
SERIKALI itagharamia matibabu ya nje ya Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi, Saidi Kubenea, aliyesafirishwa leo, Jumatatu, Januari 7, kwenda India kwa matibabu zaidi.
Serikali inagharimia matibabu hayo ya Kubenea, kama inavyogharimia matibabu ya Watanzania wengine wanaokwenda kupata huduma za tiba nje ya nchi.
Msimamo huo wa Serikali umetangazwa mara tu baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amemtembelea na kumjulia hali Bw. Kubenea kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Bw. Kubenea ambaye alilazwa Muhimbili usiku wa Jumamosi iliyopita, Januari 5, wakati watu wasiojulikana walipovamia gazeti la kila wiki la Mwanahalisi na kumjeruhi Kubenea pamoja na Mhariri wa gazeti hili, Bw. Ndimara Tegambwage.
Katika shambulio hilo, Bw. Kubenea alimwagiwa tindikali wakati Bw. Tegambwage alipigwa panga kichwani. Wakati Bw. Kubenea alilazwa hospitali, Bw. Tegambwage alitibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani.
Kama alivyokuwa ameeleza katika taarifa yake rasmi kwa vyombo vya habari jana, Januari 6, 2008, Rais Kikwete amemweleza Bw. Kubenea jinsi alivyosikitishwa na kuhudhunishwa na shambulio dhidi yake, na dhidi ya Bw. Tegambwage.
Rais amesema kuwa kama wahariri hao wameshambuliwa katika hali ya kawaida basi ni jambo baya.
Serikali inagharimia matibabu hayo ya Kubenea, kama inavyogharimia matibabu ya Watanzania wengine wanaokwenda kupata huduma za tiba nje ya nchi.
Msimamo huo wa Serikali umetangazwa mara tu baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amemtembelea na kumjulia hali Bw. Kubenea kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Bw. Kubenea ambaye alilazwa Muhimbili usiku wa Jumamosi iliyopita, Januari 5, wakati watu wasiojulikana walipovamia gazeti la kila wiki la Mwanahalisi na kumjeruhi Kubenea pamoja na Mhariri wa gazeti hili, Bw. Ndimara Tegambwage.
Katika shambulio hilo, Bw. Kubenea alimwagiwa tindikali wakati Bw. Tegambwage alipigwa panga kichwani. Wakati Bw. Kubenea alilazwa hospitali, Bw. Tegambwage alitibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani.
Kama alivyokuwa ameeleza katika taarifa yake rasmi kwa vyombo vya habari jana, Januari 6, 2008, Rais Kikwete amemweleza Bw. Kubenea jinsi alivyosikitishwa na kuhudhunishwa na shambulio dhidi yake, na dhidi ya Bw. Tegambwage.
Rais amesema kuwa kama wahariri hao wameshambuliwa katika hali ya kawaida basi ni jambo baya.
Hata hivyo, amesema kuwa ni jambo baya zaidi kama wahariri hao watakuwa wameshambuliwa kwa sababu ya kazi yao ya uandishi wa habari, kwa sababu hilo ni pigo kwa juhudi za Serikali katika kulea na kuunga mkono vyombo vya habari huru na vinavyojitegemea nchini.
Imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
Imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.


Huy JK anataka kuandikwa vizuri tu magazetini. Si umtume waziri wa Habari ?Raisi shughuliz zote ikulu unaacha kazi zako?
ReplyDeleteSalamu kwa wote
ReplyDeleteNatafuta namna ya kulianzisha lakini nahisi kupwaya kwa hoja pevu na komavu yenye kuweza kuingilika vichwani kwa binadamu na akili zao.Pongezi kwa serikali kwa hatua madhubuti waliochukua ingawa kwa miaka ya 40 uhuru tatizo lilikuwa litibike nchini.
Kenya kunani?Wale wambeya wanaopenda kuchokoachokoa mambo ya nchi zingine na kusema kwetu kuna amani,sasa hii ni ashirio la kwamba hata nyumbani kwetu wapo wenye agenda zao binafsi na hawataki sauti ya umma iongee juu ya madhambi na uchafu.
Wengine hutumia kalamu/maandishi kurekebisha na wengine hutumia kalamu hiyohiyo kuchafua na kuharibu kabisa na kupidisha maandishi ili wajilimbikizie na baadaye kutumia malimbikizo waliyojikusanyia kujeruhi wengine.
