
MWAI KIBAKI AMETANGAZWA MSHINDI WA UCHAGUZI MKUU KENYA NA TAYARI AMEKWISHAAPISHA KUONGOZA NCHI HIYO KWA MIAKA MITANO UJAO. INASEMEKANA MGOMBEA RAILA ODINGA ATAPINGA MATOKEO KORTINI...
KATIKA UCHAGUZI HUO RAIS KIBAKI KAPATA KURA 4,583,721 NA KUMPITA MPIZANI WAKE WA KARIBU RAILA ODINGA KWA KURA 230,000 NA USHEE, AMBAPO MGOMBEA MWINGINE KALONZO MUSYOKA KAAMBULIA 879,903.
kwa habari zaidi bofya hapa


Du! siamini. Ni kweli afrika demokrasia changa. Kibaki kasahau kuwa aliletwa madarakani na kura za watu leo anadhukumu na ingawa hao hao watu hawamtaki lakini bado anang'ang'ania.Ni vigumu kupata demokrasia ya kweli Afrika. haki hakuna Afrika.. viongozi wote wezi! poleni ndugu zangu wakenya kw akudhulumiwa!
ReplyDeleteHabari zilizoandikwa na TOM MALITI wa Associated Press, zinaelezea, kwa kifupi:
ReplyDeleteNAIROBI, Kenya - President Mwai Kibaki was declared the winner Sunday of the closest presidential election in Kenya's history, a contest marked by allegations of rigging and two days of deadly violence.
Elections chief Samuel Kivuitu read the results on live television after other media were expelled from the main vote headquarters. Kibaki beat Raila Odinga by 231,728 votes.
"This means Honorable Mwai Kibaki is the winner," Kivuitu said.
Hii ni dirty politics in the working.
ReplyDeleteLogically,kama mawaziri wako karibia wote wameanguka,wewe pekee ndiyo wananchi wamekuona unafaa ? Na hizo kura ulizopata in few hours,hata umpite yuke aliyekuwa anakuongoza zimetoka wapi ?
Nadhani wananchi wako macho na haya yote,hawatakubali mtu akiingia ikulu atumie nyezo zao kujitangazia ushindi.
Na sisi hapa nyumbani inabidi tujiulize,wapinzani wakilalamika huwa wanafanya hizo sababu huwa wamelewa pombe au huwa kuna
walakini ?
Kura ndio zinakuletea maendelea...hayo ni matokeo ya mwanzo au ni raia wa nchi hawakwenda kupiga kura...Kwa mahesabu ya haraka ni kura kama 6,000,000,000....ina maana Kenya ina raia wachache hivyo?
ReplyDeleteJamani tujifunze kutoka hapa...kura yako ndio inakuokoa kutoka kwa hawa wasaniii....usipopiga kura wala usihangaike kupinga matokeo
Dawa yake warudie tu kuhesabu tena kura
ReplyDeleteKenya is not a political stable country, it was fair for Bush and Kikwete to discuss them, just imagine what is it going happen?
ReplyDeleteHivi Raila Na Kalonzo si walikuwa kundi moja la ODM. Sasa ilikuwaje tena wote wawili wakagombea uraisi? Hizo kura laki 8 si zingekuwa za Raila hizo? Wanasiasa bwana hesabu zao sijui zikoje? Au mie ndio sijui hesabu? Inakuwaje mtu ana shinda kwa kura laki 2 wakati mtu mko naye kundi moja amefutika kura laki 8 na ushee!
ReplyDeleteHiki ndicho kichekesho kikubwa cha demokrasia ya vyama vingi Afrika.
ReplyDeleteKWA NINI KIBAKI AAPISHWE HARAKA HARAKA HIVYO HATA BILA MAJIRANI ZAKE KUWEPO? HUU NI UOGA WA MAKOSA YALIYOFANYIKA. TUWE TAYARI KUSIKIA FUJO HUKO NA HAKUNA BUNGE AMBALO KIBAKI ATAPITISHA KITU WAKATI YEYE ANA WABUNGE 24 WAKATI WALE WA ODM NI 72 NA HANA MPANGO WA SERIKALI YA MSETO
Tatizo ni hii tabia ya katiba za nchi zetu kuruhusu Rais kuteua wajumbe wa tume ya uchaguzi. Ndo maana tume ya uchaguzi inahakikisha inampa ushindi aliyewateua!
ReplyDelete"In accordance with Section 41 (1) of the Constitution, the Electoral Commission of Kenya shall consist of a chairperson and not less than four and not more than twenty one members appointed by the President."
Hivi ilikua ni fainali ya kombe uwanjani? Mana duh,hata washkaji zake wakulu M7 na JK kawatosa. Kweli mchawi wa Africa ni mwafrika mwenyewe!
