Ngorongoro.
Nyayo hizo zimefunikwa tokea mwaka 1997, miaka 10 iliyopita, bila kusaidia kwa namna yoyote, utalii wa Tanzania.
“Tuna wajibu wa kuzitunza vizuri kumbukumbu hizi muhimu na historia hii isiyopatikana pengine popote duniani kwa manufaa ya binadamu wote na kwa manufaa ya vizazi vijavyo,” Rais Kikwete aliwaambia maofisa wa NCAA wakiongozwa na mjumbe wa bodi ya NCAA, Elvis Musiba.
Eneo la NCAA lina historia ya binadamu isiyopatikana katika eneo lolote duniani. Historia hiyo ni pamoja na kuwapo kwa eneo linalokubaliwa kuwa asili ya binadamu, inayokadiliwa kuwa na umri wa miaka milioni 1.75 katika sehemu ya Oldupai (Oldvai Gorge), na nyayo za kwanza za binadamu zinazokadiriwa kuwa na umri wa miaka zaidi ya milioni tatu na laki sita.
Eneo hilo pia lina vilima tisa vya volcano, ambavyo inakadiriwa kuwa vilijitengeneza kiasi cha miaka milioni nne iliyopita. Kinachojulikana zaidi miongoni mwa vilima hivyo ni Mlima Oldonyo Lengai (Mlima wa Mungu), ambao umekuwa ukilipukalipuka katika siku za karibuni zaidi, na kusababisha matetemeko ya mara kwa mara katika eneo hilo.
Eneo la NCAA pia lina mabonde ya Olmoti na Embakaai, lenye ziwa dogo, kivutio kikubwa cha watalii, ambacho, hata hivyo, hakijulikani kwa sababu ya ugumu wa kukifikia kutokana na ukosefu wa barabara.
Vivutio vingine katika eneo hilo ni Milima ya Gor na Mchanga Unaohamama (Shifting Sands), unaotokana na majivu ya volcano ya Mlima Oldonyo Lengai.
Mbali na vivutio hivyo, ni wanyamapori wa kila aina wanaopatikana katika Bonde lenyewe la Ngorongoro, linalopakana na hifadhi maarufu duniani, ya Serengeti. Pia eneo hilo la NCAA lina ziwa la maji chumvi ya Eyasi, na nje kidogo tu ya eneo hilo ni ziwa jingine, la Natron.

.

Mheshimiwa Rais ana kazi kweli kweli yaani kitu mpaka apite Rais atoe oda, wakati wataalamu wapo miaka nenda miaka rudi. Basi atachoka hao wataalamu wa mambo ya kale wamesomea nini kama wanashindwa hata mbinu za uhifadhi? Na hao wataalmu waliopo huko NCAA walikuwa hawaoni kuwa hiyo njia haipitiki? Mpaka Mh Rais aje awaambie watengeneze hiyo njia ipitike. Kazi anayo!
ReplyDeleteWE MICHUZI LIKIZO YA KIKAZI MAANA YAKE NINI?
ReplyDeleteMheshimiwa Rais big UP!! Tunasubiri tamko lingine, haki za wafugaji waishio katika bonde hilo ambao ni wahifadhi wa kwanza!! Pia uteuzi wa mhifadhi atakayeweza kujumuisha mambo yote matatu yaaani utalii, uhifadhi wa mazingira na maslahi ya wenyeji. Hili tunasubiri kwa hamu sana tuone utachemsha au utaendelea kuwa rais wa watu! Heri ya mwaka mpya!
ReplyDeleteNdugu yangu Anonymous said... hapo juu nakubaliana na wewe kabisa. Yaani inaelekea wanao jiita eti wataalamu macho yanafunguka akipita Kikwete. Sasa Suburi akienda Dodoma kutembelea Reli ya kati, napo itabidi awakumbushe kuwa ilikuwa ikianzia Dar mpaka Mwanza na Kigoma. Baada ya hapo ataenda mahospitalini kuwakumbusha wauguzi kuwa ni jukumu lao na lengo kutoa huduma kwa wagonjwa. Wasio hitaji kukumbushwa ni wale Watanzania wazalendo walio wengi wenye malengo na nia ya kufanikia ingawa huwenda wasifike kule watakako, mfano wapiga debe. Hutasikia hata siku moja Raisi akiwakumbusha wapiga debe au wale wamachinga aliowatoa barabarani, instead wanaokumbushwa ni wakina "FAT CATS" maana ni wazembe. Tunako kwenda ni Mola tu ajuae ......