Mimi nadhani hatu inayofuata ni kusakwa kwa wahusika hadi wapatikane halafu warejeshe gharama iliyoingia serikali kwenye matibabu haya,siyo serikali itumie mapato yake kwa ajili ya kuwahifadhi maharamia.
I ma pretty sure that if I request the government to provide me with confluence of clues that where did the fund used come from, range of answer are expected since predominately the government is operating under medium term expenditure framework (MTEF). Every single pence fall under activities, which are aligned with target, objective and mission pamoja na mkukuta.
Ushauri wa bure na kwako wewe mwenye blog hii bwana angalia usije ukawa next target,kwa maana bwana mimi na wasiwasi wengine hawapendi kuona watu wanaishi kwa raha na wanaweza hata kujinunulia kakuku na kula kwa kutulia tu.
Nakumbuka ule wimbo wa Remi,akija mjini wanamwita mzururaji,akirudi kijijini halafu nguruwe akila mihogo anasingiziwa yeye,je mnataka hawa wajasiriamali wawe wanakuja kuombaomba kwenu kwenye vihela vyenu vichafu,
Sasa taifa letu inatakiwa lifanyiwe maombezi makubwa sana.Mimi bwana naanda pepa kali sana,white paper nategemea nikaiuze kwa wafadhili halafu nirejee nayo hapo nyumbani ittakuwa chachu ya kuzuia baadhi ya matatizo kama hayo kwa mika 100 ijayo.It is meant for 4th generation, maanake haya mapakashume yaliyobakia hayakunjiki bali yanavunjika ukitaka kuyakunja.
Michu, hebu naomba uwaulize hao jamaa wa Ikulu ni kwa nini hawataki kuongeza pesa ili mtoto Nkya apelekwe India kwa matibabu? Nimefurahi Bw. Kubenea analipiwa hizo gharama; lakini je ni kwa nini mtoto Nkya haongezewi hizo pesa zilizobaki (baada ya wasamaria wema kuchanga)?
ReplyDeletepole nyingi ziende kwake na wote waloumizwa kwenye hilo.
ReplyDeleteSheria ya kuruhusu ushahidi wa digital kukubalika mahakani imetungwa 2007 na Rais alisha asenti,hiyo ni wakati wa kuanza kufunga CCTV cameras maeneo yote nyeti na yenye uhalifu wa mara kwa mara
kusema ukweli si jambo baya na namuombea Mungu apone haraka, ila nina kinachonishangaza serikali yetu hii ni kushindwa kujenga hospitali ambazo zingekuwa zinatoa matibabu kwa viongozi hata watu wenye pesa zao badala ya kutumia gharama kubwa na pesa kidogo za kigeni tulizonazo ambazo tungewezw kujengea hizo hospitali na miundo mbinu mingine.
ReplyDeleteJamani viongozi wetu wa kiafrika sijui ndiyo kusema hawana vision ya maendeleo ila kazi yao ni madaraka tu? Eeeh mola tulinde sisi wajawako na majanga mingine kwa kwa hapa kwetu tunaishi kwa kudra zako tu
Tunampa pole na kumwombea apone haraka mwanahabari huyu. MICHUZI unakumbuka mwaka jana tarehe 10 Januari 2007, ulitoa picha ya Rais JK akimpa pole mwanahabari dada yetu HAlima Mchuka akiwa amelazwa Muhimbili kutokana na tatizo la kupooza,tunaomba utupe maendeleo ya afya yake sasa kawani mwaka umeshapita na bado hatujamsikia tina-miss sana hasa katika kipindi cha Zilipendwa cha RTD na pia katika utangazaji wa mpira wa miguu, akiwa ni mwanamke pekee aliyekuwa akitangaza mpira. tafadhali tujulishe tumjulie hali dada yetu.
ReplyDeletehali inatisha lakini I hope watuhumiwa watapatikana, na wawe watuhumiwa halisi.... kuanzia iliposukwa mipango. Hiyo mosi, pili, hivi mtu anaekuwa mwandishi wa Ikulu si anatakiwa afahamu Kiswahili fasaha? au Michu ume copy fyongo? neno ni HUZUNI, sio HUDHUNI...
