Wadu kunradhi. Kwa idhini yeni naomba nitoe hongera kwa IPP kwa kutoa habari ya mwenzetu Godfrey Stalin Mwafongo hapa http://www.ippmedia.com/ ambayo inasikitisha sana.Natoa changamoto kwa wanahabari wote wa bongo pamoja na vyama vya waandishi bongo kumsaidia mwenzetu huyu ambaye ni mmoja katika wengi wanaosota waya baad ya kuisaidia nchi kwa mambo mengi tu. Kwa kweli tuna kila sababu ya kumsaidia shujaa huu asiyeimbwa.


swali anakata masanga au hapana hiko ni cha kwanza, nina shaka na hadithi hii kuna waandishi wanafanya kazi bila vyeti yeye anashindwaje kupata kazi?
ReplyDeleteHe must have done something that lead to his situation....He has issues....story yenyewe inasema hata watoto wake hajui wako wapi..Don't you think kama aliwajibika kuwatunza vizuri watoto wake, hao hao ndiyo wangemsaidia?
ReplyDeleteHawa ndiyo wale wanaokuwaga walevi, wazinzi wakati wa madaraka, halafu wakiwa na hali ngumu ndiyo wanajitokeza kulia lia..
VUNA ULICHOPANDA BABA MWAFONGO...
1. Asaidiwe ili ayaseme yaliyompata bila kuficha. Sio lazima kuyatundika kuwa public consumption.
ReplyDelete2.Kama ni mahitaji ya kiganga asaidiwe, pia.
3. Sio Mwafongo peke yake; kuna wengi...shauri ya ulevi na kuchanganyikiwa akili (depression na kichaa)au combination ya yote.
Nanukuuu "In Dar, he joined the Daily News and Sunday News as a sub-editor, a job he lost in circumstances that he declined to disclose.
ReplyDeleteMwafongo, who keeps body and soul together mainly through the help of neighbours, has three children with whom he has lost contact. "
Hana rafiki wa kumsitiri akirudi Dar kutafuta kazi? Au mbeya mjini hamna kazi? Msomi hivi ataweza kupata kazi lakini msaada wa hela tu hautamsaidia chochote kwa vile hatujui savings yake na kufanya kazi mda wote huo " wakati wake mfanyakazi yeyote alikua anamudu kusave sio kama sasa hivi kazi zinafanyika lakini kusave ni shida" Amevuta bangi au amefanya nini mpaka akapoteza kazi na kupoteza mawasiliano na familia yake...Tuwe wakweli ili apate msaada utakao mfaa.
Hela sidhani kama itamsaidia..huyu anahitaji J.O.B
KATI YA WATOTO WALIOTAJWA,I HAVE A FEELING BUPE MWAFONGO alikuwa mmoja wa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne Ifunda tech,mwaka 1996,mimi nimemaliza pale 1997.nadhani ni mwenyewe!!its sad kuona kwamba hajui wako wapi!
ReplyDeleteHuyu bwana Hadithi yake sio ya ukweli hata kidogo. Kuna kipengele amesema kuwa hataki kueleza kwanini alifukuzwa SHIHATA, "In Dar, he joined the Daily News and Sunday News as a sub-editor, a job he lost in circumstances that he declined to disclose.
ReplyDelete". Hapo nido issue. Unavyoomuona tu huyu bwan masanga inaelekea ndio yake. Mie mwenyewe nina mjomba wangu alikuwa DC enzi za Nyerere ila masanga na nini wakamtosa, hadi sasa anaishi kijijini hana lile wala hili. Kwa hiyo michuzi unakosea sana unaposema huyu ni shujaa. Shujaa amefanya nini kwa taifa? Acha ushabiki angalia habari kwa makini.
Mdau
KAKA YANGU HADITHI IMEKUSHTUA SANA NINI HII MBONA WAKO WENGI MAISHA YAMEWAKUMBA HIVI. AU IMEKUINGIA ROHONI CAREER FIELD MOJA NA WEWE UKAPICTURE THIS IS YOU 20 YEARS FROM NOW.
ReplyDeleteWAPENDE WATOTO NA FAMILIA YAKO UKIWA UNAKWENDA JUU WAKATI WA KUSHUKA WATAKUSUBIRI CHINI
WATU TUNAVUNA TULICHOPANDA
INGEKUA KAZI TU NINGEMUONEA HURUMA HATA WATOTOT HAJUI WALIKO BASI KUNA JAMBO KUBWA ZAIDI YA HILO LILILOANDIKWA...
