Bro Michu,
Kama mdau mkereketwa wa blogu yetu nzuri nimefurahi kuona mshindi wa mashindano yote mawili ametangazwa. Ila kuipenda blogu yetu vilevile kunanifanya niulize maswali kuhusu ushindi, hasa wa shindano la mdau wa milioni tatu, kulikoni?
Mbona kuna dalili za ukibaki kama wa kenya? Maana majibu yamecheleweshwa na wakati inajulikana fika muda ambao blogu yetu ilitembelewa na mdau wa milioni tatu.
Mimi nilikutumia majibu yangu immediately halafu nikaenda kulala. Nimeamka asubuhi nikakuta hola! Labda utusaidie na maelezo ya vigezo vilivyotumika kumpata mshindi, maana mimi nimefuata maelezo yako kama ulivyoagiza, na bado nimeambulia patupu.
Nimetuma screenshot. Naona mdau mwenzangu alituma na picha kabisa? Mana hata mimi naweza kutuma picha kama hiyo! Au inawezekana kweli watu wawili kupata namba moja? Najua blog yetu inatrack IP addresses, na ndio maana nilikwambia yangu ili uweze kuhakiki.
Ila bado swali linabaki, kulikoni?
Anyway, yote tisa, cha muhimu mshindi tunamkubali. Mana waamuzi wameshaamua. Ila swali wadau tulioshinda na kuachwa solemba tunauliza, kulikoni huu utaratibu wa uchaguzi kama wa kenya uingie mpaka kwenye blogu yetu safi?!?
Asante!
Mdau Andrew

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. duh, masela! jamaa kapata kama barua pepe 3000 leo. unategemea nini; akujibu hapo hapo? tujaribu kuelewa mandhari ya shughuli na shindano nzima. kwanza, watu wote tunaoipenda hii blog ni washindi!

    bahati ya mwenzako...

    ReplyDelete
  2. mdau Andrew na wengine nenda kasome
    www.jamboforum.com

    kuna majadiri na evidence kuwa one namba yaweza patwa na two or more people.pia time ya mshindi ya uongo ilikuwa around 11:23am TZ

    Michuzi post this comment as umenichunia zangu nyingi tu leo

    hutaki niongee ukweli?

    ReplyDelete
  3. Lazima kazi ya kusoma email 3,000 ilikuwa ni kubwa. Michuzi amefanya kazi nzuri ya kujibu maswali ya wadau na tunawashukuru wadau wote waliotuma barua kwa michuzi na pia kukubali matokeo.
    Watu wote kwenye hii blog wamefanya vizuri!

    ReplyDelete
  4. Unajua siku zoote nilikuwa sielewi kwanini timu ya Taifa ya sijui Kilimanjaro au Serengeti boys iliyoshiriki mashindani ya Challenge ilivyoshindwa watu wakaanza kumrushia chupa, na mawe kocha Maximo. Kwanza na vile mi si mpenzi wa mpira hata sikuelewa mantiki yake I was like what is wrong with this people?

    Sasa nimeelewa tena nimepata somo humu kuwa WatZ au Wabongo huwa hawakubali kushindwa na hata wakikubali basi huwa na visingizio kibao. Sio suala la kuona hili ni shindano na lina mshindi mmoja basi. Hiyo hatuna its too childish ambako mwalimu huwaambia watoto tena wanasariskuli kuwa wote mmeshindaa eeh watoto wazuri! Kha shindano limekuja mtu mmoja kashinda basi na ilikuwa mshindi mmoja sasa maneno, mabarua, manini sijui majambo forum as if this was a serious issue. Ithought this was supposed to be fun, in my part it was fun, but it seems hatuna utamaduni wa kufurahi lazima tu tuharibu furaha zetu na wenzetu wengine. Imagine huyo Rehema huko aliko alivyofurahi alivyoona hiyo 3m number sasa huo ushindi wote umemtumbukia nyongo, simply because of few people who are not used to having fun in their lives.

    Grow up and stop complaining about each and every trivial things.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...