ReplyDeleteKwanza kabisa nikiwa mtanzania mzalendo, niliipokea kwa mshtuko mkubwa habari ya kusikitisha ya waandishi wa habari kushambuliwa na watu wasiojulikana wakiwa wanatekeleza majukumu yao ofisini.Natambua na kuthamini sana mchango wa sekta ya habari katika maendeleo ya nchi,hivyo basi watu waliohusika na tukio hili kwa vyovyote vile lazima walaaniwe vikali na kila mtu mwenye ubinadamu.Na zaidi ya kulaniwa, mamlaka husika ziwasake na kuwashikisha kwenye vyombo vya sheria waliohusika na ushenzi huo.Nimefarijika kwamba serikali imeunda kamati maalumu ya kujua kwa undani lengo na waliohusika na shambulizi hilo chini ya afande Tibaigana,Nina hakika kamati itafanya kazi kwa ufanisi na matokeo yake kuwekwa hadharani.Kabla ya bwana michuzi kutuwekea kwenye blog yetu ya jamii habari ya Mh.Rais Jakaya Kikwete kwenda kumjulia hali bwana Said,masaa takriban 8 yaliyopita kwa hapa Marekani, nilikuwa niikitizama taarifa habari ya saa 2 usiku ya TVT kupitia mtandao wa kompyuta na kuona tukio hilo ambalo kwangu limenigusa sana.Limenigusa kwa sababu si rahisi sana kwa viongozi wakuu wa nchi kuwajali waandishi wa habari wa kawaida tena kutoka vyombo vya habari binafsi.Kitendo cha mkuu wa nchi kuacha kiti chake cha enzi pale Ikulu na kwenda kumjulia hali bwana Said hakiwezi kupita hivi hivi bila ya kupongezwa na watu makini .Binafsi,namfahamu sana Mh.JK kama ni mtu wa watu.Lakini kama ilivyo hulka ya binadamu wengi wakipata vyeo basi hata tabia hubadilika sana .Lakini sio kwa Mh.JK ambaye pamoja na wadhifa wake wa juu kabisa kiutawala alionao,bado ameendelea kuwa mpenda watu na myenyekevu.Mwenyezi Mungu amzidishie hekima,utu na busara!
ReplyDeleteNa hata alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutoka wodini,alionyesha dhahiri amekerwa sana na kitendo hicho cha kinyama.Lakini lingine muhimu sana ni kwamba kumbe hakuishia kwenda kumfariji tu bwana Said,bali kuonyesha kwamba ameguswa sana na kitendo hicho Mh JK ametumia mamlaka yake kuiagiza wizara ya Afya kufanya utaratibu wa haraka wa kumpeleka India kwa matibabu zaidi bwana Said.Hii ndio aina ya uongozi unaofaa na unaotakiwa katika karne ya sasa.Linalowekana sasa na lifanyike haraka badala ya kuleta urasimu usiokuwa na ulazima.Big Up JK!!
Mwisho namtakia apole haraka bwana Said ili aweze kurudi nyumbani kuangana na familia yake na zaidi sana kuendelea na majukumu yake kama kawaida.
Mr Tumsifu Mwasamale.
Bowling Green State University
Ohio-USA.
Nakubaliana na mengi yaliyosemwa na wachangiaji, humu ndani kuhusiana na swala hili.
ReplyDeleteNi mategemeo ya wengi Mungu akibariki awape unafuu wagonjwa walioathirika na tendo hili la uhalifu wa hali ya juu kabisa.
Lakini tukija kwenye maswala ya utendaji kazi ya kiserikali, hii inaonyesha ni jinsi gani tuko nyuma katika maswala mengi tu, kuhusiana na Mahospitali na Elimu.
Mimi binafsi ninahisi kwamba, swala la maradhi ya kuungua kwa acid, ni maswala ambayo yangeweza kutibiwa hapo hapo Tanzania, kama serikali zetu zingekua zinaekeza ipasavyo katika maswala ya Afya na utibabu,
Swala la kujiuliza, je ikitokea mtanzania au watanzania wengine ambao wanaungua na acid, na maradhi mengine ambayo hayawezi kutibiwa Tanzania, Je wao wananafasi gani katika jamii kupata matibabu kama hayo ?
Je serikali haioni, hii inaonyesha udhaifu mkubwa kabisa katika sekta ya matibabu na Afya na ina mpango gani kuindeleza na kuikuza sekta hii ??
Ni hayo tu kwa sasa.
By Mchangiaji
By Mchangiaji
michuzi acha uzandiki,au na wewe umejiunga na genge la mafisadi?kwenye blogu yako mbona huelezi ukweli wa hisia za watu wengi kwamba Kubenea kamwagiwa tindikali na mafisadi,unaogopa nini kusema wakati bongo nzima hilo ndo gumzo?au umeshikishwa kitu kidogo?twambie bwana maana si unajua mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake isije blogu yako nayo ikawa imekuwa dili.
