wadau kunradhi. kama mnavyojua tarishi hauwawigi. sasa hii mada ya lebozzzz inakuwaje hapa?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. lebel kwenye suti huwekwa baada ya kutoka kiwandani ili kuonyesha designer wa hiyo nguo.....baada ya kununuliwa inatakiwa ing`olewe.....kuiwacha ni kutoelewa kwa wengi wetu au ni kujionyesha kuwa na sisi tunavaa designers suits......ndio maana ukiangalia waanzilishi wa kuvaa suits na viongozi wao hutaona lebel ikiwa mkononi......labda kwa hao walioanza kuvaa suits ukubwani kama wengi wetu huku dunia ya tatu......ingekuwa vyema watu waliobobea kwenye masuala ya mavazi wenye uzoefu na dunia ya kwanza watupe shule kuhusu hili....lakini mwisho wa wote ni sisi wenyewe...kung`ang`ania kuacha lebel kwa sifa zetu na ushamba au kuelewa somo!!!!!Wako watanzania wengi tu wanaofanya kazi kwenye kampuni za designers wakubwa huko dunia ya tau pia wanaweza kutupa somo kuhusu hili!!!

    ReplyDelete
  2. lebel kwenye suit ni lazima itolewe kabla ya kuivaa.
    sababu kubwa ya lebal inaanzia kwenye mambo ya trade mark.Trade mark iko pale kwa ajili ya kuonyesha dinsction yaani kuonyesha tofauti kati ya bidhaa moja na nyingine.Na hii ilianzia kwenye karne ya kumi na sita wakati wafanyabiashara wakisafirisha bidhaa zao kwa meli na dharuba ikitokea waweze kujua mali ambazo zimepatikana ni za nani.Baada ya maendeleo lebel zikatumika kutenganisha ubora wa bidhaa yaani mtu anakwenda dukani kununua kutokana na ubora wa bidhaa wa kampuni fulani hapo ndipo kwa kimombo wanaita emotional allua yaani mtu unakuwa kama addicted na bidhaa za kampuni fulani.
    sasa washona suit wanaweka hizi lebel ili wewe mnunuaji uweze jua ni nguo gani inakiwango kizuri kutokana na imani yako kwa designer na hapo ndi maana unaweza mtuma mtu suit ya specific designer na ukishaletewa lebel haina maana tena inatakiwa uitoe maana kazi yake imeisha.kuiacha ni ushamba na tuwaachie wanamuziki kama wa FM kwenye shoo zoa huwezi jua labda wanakodi zike suit

    ReplyDelete
  3. Lakini kuna suti zingine ukitoa label panabaki na katundu kadogo ambako kana onyesha mshono kama kifungo kimetolewa hivi na suti ina kuwa kama imeharibika ama kuonekana ni ya zamani. Mimi naona label zibaki pale pale wala si ushamba walioziweka wana makusudi yao.

    ReplyDelete
  4. Kuacha lebo haikubaliki, inakubalika pale tu mtu anapoenda dukani kukodisha au kuazima, baada ya kusherekea kama ni harusi au ukimaliza matumizi yako unamrudishia mwenye duka ili iuzwe tena au kukodishwa.Vinginevyo watu wanavaa kwa kiburi ili kujionyesha na wao wamevaa suti ya dukani, na bei yake kubwa.

    ReplyDelete
  5. Ninakubaliana na wadau hapo juu, lebel kwenye suti inatakiwa uitoe baada ya kununuliwa. Hiyo lebel haiongezi kitu chochote katika dressing yako, sana sana watu wataona kama umeikodisha na sharti moja wapo ni kwamba unatakiwa kuiacha hiyo lebel. Kwa wale wanamiziki kwa kuwa ni watu wa kujishow-of basi huwa wanaziacha kwa maslahi yao ya ubishoo.

    Ki ujumla lebelz hazina msingi wowote baada ya kununua suti inabidi itolewe!!!!USHAMBA HUO

    ReplyDelete
  6. Mheshimiwa kamongo......kweli inahitajika shule kali zaidi ili watu kama wewe waelewe kuwa lebel zinatakiwa zing`olewe.....suti ziko za aina nyingi kwa maana ya quality ya hizo suti......inawezekana suti yako ambayo unadai uking`oa lebel inabaki tundu material iliyotumika kutengeneza suti ni ya kiwango duni.....sijapata ona au kusikia mtu ameng`oa lebel kukabaki tundu.....labda ufanye utafiti kwenda kwenye drycleaners wakupe uzoefu wao kuhusu suti usikimbilie kujustify ufinyu wa suti yako kama ndio standard ya suti zote duniani

    ReplyDelete
  7. Ao walioziweka nje hizo lebo sio wajinga na kuziondoa kunafanya kuacha matundu kwenye suti maana zinakuwa zimeshonewa kabisa,mimi nadhani tutoe zile zinazoning'inia tuu sababu awa designer naona wameongeza manjonjo tuu kuweka lebo nje na njisi walivyoshonea sijui kama ni za kutoa.

    ReplyDelete
  8. Suti zimeletwa na wazungu hivyo tunaiga kwa hiyo lazima tuige kila kitu.

    Kuna wakati fulani nikiwa nchi moja ya Ulaya(sikuenda kubebe boksi ila mkutanoni)basi nikatumia fursa hiyo kununua suti nikiwa katika duka moja nikachagua suti nzuri(ikiwa na kilebo mkononi) nikailipia.

    Sasa ikiwa suruali ni ndefu(mara nyingi huwa hazijapindwa chini)nikataka ipunguzwe urefu na pia ipindwe hapo ndio nilipotoka ushamba ninaouona hapa bongo.

