Bwana Michuzi,
naomba unifikishie ujumbe huu kwa watanzania. mimi ni mdauniko ukerewe(uk).
Leo nimeenda western union kutuma hela ziende nyumbani kunadharura na nikaona nifanye ivyo haraka iwezekanavyo nikatuma hela leoasubuhi mnamo saa tatu na na nusu (saa za uk) nikampigia sm mama akazichukue, nae kwa bahati nzuri alikuwepo mjini posta (tz) Extelecoms Annex, Samora Avenue.
Lakini cha kushangaza walitaka copy ya passport yangu,nikajiuliza copy ya paspot ya nini tena? lakini kwa kuwa hela ilitakiwa haraka sikuwa na la kufanya nikaenda home nikachukua copy nikaituma kwa njia ya fax.
Copy ya passport yangu ina picha na tarehe ya kuzaliwa nafikiri ukurasa wa mbele wapassport yetu tunaufahamu wote Baada ya muda mfupi akanipigia simu mama kwambawamekataa wanataka visa.
sasa visa mimi passport yangu nimeituma home office hata kama nikiwatumia itawasaidia nini ? na muda wake umeisha nimetuma kwa ajili ya kurinew visa. pili kwenye web site yao wametoa maelekezo yafuatayokwa mtu anaetakiwa kuchukua peza afute maelekezo yafuatayo:
What do we need to collect our money?
Name of the sender jina nimemtumia
Country / City of transfer's origin nchi yangu niliko hali kdhalika
Expected amount of money to be received kiwango pia nimemtumia
Valid ID and the Test Question Answer
yeye pia anayo copy ya passport amekwenda nayo.
kwa anaye pokea ndio anatakiwa awe na vitu hivi ama sio. imenisikitisha sana bwana michuzi na nashindwaa kuelewa Tanzania paka leo kuna habari ya rushwa?
ni hayo bwana michuzi.
shukran sana
Email yangu mwakidila@hotmal.com
ni mdau mwakidila ally wa uk


Hii ni kali sana.Pole mdau. Mie natuma pesa mara nyingi na haijawahi kutokea hata mara moja nnaowatumiwa kuambiwa walete copy ya passport yangu. Inawezekana hao jamaa wa posta walikuwa hawana hizo pesa na katika janja yao ya kupoteza muda ndio wakaona wazungushe namna hiyo.
ReplyDeleteInawezekana pia hao western union wamechoka.Dawa yao ni kuwatumia jamaa wanaotuma pesa kwa njia ya binafsi. They are very reliable.
Hi
ReplyDeleteMimi ni Mtanzania niishie Columbus,Ohio na hivi karibuni nimetuma hela nyumbani kwa ajili ya Sikukuu kwa Kutumia Western Union.
Kwa kweli sijui kesi yako ikoje lakini sidhani kama hawa jamaa wa Western Union wana haki wala mamlaka ya kuomba nyaraka zozote zaidi ya majina,addresses and details za kawaida kwa ajili ya kutuma fedha.Kwa kesi yangu wala hakuna nyaraka yoyote waliyoniuliza.
I guess you might wanna check with their customer services department.
Nice Day
Bwana Mwakidila pole sana kwa hilo.Kwa kweli hapo ni pagumu na hata sijui nikupe ushauri gani labda alternative ya kutuma pesa nyumbani next time.
ReplyDeleteNadhani hilo sio suala la rushwa ila ni utaratibu wa hao Wetsern Union kwani nami yalishanikuta na hata nilipowatumia copy ya visa walisema imekwisha wakati wake.(mimi ni mwanafunzi),hawaelewi kitu chochote kuhusu I-20 (kwa US).
Baada ya hapo nilighafirika na ndipo mtu mmoja akanijulisha kuhusu MoneyGram,hawahitaji vitu vyote hivyo and since then I have never been back to Western Union.
Kwa hiyo you may try MoneyGram,sijui inakuwaje kwa UK,lakini kwa US ni bei rahisi,unaweza kutuma hadi $500 kwa kama $10.Unaweza ku-google uone.
Kitu kingine ni kuwa unapotuma pesa nyingi ndivyo maswali yao yanavyoongezeka na hizi ni sheria walizopewa kufuatia mambo ya ugaidi.
Sam.
Usiumike kichwa biashara ushindani.sikunyingine tumia MONEY GRAM . Hawana usumbufu kama uo
ReplyDeletepole sana ndugu yangu ya kwa usumbufu uliokupata,yaani bongo kuna urasimu usio maana hata kidogo, nami leo asubuhi nimetuma pesa kwa western union kwenda marangu, niliyemtmia alipofika ofisi za western union wakamwambia kuwa hawana pesa za kumpa labda ajaribu jumatatu,yaani imekuwa kama posta zamani. sijui kama ingekuwa ni dharura ingekuwaje, kwa kifupi suala zima la utoaji wa huduma bado lipo kwenye kiwango duni mno huko nyumbani, kwa mfano NBC wana ATM sehemu mbalimbali lakini utakuta nyingi hazifanyi kazi hivyo mtu anabidi afunge safari aje posta makao makuu ya NBC. Vitu kama hivyo ndivyo vinavyotofautisha nchi za dunia ya tatu na zile zilizoendelea
ReplyDeleteKama umetuma zaidi ya dola 999 unaweza kupata usumbufu kama huo.Hayo yote yalianza baada ya 9/11.Lakini kama umetuma kidogo tu na bado unapata matatizo kama hayo basi hatuna budi kuhoji.