ReplyDeleteMMH, JAMANI HUYU JAMAA NA MKE WAKE WANA SURA NZITO KWELI...Yaani hawa jamaa wakenya na majidai yao yote wanayoyaleta haswa ughaibuni huku, kumbe hii ndo figure inayowarepresent duniani, mmh balaa...
ReplyDeleteduh!kibaki kabaki,hayo macho yake tu ni ushahidi tosha kuwa huyu ni mwanga
ReplyDeleteWatu wengine bwana.Watu wanazungumzia uchaguzi mtu ana comment kuhusu sura.Uvivu wa kufikiri at the best.
ReplyDeleteKwani leo ndio mara ya kwanza kuwaona.Wacha kufuata mkumbo sio lazima u post a comment.
ReplyDeletemambo gani haya ya ma nchi ya Africa??ndo maana sisi wabeba mabox tumeng'ang'ania huku kwenye nchi zilizostaarabika zenye utawala wa sheria na maisha bora.
ReplyDeleteWatu hawakutaki li rais linalazamisha.mnaapishana usiku mambo ya ajabu haya ndo sometimes wazungu wanatuona mapunguani.
Yule aliyesema Mwai kibaki hashindi yuko wapi?
ReplyDeletekura ziibiwe zisiibiwe, hiyo ndo ishatoka. Ziliibiwa kura na Joji kichaka akashinda Marekani itakuwa mwana wa kibaki
Na huyo mama hizo ngumi zake mkononi, mara kawalamba makofi waandishi wa habari mara kafanya vituko vile, vimesababisha hata mumewe anyimwe kura. Lucy mbabe kweli kweli, inawezekana alikwenda kumkwida shati Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi!! Wee unacheza na Lucy!!
ReplyDeleteTusaidiane kidogo hapo juu washikaji:
ReplyDeleteKwanza hiyo namba 6,000,000,000 ni kioja - hii ni bilioni sita. Kenya ina watu zaidi ya milioni 30 na waliojiandikisha ni milioni 14 na waliopiga kura ni kwenye milioni 8 ingawa baada ya kura kujumlishwa wamezidi hapo. Kwa msaada tu mshikaji milioni ina masifuri sita tu. Hii tofauti ya wapiga kura na jumla ya matokeo hapana shaka ni kutokana na uhuni wa wizi wa kura. Mfano watazamaji wa Jumuiya ya Ulaya wanasema kwenye Jimbo la Molo tu, Kibaki alipata elfu 50 walizoshuhudia wenyewe zikihesabiwa, lakini Tume imetangaza elfu 75. Kibaki ameshinda Jimbo la Kati na la Mashariki, mwenzake kashinda yote yaliyobaki. Huu ni uhuni wa nyang'au.
Pili, si kweli kwamba wamekimbilia kumwapisha Rais Kibaki ili kukwepa kitu. Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya Rais huapishwa haraka, mara nyinyi siku inayofuata. Na kwa mujibu wa Katiba, kufikia Jumamosi usiku saa sita ndiyo ulikuwa mwisho wa Kibaki kushika madaraka, hivyo aliongozewa kwa mujibu wa Katiba hiyo hiyo ili zengwe liishie. Wanajeshi wa gwaride walijiandaa pia kwa sherehe za kumwapisha Odinga kama angetangazwa mshindi. Sahihisha hapo mshikaji.
Tatu, Kenya haifuati mfumo wa serikali ya Kibunge kama ilivyo India au Uingereza, n.k. Hii ina maana Rais anaweza kuongoza nchi bila kuwa na wabunge wengi bungeni. Pia kwa kuwa mfumo wa serikali ya Kenya kikatiba si kama ule wa Marekani wenye kitchen cabinet na checks and balances zinazoegemea bungeni, Rais hatajali chochote iwapo Wabunge watampinga, atasonga mbele tu. Ni mfumo mbaya.
Naishia hapa, nitarejea tena kuelimisha mwingine atakayeboronga, inafaa kusaidiana.
Wasalamu.
A sad day for Africa. Jamani viongozi wetu, watu wakisema basi, basi jamani mnatuletea machafuko kwasababu ya ulafi wa madaraka. Hii inanikumbusha nchi moja ya Ulaya mashariki sijui Ukraine vile, kiongozi aliiba matokeo watu wakamvua madaraka baada ya kama wiki mbili hivi.. Pamoja ya kuwa mimi ni mpenda amani lakini nashindwa kuwaambia ndugu zangu Wakenya wakubali matokeo maana haki yako mtu husubiri kupewa, unachukua.
