mhariri mkuu wa gazeti la mwanahalisi seed kubenea akiwa hositali india (juu) na chini akipewa pole na waziri wa nchi ofisi ya rais (utumishi wa umma) mh. hawa ghasia alieko huko india kikazi na kulia ni balozi wetu huko mh. john kijazi. imeelezwa kwamba kubenea anaendelea vizuri baada ya kufanyia upasuaji wa jicho lake la kuume

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Bwana Kubenea naendelea kukupa pole, na Mungu akuponyeshe uje kuendelea na harakati zako za kuandika habari kali kali kama zile za JK KUMTOSA LOWASSA, KIKWETE KUBADILISHA BARAZA LA MAWAZIRI na nyinginezo nzuri kama hizo unazozifanyia utafiti wa kina.

    Wewe ni mwandishi bora sana unaandika habari za ukweli kabisa na zenye utafiti wa kina.

    Wewe huandiki fitina na mambo ya uzushi kama yalivyo magazeti mengine.

    Inabidi ukirudi India uje kutoa mafunzo kwa wahariri wengine ili waige mfano wa kazi yako.

    Pia inabidi ukutane na waandishi kila wiki pale maelezo na uwafundishe namna ya kuandika habari nzuri na za uhakika kama ufanyavyo wewe.

    Hii imethibitika baada ya taasisi nyingi kuunga mkono kazi yako.

    WALAANIWE SANA WALE WOTE WALIOTAKA KUANGAMIZA MAISHA YAKO.

    ReplyDelete
  2. Thanks God atleast I Can see one of his eyes is open and stable.
    WISHING U A QUICK AND COMPLETE RECOVERY.

    ReplyDelete
  3. Jaman watanzania wenzangu pamoja na mheshimiwa sana rahisi tumsaidie basi na kile kiumbe malaika ili akatibiwe jina lake ni somebody Nkya maana kweli baba yake kasota muda mrefu. kama serikali imeweza kumtolea mandishi wa habari why not yule mtoto tena bado ni mdogo sana jaman,Mimi ananiuma sana sema tu uwezo wangu ni mdogo sana.basi tunaoma mheshimiwa JK uliangalie na hili pia.

    ReplyDelete
  4. dah tanzania ni nchi ndogo lakini ina mawaziri lukuki.Hizi wizara nyingine wala sijui zina kazi gani kwa kweli?

    ReplyDelete
  5. Kushika kalamu kuzuri (Uandishi wa Habari)Mbio India! Ungekuwa kama mimi saa hizi ulishapofuka. Mbona Tindikalists wanasema macho usirudi nayo, kwanini?

    ReplyDelete
  6. Mawaziri wetu kwa kutanua nje...na hizi idara sijui utumishi umamma naibu ....mhhhh....mimi bongo basi tu....

    ka nchi kadogo maidara kibao na madaraka mengi tu....mwishowe nchi nzima itakua wote wmawazini , wabunge, wakuu wa wilaya sasa sijui nani atamuongoza mwenzake.......

    ReplyDelete
  7. Pole sana kwa yaliyokukuta na tunamwomba Mungu akupe nafuu upesi iwezekanavyo. Jambo lililokupata limetufungua wengi macho pia kwamba we are all equal BUT some are more equal than others. Kuna mtu kauliza hapo juu kwamba kwa nini serikali haimsaidii yule kijana Nkya kwa ajili ya matibabu? Angalao hata kuchangia kiasi fulani? Yeye kafanya kosa gani au mpaka amwagiwe tindikali? Tafadhali serikali ipime hilo. TAFADHALI SANA!!

    ReplyDelete
  8. Hongera sana Mheshimiwa Kijazi! Natamani sana kuwasiliana na Mhe. kwa kuwa ni rafiki yangu wa siku nyingi lakini kipindi kirefu tukawa tumepoteana sababu niko huku Botswana nabeba mabox. Kama kuna mtu ana email yake au hata ya ubalozi naomba sana aiweke kwenye blog hii. Shukrani.

    ReplyDelete
  9. michuzi hata sina habari kama india kuna balozi mpya jamani.

    ReplyDelete
  10. Waziri Ghasia alikuwa India kwa mumewe aliyehamishiwa Ubalozi wa TZ na siyo kwamba alikwenda kikazi

    ReplyDelete
  11. Kama raisi alivyo sema "Kama sio mambo mengine ".... kuna tetesi mitaani ni masuala ya kutoka na Mke wa mtu!.
    Kama alipokea vitisho ,lazima aliambiwa asiandike habari fulani,so lazima atakuw ana ajua ni nani na na mjeruhiwa anadai hajui, je ina wezekana ni masuala yasiyo husu kazi yake?

    ReplyDelete
  12. inavyoonekana tasnia hii ya washika kalamu imepeta watu muafaka wanaojua kutumia vema risasi na wino wa kalamu zao kuelezea mambo mazito yanayoweza kuwatishia ustawi wa hao mabarazuli kikwete alitazame kwa umakini swala hili hakika ni miongoni mwa watendaji wake wasiostahiki ndio waliohusika.serious huwezi kujenga ghorofa huku foundation yake ikawa ya nyumba ya udongo.i pray to lord jamaa apate quick recorvery na hii iwe changamoto kwa wadau wengine wa habari

    ReplyDelete
  13. mungu amsaidie bwana kubenea apone haraka na hii inaonesha ipo haja ya waandishi wetu kupitia mafunzo ya mpigano ya kujihami(martial arts)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...