ReplyDeleteQUOTE FROM MWANANCHIPAPER OF TODAY 08/JAN/2008
ReplyDelete".........Akielezea historia ya wahariri hao kabla ya kuvamiwa kwao juzi, Ngaiza alisema Desemba 7, mwaka jana, MCT ilipokea barua kutoka serikalini ikilitaka liwashughulikie wahariri hao kutokana na makala zao ambazo ilidai kuwa zinaandikwa kinyume na misingi ya uandishi kwa kuwa zinawadhalilisha Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Barua hiyo iliwataja wahariri hao wawili wa Mwanahalisi, Saed Kubenea na Ndimara Tegambwage kwamba walikuwa wanaandika makala kinyume na maadili ya uandishi wa habari na kuuliza ni hatua gani Baraza lingechukua dhidi yao, alisema Ngaiza na kuongeza.
Nimeeleza haya ili kuifahamisha jamii ya wanahabari na wamiliki wa vyombo vya habari juu ya malalamiko hayo ya serikali dhidi ya gazeti la Mwanahalisi na waandishi hao ambao wamefanyiwa kitendo cha kinyama......"
WACHAMBUZI MAKINI NA WATU WANAOFIKIRI KWA KINA WATAKUWA WAMESHAJUA NI NANI ANAWEZAKUWA AMEPANGA NA KUDHAMINI UOVU HUU.
HATA HIVYO PUNDE MUDA UTATUMBIA.
Kwako ndugu Michuzi na ndugu aliyepiga picha hii ya Mheshimiwa rais akimjulia hali mwandishi wa habari aliyeshambuliwa na wahuni ofisini kwake.
ReplyDeleteKwanza naomba kutoa pole za dhati kwa ndugu waandishi wa habari kwa Gazeti la Mwanahalisi wa dhahama hii iliyowakuta. Kwa kweli wamefanyiwa kitendo kiovu ambacho kinapaswa kukemewa vikali.
Baada ya kusema hayo machache, nakuomba wewe ndugu yetu bwana michuzi, wasiliana na huyu mpiga picha wa rais au Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais mtusaidie kulete na picha ya mheshimiwa rais alipomtemblea Mheshimiwa gavana wetu, Daktari Daudi Ballali ambaye tumeambiwa sasa amelazwa anapatiwa matibabu nchini Marekani kwa zaidi ya miezi mitatu.
Taarifa zilizosambaa kwenye vyombo vya habari zilisema kuwa rais Kikwete alimtembelea gavana Ballali alipokuwa kwenye safari yake ya Marekani mwaka jana. Sasa tunaomba na hiyo picha tuone basi.
We ano wa 9:20 AM mbona kama unaleta bifu lisilo la lazima kwa michuzi.Sote tunalaani kuumizwa kwa Kubenea na mwenzake na inawezekana ni sababu ya mafisadi au la.Je unapomshutumu Michuzi kwamba AELEZE UKWELI WA HISIA ZA WATU WENGI KWAMBA Kubenea KAMWAGIWA TINDIKALI NA MAFISADI SABABU BONGO YOTE WAJUA HILO.Sidhani kama Michuzi anayo mamlaka ya kufanya ivyo japo blog ni yake.Nampongeza michuzi ametuhabarisha hili swala na watu wametoa hisia na maoni yao.Otherwise sioni kama michuzi anao uwezo wa kwenda zaidi ya hapo.Jaribu Busara tu si kitu kingine itakusaidia maishani.
ReplyDeletehiyo safi sasa vipi yule malaika wa mungu uliyemtoa anaomba msaada inamaana serikala inashindwa kumsaidia mtoto anateseka muda wote?niyule aliye pasuka mdomo na wewe mwenyewe ndio uko mbele kumuombea mosaada wakate selrikali kumbe ina uwezo wakusaidia raia wake ama kuna watu maalamu wakusaidiwa na serikali?
ReplyDeleteNasikitika kwa yaliytokea kwa mhariri wa Mwana Halisi. Swali langu ni kwa nini serikali imeamua kumsaidia na yeye ni mhariri wa gazeti binafsi? Ni njia moja ya kujikosha au???
ReplyDeleteJamani Watanzania tumezidi kuzorota . Hizo hela wanazotumia kuwapeleka watu india south afrika na nchi nyingine za nje kwa matibabu zingekuwa zina kuwa invested kwenye hospitali zetu ziendelee. Watu wansomea udaktari bongo wa nini sasa ? wawe wanatoa dawa zilizo expire na kimisdiagnos magonjwa ? we can do better people
ReplyDelete