
MAONI YA BALOZI WA UINGEREZA, PHILIP PARHAM, JUU YA MAAMUZI YALIYOCHUKULIWA NA SERIKALI KUHUSU REPOTI YA UCHUNGUZI BENKI KUU
“Mara nyingi nimekuwa nikisema jinsi ilivyo muhimu kwa serikali kuonekana ikishughulikia kikamilifu tuhuma nzito za rushwa.
“Mara nyingi nimekuwa nikisema jinsi ilivyo muhimu kwa serikali kuonekana ikishughulikia kikamilifu tuhuma nzito za rushwa.
Hivyo nimefurahi kusikia kwamba ukaguzi maalum uliofanywa kwenye akaunti ya "External Payment Arrears" (EPA) Benki Kuu sasa umekamilika, na kwamba Rais Jakaya Kikwete amefanyia kazi kwa haraka kabisa yaliyogunduliwa. Tunampongeza Rais Kikwete kwa maamuzi aliyochukua.
Ni sahihi kabisa kwamba hatua za kinidhamu zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya wale waliohusika na ulipaji wa fedha hizo kwa njia zisizo halali, na vilevile dhidi ya wale walioshindwa kuchukua hatua pale ambapo ishara za "mambo kutokwenda sawa" zilipojitokeza kwa mara ya kwanza.
Pia itakuwa muhimu kama uchunguzi ulioanzishwa na Rais utafanyika kwa haraka na kikamilifu. Ni vigumu kuamini kama ufisadi wa uzito na kiwango hiki unaweza kuhusisha Benki Kuu yoyote.
Pia itakuwa muhimu kama uchunguzi ulioanzishwa na Rais utafanyika kwa haraka na kikamilifu. Ni vigumu kuamini kama ufisadi wa uzito na kiwango hiki unaweza kuhusisha Benki Kuu yoyote.
Wale wote waliohusika, na waliojinufaisha kwa fedha zilizoibiwa, lazima wawajibishwe. Kufanya hivyo ni muhimu sio tu kujenga imani kwa Washirika wa Maendeleo, bali pia imani kwa Watanzania na wawekezaji wa nje, ambao ustawi wa Watanzania unategemea.
Tunasubiri kusikia zaidi juu ya ukaguzi uliofanyika, na pia hatua ambazo serikali itachukua katika kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa.
Tunasubiri kusikia zaidi juu ya ukaguzi uliofanyika, na pia hatua ambazo serikali itachukua katika kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa.
Vilevile tunasubiri matokeo ya uchunguzi ambao Rais ameuanzisha, na tunatumaini tuhuma nyingine nzito za rushwa nazo pia zitashughulikiwa kikamilifu.”
John Bradshaw
Press Officer
British High Commission
Mobile: +255 (0)754 764276
Email: john.bradshaw@fco.gov.uk
ANKO MAKAMBA YUKO WAPI AKANUSHE TUHUMA ZA BOT NA HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA RAISI. MSIMAMO WA CCM UWE ULEULE ILI KUKIJENGE CHAMA HESHIMA, HATA HIVYO TUKIENDELEA NA CHAMA HIKI MAENDELEO YATAKUWA NDOTO KWANI VIONGOZI WAKEWANAJALI MASILAHI YA CHAMA ZAIDI KULIKO TAIFa.
ReplyDeleteHili suala ni changa la macho, Balali hakuwa peke yake kwenye wizi huu, nashangaa Kikwete anataka bodi ya Benki kuu ikae tena chini kuangalia nani aliiba. Hiyo bodi si ilikuwepo toka mwanzo wakati wizi unaendelea. Naibu Gavana Ndugu Juma Reli alikuwepo toka mwanzo wakati wizi wote huo unafanyika. Huu ni usanii wa hali ya juu kuwafanya watanzania wote wapumbavu. Balali alishaandika barua ya kujiuzulu toka Dec 2007halafu serikali ikajifanya haijui na leo Kikwete anajifanya kutengua uteuzi wake. Nawaambia watanzania hakuna lolote litakalofanyika, you mark my words. Wahusika wakuu ni hao hao viongozi wakuu wa nchi na kampuni zao feki walizozianzisha ili kuiba fedha za watanzania.
ReplyDeleteWakati Watanzania mamilioni wanaishi kwenye umaskini mkubwa kwa kukosa huduma muhimu kama za maji, umeme, barabara, afya na elimu bora, Hawa mafisadi wanaishi maisha ya hali ya juu bila ya matatizo. Inatia hasira na inatia huruma. Iko siku tutawafikisha hawa mafisadi kwenye vyombo vya sheria.