ReplyDeletewe mwakidila, next time ndugu yako akiulizwa ku-provide vitu viinyomake sense, wapigie simu na uwaambie kuwa utawaripoti makao makuu, usikubali kuwa mlaini, sasa jamaa hao unawaamini vipi mpaka unawatumia passpoti yako(copy)?
ReplyDeletetanzania nyodo yu....waspanish wanatuma hela hawana hata id huku bahati yako huko una passiport
ReplyDeletewanataka visa wao wamekua immigration officer?
nashangaa kwanini wengi bado mnatumia western union...sioni kama ni cheap kwa vile kule bongo mtu analipwa na fee wanachukua tena...tumia crdb mwambie mama awe na foreign account ....mweee hiyo ukiweka hela ziende wanacharge dollar 15 tu bank yangu per transaction halafu bongo hela inaonekana kwenye account yake the same na kama akitoa kidogo leo wanampa kwa rate ya siku ya leo na kesho kwa rate ya keshi etc....halafu siku hizi na transfer kwenye pc sio lazima niende bank...
....achana na wajinga badala ya kufanya biashara wanakua ofisa uhamiaji
Pole sana mdau Mwakidalu kwa kero uliyoipata.Ninavyofahamu ni kwamba kuna utaratibu mpya katika kutuma pesa nje ya nchi.Utaratibu huo upo kwa muda sasa.Serikali ilianzisha utaratibu huo kwa lengo la kuthibiti utoroshwaji wa fedha za kigeni nchini Tanzania na pia kuthibiti matumizi ya pesa hizo zisitumike kwenye biashara haramu.Kwa hiyo,pindi ukitakiwa kutimiwa pesa kutoka nyumbani ni lazima utume nakala ya pasi ya kusafiria ukiambatanisha na ujume mfupi unaoelezea lengo la hizo pesa.Binafsi nilishangaa nalipotakiwa kufanya hivyo nilipokuwa nitumiwa pesa.Niliambiwa nifanye hivyo,niliona ni kero lakini nililazimika kufanya hivyo baada ya kuridhika na hoja za serikali.Kwa hiyo nimekuwa nikafanya hivyo kila nipotumiwa pesa.Na hakuna suala rushwa hapa mdau,ni utaratibu tu.Lakini kitu kipya nilichokiona kwako ni kwamba wewe ulikuwa unatuma pesa sio kutumiwa kama mimi.Sasa hapa sijaelewa madhumuni halisi ya kufanya hivyo.Maana sasa wewe unaingiza pesa za kigeni nchini Tanzania na sio kwamba kuzitoa nje.Nitafuatilia kuelewa lengo la utaratibu huu mpya wa mtumaji kutuma nakala ya pasi ya kusafiria.
ReplyDeleteMdau,Tumsifu Mwasamale
Bowling Green State University,Ohio-USA
Pole sana Ally hawa watu niwapumbavu sana kulikuwa hakuna sababu ya yote hayo labda wanataka posho kama kawaida yao wapenda jasho la watu,nilienda bongo juzi juzi yaani umelipia parking ,parking attendant anataka tena chochote kitu eti amekuangalizia Gari ,benki eti ili huduma ufanyiwe haraka uache kitu tena nakumbuka hata sura ya huyo dada wa benki ,Airport zile trolley zote wameshika wale attendant wanasema shilling 1000 kukutolea mzigo nje inabidi uwape maana unamizigo na trolley zote wamehold wao na nguo zao za brown so. nchi inabidi ibadilike sasa
ReplyDeleteKwanza kabisa na kupa pole.Tz wanasumbua sana kila mtu hanakaa kwenye kiti Ofisini Hana weka mdomo juu.mimi mwenyewe pale huwanja wandenge wanawake wanakaa pale wananiuzi sana.wakikuona tu hunatokea wanahanza kuweka midomo juu kama hunanuka mazi.
ReplyDeletedah! naona wewe umetuma western union tawi la immigration!! wakatie kidogo ndio mambo ya nyumbani mishahara haitoshi!!!
ReplyDeleteBwana michuzi hapa kuna walakini, mi niko UK pia na nimekuwa nikituma pesa sana tu TZ kupita huduma hii hii lakini hatasiku moja ninaowatumia hawajawahi kuulizwa passport yangu, mi pia nikiwa TZ wakati fulani kunarafiki yangu alinitumia pesa nyingi tu na nilichukulia pale ubungo kwenye jengo jipya nadhani linaitwa UBUNGO PLAZA, sikuulizwa passport ya aliyenitumia.
ReplyDeleteKuna mambo mawili, labda wamebadili sheria baada ya 31 Dec 2007, au Lah, huyo waliomkuta ni mtumishi mpya anajifunza kazi. Au huyu jamaa yetu wa UK anataarifa zenye walakini, kwa nini wahitaji VISA?? nachojua visa ni wakati wa kutuma tu, hata hapa UK lazima uonyeshe passport wakati wa kutuma kama ni pesa nyingi.
Nachomshauri jamaa alitakiwa kuwakolomea, angewapigia simu moja kwa moja western union. Maana kunarafiki angu yuko america aliwahi kutumia money order Twiga ndio wanamchezo huo wa kijinga wa kusumbua watu, mara vitambulisho mara hawaamini na sio western union. Sasa jamaa aliwapigia simu na akawambia kama hawampi pesa huyo ndugu yake anakwanda cancel azichukue pesa zake, ndio wakampa huyo ndugu yake Bongo. Unajua watu wengine home utadhani wameenda shule kama fashion tu, hata haziwasaidii.