ReplyDeleteAkili, US
Sikilizeni,
ReplyDeletehiyo ya kura za Musyoka Kalonzo ni fundisho kwa wanasiasa wetu wa Bongo kwa ubinafsi wao, kwanza inawezekana hata Kalonzo akawa Mamluki a.k.a Pandikizi.
Mi nachouliza ni hao wabunge wake 24. Kwa utaratibu wa kikwetu mtu akipiga kura kwa Mgombea flan wa Uraisi bas hata mbunge atampa wa chama kile kile.
Kwa hiyo kura za hao wabunge 24 ndio zimempa Urais??
Tujiandae kupokea wakimbizi kutoka jamaa zetu wa Jirani
Ningeshangaa sana kama Raila angeshinda. Demokrasia ya kiafrika hairuhusu aliyeshinda kutangazwa mshindi. Mara nyingi kinachotokea ni kinyume na kura zilivyosema. We have years to go before we enter into a democracy class in Africa.
ReplyDeleteAs riots shook parts of Nairobi and other major cities, Kibaki told Kenyans to "embrace one another as brothers and sisters" and declared Monday a national holiday.
ReplyDeleteSoon after, he suspended live television coverage. Stations that had been airing election news almost nonstop suddenly began showing reruns of "ER" and music videos.
The streets were mostly empty. Many people had stocked up on milk, water and food earlier in the day, expecting to remain holed up at home for at least two days of rioting.
At sundown, police helicopters hovered over fires burning across the poorest neighborhoods of Nairobi, where Joshua Mukabwa, a Luo, stood in the smoky haze.
"We are telling all Kikuyus -- we want them all to go back to Central province, and we should have two countries in Kenya," he said.
Among other boozy young Kikuyu and Luo men, tensions seemed to turn to bloodlust.
Walking along an empty street near Kibera, Andrew Ndegwa, who is Kikuyu, said he'd barely escaped a machete-wielding crowd where he lives, and where his wife and baby son remained Sunday night.
"I've just escaped from that place," he said. "They are just going house to house and if they find any Kikuyu, they just start cutting. I'm very afraid."
Special correspondent Charles Wachira contributed to this report.
quote 'The people who cast the votes don't decide an election, the people who count the votes do.' - STALIN 1963
ReplyDeleteHamna utaratibu kama huo hapa kwetu.Unaweza kumchagua Kikwete na kwenye ubunge ukampa mpinzani.Ni chaguo lako tu hakuna anayekulazimisha.Central Kenya kulikuwa na vyama vingi vilivyogawana kura za wabunge kama Safina,Kanu,kadu.Sisi kwa sisi lakini kwenye urais wakampa Kibaki.
ReplyDeleteHiyo picha ya Kibaki na mke wake ni mbaya kweli kweli. Au ni weusi tii hivyo?
ReplyDeletekama kibaki angekuwa msukuma angekuwa keshachomwa moto kwa kuhisiwa kuwa ni mchawi.Ona hiyo sura na hayo macho yake yalivyo..
ReplyDeleteDah Kibaki kaapishwa kama kwa staili ya "ndoa ya mkeka".Naona hata sheikh(hakimu mkuu) alisombwa msobemsobe hadi Ikulu kwenda kumwapisha huyu mchizi.Wala sishangai kuona Wakenya wanachinjana juu ya hili.
ReplyDeleteMkewe Kibaki akivuliwa hilo wigi anakuwa mwanaume tosha. KEnyans are Ugly jamani, wanatuangusha wa east africa
ReplyDeleteJamani hapo bila kumwomba rais wetu wa dunia Bush atume majeshi pale,hawa jamaa itageuka kuwa Hutu and Tutsi nyingine maana nimecheki news za africa jana thru a local channel hapajamaa wanauwana kama vile nini sijui kisa tu kibaki kashinda na wao wanamtaka Odinga...hiyo ni jimboni alikozaliwa Odinga huko..ukionekana ni shabiki wa Kibaki basi unachomewa nyumba moto unapigwa...!Demokrasia iko wapi jamani? hata kweli mimi nasema hizi kura za Kibaki sio halali maana a day after elections i heard Raila had possession of most of the Polls...!!kwamba karibia kila kituoa likuwa anaongoza ...siku moja sijui mbili after tunasikia rais ni Mwai Kibaki is it really fair? If i was a lawyer i bet i would stand for Raila when he appeals at the court..!! We Need Democracy in Africa.
ReplyDeleteKichefu chefu tuu..!Sasa kuna faida gani kujiita mshindi wakati watu wanauana kupinga ushidni huo?Miaka mliyokaa madarakani si mshaiba vya kutosha?Sikilizeni sauti za walio wengi.Watu wamechoka na wanataka mabadiliko katika nchi yao!!
ReplyDelete