Kaka Michu,
Kheri ya Mwaka Mpya.
Napenda kumjibu huyo muwakilishi wa WU. Inabidi akili kwamba kuwa nchini kwetu bado kuna wafanyakazi wanaopenda kujitungia sheria mbali na maadili ya ofisi zao.
Hii inaweza kuwa either ni sababu ya rushwa au (dharau kwa wateja wao) kutaka kuonyesha kwamba wana power kwenye kazi zao bila kufikiria consequencies kwamba bila wateja hawawezi kuajiriwa kwenye hizo positions walizonazo.
Mimi ni mteja wa Western Union kwa muda mrefu, huwa ninatuma pesa sehemu mbali mbali nchini so far sijawahi kupata matatizo yoyote mpaka Ijumaa iliyopita nilipomtumia pesa mdogo wangu anayeishi Musoma.
La kushangaza ni kwamba amekwenda General Post Office ya Musoma wakaanza kumzungusha na maswali mengi. Bahati nzuri alikutana na mtu anayemfahamu akamsaidia kufuatitlia.
Hata hivyo hakufanikiwa kupata pesa walimwambia kuwa siku pesa zote zilikuwa zimetumiwa kiofisi na hivyo hawakuwa na pesa za kumpa akaambiwa aende Jumatatu.
Mimi hapa nimepata message kwamba pesa zimewasili na kwamba ndugu yangu anaweza kwenda kuzituchukua. Je itakuwaje Post Office itumie pesa ambazo si zao? Nimetuma pesa ili ndugu yangu atimize mahitaji yake itakuwaje yeye ateseke kwa kuinufaisha Post Office (Kama ni kweli ati P.O. inatumia pesa za watu) kitu ambacho siamini.
Nimemwambia kesho aende na kama hawatampa pesa zake anijulishe mimi nitawareport kwenye office ambayo nimetumia kusudi wafahamu kitu gani mnachofanya kama ma agents wao.
Kama tunataka nchi yetu iendelee, kila mfanyakazi anapashwa kuheshimu kazi yake na muhimu kuwaheshimu wateja watanzania wengu tuna kasumba ya kuwadharau wateja kuhudumiwa mpaka unyenyekee as if unahudumiwa bure.
Natumaini kama kiongozi wa Western Union utafuatilia huu utatanishi unaojitokeza kupitia kwa waajiri wenu from time to time.
Asante.
Mdau Ughaibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hizi habari za Western Union ni za ukiukaji wa haki za binadamu. Naelewa muelekeo wa mratibu wa Western Union wa Tanzania, lakini hata hivyo kasumba na ukiritimba kama huu haujamtokea bwana Mwakidila peke yake, imewatokea wengi mimi ikiwa mmoja wapo.

    Na yote hayo maamuzi ya ajabu ajabu, kuwatopatia pesa wapokeaji au kusumbuliwa kwa kutuma pesa watumaji, yanasababishwa na Western Union Marekani, kwenyewe.

    Je unajua kama ukituma US Dollar 1000 au Euro 1000, unatakiwa kutoa copy ya passport, ambayo jina lako linakwenda disclosed to FBI, na government agency za Marekani, kabla ya kuweza kupewa go ahead kwa Western Union, kurelease pesa zako, kwa mpokeaji au kupata refund back.

    Na hii yote, inatokana na Western Union, kujaribu kuaccomadate hizi sheria za ajabu ajabu, ijapokuwa wewe si raia wa Marekani, unakuwa subjected to this stupid behaviour by Western Union, Tanzania Western Union, they cannot do anything about this. the only way foward ni kuboycot services zao.

    Kama watadeny haya, basi Western Union wa Tanzania watoe statement kupinga hili kama haya ninayoongea ni ya uongo.

    Yote haya ni kuhusiana na vita dhidi ya Ugaidi, aambiwa. Uhuru, haki ya mtu unadhalilishwa bila kujali.

    ReplyDelete
  2. Mdau wa Ughaibuni nakubaliana na wewe kabisa.

    Actually nimemuandikia Ndugu Tawa Ujumbe binafsi kumwambia hili. Nimeisha pata tatizo kama lako kwenye ofisi ya Western Union za Arusha na Mwanza. Kuna rafiki yangu tunaishi naye huku nje ameniambia tatizo hilo pia limezidi Western Union Musoma. Business model ya Western Union ni kwamba pesa zinapatikana mara moja. Sasa inakuwaje mpokeaji azungushwe? Hivi ni lini benki ya posta itabadilika? huu ni mwaka 2008. Ile tabia waliyokuwa nayo wakati mtu ana account ya WADU bado ipo.

    If Postal Bank in Tanzania fails to live up to Western Union standards in some of their branches then they should not be allowed to even put a Western Union sign on those branches, let alone claim they can offer service

    I believe payment delays by some of WU branches in Tanzania is the biggest single but widespread problem that will drive customers away.

    Mambo ya vitambulisho vya mtumaji was just an isolated anomaly.


    MbebaMabox@yahoo.com

    ReplyDelete
  3. Mdau napaswa kufahamu kuwa WU hawatumi pesa taslim kwa wakati unapotuma pesa, isipokuwa mawakala wanapswa kulipa wateja kwa pesa waliyonayo wakati huo na baadae wanajua jinsi wanavyomalizana. Suala hapa si kwamba P.O wametumia pesa yake isipokuwa wakati mteja alipoenda kuchukuwa pesa alikuta hawana, na hili siyo suala geni kwa P.O kutokana na hali yao ya kiuchumi na hasa kwa ofisi ndogo kama Musoma. Hata wakati wa kutuma T.M.O za ndani hili tatizo ni maarufu.

