Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hii ni kweli kabisa, na sina shaka huenda hata Kikwete anafahamu hili na ndio maana alikwenda kutoa pole pale hospitalini. Viongozi wenyewendio wanawabana watu wanataka maovu yao yasitajwe ila ushujaa usiokuwa na akili ndio uandikwe...tutafika kweli?

    ReplyDelete
  2. Ivi kuna fununu gani ya kwanini huyu jamaa alimwagiwa Tindikali? Ivi haiwezekani kuwa alikuwa anashugiwa ugoni? Naona sio tulioko huku nje hatujawahi kusikia penyenyepenyenye yoyote. au ni mie tu ndio niko gizani? Hebu tuelezeni kuna fununu gani kuwa kushambuliwa kwa huyu jamaa kunahusiana na uhuru wa habari?

    ReplyDelete
  3. Mie pia nina wasiwasi kuwa wanatumia hilo suala la yeye kuwa mwandishi wa habari/Mhariri wa gazeti kuhitimisha kuwa kamwagiwa tindikali kwa sababu ya kuandika habari za mafisadi.
    Nina maswali kwa waandishi wenziwe wanisaidie kunijibu. Kuna haja pia ya kumuangalia Saidi kama mtu wa kawaida na si mwandishi na maisha ya kawaida anayoishi na watu ili kubalance na kutuwezesha kufanya analyasis ya yaliyomkuta.

    1. Je Said Kubenea ni mwandishi wa kwanza kuandika habari za ufisadi? Na je gazeti lake ni la kwanza kuandika habari za ufisadi?

    2. Kama si wa kwanza mbona waandishi wengine hawajakuwa attacked au hao na magazeti yao habari zao ni za uwongo za huyu ni za kweli?
    3. Kama issue ni kumnyamazisha kwanini wamwagie tindikali na wasifanye kubwa zaidi ya hilo ili anyamaze maana kama kuna issue yoyote waliyokuwa wanaizuia isitoke itatoka tu kwani itakuwa iko katika computer za ofisi hiyo?

    4. Nitaamini tu kuwa hii issue ni ya kuzima habari iwapo kungekuwa na uharibifu wa vifaa vya ofisi pia ili kufuta habari isiandikwe?

    5. Kwa kawaida mfagizi wa ofisi hawezi kuiba katika ofisi anayofagia kwa sababu atakuwa suspect no. 1. The same apply kwa wale waliokuwa wanaandikwa na gazeti la Mwanahalisi, labda kama akili zao hazifanyi kazi sawa sawa.

    6. The way hiyo ofisi iko walivyokuwa attacked na kuna taxis jirani na hapo kwanini wasipige makelele ya wimbo wa taifa (Mayowe ya wezi/majambazi) ili watu wakaja kuwasadia kwa nini walipambana kimya kimya bila majirani walio karibu kujua kilichotokea. Kulingana na mwenzie (Ndimera)alivyoripotiwa na gazeti la Guardian hata walipotoka nje anasema hiyo gari ya watu waliowashambulia ilikuwa inajikokota kuondoka na hawakuweza kuifuatilia kwa sababu walikuwa wanawahi matibabu. Taxi driver waliiona kwa nini wasiwaambie watu wa Taxi driver kuwa hao inabidi wafuatiliwe wakamatwe? Au kwanini wasipige simu polisi kwa kutumia hata simu za mataxi driver ili polisi waje haraka hapo eneo la tukio.

    7. Kuna maswali mengi kuliko majibu na issue yote imegubikwa na habari za ufisadi lakini ukifungua macho there is more to it than hiyo issue ya ufisadi. Na hapo Dar mtu yuko radhi akufanyie kitu mbaya hata kukumwagia tindikali kwa sababu ya mwanamke/ugoni au kudhulumiana madili/kula hela ya watu halafu usitimize ahadi. Ni Saidi Kubenea peke yake na hao waliomshambulia ndio wanaojua kisa cha kushambuliwa. Midamu mashati yao na upanga ulibaki ofisi ya gazeti la Mwanahalisi na mataxi driver (aaccording to Ndimera alivyoripotiwa na gazeti la guardian) waliiona hiyo gari ikijikokota basi polisi watafanya kazi yao na ukweli utajulikana.

    Mwisho pamoja na kumpa pole Saidi Kubenea na kumtakia tahfifu apone haraka, tunamuomba awe mkweli ili awatoe hofu waandishi wengine wafanye kazi ya kuanika uovu bila wasiwasi wa kudhuriwa na wasomaji au wanaowaandika.

    Waswahili huwa tunamsemo, aliyeibiwa huchuma dhambi kubwa kuliko aliyeiba kwa sababu humdhania kila mtu ni mwizi wake aliyemo ana asiyekuwemo.

    Huyu si alikuwa mwandishi wa magazeti ya Habari corporation siku za nyuma akakumbwa na skandali ya kupika data/habari, enzi za Jenerali Ulimwengu huko Habari corporation wakamtimua? Kama sie naomba anisamehe!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...