ReplyDeleteViongozi wa kiafrika ndiyo matatizo yao kazi kutoa tu maagizo bila kuwa na mipango dhabiti. Mi hapo naona Kikwete anajikosha tu hana lolote. Na yeye yupo tu kama mkuu wa mkoa fulani aliyefuta likizo za wenzake kisa madarasa wajengwe. Kazi bila mipango madhubuti na kwa maagizo yasiyokuwa na mipangilio hatufiki nchi hii
ReplyDeleteNi aibu sana mh.Rais kupita kuwakumbusha watu majukumu yao hivi wanafikiria nini hasa hawa watu wanitwa wataalamu? Kwa kweli hili ni tatizo kubwa kwa nchi etu kwani watu wanafurahia madaraka tu na kujivuna mie nimesoma mpaka nimepata digree, shahada ya pili , mie profesa na mengine mengi lakini hakuna wanchofanya zaidi ya kupiga talalila humo makazini in abidi wabadilike wawe wabunifu waone sio wakumbushwe na mh rais. Tena washukuru hajawatimua kazi inatia kichefuchefu sana na ndio maana wanakuja wazungu hata ujuzi hawana wa kutosha lakini wanfanya mab o mengi kwa sab abu moja tu kutaka maendeleo na kuona mbali hawa watanzania wenzangu manen o maneno tu uzembe mkubwa tu inanikera sana mie na inanisikitisha kwa kweli. Rais ana majukumu mengi jamani hivi vingine tufanye sisi sio aje kutukumbusha mpaka kazi zetu. Mh hingera kwa kazi nzuri na ngumu unayoifanya tutafika tu na ninaamini taratibu hawa wazembe utawarudisha wanakostahili hizi sehemu muhimu uwape watu wenye uwezo mabadiliko yanatakiwa kila kona ya nchi yetu . Niko pamoja nawe
ReplyDeleteWatu wengi sana hwaelewi hali ya halisi ya Tanzania. Ndo maana annon wa kwanza na wengine wanaomuunga mkono wameingia kichwa kichwa.
ReplyDeleteSi kweli kwamba hakuna wataalamu na si kwei kwamba hakuna asiyeweza kufanya alichosema Kikwete. Mara nyingi sana kuna wataalamu amabo kwa kifupi wamekata tamaa maana wakiwa na mawazo ya maendeleo, pindi wakiomba pesa tu wanakataliwa! Wanaambiwa pesa hakuna kwa kazi hiyo. Na hiyo ndo sababu kubwa sana section hiyo ya Idara ya mwambo ya kale imelala sana.
Kuna wataalamu wengi sana wameacha kazi pale idarani kwa SABABU YA KUKATA TAMAA. Kila waombapo fedha kwa ajili ya miradi wanayobuni wanaambiwa hiyo siyo priority. Idara ya mambo ya kale ni moja ya idara za serikali zinazokusanya fedha nyingi sana chini kutokana na mapato kwenye sehemu kama alizokwenda Kikwete.
Sasa, kwa agizo hilo la Kikwete, basi utaona hata Katibu mkuu wa Wizara na Waziri wake ndo wanajifanya kupnga fugu la kwenda huko! Nyie hamshangai tu, kwanini mpaka Kikwete aseme wakati waziri na katibu mkuu pamoja na wakurugenzi wanaona hayo!
Ni tatizo la kitaifa na si la wataalmu. Chukue posts za serikali, ndo mtaweza jua nina maana gani. Vinginevyo, Rasi kuna vitu vingi sana vinamsubiri IKULU ikiwemo report ya BOT, kwenda kuwaagiza jamaa wa NCAA warekebishe makumbusho ni upoteza wa muda bila sababu!
