februari 14, 1992: waandishi godfrey lutego wa uhuru na mzalendo (shoto) na chemi che mponda wa daily news wakiwa na mwanyekiti wa uwt mkoa wa dar mh. mary kabigi wakitoka kituo cha polisi cha msimbazi walikowekwa chini ya ulinzi kwa kuvamia ofisi za uwt mkoa wa dar na kuhatarisha usalama wa katibu mkuu wa uwt mkoa huo e.h. stima. hapo wanatoka kituoni hapo baada ya kuandika maelezo yao. da'chemi tupe stori nini kilitokea na yaliishaje?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Chiku yalikukuta underarresti sio ..Michuzi naomba kutoka nje ya mada nakuomba utuletee picha na maelezo juu kufariki kwa major generali Mwita Marwa
    R.I.P

    ReplyDelete
  2. Itakuwa lazima kuchukuliana mabwana tuu, hakuna lolote!

    ReplyDelete
  3. Michu umenikumbusha mbali sana. Lutego tulikuwa wote A'level. Thanks.

    ReplyDelete
  4. Hi Michuzi,

    Asante kwa hiyo picha. Umenikumbusha mbali! Wakati huo mimi ndo nilikuwa mpigania haki za akina mama hasa na ndio maana nilipangiwa hiyo kazi siku hiyo.

    Yalikuwa hivi. Nilienda kazini Daily News kama kawaida. Baada ya post-mortem nilipangiwa kazi UWT kumhoji Mama Mary Kabigi (sasa marehemu) alikuwa na tangazo fulani. Kule nilikutana na na Godfrey Lutego wa gazeti la Uhuru.

    Tulikaribishwa vizuri mle ofisini, ilikuwa na deski mbili. Kulikuwa na viti mbele ya deski ya Mama Kabigi na tulikaa hapo. Kwenye deski nyingine kulikuwa na mama mwingine Mama Eshe Stima. Mama Kabigi alilmtambulisha Mama Stima kwetu. Ajabu Mama Stima hakujibu. Mama Kabigi alianza mahojiano huko Mama Stima ana nuna na kuguna. Ghafla aliinuka na kutoka ofisini na kufunga mlango. Tuliendelea na mahojiano na Mama Kabigi. Kukaa kidogo tukasikia mlango unafungwa na ufunguo.

    Mama Kabigi aliuliza kama tumesikia mlango unafungwa. Mimi na Godfrey tulibaki tunatazamana na kujibu ndiyo. Basi tulimaliza mahojiano na kutaka kuondoka. Tulishindwa kutoka mle ofisini kwa vile mlango ulikuwa umefungwa kutoka nje.

    Basi Mama Kabigi alisema tukae tusibiri. Kulikuwa hakuna simu mle ndani ya ofisi na enzi hizo hakuna cell phone. Tulisubiri kama saa moja hivi, mlango ulifunguliwa.
    Ilivyofunguliwa Mama Stima kaingia mle na mwanaume na mwanake waliokuwa serious kweli na kuelekea kwetu kwa hasara. Kumbe walikuwa ni polisi waliovaa kiraia.

    Mama Kabigi, mimi na Godfrey tukaambiwa tuko chini ya ulinzi na hao watu! Doh! Tukaanza kuwauliza sababu ya kutuweka chini ya ulinzi.
    Hawakusema kitu zaidi ya kuwa tutaelezwa kituoni. Tuliwaambia kuwa sisi ni waandishi wa habari tuko hapo kikazi na tuliwaonyesha vitambulisho vyetu. Hawakutuka kuviona.

    Basi tulikamatwa na kutembezwa kwa kushikwa mikono kipolisi barabarani hadi kituoni. Tulivyokuwa tunavuka barabara mhariri wa Daily News na aliyenipangia assignment hiyo, Mkumbwa Ally alipita na gari. Nikafoka, "Mkumbwa!"

    Mkumbwa alisimamisha gari huko najaribu kumwelezea kuwa tumekamatwa na polisi. Wale polisi walinifokea ni nyamaze. Mkubwa alitoka kwenye gari alinishika mkono mwingine na kumwambia yule polisi wa kike, “Huyo anakwenda na mimi!” Yule polisi akasema Hapana wanakwenda kituoni wako chini ya ulinzi!” Basi Mkumbwa alikuwa hana la kufanya. Aliwauliza tunapelekwa wapi. Walimwambia na yeye aliondoka.

    Kufika kituoni, tulikalishwa kwenye benchi ndani ya kituo kama masaa mawili. Eneo tuliyokalishwa ilikuwa chafu sana halafu ilikuwa giza. Kila tukiuliza sababu ya kukamatwa hatuambiwi!