Pole sana mdau wa UK, na nyinyi ndugu zangu mmezidi mbwembwe usikute umewatukana au umewadharau ndio wanakuonyesha sasa.
kweli bongo tambarare.Yaani wanataka mtowe rushwa kupata pesa zenu wenyewe.Huu ndiyo upuuzi wa nyumbani,hakuna kitu kilicho straight.Rushwa imeshakuwa ni desturi kwa maisha ya home.Halafu kuna mijitu inaendelea kusema bongo ipo kama Marekani,huu upuuzi haupo kabisa huku.
ReplyDeletePole sana kwa usumbufu ulioupata. You are not the only one with such a bad experience with Western union Dar. Mimi binafsi nimeamua kuacha kutumia service yao kutokana na usumbufu na karaha walizonazo. sikuhizi natumia bank transfer. Haina usumbufu na pia hawachaji pesa nyingi kama Western Union plus, mtu unayemtumia pesa Bongo anapokea transfer in $ not in TSH.
ReplyDeleteKijana kwanza pole sana kwahilo.Mwambie mama aende akachukue jina la mtu aliye muatendi(CASHIER)hapo w.union/acheck receipt.Hayo ni mazingira ya rushwa ya lazima.Halafu tuwasiliane ili tabia kama hii isije ikajitokeza tena.Mtu unapotuma pesa sehemu yeyote ile Duniani haitakiwi mtumaji kuproduce docs zako ila mpokeaji waweza kuombwa extra docs kama amount ni kubwa au ni regular receiver.yawezekana wamefanya hivyo ili NEXT TIME wakuwahi hizo pesa zako kwani yawezekana kabisa mama ni regular receiver.u have to be very careful.Naomba hilo jina la Muhisika,time service offered ili tuweze kukomesha hii tabia. maddidy@hotmail.co.uk
ReplyDeletemwakidila umeandika baadhi tuu ya maelekezo nnavyo fahamu mimi ukituma pesa kiasi kikubwa lazima uonyeshe valid passport na mpokeaji pia awe na valid ID maelezo ya kiwango yamo kwenye leaflets zao,kwa maelezo yako ulipeleka copy not original,original iko home office kwa ajili ya renewal,ina maana huna ID.Si dhani kama kuna rushwa inapo kuja swala la western union.
ReplyDeleteBwana Mwakidila, Pole sana ndio maana sisi wengine tunaona bora kutumia wapemba rate ndogo na kutuma fee ni £2 tu, kuliko hayo mambo ya visa etc Njaa sana bongo!!
ReplyDeleteHuyo muhudumu aliekua anatoa huduma ni mzushi tu. Mie nilituma pesa majuzi tu na ikapokelewa kwa kutumia kitambulisho cha kujiandikisha kupigia kura tu (unajua tena katika nchi kanchi ketu ka bongo... wenye passport ni wale waliotoka nje ya nchi tu na ndugu zangu wasio na kazi rasmi vitambulisho vya kazi ni msamiati. Nimekumbuka enzi zile mtu alivyokua anajitambulisha kwa kutumia kadi ya chama!! teh teh!!!.
ReplyDeleteWestern Union hapa nilipo waliniambia kua hakuna hata haja ya kuuliza swali bali kinachotakiwa nimpe neno la siri tu na yeye akilitaja anapatiwa pesa yake.
Hata hivyo walimsumbua kidogo kuhusu kukosekana kwa hilo swali... wabongo bwana kwa kukariri vitu!!!
Mripoti huyo anaeharibu biashara za watu akome ujinga wake!!
Du pole sana mdau wa Ukerewe, hata na mimi naomba nikuunge mkono kwa hilo, maana si wewe wa kwanza kulalamikia hilo, sijui Bongo kuna nini????, mie nilituma fedha siku chache kabla ya Xmas, Tarime licha ya kwamba huduma ya western union ni masaa 24, lakini, ndugu yangu huyo alizungushwa, mara hela haipo, mara mtoa hela hayupo, mara njoo kesho, yaani alienda zaidi ya mara nne na hatimaye alipata pesa baada ya wiki moja!!! Wakati ukishatuma hela kwa western union unaweza kuitrack, mie niliangalia kwenye mtandao ikanionyesha pesa imefika inasubiri kupokelewa!!
ReplyDeleteBinafsi mie naona ni baadhi ya wafanyakazi wa W.Union bongo ambao kwa sababu ya njaa zao, wanatengeneza mazingira ya rushwa. Kutoa COPY ya PASSPORT ya mtumaji pesa HILO HALIPO!!!!
Pole sana mkuu!!!!!!!!
uwiii jamani huu ndio ukimwi.
ReplyDeletewajameni nimetumiwa hii leo nimecheka.....http://www.youtube.com/watch?v=qgcZAE1ULYI&feature=related
hayo ni maajabu ya rajabu, your passport na hiyo visa ni non of their business. Cha muhimu ni identity ya mpokeaji. Labda jamaa walitaka wapewe kidogo ndio maana wakaamua kumsumbua. Vipi iliishia wapi?
ReplyDeletehey, pole na habari yako. I am not suprised though!! Typical Tanzania. I would have called hao western union bongo, perhaps imemkuta mtu bogas. You should have called uwaeleze. I know couple of people have been asked to provide letter inorder to receive money kwasababu ya the so called 'MONEY LAUNDERING w
ReplyDeleteMDAU ACHANA NA WESTERN UNION TUMIA MONEY GRAM HAWANA HAYO MALOLOSO NA CHARGE YAKE NI RAHISI A HALF THE PRICE YOU WOULD PAY AT THE WESTEN UNION.MIMI NIPO US NA NINATUNIA HIYO NJIA NA HAKUNA USUMBUFU WOWOTE WALIOPATA HUKO TZ.NENDA KWENYE POSTAL OFFICES YEYOTE HAPO UK AND THERE UR COZ YOU WILL B AMAZED
ReplyDeleteHiyo sijawahi kusikia. Piga western union (ya mtoni of course) waeleze. Hao jamaa watachukuliwa hatua kali kweli kweli Au unaweza kula bingo la kulipwa fidia kwa usumbufu.
