kila kukicha majengo mapya yanazidi kuchipua kariakoo. yaani wamatumbi hata sijui utuambie nini tuelewe. hii sehemu sio tu imejaa bali pia huduma za miundombinu yake haina ubavu kupambana na kuongezeka kwa majengo. yaani maegesho mapya hakuna, bomba za maji machafu na safi ni yale yale na hapo moto ukiwaka hata sijui faya litapita wapi. inatia hasira wallahi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hasira hasira babu...usipinge maendeleo kwetu Kariakoo,tuacheni sie wana Kariakoo tutatue maslahi yetu wenyewe bila ya kila 'tomu,diki na harii'kutuingilia ingilia...kama hukipendi kitongoji chetu basi rudi kwenu popote ulipojitokea na nauli tutakusaidia!!!walahi yakhe...

    ReplyDelete
  2. sasa nani wa kulaumiwa si kuna watu wa mipango miji na wanlipwa mishahara minono kwa kukaa chini tuu
    wanakula pesa za bure kabisa kwa infrastructure ni zile zile za mwaka 47

    ReplyDelete
  3. halafu kwanini bado wanajenga maghorofa kwa teknoloji ya mwaka 1920...yaani mitofali tuu,kwanza halipendezi na ni gharama kubwa,its time waanze kutumia steel & glass sasa maana ndio mambo,na hao watu city miundo mbinu inabidi mtu awashtaki mahakamani ili wasimamishe ujenzi kama huu mpaka wajenge miundo mbinu,hatari sana hapo kama kuna moto na wala hakuna parking,disaster in the making

    ReplyDelete
  4. weee mzungu mweusi...hizo teknologia unazozisimulia hapo,ziweke kwako kule ukimbizini,
    hapo Kariakoo hatuzitaki nasaha zako...

    ReplyDelete
  5. hilo bango lililoandikwa" TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA" Kwa kweli lanikwaza,bro michuzi hebu naomba uipost hii wadau waione na watoe comment,mimi naona kama vile linachochea unyanyapaa vile,je wale waliotayali na virus vya ukimwi na wenye ukimwi watafeel aje,ni kama wao hawatakiwi ktk jamii na they are bound to die!,sijui lakini ila kwa mtazamo wangu nadhani lingeandikwa "TANZANIA BILA MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI INAWEZEKANA",kwanini?,sababu wale wenye virusi na wagonjwa wa ukimwi wangeweza kutazamwa kwa umakini,kupewa ushauri,kujitokeza kwa jamii na kutoa ushuhuda juu ya kufanya ngono zembe na aina zote za maambukizi,then, serikali au taasisi binafsi au whatever wangeweza kuwatake care,kivyovyote ili hao waathirika wasiendelee kusambaza virus,kwa hilo bila shaka TANZANIA BILA MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUS VYA UKIMWI ITAWEZEKANA,.VP IMEKAAJE HIYO!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...