JK akipokea zawadi toka kwa kiongozi wa Cuba Fidel Castro aliyoletewa jioni hii ikulu alipokutana na makamu wa rais wa nchi hiyo Estaban Lazo Hernandez . katikati ni mkalimani wa makamu huyo wa rais wa cuba.
TANZANIA NA CUBA KUSHIRIKIANA KUPIGA VITA MARADHI
Tanzania na Cuba zimekubaliana kushirikiana kwa karibu katika vita dhidi ya magonjwa ya malaria, ukimwi na kuwapatia uwezo wakuona wananchi wenye matatizo ya macho kupitia mpango ujulikanao kama miracle cure, ambao umewapatia uwezo wa kuona mamia ya wananchi wa cuba uwezo wa kuona kwa muda mfupi.
Makubaliano hayo yamefikiwa leo kati ya rais J akaya kikwete na makamu wa rais wa cuba, Bw Estaban Lazo Hernandez, wakati walipokutana ikulu, Dar es salaam.
Ushirikiano katika maeneo hayo matatu, unatokana na ukweli kwamba Cuba imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na magonjwa hayo kwa kufanya utafiti wa tiba, kinga na watalaamu.
Rais alimweleza makamu huyo wa rais wa cuba kwamba Tanzania ingependa kupata utaalamu na wataalamu katika maeneo hayo matatu kwa kuwa nchi hiyo imepiga hatua kubwa sana katika maeneo ya utafiti na utabibu.
Makamu huyo wa rais alimweleza rais kikwete kwamba hivi sasa Cuba ina uwezo wa kutengeneza dawa za kuwaongezea maisha wagonjwa wanaougua ugonjwa wa ukimwi, ARV pamoja na mikakati mbalimbali ya kupambana na ugonjwa wa malaria.
Amesema mikakati hiyo imeonesha mafanikio makubwa nchini humo na kwamba kwa upande kwa kutibu matatizo ya upofu, ameeleza kuwa nchi yake imegundua matibabu mapya yanayompatia mtu uwezo wa kuona katika kupindi cha dakika kumi na tano baada ya kufanyiwa upasuaji.
Akasema ili hayo yote yaweze kutekelezeka, serikali yake inamwalika waziri wa afya na ustawi wa jamii wa Tanzania kwenda nchini Cuba ambako atakutana na wataalamu wa afya wa nchi hiyo na kupanga utekelezaji wa masuala hayo.
Aidha akasema njia nyingine ya kuharakisha utekelezaji wa masuala hiyo ni kupitia kamisheni ya pamoja katiya nchi hizo mbili itakayokutana mwakani nchini cuba.
Makamu huyo wa rais pia amemweleza rais kwamba nchi yake hivi sasa imeanzisha utaratibu wa kutoa mafumzo kwa madaktari katika nchi husika badala ya ule wa mwanzo ambao nchi hiyo ilikuwa ikiwapeleka madaktari wake kufanya kazi nje ya Cuba.
Katika mazungumzo hayo, makamu huyo wa rais wa Cuba aliwasilisha kwa rais Jakaya Kikwete, salaam maalumu kutoka kwa rais Fidel Castol ambaye katika salamu hizo amemwalika rais kikwete afanye ziara rasmi nchini humo.
Akielezea hali ya afya ya rais huyo wa Cuba, Mh. Hernandez amesema kiongozi huyo anaendeleza vizuri na anatekeleza majukumu yake bila wasiwasi.
Akipokeza mwaliko huo rais Kikwete amesema ataangalia uwezekano wa kufanya ziara rasmi mwakani na kwamba anamtakia afya njema rais huyo wa Cuba ambaye alimwelezea kama kiongozi shujaa na anayetumainiwa na mataifa yote yenye kupenda haki na maedeleo.
Rais pia alitumia fursa hiyo kuishukuru Cuba kwa ushirikiano wa karibu na endelevu kati yake na Tanzania pamoja na misaada mbalimbali ambayo taifa hilo imekuwa ikiipatia Tanzania katika maeneo ya afya, elimu na taaluma mbalimbali. Makamu huyo wa rais ameondoka nchini jioni hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. "La Patria O Muerte" (The Mother country Or Death), "Hasta la Victoria Siempre" (Until the Victory Always) These and many other Cuban slogans keep them strong as they are now!!! If we could only copy the first slogan.... (dRU)

    ReplyDelete
  2. Bro Michu, katika maongezi ya hawa wawili (watatu samahani) haukunasa habari yoyote kwamba ki-cuba kipendekezwe kufundishwa shule za msingi za TZ?. I think braza you can recall maongezi ya "mzee wa ndege ya kupaa" pale alipotembelewa na ujumbe mzito wa China. Ebu tu-update kidogo kama ulisikia lolote...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...