ReplyDeletePole ndugu yangu, thats weird!
ReplyDeletemmh, hii kali. Anyway, hivi bado watu mnatuma pesa Bongo na Western Union au Money Gram??? Fungueni checking account mpya, tuma ATM card nyumbani. ATM zimejaa Bongo, as long as ina visa logo mtu unaweza toa hela sehemu yoyote duniani. Na the only fee unayolipa ni ya kutoa hela kwenye bank nyingine kama kawaida ambayo bank nyingi ni $2. Unaweza kutransfer pesa online kutoka account moja mpaka nyingine, so hata usiku wa manane you can do it na hela zinakuwa available right away. Na ukideposit pesa kwenye branch zinakuwa available right away. naona hiyo ni njia rahisi, Unless uwe unatuma pesa nyingi zinazobidi zitolewe zote maana Bongo limit nadhani ni Tsh 400,000 a day, so multiple withdrawals charges zitakuwa nyingi.
ReplyDeleteWestern Union mpokeaji/receiver wa pesa anapokea pesa kwa kitabulisho chake sio cha aliyemtumia/sender. Hamna mabadiliko yeyote, sio 9/11 au vinginevyo. Na kama kiwango ni kikubwa say zaidi ya $1000 kwa USA mpokeaji anatakiwa ajibu swali la siri ambalo mtumaji atakuwa amemwambia mpokeaji. Under no circumstance whatsoever kitambulisho cha mtumaji kinahitajika kama ulivyoambiwa wewe. Inabidi tu mpokeaji afahamu jina kamili la aliyetuma pesa pamoja na MTCN number.
ReplyDeleteNINAKUTAADHARISHA Hapo ulipotuma nakala ya ukurasa wa passport yako wamepata taarifa zako zote [HAWAPASWI]. Kitakachofuatia ni wao kukuliza/kukuibia pesa utakapotuma tena.
Huku viwanja vikubwa America, Western Union wala hawahitaji hata kitambulisho chako wakati wa kutuma pesa. Wanataka tu anuani yako na namba ya simu [Watapata information zako kutumia anuani na number ya simu kama watakuhitaji].
Ni muhimu pia watumiaji wa huduma mbali mbali kama Western Union au MoneyGram tujue haki zetu lasivyo unaweza kusumbuliwa bila sababu na wewe usiweze kuhoji kwasababu hufahamu. Kusumbuliwa kunakuja ama kwasababu mhudumu ana hila zake [njaa na wizi] ama pengine ni kutoelewa kwake.
Usumbufu wa Western Union ambao naufahamu mimi ni ule wa uliyemtumia pesa kutopewa hizo pesa maramoja. Anazungushwa maramoja hali ambayo pesa zinakuwa zimefika immediately. Yanakuwa ni mahesabu ya kutoa na kujumlisha tu kwa matawi ya Western Union
Ushauri wa Bure
Kutatua hili nilimpelekea mzee wangu ATM card toka huku ninakobeba mabox akae nayo kwa matumizi ya kupokelea pesa, kwavile anapoishi yeye ni karibu na ATM Machine ya NBC. Ikibidi kutuma pesa nazi deposit huku alafu namwambia akazichukue kiasi gani kwenye ATM kule bongo. Ina cost about $3 per withdrawal, Much much cheaper.
MbebaMabox@yahoo.com
CHONDECHONDE Wadau.
ReplyDeleteTafadhali msiniripoti.Ni mimi mfanyakazi wa western Union.Sikuwa na jinsi ndugu zangu.Mnisamehe nimekosa.Familia baba na mama wananitegemea mimi.Nikifukuzwa kazi da washikaji,nitaaibika.
Wasalaam
Pole sana kaka, Michuzi keep it Up, sijawahi kuandika comment hapa ila hili limenikuna. Hao watu ni wababaishaji .Kaka Michuzi mie nakuomba fanya jitihada zako binafsi(mtu mkubwa wewe) tupate jinsi ya kufikisha kero kama hizi japo magazetini ili watu wasuse huduma zao na pia waumbuke na waboreshe huduma zao au wakose wateja. Mimi nimetuma hela mara kibao bila kupata kasheshe yoyote . Inaudhi sana maana mtu anasaidia watu huko harafu wanaleta za kuleta. Watu wengine nilio na usongo nao ni TRA ukituma ka mzigo kadogo tu ushuru unazidi thamani ya mzigo. tusiwalazie damu watu kama hawa itoe hiyo habari gazeti harafu umtaje jina mhusika maana wametuchosha na sheria zisizo na kichwa wala miguu. Mzee Kikwete anasema walio nje mkumbuke kusaidia nyumbani sasa hapo mtu asaidiaje anapotumia hela kwa mzazi wake harafu jasho linamtoka . Baba yangu alinambia yaani ukitumiwa kitu inakuwa kama umepewa adhabu , mambo gani hayo. Kaka michuzi tunakuaminia .Pole Kaka usife moyo kutuma .
