Ile Timu kabambe ya Watanzania waishio Atlantainapenda kuwatakia heri na fanaka katika kutimizamwaka 2007 na kuukaribisha mwaka mpya 2008. Hakikamwaka 2007 utakumbukwa kwa kila namna jinsi ulivyokuwawa mafanikio katika soka la Tanzania kwa ujumla ndanina nje.
Pia tunapenda kutanguliza shukrani kwa timuzote za Watanzania zilizojitolea kusafiri kujakushiriki nasi katika mechi mbali mbali jijiniAtlanta. Shukrani za pekee ziwafikie Houston naWashington DC kwa urafiki mkubwa mliouonyesha. Piabila kuwashau Wichita Kansas ingawa mipango haikwendafresh kwa upande wenu katika tamasha la mwaka 2007.But we are looking forward to have you guys in 2008tournament.Bila kuwasahau wazee wa Seattle karibunisana ATL 2008.
Mwaka 2008 utakuwa na program zifuatazo:
(a)Kubadilishwa rasmi kwa jina la timu na kuitwa TANZANITE FC. Ili kuweza kutoa mchango katika kuitangaza nchi yetu nzuri ya Tanzania na madini ya Tanzanite yanayopatikana pekee nchini mwetu.
(b)Kuisajili rasmi timu ili iweze kushiriki katika Semi-Pro league hapa Atlanta ADASL. Mwaka 2008 timu itashiriki rasmi katika ligi ya ADASL katika DIV III. Habari zaidi pitia website ya timu.
(c)January 2008 timu itashiriki katika mashindano ya ndani maarufu kama Indoor Soccer huko Lawarenceville GA.Mashindano yataanza Jan. 12th. Timu itatumia michuano hiyo kwa kujiandaa kwa ligi ya ADASL na Tamasha maalum la Watanzanialitakaloandaliwa hapa hapa ATL 2008. (Timu zitakazopenda kushiriki zinaweza kupata informationskatika website ya timu.
(D)Website ya timu imeshafunguliwa na bado inaendeleana matengenezo ya hapa na pale. Please pitiawww.tanzanitefc.com
(e) Ziara mbali mbali zimepangwa ikiwemo ya NchiniTanzania (Nyumbani) ambapo timu inatazamiwa kujipimanguvu na vilabu mbali mbali vinavyoshiriki katika ligikuu Tanzania zikiwemo vigogo kama Dar Young Africans, Simba Sc na Miembeni FC. Kwa tarehe zaidi please pitia mtandao wa timu.
Tanzanite Fc pia ipo mbioni kunyakua wachezaji kadhaa Watanzania waishio miji mingine ili kuongeza nguvu katika kikosi chake. Habarizi kishafahamika mtafahamishwa majina yao, mazungumzoyapo mbioni.
Pia timu inatoa nafasi ya udhamini kwamtu binafsi au Kampuni itakayopenda kudhamini timu nasafari hiyo. Kwa mawasiliano zaidi pitia Website ya timu.
TUNAWATAKIA HERI NA FANAKA KATIKA KUSHEHEREKEA MWAKAMPYA 2008.


Hongereni sana washikaji. Haya ndiyo maendeleo, fanyeni juhudi timu itambulike, ifanye mambo ya maana na hatimaye iwe professional team yenye wadhamini na kugeuka kuwa ajira kwa vijana wenye vipaji vyao. Hii itasaidia mambo mengi kwa nchi yetu na watu wake. Hongereni sana, msiwasikilize Watanzania watakaowakatisha tamaa maana huwa hawakosekani. Safi sana Atlanta na tafuteni Watanzania wote Marekani wahamie huko kutandaza soka badala ya vitimu vidogo vidogo kuundwa kila kona. Mwanzo mzuri.
ReplyDeleteBwawa la maini hoyaaaaaa,mdebweeedo.
ReplyDeletewadada ughaibuni mbona hatuoni timu zenu za netiboli,voliboli au chochote.Msituambie hamna activity yoyote,tobaa michibaga!!!!!!!
ReplyDeleteHebu ona anony 6:29 AM utaona tu watu wenye chuki na wivu kaona hamna cha kukosoa kwa hawa wacheza mpira kaona aseme wadada ...jamani waboongo viroho vyenu hivyo mtakufa na BP ...vijiba vya moyo saaaana tu vitawamaliza....nung'gu nung'u zenu hizo ndio maana baraka zinakupitia pembeni...asubuhi asubuhi umeamkia majungu......unaaga mwaka na majungu .....si ajabu hata kesho utakua wa kwanza kuweka majungu yako humu...ndio maana life yako iko hivyo usishangae kwanini jibu unalo mwenyewe...nakuonea huruma kweli
ReplyDeleteThis is too good to true.
ReplyDeleteKama mwana Atlanta nimekuwa nikifuatilia kwa makini juhudi zenu. Mungu awabariki. Ila maoni yangu ningependa mtujulishe kama baadhi ya Wachezaji wetu ambao tayari wanachezea timu mbali mabli hapa ATL watarudishwa kundini au vipi? Hapa naongelea Wachezaji kama Kombo DivI, Amani D-1, Hamza Liganga "Liga", Togo, Haji nk. Mana nimefuatilia hiyo website ya ADASL nikaona statistics sio mbaya Liga ana magoli 5 kwa mechi saba alizocheza. Si haba!! Tusiwaachie Wazungu watuibie vipaji vyetu. Warudishwe kundini. Ni hilo tu!! Happy New Year!!
ReplyDeletemsitudanganye kuwa mtakwenda bongo kimichezo.Nyinyi mtakwenda bongo kupunguza stress za maisha ya hapa,kila mtu anajuwa hilo.Pia nashangaa mnavyojitangaza kuwa chama lenu kali,muda wenyewe wa kupata tizi la nguvu ni dakika 30(lunch brake)mtawezaje kuwafunga Simba au Yanga wanaopata tizi kwa saa 1+?Msijidanganye hata kucheza na kombaini za mchangani watawaaibisha.
ReplyDelete