Huyu 'kalumbu'wangu Mwafongo ana tatizo kubwa sana ambalo hataki kusema hapa-So we do not need to discus his jibe
ReplyDelete1,Huwezi kuwa na watoto wako tena 3 ukawa hujui wapo wapi na wanafanya nini ili wewe unauza maparachichi ili kuishi
2,mwandishi mwenye elimu kubwa kama yeye{alisoma kozi hiyo Poand}hata kama meangukia kwenye"conflict of interest"na serikali huwezi kosa kazi ja[po ya kukupa hela ya kula na kulipa bill zako
3,sidhani kama anaweza kosa hata mtu mmoja Dar amuweke ili kwa elimu yake ni"lazima"tu atapata kazi kwenye taasisi za utangazaji zinazochipua sana tz hivi sasa
Mzee Mwafongo,nimechomwa sana na habari zako,please tuambie ukweli hasa nini kimekupata,ten we gonna help yuu hugely
Mimi kwa bahati nzuri natoka kijiji kimoja na Mzee Mwafongo,na najua hata mitaa hiyo,lkn Yeye mwenyewe likely simjui
Kwa kaka Michu,kuwa makini sana na"blog yetu hii"{sio yako ingawaje umeanzisha wewe,ni yetu sote wewe na sisi},huyu assitwe shujaa hadi tujue iweje mtu msomi kama huyu awe anaishi hivyo kijijini???
unajua michuzi wazee wengi waliofanya kazi enzi hizi na ambao walikuwa waaminifu serikalini maisha yao yanasikitisha sana na naona ndiyo maana hawa waliobaki wameamua ni kipindi cha kuvuna hata kama tutasema kwamba ni ufisadi.Kamshahara kenyewe ka serikalini kalivyo kadogo hata ukienda kuchukua pensheni yako unabaki kushangaa tu na pesa kichele. Hata kama mkimita muongo ni cha muhimu tujiangalie sisi je kuna chochote tulichonacho kwa maisha ya baada ya kuacha kazi ya kuajiriwa?
ReplyDeleteMi ninachojua kama ni pombe wengi tu wanakunywa. Tujiandae
Mimi nasema hana mtu wa kumlaumu. Hawa ni mmoja wa wazee wa zamani ambao walimesa maji ya bendera ya Taifa na kuasahu kuhusu maisha yao. waliaambiwa na Nyerere kuwa ukiwa na mali ni kosa la jinai. Sasa matokeo yake anahangaika sasa. Wako wengi sana wa namna hii. Politics za ujamaa ziliwaangamiza.
ReplyDeletehata baadhi ya wazee siku hizi, akiwemo mzee wangu wanoko sana. Ukitaka kufanya hiki wanakupandishia na kukusahauri kuwa ni hiyo ni hatari! Wanachukulia vitu vya uangalifu ambao hauna maana.
Sishangai Ma-colonel waliostahafu sasa hivi wanafanya kazi za ulinzi au hata ma-OCD wakihenya kulinda night! That was very bad in Nyerere time.
Ndo maana siku hizi mtu akipewa post ya juu anahakikisha anakamua mpaka povu linatoka! Mfano issue kama Balali na wenzake.
Wazee wetu hawa wamebakia kutupa stories tu za ujamaa na ujasiri wa CCM. Hakuna mpango wowote.
Mwafongo naye alijifanya mwaminifu. Sasa anauza makatapera na ndevu zimechakaa kabisa!
Huyu lazima alitaka ku-publish uzushi kwneye gaezti la serikali kama ilivyo siku hizi. Enzi hizo Nyerere na watu wake walikuwa macho sana. Nakumbuka mjomba wangu alifungwa miezi sita baada ya kutoka UK na alipofika airport akaficha UK pound 150 tu. Hilo likawa kosa na wakamkomalia mpaka akafungwa. Alikuwa state house.
ReplyDeleteSasa hivi ni bonge na Borgeous (Bhushwa) la nguvu Dar na anamiliki chains za business.
Ana laani sana kujifanya eti wewe ni mzalendo katika nchi za kiafrica. Alikaa jela bila sababu, kisa pound 150 ambazo hakuziona na kuzionyesha airport!.