ReplyDeleteKuna point ambayo wadau mnamiss .Katika xperiensi yangu ya kukaa na kusoma mamtoni(unyamwezini),baaada ya 9 November unapokwenda kutuma pesa ,jina likishaingizwa kwenye komputer kuna agencies nyingi , goverment and non-goverment wanaona na wanaonanisha na majina ya watu wanaowahitaji au kuwatamani.Sasa kama jina lako litakuwa linafanana, process yako ya kutuma pesa either itakuwa denied au itakuwa ndefu.Kwa hapa US Hatuna mambo ya kuulizana passport au visa ,Hapa ni mambo ya Driver`s licence .Agencies can pull all other infos they need from the licence , sio mambo ya michosho kama ya UK.Sasa huyu rafiki yetu wa Uk kuna factors nyingi zinaweza kuwa involved.mdau ,VA
ReplyDeleteBWANA MWAKIDILA POLE SANA, HILO SIO TATIZO LA BONGO NI WESTERN UNION WENYEWE.MIE YALIKUWA HIVYO HIVYO KAMA WEWE NILITUMA PESA NYINGI UGANDA NA WALITAKA VITU HIVYO HIVYO.
ReplyDeleteNI KWAMBA WATU WENYE MAJINA YA KIARABU(YA AKINA OSAMA)WANAKUWA WANATAKA I.D. ILI UINGIE KWENYE DATA ZAO.KWA HIYO HILI SIO TATIZO LA BONGO NI LA WESTERN UNION .TOKA SIKU HIYO NATUMIE PESA KWA LOCAL SENDERS WA KITZ HUKU UK.POLEEEE.
Michuzi bwana hii glob yako inaniuzi mambo mawili.
ReplyDeletePoint 01
Mtu akiweka web au link huku kwenye comments haitokei kama link na wala hai-copy-ki, matokeo yake inabid mtu ufungue webingine then uanze ku-type hiyo link.
Mfano kama hi hapo juu ya YouTube nimeshindwa kuipata kabisa
Point 02
haya maneno ya WORD VERIFICATION mi wala sioni faida yake, kwan kuna watu wanayewezea na tunaona spelling mistakes kibao tu.
Bonus Point
Aisee su uiweke hata mtu aweze ku-bold, italic, underline mzee wa uganda?
Embu cheki cheki mkuu wangu then mambo yakae sawa wachangiaji tiendelee na rubudani,
Asenti
kIJANA usijaribu kutuma pesa kwa wapemba £2 kwa amount yeyote.NI VIBAKA WA RATES.ukilinganisha na w.union au money gram.Utapoteza pesa nyingi sana na wala hakuna security kwani hakuna send/receive form.hao ni wa zuri kwa vibaka tu wanaotuma pesa za bila jasho.
ReplyDeleteBwana MICHUZI, habari ya siku nyingi. Mimi ni Kiongozi, na mwanzilishi wa huduma nzuri ya Western Union Money Transfer, Tanzania. Tuna zaidi ya Miaka 10 kwenye huduma hii hapa Tanzania. Habari hii ni ya KUSIKITISHA NA IMELENGA KUPOTOSHA ukweli kwa wanaotajia kutumia huduma hii baadae. Wale waliokwisha itumia, IKIWA NI PAMOJA NA BWANA MICHUZI, watakubaliana na Mimi kuwa MPOKEAJI HATA SIKU MOJA haombwi KITAMBULISHO cha Mtumaji. Mpokeaji huhitajika kufanya MAMBO MATANO yafuatayo ili apokee hela. 1)Awe na kitambulisho halishi chenye picha, 2)Ajue jina la mtumaji,3) Ajue kiasi kilichotumwa angalau +/-10%ya kiasi alichotumiwa, 4)Ajue hela zimetoka nchi gani, na 5) Ajue jibu la swali ambalo mtumaji amemtungia. Haya yote Bwana Mwakidila naamini aliambiwa na Ofisi alipoenda kutuma hela afanye nini ili Mama apokee hela baada ya kutuma, na nakala yake anayo. Hata kama alipata taizo, alipaswa aende alipotumia hela ili kujua ukweli wake muda ule ule. Hata hivyo, anaweza kupata uhakika kupitia kituo chochote che Western Union au website hii "www.westernunion.com"..angalia taratibu za kutuma au kupokea hela "Tanzania". Kila nchi imetoa taratibu zake, ambazo hazifanani kwa nchi moja na nyingine...hasa ukilinganisha nchi za mabara mengine na Africa...CHUNGUZA.
ReplyDeleteUSHINDANI. Bwn Michuzi dunia ya sasa ni ya ushindani, isije ikawa inalenga kitu kingine zaidi.
Huduma ya KUTUMA na KUPOKEA hela Kupitia Western Union na MoneyGram kwa Tanzania MASHARTI na TARATIBU ni zile zile, kimsingi. Wote ni MABENKI na tunaongozwa ni SHERIA za fedha chini ya Benki Kuu ya Tanzania. Hivyo,alichokieleza Bwana Mwakidila hakipo katika taratibu za kupokea hela kupitia huduma hii.
OMBI: Namuomba Bwana Mwakidila atusaidie kujua undani wa jambo hili kwa kuwasiliana nasi moja kwa moja, au atupe namba ya simu ya Mama hapa Dar es salaam, ilituweze kulifanyia kazi kwa manufaa yetu wote. Labda ni kitu kingine kimejificha hapa!!!!!Kicha atueleze kama Mama alilipwa au nini kilifuata baada ya hapo.
HITIMISHO: Namuomba Bwana Mwakidila awasiliane nasi kupitia namba za ofisi alikotumia hela, ziko nyuma ya fomu aliyopewa, au kwetu (Tanzania) moja kwa moja.