Visingizio visingizio visingizio ndio jadi yetu tukishindwa kutekeleza jambo. Kusema ukweli utendaji wetu wa kazi ungekuwa robo to ya utendaji kazi wa wazungu angalau tungesogea. Kazi kutwa kwenye semina, midahalo, warsha, na mengineyo. Linapokuja suala la uwajibikaji ni ziro! Kama ingekuwa watendaji duniani wanapimwa uwezo wao kwa idadi ya semina na warsha, basi sie tungekuwa namba moja. Lazima tubadilike tufanyeni kazi kwa bidii. Mbali na hiyo sekta kuingiza pesa nyingi kwa kupitia utalii kwa nini iko nyuma? Kama hapo idarani kwao yamekwama siku hizi kuna mbinu nyingi tu za kusema mbona hatujasikia wakisema mpaka wamesubiri Raisi kasema.
ReplyDeleteHawa sio wa kwanza nakumbuka kuna siku aliwaambia watu wa mamlaka ya viwanja vya ndege, mnaacha kutafuta maeneo ya kujenga viwanja sasa ambako kuna maeneo yako wazi mnasubiri nini? Anzeni kutafuta maeneo?
Hayo aliyoyatamka huko Arusha ni baada ya kupewa taarifa kuwa kuna tatizo hili na lile, ni kawaida yetu wakati wa kutoa taarifa kuorodhesha matatizo, sidhani kama walimwambia kuwa tatizo hili tunataka kulitatua kwa njia hii lakini tunakwama na ukosefu wa fedha. Ndio maana na yeye akaanza kutoa suluhisho la matatizo aliyoambiwa na kutaka yafanyiwe kazi. Huko kwenya sekta ya uhifadhi na utalii kuna urasimu mkubwa lakini mkinyamaza nani atajua? Mnabaki visingizio huku sekta nzima inawafadisha watu wachache.
nd.anon wa dec.31 6:41 nilikua nataka nimkumbushe kaka michu kivutio cha mwisho kakisahau, hali ya wafugaji waishio katika bonde na pori hilo, kwa kweli kimekua kivutio kikubwa, huko mbugani ukipita wakisikia mgurumo wa gari wanajitokeza wanajua wazungu wamekuja hivyo kwa jinsi ya mavazi yao na jinsi wanavyojipakaa rangi usoni na kuvaa lubega la kaniki nyeusi na manyoya wazungu huwapiga picha kisha wanawarushia coins 100/-au 200/- wanafurahi na wazungu wanafurahia na wanapewa maelezo na wanaowatembeza mle wanapata hadithi za kuwasimulia wenzao wanakuja kwa wingi? sijui lini watampeleka huko kwa watu hai wa sasa kuliko kwenye nyayo za kale? na wengi wa wabarabaidi, sijui wamang'ati au wasandawi mimi sikuweza kuwatafautisha ni wakina nani watoto au vijana hao sijui hata kama wanasoma maana kipindi tunapita huko ilikua kipindi cha masomo shule hazijafungwa,sasa huko watampeleka lini akawajulie hali? au huko hapelekwi kuona aibu yao.Sijui wabunge hawajaliona hilo? au ndo hayo aloyasema anon wa jan, 4:29. Mungu ibariki Tanzania
ReplyDeleteJamani tuwe wakweli tuu na sio kuzunguka zunguka hapohapo
ReplyDeleteBongo kila kitu kinafanyika kumridhisha rais tuu watu wote wanaacha utaalam wao na kuwa wapambe tuu
Sasa utaona waziri anaamuru kutu ambacho sio profesional na hakina maslahi ya nchi kabisa ili mradi ana easy access na rais kila mtu anamkubalia ijapokuwa anaweza kupata hicho cheo kwa ukuwadi au kwa fitina tuu
Sasa nchi imesomesha wataalam wengi sana lakini haiwatumii kabisa kila kitu siasa tuu