    Mdau nilie ughaibuni

    ReplyDelete
  4. Jamani mimi sijawahi kupokea Pesa kupitia western union wala money gram,huwa natuma kupitia WU.Swali langu ni hili hivi mtu anapopokea pesa anachajiwa wakati MTUMAJI pia anachajiwa kutuma pesa?

    ReplyDelete
  5. hili suala la western union lipo pia money gram kwani nimetuma pesa before chrsmas kwa ajili ya familia yangu na alipokwenda kuchukua pesa pale exim bank mwanza aliambiwa hawajapata maelezo yoyote arudi kesho na alijaribu kunipigia na nikamweleza kumpatia huyo aliyemwambia simu ana nikaongea naye na kumwambia nitaongea na meneja na asipoangalia atafutwa kazi akasema basi asubiri kama dakika 15 atapata pesa na kweli alipata pesa kwa hiyo hawa watu huwa wanataka tu kumbabaisha mtumiwaji na wao wanatumia wao hili halitakwisha

    ReplyDelete
  6. Jamani hawa western union mfano Arusha wanamatatizo sana na inauthi sana.mimi nilishasumbuliwa sana na hela nilizotuma kwa mama yangu walimsumbua almost a week!nilipoteza muda mwingi sana kwenye simu kuongea nao na tangia wakati huo nimeacha natumia Moneygram they are even cheap
    you can send up to $500 for 9.99
    and exchange rate is better than western union. you should check it that out.
    mdau Canada.

    ReplyDelete
  7. Ndg,
    Tatizo sio la uongozi wala taratibu za WU.Tatizo ni kuwa huwa hawasomi sanduku lao la maoni au wana undugu au sababu ya kuwa favour wale cashiers wao-mfano ni wa hapo Extelcoms.
    Mimi binafsi niliisha waandikia mara kwa mara kuwa kwanini wanahusisha mambo ya uhamiaji na utumaji au upokeaji wa pesa.
    Niliwahi kuulizwa visa ya mke wangu anayeishi nje ambako ni kwao na mimi nilikuwa namtumia pesa ya watoto.Kwa ufupi huwa wanatafuta njia ya kula rushwa na ikiwa ndio ilikuwa siku za kukaribia mwaka mpya utaulizwa hata maswali ya trafiki.Huyo anayejibu hawezi kuyajua au hataki kuyajua, lakini kuna karaa nyingi pale haswa ukizingatia mara nyingi pesa za WU huwa ni za kuokoa jahazi mtu unakuja kumpa baada ya masiku-hilo balaa linakuwa bado linasubiri tu???

    ReplyDelete
  8. Jamani nitaenda nje kidogo ya mada, japo suala ni hili hili utumaji pesa nyumbani.

    Mimi nipo ughaibuni nabeba box, nilikuwa natuma pesa kwa Western Union zamani, honestly sijawahi pata tatizo labda vile pesa ninazotumaga huwa kidogo, sijui.

    katika harakati za kutaka kusave, nikaongea na home wafungue foreig account (USD), wakafungua Benki moja hivi (jina kapuni) mi ntakuwa nafanya online transfer basi.

    Noma yake ni kwamba, sometimes pesa zinachelewa mnoooo kufika (sijui ni kweli yarabi)? Na mbaya zaidi, kwenye account yangu inaonyesha kabisa pesa zimetolewa siku kadhaa, address na kila kitu sahihi, lakini wakienda chukua pesa wanaambiwa hazijaingia bado! Sasa wajame, hizi pesa zinakuwaga wapi tena na kwangu zimeshatolewa na ABA, SWIFT Code na kila kitu niliweka sahihi jamani?

    Jamani nitoeni ushamba isije kuwa nalalamika bure. Je na wengine mnapataga shida kama mimi au basi tu? Nisaidieni jamani manake japo nasave kiaina, ndugu zangu wanaumia kwani sometimes inachukua wiki tatu eti pesa hazijaingia!!!!!!!

    Mdau bahili

    ReplyDelete
  9. jamani hata kama uchumi mbovu P.O wanasikitisha sana mimi nikiwa bado hapo dar nimetuma hela express many times baada tu ya kusainiwa na officer unaambiwa hakuna mawasiliano.pesa siku nne ndani ya nchi.jamani tupunguze utanzania twende kibiashara zaidi.tutafika?nikifananisha makosa yanayozuilika tunayofanya na ughaibuni nabaki kuangua kilio

    ReplyDelete
  10. Nadhani hii inatokana na hii huduma kutolewa na Benk moja tu,huku nje kila Benk inatoa huduma ya western union.Kukiwa na kila Benk inatoa hii huduma hakutakuwa nakulinga linga kwa kisenge wako wafanya hao watoa huduma wa hicho ki-benk cha posta.

    ReplyDelete
  11. TANZANIA KILA HUDUMA NI FINYU. MTEJA HANA HAKI HATA KAMA UNATOA PESA YAKO KUHUDUMIWA, OUR CUSTOMER SERVICE IS ZERO 000 KILA MAHALI HATUNA KABISA DESTURI YA KUMTUMIKIA CUSTOMER HATUNA KABISA KILA UNAPOKWENDA SI MAHOTELINI SI BANK SI SOKONI. INASIKITISHA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...