Nawaomba WA-TZ wote mtume hela nyumbani, tusaidie ndugu, jamaa, rafiki na familia zetu, na Taifa letu changa la TANZANIA, KUPITIA HUDUMA NZURI YA WESTERN UNION.
TAWA,KPR
"tawa@postalbank.co.tz",
We uliyetumiwa hiyo link ya youtube, kwani huwa huangaliagi sinema za kipopo? Hiyo ni part ya moja ya sinema zao! Jenga tabia ya kuangaliza sinema za kipopo utakuwa unacheka sana!!!
ReplyDeleteHATARI NYINGINE AMBAYO WADAU HAMJAIAINISHA NI KWAMBA INFO ZAKO ZA PASSPORT WANAWEZA KUZITUMIA KUFOJI PASSPORT ZA BANDIA....
ReplyDeletePengine hiyo ni changamoto kwetu Watanzania popote tulipo kuiga mifano ya wenzetu Nigerians+West Africans,Wakenya,South Africans,Zimbabweans+nchi kadhaa za Afrika ambapo "wajasiriamali" wanaoishi ughaibuni wamekuwa wakijihusisha na utumaji wa fedha ,mizigo na hata topping-up credits kwenye simu.Simlaumu mtu lakini kuna ukweli kwamba sie wenyewe ni sehemu ya tatizo hili:utegemezi wa taasisi (kama western union) ambazo hazijali sana ukiwachunia kwani wanajua wenzio watakwenda kufata huduma yao,contrary to mjasiriamali ambaye survirval yake inategemea ujio wa wateja wake kila siku.
ReplyDeleteWapemba wanajaribu kwa namna flani katika baadhi ya maeneo ya UK lakini bado hawajawa established kihivyo.
Anon Sir b the g
ReplyDelete--- nanukuu kauli yako ---
Michuzi bwana hii glob yako inaniuzi mambo mawili.
Point 01
Mtu akiweka web au link huku kwenye comments haitokei kama link na wala hai-copy-ki, matokeo yake inabid mtu ufungue webingine then uanze ku-type hiyo link.
Mfano kama hi hapo juu ya YouTube nimeshindwa kuipata kabisa
Point 02
haya maneno ya WORD VERIFICATION mi wala sioni faida yake, kwan kuna watu wanayewezea na tunaona spelling mistakes kibao tu.
Bonus Point
Aisee su uiweke hata mtu aweze ku-bold, italic, underline mzee wa uganda?
--- mwisho wa kunukuu ---
Majibu:
Point 01 - Ni kweli link huwa haitokei kama link automatically (yaani haiwi parsed kwa lugha ya IT). Ukitaka itokee hivyo tumia HTML tag yenye herufi a kama ilivyoonekana chini ya kisanduku cha maoni. Hata hivyo ukitaka ku-copy sio lazima utype upya. Highlight hiyo link (au maneno yoyote unayotaka ku-copy). Then bofy "Ctrl + C" kwa pamoja (yaani Control key na herufi C kwenye keyboard yako) utakuwa umeshakopi.
Hata hivyo naungana na wewe kuwa hizi restrictions za kuzuia ku-copy alizowekewa Michuzi na web designer wake Bwana MK GROUP ni za kishamba kwa kuwa ukishaweka kitu kwenye Internet kwa kweli hakuna jinsi ya kuzuia kisichukuliwe.
Point 02 - WORD VERIFICATION kazi yake sio kurekebisha spelling mistakes kama inavyoelekea unadhania. WORD VERIFICATION kazi yake ni kuhakikisha kuwa anayetuma hizo comments ni mtu halisi na sio software. Bila hiyo WORD VERIFICATION mtu anaweza akatengeneza software ya kutuma comments automatically na hivyo kumsumbua sana Bwana Michuzi kwa sababu itabidi apoteze muda mwingi kudelete hizo comments zinazorushwa automatically.
Point 03 (aka Bonus Point) - ukitaka kubold na italics tumia HTML tags zilizoko pale chini ya comment box.
---- mifano ---
Hii ni Bold
Hii ni italics
Hii hapa chini ni active link --> Barack Obama akiongea New Hampshire
Ukitaka kujifunza zaidi weka e-mail yako hapa nitakuandikia.
Mimi naona watu wanaropokaropoka tu hapa. Ni kwamba baada ya shilling kuwa inacheza sana mwaka jana serikali imechukua hatua kali sana kuidhibiti. Mojawapo sasa hivi, kuanzia january hii, ni kwamba huwezi kupata pesa bila na kitambulisho cha maana. Pia exchange rate imerekebishwa ili kudhibiti watu wanaotaka dolla at random.
ReplyDeleteHii system inafanya kazi sana sana kwenye developing world with weak economies. Maana kama watu wanachukua au kuingiza dola ambayo ndiyo main exchange mediaum kwa bongo, mnaharibu sana trend ya shilling, na inakuwa ina-fluctuate hovyo hovyo. Mfano mzuri ni mwaka jana na juzi. Ilifgika sehemu ukienda na shilling kenya au uganda hawataki kukubadilishia. Kwa sababu ilikuwa inabidilika kila saa. Sasa hivi angalieni, imekaa stable kwa muda gani, lcha ya price ya petroleum kuchezacheza na kuwa all time high!
Haya mambo ya kubadilisha fedha yako kila sehemu na inategemeana na nchi ilivyo. Kw amfano, pale Bombay ay Delhi, huwezi badilisha fedha mitaani kama hapo Bongo. Ni lazima uwe na passport na sehemu maalumu. Hivyo hivyo huwezi kuingia kwenye Hotel yoyote ile, regardless of its status ukapewa huduma kama una foreign currency. wanataka Rupia tu.