Mwafongo lazima kuna issue. Na anaweza kuwa mtu wa usalama wa Taifa ndo maana hasemi nini kilitokea pale Daily news. Nasikitika sana kwa hali yake.
Mungu amsaidie aweze kuishi zaidi na zaidi.
ahhhhhh watani wangu wa Mbeya! hii ya Mwafongo kali sana sana. Kwisha habari yake na ndevu zake. Inaonyesha huyu ni drinker wa nguvu na totoz za kienyeji ni issue! Nimefurahi sana siyo kwa kufurahia hali mbaya ya Mwafongi, ila evolution ya mambo!
ReplyDeleteDamn! Hii hadithi ni ya ajabu kidogo hasa kwa msomi kama huyu. Ina maana akili yake ilishagota kabisa hapo hata hana mpango wa kuendelea tena hana na wala hajishughulishi kuwaza mbinu mbadala. Ameshindwa hata pa kukoppa!! Hata kwa correspondents wa hayo magazeti! Bo there must have been something odd with him. Any way kutoa ni moyo, tumsaidieni labda atachenji! Ila kuna watu wengine hata uwafanyeje hawasaidiki!!!
ReplyDeleteAchana na huyu kuna watu walikuwa mawaziri,manaibu waziri,wakuu wa mikoa,majaji nk enzi za "MCHONGA" wakacheza sasa wako "juu ya mawe" kama magari mabovu.Inaonekana kuna kitu huyu jamaa anaficha hataki hata kukisema.Michuzi fuatilia SHIHATA ujuwe ni kisa gani kilichomfanya atemeshwe kazi kama hujakuta ni si ulevi nk(just my thoughts)na ukiuliza marafiki,jirani utasikia "ooh jamaa karogwa,ooh walimchomea nk" wabongo ndivyo tulivyo hata mtu akifa kwa ukimwi haya ndiyo yanayosemwa.
ReplyDeleteYeah wabongo walisema kutesa kwa zamu.Sasa ni zamu yetu kutesa.
ndugu wananchi.
ReplyDeletesi vizuri kutoa maamuzi kuhusu mtu kabla hujajua hadithi nzima.wapo walioanguka kutokana na tabia +vibweka vyao wakiwa madarakani lakini pia wapo 'waliotengenezwa' na waheshimiwa kwa kuingilia 'maslahi'.sasa katika 'giza' lililopo saivi, si vizuri kuhitimisha na kumdhihaki huyu mzee wakati hatujui nini kilimsibu.inakuwaje pia hana mawasiliano na wanae?hapa napo pana utata sana.
pamoja na yote,wazee wengi waliokuwa waaminifu enzi hizo leo hawana mbele wala nyuma kwa kuwa mfumo wetu upo shaghalabagala linapokuja suala la mafao ya uzeeni na matunzo.
Binafsi nimepokea kwa masikitiko sana habari hii.
ReplyDeletekwangu haijalisha nini chanzo cha yeye kufika hapo,nachukuan kauli yake ya sasa ambayo ni ya mtu ambaye anaomba msaada ili kurejea kwenye game.
hata kama makosa alifanya still yeye ni binadamu kuna kuanguka na kujikwaa katika maisha.
Kikubwa ingependeza kujua kwa undani nini chanzo cha yeye kushindwa kuendelea na fani yake ya habari.
maana itakuwa haileti maana kumsaidia kurejea kwenye fani bila kujua nini kilichopelekea yeye kutoswa.
Pole sana mzee wangu!!!Usijitoe uhai komaa tu mpaka kieleweke!!!
Nakubaliana na Andy,
ReplyDeletesisi wote ni binadamu hatujui tunapoekelekea kesho tunaweza kukutwa na majanga kama haya. Si vizuri kumkashifu mtu ambaye yoko kwenye hali kama hii.
Ni kweli inawezekana kuna kitu kibaya alikifanya wakati ana madaraka, lakini sisi hatuna haki ya kumhukumu na kumdhihaki at list kwanza tungeuliza ni kitu gani hasa kilichompata kabla hatuja tuma comments ambazo badala ya kumsaidia zinamuumiza zaidi.
Binadamu inabidi tujifunze kusaidiana hata kama siyo ki pesa iwe kimawazo. Hivyo huyu mzee wetu anahijati mawazo na ushauri ambao utamsaidia angalau kuboresha maisha yake au kumsaidia apate mawasiliano na watoto wake ili awaombe msamaa kama aliwakosea.
