jk akiagana na mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalamakmstaafu jenerali ernest mwita kiaro wakati jk alipokwenda kumjulia hali nyumbani kwake wilayani tarime juzi. jk alikuwa tarime kuhudhuria mazishi ya meja jenerali mstaafu mwita marwa.

jenerali kiaro hakuweza kuhudhuria maazishi hayo kwa kuwa alikuwa mgonjwa na hivyo Rais akaamua kumtembelea ili kumjulia hali. katika mazungumzo yao jenerali kiaro alimshukuru jk kwa kumtembelea na kumtakia mafanikioa mema katika kutimiza majukumu yake kitaifa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. POLENI KWAKWA MSIBA WATOTO WA MZEE MWITA MARWA AKINA JAMES MARWA,ALBERT MARWA NA WENGINE WOTE MLIOBAKIA,MUNGU AILAZE ROHO YA MARWA MAHALI PEMA.AMIN

    SINGIDA

    ReplyDelete
  2. Huyu Jenerali Kiaro ndiye aliyekuwa afande wa Kikwete au siyo? Raha sana! Sasa walipokutana hapo nani aliyepaswa "kubana miguu"?

    ReplyDelete
  3. Aliyebana miguu ni Kiaro kwa Commander of the Armed Forces!

    Lakini kaone kaa-Rais ketu...sa dhahabu tupu...miwani...dhahabu tupu kwa sababu TZ ni nchi ya tatu katika Afrika kwa kuchemichemisha dhahabu!

    Lakini kwa nini tunatiliam mkazo kuwa "Rais na Kamanda Mkuu wa Majeshi?

    Maana u-Kamanda huo tuliurithi kutoka kwa Waingereza.

    Ikiwa Jeshi ni Wizara ya Serikali, kwa nini tunaibagua hivyo?

    Huko Uingereza ni lazima Jeshi walibague hivyo kwa sababu Kamanda wa Majeshi ni Malkia sio Waziri Mkuu na serikali yake.

    Ni upuuzi huo huo wa kidplomasia wa kuita mabalozi wetu kwenye nchi za Madola, "High Commissioners".

    Waingereza ni budi wawaite hivyo mabalozi wao kwa sababu mabalozi ni wa serikali ya chama tawala na wala dio dola ya nchi "State".

    Waliitwa hivyo kwa sababau kabla ya kuwa Jamhuri, Malkia (State ya Uingereza) alikuwa anawakilishwa na ma-Gavana Jenerali na serikali ikiwakilishwa na High Commissioners.

    Tuache kutumia Kamanda wa majeshi kwani Jeshi ni Wizara tu na kila wizara iko chini ya Rais.

    Tuache kutumia neno High Commissioner" kwa mabalozi wetu!

    Naomba kutoa hoja!

    ReplyDelete
  4. Wewe michuziMisosi wa hapo juu mbona unajiuliza na kujijibu maswali wewe mwenyewe?? Hiyo sio hoja uliyotuma...tutaendelea kuwaita High Commisioners wakati tukiwa bado wanachama wa jumuiya ya madola...Tujivunie nchi yetu kwani Tanzania ni moja ya nchi pekee katika Africa wakuu wake wa majeshi wa zamani mpaka sasa wanaweza kukaa chini na kupiga stori...kama tungejali ukabila kama jirani zetu wa-kurya wangeshachukua nchi miaka hiyo...

    ReplyDelete
  5. Anoy wa Singida samahani kama ulikuwa huna taarifa, James Marwa alifariki dunia mwaka jana. Alipata mshtuko wa moyo kufariki few days later.

    ReplyDelete
  6. tunashukuru sana jamani kweli ulikuwa ni msiba mkubwa na pia anon wa hapo juu hata James Marwa na yeye pia alisha fariki yani baba kamfuata mtoto Mungu azilaze roho zao mahala pema peponi amina.

    ReplyDelete
  7. Bw.Michuzimisosi,naomba kurekebisha jambo kidogo tu:
    C.I.C = Chief In Command(Rais)
    C.D.F = Chief of defence Force(Generali)

    Kwa hayo mengine ya Kiitifaki uliyo yataja sijayaelewa,ila naona umejijibu mwenyewe hapo.

    ReplyDelete
  8. Nawashukuru wadau kwa kunifaamisha habari za james nawapa pole familia kwa misiba yote iliyowapitia.niko masomoni ulaya ndo maana mambo hayo yalinipita blog izidi songa mbele kwani yaleta mambo mengi

    Singida

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...