Siyo kwamba ni urasimu. This has got to do with control of inflation. Nyi wabeba ma-box kwa kuwa mlienda huko hata shule hamna, basi muuulize kwanza. siyo kuanza kuponda issue msizozijua. Inahitajika shule sana kuweza kuishi duniani wandugu.
Tulieni. Siyo kweli mambo ya mwaka jana yawe sawa na mwaka huu. Kuna mengine mengi yanakuja bongo. Tutaona mambo mwaka huu kuhusu financial regulations.
pole sana mdau.katika matukio yote niliosikia lako linashangaza na mengine pia hapo juu ya kuzungushwa hela yako kwa wiki moja pia mnatakiwa kupiga simu western union head quaters nakuripoti hio branch.namba ya branch au location hipo kwenye form za western union hapo hapo.hio itasaidia kuwakomesha hawa ndugu zetu ambao wanapenda kutunyanyasa kwenye kila kitu.hukutakiwa kutuma kopi yako ya passport au viza huko bongo kama unatuma hela nyingi hio ilikuwa kazi ya hio branch ulikuwa unatuma hela kuuliza hayo yote.wewe ukituma hela inama tayari umalizana nao .huko nyumbani wao kazi ni kuuliza vitambulisho vya wanaopokea.ningekushauri upige simu western union headquaters huwashitaki hao watu hili huondoe usumbufu kwako na watu wengine baadae.
ReplyDeleteHey Sir B the G, kwanza hii ni BLOG na sio GLOB
ReplyDeletepoint 1:
we hujui mambo ya data protection?? lakini inakopika zidisha utundu kidogo tuu badala ya kuright click nenda juu kwenye menu bar the edit then copy...
point 2:
kila kitu kina maana yake hivyo kwa michuzi hii word verification ina faida..na ndio maana yake upate ugumu wa kuyasoma hayo maneno
jumapili njema
Mdau wa western union... angalia comment za watu then work from there. Mimi sina any bad experience na western union.. niko UK. Nakubaliana na watu wanaosema kuwa zaidi ya a certain amount huku utaulizwa ID... lakini sio kule bongo mtu aulizwe ID ya mtumaji lazima kuna walakini..vinginevyo deal nao ikibidi we ripot Western Union hapa. Maana kama kungekuwa na problem wangenotice hapa ....
ReplyDeleteall the best
Could be the price of “Tambararerism"! No surprise; Guys! I don’t know the starting point; I think it sounds like a ridiculous taunt, Get ready to receive my comments.
ReplyDeleteEveryone has his own perceptions on analysing issues which is commonly influenced by the way he/she receives the image. Generally, the scenario has ranges of the causes, definitely below are few to be outlined:
Mporomoko wa Maadili “Ethical issue is fragile”
Inawezekana kabisa kwa sababu thabiti,zimewekwa sheria ngumu na kali ili kulinda fedha zinazotoka kusipofahamika,ikiwa na kuangalia status ya mtumaji,mimi na wewe hatujui kwa sababu hatupo kwenye mfumo wa utendaji wa kila siku wa shirika linalotoa huduma hiyo.Lakini yote hayo yamechangiwa na vitu kama UGAIDI,FEDHA CHAFU,NA UTAPELI,I remember,at one point of time I was in South Africa Durban,Western Union over there is completely out of operations,watu walikamata mfumo Western Union na wakawa wanaiba hela za watu sana accoprding to the operators, the threw allegations stones to Nigerians as earmarked people for the dubious instances.
Pili inawezekana ni controls zinazotolewa na Benki Kuu katika kuhakikisha ya kwamba hakuna mianya ya fedha haramu,nikimaanisha kwamba wanataka waelewe chanzo kamili.
Tatu hawa watendaji wanatakiwa watoe maelekezo fafanuzi kuhusiana na huduma hizo nay awe yanakubalika kimataifa,sasa ni ni maana ya zama za teknolojia ya Habari mawasiliano “TEKNOHAMA” a.k.a ICT information communication technology which the government of URT affirmed the declaration under WSIS summit in Geneva and Tunis.Manayake ni chachu ya maendeleo kwa mfumo wa teknolojia mpya,sasa kama kunakuwepo ukiritimba mimi na wewe ni budi tushangae
Nne inawezekana iiiinatokana na mtendaji aliyekuwa kwenye dawati,ni mgumu wa kuelewa kama Tomasi wa kwenye Bibilia “Am sorry for quoting the Bible”Kila mtu ana jinsi yake ya utendaji wa kazi na kama alikuwa mwana mama labda nyumbani mzee alimghafirisha,na kama alikuwa kidume inawezekana mamao ya mitala na Nyumba ndogo yamechangia,Ha haha ha ha haaaa!!!
Mwisho ningependa hao operator watoe waraka kamili unaoonyesha ni viambatanisho gain vinavyohitajika ili kupata haki yako. “Justice delayed justice denied”Hajatendewa haki huyu mama wa watu kabisa.