Its very sad Bro Michu mtafute basi tumpe deal la kwenda barber shop maana mmh hali siyo nzuri kabisa anaweza hata kuwa na chawa huyu.
ReplyDeleteMpe ofa kwa bitebo afanyaiwe na massage na wale kinadada ila anahitaji msaada mkubwa jamani hujafa hujaumbika wote sisi ni binadamu tunaweza kuchemsha kwa nguvu za Ibilisi ukajishangaa hivi kweli ni mimi au nimesimgiziwa? ukijikuta na bonge la sooo kwa hiyo msipime cha maana ni kumsaidia
ReplyDeleteChonde Chonde Jamani!!! Kama kuna namna ya kumsaidia basi ni wenye hiyo namna na niya wamsaidie.. Hakika kutakuwepo na jambo zito ambalo lilijiri Bw. Mwafongo kufikia hatua hii. Haya yamewakuta wengi na hasa ambao walikuwa wachapa kazi, yaani kazi na wao kipindi cha awamu ya kwanza. Hawa walipenda kazi na hata kusahau maisha yao na ya familia zao, na haya ndiyo yalikuwa mafunzo thabiti ya Mwalimu kwani hata yeye ilibidi serikali imuenzi ama sivyo naye alikuwa hali mbaya. Ni jambo la kujivunia sana ucahapa kazi lakini vilie vile lazima pawepo na akiba kwamba kazi ina mwisho wake na malipo baada ya kazi huwa hayalipi gharama zako hata nusu za maisha... Msaada ni jambo analohitaji sana Bw Stalin... ninamkumbuka wakati boss wa SHIHATA mkoa wa Rukwa (ofisi ilikuwa ndogo tuu yeye na katibu wake muhutasi, dada Mary).. alikuwa mtu madhubuti na wala hakuwa mlevi wa "Sute" wala nini... (dRU)
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteYaani huyo kwenye picha ni yule Mzee Mwafongo ambaye tulikuwa tunafanya kazi naye Daily News? Mungu wangu duniani kuna mambo. Mzee Mwafongo alikuwa mtu wa busara sana na kiingereza safi sana na ni mtu anayependa nchi yake. Lakini alikuwa na tatizo moja kubwa na sitaitaja hapa. Na nakumbuka aliondoka Daily News na hawakusema sababu ya kuondoka kwake.
Kweli inasikititisha kuona mtu aliyewahi kuwa Mwandishi wa Rais kuwa na hali mbaya hivyo.
Kaka Misupu, ili wadau waweze kuisoma habari yenyewe kutoka kwenye toviti ya ipp, inatakiwa wabofye hii link:http://www.ippmedia.com/ipp/observer/2008/01/06/105738.html
ReplyDeletethanx anon wa 10:00 jan 7, kwa link hapo juu, link aliotoa misup inafungua tu front page nikasaka habari hadi nikachoka na sikuiona, link yako inakupeleka moja kwa moja,
ReplyDeletemichuzi next time pls tupe basi link ya moja kwa moja,kama mdau hapo juu,
kazi njema vyote.
Duh!huyu Mze ameniamsha usingizi basi kuanzia leo ntaanza kusave na kupunguza kunywa mshahara.
ReplyDeleteMsaada wangu kwake ni kumshauri kuandika kitabu na kukiita "Kupanda na kushuka, Mwafongo the true story". (hapa atuelezee vijana how life was back in the days, pia atupe historia yake nakadhalika jinsi alivyopanda mpaka siku akanyamba, stori lazima itakuwa tamu.
Chini yake kuwe na vikwombolezo kama vile encounters with two presidents who served Tanzania, i.e. Nyerere and Mkapa. Hii aiandike tu kwenye daftari kwa mkono, halafu amfuate mbunge wake ili amkonekti na makampuni ya uchapishaji wataingia nae mkataba na kuchapisha kitabu huo utakuwa mwanzo of the coming back.
Hivi TV za Tanzania au magazeti waanzishe basi series, ambapo wanatinga kijijini na kuwatafuta watu waliofanya kazi enzi hizo na sasa wako juu ya mawe, ili vijana tujifunze kutokana na yaliyowakuta wenzetu, nobody is getting young, ili na sisi tupange jinsi ya kuukabili uzee miaka ijayo.