Ndugu Michuzi, Mjengwa
ReplyDeleteSwala jingine, la kufuatilia ni kuhusu hawa jamaa wa TBS na mawakala wao wa kukagua magari.
Hivi sasa Dubai, kuna vituo vitatu vya kukagua magari, tunataka kujua ni kiasi gani za fedha za kigeni ambazo zimepatikana katika sekta hii, na wao mawakala wamepata kiasi gani, tangu huu utaratibu umeanza. la kujiuliza je hizo fedha zimesaidia vipi katika maendeleo ya Taifa, ikiwa kuborosha usalama barabarani. Je magari yetu salama barabarani (ajali zimepungua)?
Kwa sababu kila kukicha tunaona maajali mengi tu, kuanzia ngazi za taifa, mawaziri, wabunge mpaka watu wakaida.
Je kuna ukiukwaji wa Safety katika haya magari, tunaletewa magari mabovu Tanzania, au je sio vyema kwa Taifa likaangalia upya hili swala zima la ukaguzi wa magori, na kuanza kitengo maalum cha ukaguzi wa magari ndani ya nchi katika mikoa na vitongoji vyake, kama vile MOT-UK, NCT-Ireland, badala ya ukaguzi wa magari nje ya nchi.
Tunapendekeza hili, kwa sababu kuu mbili.
Kwanza magari yote yatakuwa yanakaguliwa kila baada ya miaka miwili, kuangalia kama hayo magari yako salama kuwa barabarani.
Pili, kazi/ajira nyingi zitajengeka ndani ya Taifa, badala ya nje ya nchi, kwa manufaa ya vijana na wananchi kwa ujumla.
www.tbswtmuncovered.blogspot.com
kwikwikwi KP endeleza kazi, hii ndio kitu sisi walavumbi tunapenda.
ReplyDeleteWe want our money!
ReplyDeleteWhen we want ?
NOW !
No if no buts ,just bring our money home and send the culprits where they belong.
There are hospitals there too.
The British ambassador need to be proud of himself and of ppeople he represent .
KEEP THE PRESSURE .
If not, these people will simply and quietly wipe their mouths and keep quiet.
What happened in Kenya means ,
"YOU CAN FOOL SOME PEOPLE SOMETIMES BUT YOU CANT FOOL ALL THE PEOPLE ALL THE TIME "
Bob Marley
There is no sleep till our money is back
Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika
Mr Dar
HIVI KWANINI SERIKALI INASITA KUTENGUA URAIA WA KP.NASIKIA SIO MTANZANIA NI ILLEGAL MIGRANT.
ReplyDeleteKutokana na hili suala nampa hongera sana Dr. Wilbroad Slaa kwa kuleta ile hoja bungeni pamoja na kupingwa na watu wengi wa CCM ambao walifikia kumuita mzushi. Nadhani Slaa anafaa kabisa kugombea urais wa Tanzania mwaka 2010.
ReplyDeleteMakamba wa CCM, Spika wao Samuel Sitta na kina Lowassa si mlisema kuwa Dr. Slaa ni mzushi, sasa yako wapi sasa. Mnaona hata aibu. Lowassa tena kutaka kuonyesha kuwa ana confidence na Balali, aliamua kumtumia mpaka ndege ya Serikali ili impeleke Balali Dodoma kwenye kikao cha Bunge.
Jamani watanzania tusiendelee kukubali huu usanii tunaofanyiwa kila siku huku sisi tukiwa tumenyamaza kama Mabubu, hata Mabubu inafika wakati huwa wanaguna kwa hasira kama huwakubaliani na wewe.
Hi Michu,
ReplyDeleteUsiibanie hii Kaka.Ninavyofahamu mimi ni kwamba pesa inayotumika Tanzania ya aina ya sarafu na Noti inchapishwa nje ya nchi. NAULIZA; Je ni nani anahusika na kutoa order hiyo ya kuchapa hela? na je ni nani huwa anayemdhibiti/kumhakiki huyo anayetia hiyo order kujua kama ameagiza idadi au thamani inayotakiwa sahihi? KWANINI NIMEULIZA HIVYO:
Kama ni BOT wanafanya hiyo Kazi basi TUMEKUWA TUKILIWA..na wajinga ndiyo waliwao....kwa sababu kwa UFISADI walioshirikishana na vyombo vyote vya fedha kuanzia hazina..na kwingineko..ni wazi kwamba hata kujitengenezea pesa zao za ziada wanaweza kabisa kufanya bila bughudha yoyote...Naomba nielimishwa kuhusu hili swala.Ndiyo maana haka kauchumi hakipigi hatua kabisa. SINA IMANI KABISA NA JAMAA WA BOT!!
