Kaka Michuzi,
Tumeshapoa na msiba na maiti imepatikana. Yaani kwa kushirikiana kwetu ndio kumefanya maiti ipatikane. Tungechelewa kidogo tu! basi kwa sheria za huku angechomwa moto. Kwahivyo, shukran!
Tumeweka kwenye mtandao wetu matangazo yafuatayo kwa waliosaidia kumtafuta marehemu kwa kupiga simu. Na wengi wao walikuwa wanataka kujua nini kimetokea na nini maendeleo yake mpaka hivi sasa.
"
KUHUSU NDUGU YETU MAREHEMU RASHID OMAR HAMADI
Kwanza kabisa tungependa kutoa shukran za dhati kwa wote waliofanya jitihada za kusaidia kumtambua ndugu yetu marehemu Rashid Omar Hamadi, na kupata watu wahusika kutupatia maiti yake kwa kusafirishwa Zanzibar.
Baada ya kutuma (text message) katika jumuia, tumepokea simu nyingi tu na (text message) za watu waliotaka kujua nini kimetokea na mpaka sasa tumefikia wapi? Kwahivyo tunachukua nafasi hii kukujulisheni wapi tumefikia mpaka sasa.
Ndugu yetu marehemu Rashid Omar Hamadi ambaye ni mtu wa maeneo ya Nungwi, Zanzibar, amefariki dunia tarehe 12/12/2007, mjini London.
Mpaka tarehe 20/12/2007, vyombo husika vya UK hawakupata kumjua maiti ni nani na watu wake wa karibu ni nani ili wapate kuitoa maiti kwasababu ya maziko.
Kwa jitihada za Ustadh Khamis wa East African Education Foundation na kushirikiana na Zenjydar Community Association na kaka Issa Michuzi, tumewezesha kupata majibu ya haraka kutoka katika jumuiya yetu ya Waswahili kwa kupitia vyombo vya habari.
Ni 'network' iliyotumika ndiyo imewezesha kumpata ndugu wa marehemu, kwahivyo, shukran.
Maiti yake imepatikana tarehe 24/12/2007 na imeswaliwa katika msikiti wa Chapeltown, East London, baada ya sala ya Alasir. Baada ya kuswaliwa, maiti imesafirishwa kuelekea Tanzania kwa wazazi wake kwa maziko kamili ya kiislam.
Mungu amlaze mahala pema peponi.
Amen.
Saleh Jaber
Zenjydar Community Association
Alhamdulillahi,M'Mungu amlaze marehemu mahala pema peponi AMIN.
ReplyDeleteNa asanteni ZENJDAR for your good work.Na pole kwa wafiwa popote walipo.
Tunawapa pole na asanteni kwa yote mliofanya. Japo simfahamu lakini inatia moyo sana kuona watu wanasaidia kwa nguvu na mali..
ReplyDeleteThanks to you all.
May the almighty God rest his soul in peace