Hizi ni zama za strategic competition,kwa sababu kuna kampuni nyingine zinazotoa huduma bora,hivyo wanajiweka kwenye matattizo hawa watu.Mimi hutuma fedha kutumia CoinStar amba agent wake Dar ni TIB na benki moja hapo haidari Plaza hakuna maajabu haya,nilipokuwa south nilikuwa natumia Money Gram
Lakini na sisi tunaokaa nje tuwe na vibali kamili vya kuishi ughaibuni,kama ulikuja kimichoro malizia michoro yako kabisa ili ujulikane umesimamia wapi sio longolongo,tunaweza kurushia mawe upande mwingine kumbe tatizo lipo upande mwingine.
kaka kesi yako sio kukosa pesa au kutaka kopi ya pasporty yako,kumbuka kwamba muhusika na shilika hilo ni mnyamwezi na kama kuna kitu kinatia wasiwasi bongo wanaambiwa tu wafanye nini, kuna watu pesa zao zinakaa zaidi ya miezi kabla hawajapewa unajua kwanini,hayo majina yenye sijuhi husein ndani lazima jasho ikutoke sio bongo tu,pole kaka badili jina jiite John utakuwa unamatatizo.
ReplyDeleteVERY SIMPLE AND CLEAR,
ReplyDelete1. KWA UZOEFU WANGU KUTUMA HELA KUTOKA HAPA USA, KUANZIA DOLA 1000 KWENDA JUU, LAZIMA UONESHE KITAMBULISHO CHAKO KAMA PASSPORT AU DRIVING LICENSE. INAONEKANA WEWE ULITUMA KUANZIA DOLA 1000, AU POUND SAWA NA DOLA 1000.
2. Hakuna anayechukua rushwa ya mtu kwa hela za western union. Home kuna rushwa ndiyo, kama nchi yoyote ile, lakini tusiiabishe nchi kwa mambo ya kufikirika bila undani wa tatizo lenyewe.
3. Ila sema Bongo sometimes wanasumbua kuchukua hizi hela sababubaadhi ya wahudumu saa zingine hawasomi au hawayajui masharti ya uchukuaji hela hizi. Na hiyo si rushwa. Mimi kuna mtu alishaulizwa kitambulisho, wakati mimi nilichagua mchukuaji apewe bila kitambulisho, bali kwa TEST QUESTION & ANSWER. Unaweza kuonesha vyote viwili au kimoja, si lazima vyote.
Masharti yao western union yako online, kila mtu anaweza kujisomea.
NARUDIA TUTUIE TU LUGHA YA KAWAIDA KUMAANISHA UOVU UNAOTENDEKA AU MAKOSA FULANI, NA SI KUSEMA TZ KUNA UOZO, KUNA RUSHWA, NK. WAPI HAKUNA VITU KAMA HIVYO?
Mimi nilienda Western Union pale Kariakoo Benki ya Posta nikataka kutuma shilingi elfu mbili za kenya ambazo ni kama shilingi elfu 36 za kenya kwa dada yangu alyekuwa nairobi kapungukiwa nauli ya kuja.Sikuwa na hela za kenya nilitaka waniuzie halafu wazitume hapo hapo.Wakaniambia niwape copy ya passport yake na zile kurasa za visa zilizogongwa.Nikawaambia hata Kenya ambapo ni sehemu ya jumuiya ya Afrika mashariki mna usumbufu huo? Wakasema lazima ulete ndio utume.Hivi hivi hutumi haijalishi unatuma wapi?
ReplyDeleteBahati nzuri pale kwenye foleni kulikuwa na mtu akasema twende nikueleze cha kufanya nje.
Akaniambia yeye mwenyewe yalishamkuta.Akaniambia nenda ubungo stesheni ya mabasi ukimwona kondakta fulani wa basi fulani mpe shilingi Elfu moja mia tano tu ya Tanzania na hizo hela za hizo unazotaka kutuma atampigia mtu wake kule Nairobi na atampa dada yako pesa dakika hiyo hiyo.Basi nikaenda nikampa huyo kondakta akaniambia mwambie dadaako awepo stendi. huyo kondakta akapigia huyo mtu kule nairobi wakampa Pesa kule nairobi hapo hapo bila usumbufu wala kitambulisho na tena wakamwuliza anataka wampe zipi za tanzania au kenya achague zile anazotaka.
Nalaani kitendo hata cha kubana kutuma pesa hata ndani ya jumuiya ya Afrika mashariki hela zenyewe wala si dola ni haya mashilingi ya nchi zetu! Kweli inatisha.Hii jumuiya itaimarika kweli ikiwa hata pesa zetu haziwezi kutembea free ndani ya nchi zetu.
Hivi hao maafisa wa jumuiya wanafanya kitu gani? Hivi jumuiya ya Afrika mashariki ni jumuiya ya nini ya maraisi kutembeleana au ni kitu gani? Ni jumiya kwenye nini hasa mnaojua mnisaidie!
Sasa hivi nikitaka kutuma hela natafuta tu kondakta wa basi hata ndani ya nchi wabaki na mikampuni yao na kaunta zao.
Du TAMBARARERISM Dr Confusion kianzio chako cha sentensi kimenimaliza.Nilikua nimeshachoka kusoma comments za watu jinsi zilivyo nyingi lakini kuona comment yako nikaanza kucheka kwanza halafu nikapata ngumu yakumalizia maelezo yako marefu.
ReplyDeleteMwakidila tumia Wapemba just £2 pamoja wanakwambia unaibiwa si kweli,angalia rate ya W'Union ya kutuma pesa halafu angalia ya Wapemba,faida unayo wewe mtuma pesa huumii sana kwa ajili ya kusaidia nyumbani.
We Dr. Confusion unaonekana mhuni, lakini uliyeenda shule!. Hiyo safi sana. Comments zako zidumu. Maana ume-cut across importnant issues. Mwenye kuelewa aelewe na asiyetaka shauri yake!
ReplyDeletePia na annon January 6: 7:20 na Janury 6 4:08 mmetulia sana.
Wengine, mhh!Kateni issues na si kurukia.