KWA NINI KESI HII ISIWEKWE CHINI YA UHUJUMU UCHUMI?
ReplyDeleteWAHUSIKA WOTE WAKAMATWE MARA MOJA NA KUWEKWA NDANI WAKATI HUO "UCHUNGUZI" ULIOTAJWA UNAFANYIKA? WAKAWA NJE UNATEGEMEA NINI? SI NDIO KIPINDI HIKI WATAKITUMIA KUTOKOMEZA USHAHIDI, KUFICHA MALI, KUBADILISHA MAJINA YA WAMILIKI MALI, KUTOA RUSHWA KWA WAFUATILIAJI N.K.
BWANA BALALI ANATAKIWA AREJESHWE NCHINI AKIWA CHINI YA ULINZI MKALI. KAMA NI MATIBABU ATAYAPATA HAPA NCHINI.
HATA WALE WALIOACHA, KUJIUZURU KAZI NA WENGINEO WALIOHUSIKA WAKAMATWE WOTE MARA MOJA!!! VINGINEVYO TUTAHISI KUWA VIONGOZI WALIOKO MADARAKANI NAO WALIKUWA NA MIGAO, KWA HIYO WANAWALINDA.
HIVI HAYA MAPESA YOTE YAMEKUWA YAKICHUKULIWA MIAKA YOTE HIYO...! WAKAGUZI WAPO?? WALIKUWA WANAKAGUA AU KUCHUKUA MGAO??
NINAANDIKA HAYA NIKIWA NA UCHUNGU MKUBWA KWA VILE NAJUA WATANZANIA WENGI WAMEPOTEZA MAISHA NA WENGINE WANAENDELEA KUPOTEZA MAISHA KWA KUKOSA HUDUMA MUHIMU AMBAZO GHARAMA ZAKE PENGINE NI NDOGO SANA....WAKATI HUO-HUO KUNA WATEULE WANAENDELEA KUJINUFAISHA WENYEWE , FAMILIA ZAO NA MASWAHIBA WAO.
JE TUFIKE MAHALA TUSHIKE MAPANGA KAMA WATANI ZETU? AU TUANZE KUCHOMA MAJUMBA NA MAGARI? MUNGU IBARIKI TANZANIA! IPO SIKU MAFISADI HAWA HAWATAKUWA NA NAFASI... HAKUNA MAREFU YASIYOKUWA NA NCHI. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE. MBARIKI BALALI ARUDI AKAJIBU TUHUMA.
Billion 133 zimeliwa kwa kipindi cha mwaka 2005 - 2006. EPA imekuwepo kwa miaka 15. Je kwanini uchunguzi mwaka mmoja tu? Nisaidieni kuelewa hili? Ama kunakitu kimenipita?
ReplyDeleteHaiambatani sana...lakini ni shauri ya kuchunguza na kuchukua hatua zinazostahili:
ReplyDeleteTanzania: Govt Wins Legal Battle Against British Water Company
World Development Movement (London)
PRESS RELEASE
11 January 2008
City Water Services, a subsidiary of British-based water company Biwater, has lost an international legal case for breaching its contract to deliver water and sanitation services in Dar es Salaam, Tanzania between 2003 and 2005.
The contract with City Water was issued following a controversial water privatisation, supported by the UK government.
The outcome vindicates the Tanzanian government’s decision to terminate the contract due to its dissatisfaction with the standard of service delivered by the water company. Tanzania has been awarded over £3 million in damages and over £500,000 in legal costs.
Namfagilia british ambassador ni mmoja wapo aliyeweka pressure ya ukaguzi BOT.Hao ni wadau muhimu sana nchini.enzi za wana ccm kukilinda chama kwa kulaghai zimekwisha inabidi warealize kuwa sasa watu wanaona mbali.only performance will determine na si bla bla bla all the time.iam frozen.huo udoctor wanapata wapi?waweke majina kwa kuperform c corruption na uozo.wanakatisha tamaa wanaoendelea kusoma.doctor kutenguliwa ni big shame kwa taifa lililomsomesha.rubbish
ReplyDeleteSINA MAKOSA sa...
ReplyDeleteHIVI KWANINI SERIKALI INASITA KUTENGUA URAIA WA KP.NASIKIA SIO MTANZANIA NI ILLEGAL MIGRANT.
Friday, January 11, 2008 9:38:00 PM EAT
lol kusema kwelii hii imenikuna mie hata siasa za tz sizijui na wala sitaki kuzijua kwani sizielewi ila nataka huu udaku, SINA MAKOSA... unasema KP sio raia wa tz? ni raia wa wapi kwani? na ni KP gani unayemzungumzia? ALLY MASOUD AU?