    Basi kama baada ya masaa mawili na nusu hivi, tulipelekwa ofisini kwa mkuu wa kituo. Tuliingizwa mle moja moja na kuulizwa ilikuaje. Nakumbuka nilimwonyesha huyo mkuu wa kituo kitambulisho changu na kumwelezea mambo yalivyokuwa na kurudishwa kwenye hiyo benchi. Baadaye tulikalishwa wote pamoja na huyo Eshe Stima ofisini kwa huyo mkuu wa kituo.

    Mama Stima alisema hivi, "Nilikuwa nimekaa ofisini kwangu. Huyo Mama Kabigi kamleta huyo mwanamke na huyo mwaname mle. Walinitishia kuwa wataniua, walianza kunipiga, niliweza kukimbia kwenda kituoni kutafuta msaada!"

    Alisema kama mara tatu. Wewe! Mbona tulibakia kushangaa na kusema huyo huyo mama Stima ni mwongo mkubwa. Tukasema yeye ndiye alikuwa mkali kwetu maana tulimsalimia ha hakujibu halafu alitufungia ofisini.

    Sasa huko nje, front deski ya kituo kulikuwa na mambo, alikuja Mzee Millinga kutoka Daily News, mwakilishi wa gazeti la Uhuru (jina nimesahau), mtu wa RTD na Lucas Lukumbo wa SHIHATA. Nakuambia habari zilienea haraka kweli. Nje ya kituo kulikuwa na magari ya vyombo vya habari na wananchi nje wanauliza kuna nini mle ndani.

    Basi baada ya muda yule Mkuu wa Kituo alisema kuwa tunaruhusiwa kuondoka. Nikamwuliza sababu anaturuhusu kuondoka alisema, kuwa sisi wote tulikuwa na story sawa. Godfrey alimwambia mkuu wa kituo kuwa kwa kweli hajafurahi kunyimwa uhuru wake!

    Mimi nililalamika kuwa tumeshikwa kwa upuuzi. Nilisema kuwa ina maana kuwa mtu yeyote anaweza kutunga uwongo na mtu akamtwe hivi hivi! Wale wakilishi wetu walituambia tuchukue vitu vyetu tuondoke.

    Mbona ilikuwa raha kutoka nje ya kituo cha polisi ukiwa mtu huru.

    Na kesho yake, hiyo habari pamoja na picha ilikuwa FRONT PAGE news kwenye magazeti ya DAILY NEWS na UHURU.

    Huyo Mama Stima aliishia kuaibika, hasa kwa vile alituingizia kwenye ugomvi wake na Mama Kabigi. Mpaka sasa sijaelewa hasa ugomvi wao ulikuwa nini, lakini nilivyosikia ni kuwa yule Mama Stima alionywa vikali kuhusu kusema uwongo polisi, na wale polisi walionywa maana walivyotukamata ilikuwa si sahihi. Nadhani aliharibu urafiki wake na yule Rafiki yake polisi siku hiyo maana majina yalitoka kwenye gazeti! Wengine walisema kuwa walikuwa wana ugomvi juu ya nafasi ya uongozi wengine walisema waligombania bwana. Sijui ukweli uko wapi. Ila nilijikutwa nimeingizwa kwenye ugomvi wao.

    Siku hiyo naiwrite off kama, "Ajali Kazini! - Adventures of a Journalist!”

    Lazima niseme kuwa niliendelea kuwa na uhusiano mzuri na Mama Kabigi. Baadaye alikuja kuwa Mbunge wa akina mama (viti maalum). Na nilimwona kama mtu anayependa kutetea haki za akina mama. Huyo Mama Stima sijui aliishia wapi.

    ReplyDelete
  5. Upuuuzi wa Polisi Tanzania ndo huu sasa, mi wananikera hapo tu! Wanaweza tu kukukamata bila kukueleza wanakukamatia nini!! huu ujinga tu, huku Marekani subutu Polisi akukamate tu, kwanza utamsue upate na ulaji. Tanzania jamani tuwe na ustaarabu na haki kwa binadamu sio tu kujifanyia mambo kisanii. Hizi ndo baadhi ya vitu unaogopa hata kurudi bongo, maana ukisingiziwa tu kazini tayari uko sello.Bongoo bwana!!!

    ReplyDelete
  6. Pole Dada Chemi. Ni kweli mambo Bongo yanaudhi. Huyo Mama Stima aliaibika kweli siku hiyo na baada ya hapo alianguka UWT. Alivyofanya ni vibaya na yeye si wa kwanza kwenda kusema uongo polisi. Na huyo mtu aliyemsaidia polisi alikiona! Bora angewanfanyia watu wengine lakini aliamua kuwafanyia fujo waandishi wa habari tena wanafanya kazi kwenye magazeti ya serikali na ya chama!

    ReplyDelete
  7. Hivi huyo mtu Dada Chemi amemtaja ni yule Esha Stima wa NEC? DUH kumbe yuko ovyo hivyo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...