Hatimaye Clinton ameibuka na ushindi mwembamba huko New Hampshire, asilimia 2 hazikatishi tamaa, na mapambano bado yanaendelea, bado Obama jogoo.

Hillary Clinton 39%
Barack Obama 37% si haba wajameni.

Najua waosha vinywa wataichukulia dei ofu hii hoja lakini ndio mchezo unavyonoga!

Mhabarishaji maalum wa uchaguzi Marekani,
Jacob.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Unajua wewe jacob unachonga sana kiasi kama ungekuwa wakara wa kuhesabu kura huku kwetu bongo ungefanya watu wachukiane bure siku nyingine acha kuchonga lete taarifa zilizo sahihi siyo mambo ya kushabikia tu. Kweli sisi wote ni waafrika na tungependa mmatumbi kama sisi atawale marekani lakini siyo kuanza kupotosha we fikiria kwa mtu ambaye ulisema anaongoza kwa 80% ghafla unasema kashindwa hata kwa hesabu za darasa la ngumbalu hainipi kabisa.
    Nadhani kinachokusumbua hujui taratibu za uchaguzi marekani zinakwendaje ndiyo maana unakurupuka kutuletea habari za kizushi tunakuomba usije kuharibu blog ya Misupi ikaonekana ni ya kizushi

    ReplyDelete
  2. Wewe Tumekuchoka,Hata uku bongo Habari tunazipata WEWE kutwa kuchwa Obama ...Clinton Uku pia tunaona CNN BBC tena bbc kishwahili tunaelewa kila kitu. Nitakuona wa mahana iwapo Utafatilia Taharifa ya Mahesabu aliyopewa RAIS wako JK na marekebisho ya kipumbavu anayofanya

    ReplyDelete
  3. Naona michuzi hutaki kuandika maoni yangu kumjibu ndugu yako jacob, poa tu ila sitoacha kuandika pale ukweli ulipo na kutoa kile ninachoona kina ukweli

    ReplyDelete
  4. Wacha uzushi wewe.Au una asili ya kuandika uongo???Au ushabiki umekuzidi kiasi???
    NH Votes
    Hillary Clinton 39%
    Obama Barack 36%
    Hao ndio matokeo sahihi ya wagombeaji hao wawili.

    ReplyDelete
  5. Hivi uchaguzi wa rais mpya wa Usagara utatusaidia nini sisi wabongo?

    ReplyDelete
  6. Jacob, nilifikiri jana ulisema kuwa Obama kashinda???? si unaona, badala ya kwenda kubeba maboxi, unakalia kuchonga, utapotea wewe.

    ReplyDelete
  7. MUACHENI JACOB ATUHABARISHE, SIO LAZIMA MSOME. JANA ALISEMA AMESHINDA "KWENYE KITONGOJI KIMOJA CHA KWANZA KUPIGA KURA", SIO JIMBO ZIMA, MBONA HATA POLLS ZILITABIRI OBAMA ATASHINDA NA HAZIKUPATIA? NAZO ZIACHE KAZI?

    ReplyDelete
  8. anoy wa 10:35 kusema ukweli uchaguzi wa nchi kama marekani una athali zake kwa uchumi hasa kwa nchi changa kama TZ. hawa jamaa wakichagua mtu mgomvi kama Bush dunia nzima uchumi unayumba hasa anapoanzisha vita kama ilivyo sasa hivi bei ya mafuta iko juu sana tofauti na wakati wa Saadam. Kwa hiyo watu kufuatilia chaguzi kama hizi ni muhimu sana kwani inatupa muelekeo wa uchumi wetu baada ya miaka kadha.

    ReplyDelete
  9. kwako kaka jacob naomba nikuulize mbona hutupi habari za republican party sisi tunashukuru kwa kutupa habari lakini inaelekea kama wewe unashughulika na democratic tuuuuuu
    asante

    ReplyDelete
  10. Mdau Jake hebu twambie siri ya urembo,wanakulipa kiasi gani?anon wa 9:42 nakubaliana na wewe,news za huyu bwana ziko kila pahala na isitioshe ni Breaking Nyuuuuuuuz as it happens we here about it,sasa wewe dogo kujitia kazi ya Michuzi inahusu nini kua tarishi,at what rate is your wages per advert on Michuzi's blog,to be honest it doesn't affect us who wins the presidential race, why cant you try and get some sleep ili ukafanye ukuli wa mabox.Najua unategemea wasuuza vinywa kwa wingi basi smile dogo nimechangia ili uridhike,mie unanifurahisha sana unavyo shughulishwa na Barack Obama he's an inspiration but I love Mrs Clinton too,for me whoever wins I'm happy for them.If there wasn't Obama this year Hilary could have a better chance but with New Hampshire's results you can never predict either.Kwahiyo acha kukurupuka.

    Have A Nice Day And G'Luck With your Quest To Be A Political Reporter tehe tehe tehe.

    ReplyDelete
  11. not everyone ni mbeba box,do u guys have nothing else to do? damn get a life.

    ReplyDelete
  12. Hivi wewe Yakobo na uchaguzi wa bongo ulikuwa ukiufatilia hivi au ulikuwa bize na box. Hapa kinachoonekana wewe ndio ulieamua kuchukulia hili swala la uchaguzi dei off.

    Nenda kafanye kazi achana na mambo ya siasa za usagara, obama mwenyewe hata hakujui

    ReplyDelete
  13. Jacob waosha vinywa wasikukatishe tamaa, wewe leta hizo habari, Mbona wao wakileta habari za mpira wa PL,UK watu wanakaa kimya, kwanini msishabikie Majimaji, Simba au Yanga. Kila mtu na hobby zake. Mimi niko na wewe, ni mshabiki wa Obama na jana iliniuma sana alivyoshindwa, Clinton bila kulia alikuwa aende na maji.Tanzania tungepata viongozi japo watano kama Obama, tungemaliza matatizo mengi. "YES WE CAN"
    Angalieni hotuba yake:
    http://www.youtube.com/watch?v=Fe751kMBwms

    ReplyDelete
  14. Huyo Jacob tunamjua sana..kama ni yule yule wa Los Angeles..ana matatizo sana..Muongo, masifa kibao..hana mpango..kwani watu hawawezi kusoma wenyewe magazetini? Hana cha kufanya..alijaribu kuanzisha blog kichaa haikudumu sasa anatafuta namna ya kujijengea jina hapa..mwambie aende Mwanza akavue samaki..hana deal wala nini....!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...