    Ikapunguzwa basi nikaletewa lakini koti limetolewa leboz nikasema kwanini sikubali wanirudishie lebo yangu kama ilivyokuwa.

    Basi wauzaji(wazungu na weusi) walicheka sana wakasema hii inatakiwa kutolewa hata tungeacha ukienda nayo inatakiwa itolewe tu aisee nilibisha wakanipa shule na mifano aliyotoa ann wa kwanza na pia wakasema nitakuwa nawatangazia biashara madesigner bila malipo huu ni upumbuvu.

    Toka wakati huu nikatoa lebozzz kwenye kasuti kangu kingine.

    Hivyo lebozz ni ushamba sana kuziacha acha labda uwe umekodi suti dukani.

    ReplyDelete
  9. Hili ni somo kwa banana au? Maana naona siku ile watu walimponda kuwa hajatoa lebozz kwenye tux yake,mara ya kuazima haruhusiwi...duh kwale siye wala vumbi hatukosi neno! Naona mmeamua kuposti kabisa mada ili ajue next time anasimamia harusi ya Chidi benz na yeye...!!

    ReplyDelete
  10. Kwako JP MWANZA hapo juu
    "....yaani kuonyesha tofauti kati ya bidhaa moja na nyingine."
    Statement yako sio kweli.
    Trade Mark huonyesha tofauti kati ya bidhaa ya aina moja ilele ila inayotengenezwa na watu tofauti.
    Na sio bidhaa moja na nyingine.
    Mfano ni PILSNER na SERENGETI zote ni bia lakini TM hizo ndio zinazitofautisha.
    Lakini huwezi ukafanya comparizon ya TM ya Bia na Sabuni, kwa mfano.
    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  11. Kuvaa suti bila kutoa lebel ni sawa na kuendesha baiskeli bila kutoa ma-lailoni yake.

    ReplyDelete
  12. Kwa hili la LEBO, leo nimeelimika. Sikuwa na hili wala lile, nilikuwa najionea sawa tu. Mada kama hizi michuzi zimetulia. Nikiuza korosho zangu, nina mpango wa kununua suti moja kali sana. O'C-Chikukwe, Masasi.

    ReplyDelete
  13. Kuacha label ni kujitangaza kuwa umevaa suti ya namna flani kwa hali ya chini kabisa. Inaweza kulinganishwa ni ile methali isemayo "Maskini akipata nanshii hulia mbwata"

    ReplyDelete
  14. Sasa kwa nini wasimuulize michuzi maana yeye anasafiri sana na matokeo yake majambo anayastukia.Michuzi yeye leboz anatoa lakini wenzie anawatosa!Wabongo kama mambo ya suti hamuyajui sanasana watu wa dar nendeni kwa watani wa jadi au hata Arusha Moshi kuna watu wana uzoefu wa kuvaa suti kwa sababu ya hali ya hewa muone.

    Lebo inakusaidia kujua aina ya suti bila kupekenyua ukishanunua inatolewa.

    Dar kumejaa washamba sana siku hizi bora Ditopile arudi!

    ReplyDelete
  15. Halafu wewe michuzi na hizi KEA OFU zako hizi..........., si umseme tu (mtaje jina) uliyemkusudia na ujumbe huu! Au tukusaidie kumtaja???????????

    ReplyDelete
  16. jamani ee hivi hizo lebo inakuwaje,

    mie nafikiri hizo suits za malebo ni zile za wamachinga wa kariakoo, mbona suits suits kweli za maana hazina ma lebo kwa nje, nijuavyo mie, nguo aina yoyote inakuwa na lebo kwa ndani sio nje, hivyo hata huku mamtoni suits zenye majina makubwa kama Austin Reed,Jaeger,TM Lewin zina lebo kwa ndani,sijawahi kuona malebo yananing'inia nje, sasa hizo lebo za nje sijui wana import kutoka wapi, na ni ma designer gani jamani hao... isije ikawa hizo suti zinatoka tu hapo urafiki au temeke kule wanakotengeneza kanga, kwa mtindo huo kama zina lebo nje basi zivaliwe hivyohivyo kwani ukitoa lebo na kitundu kikatokea bora ipi sasa??

    ReplyDelete
  17. mambo ya label ni uamuzi wa mtu anayemiliki suti.suti zingine unanunua label tu na sio suti. mfano canali inacost dala 1000 au zaidi kutegemea na unanunua mtaa gani China,Italy,Kariakoo au New York au online. Hamna sababu ya kujadili iondolewe au ibaki ni choice ya mtu na integemea suti hiyo inavaliwa katika occassion gani. Kama naenda kwenye interview ya kuomba kazi no matter what the label is it is not a good idea to show off.Kama unaenda kwenye party au wedding ni uamuzi wako tu na sio ushamba wala ujanja.What you do with your suit is your business.There is no acceptable universal standard or formality.

    ReplyDelete
  18. suti na label yake na fundi wake na taifa lake na designer wake. Eti kwa vile suti inaitwa Canali au prencipe haina maana kuwa ni bora kuliko suti ya kutengenezwa na mkono na Issa Rashid wa mtaa wa mchikichini Kariakoo.Ubora wa suti ni uhodari wa fundi na ubora wa kitambaa. Hivyo inawezekana kabisa suti ya Magomeni ikawa bei ghali kuliko suti ya Italy ya designer mkubwa. Kuna inequality katika biashara na watu wanafavor vitu kutoka mataifa ya magharibi. Wao wanajua biashara zaidi lakini si kweli kuwa vyote vitengenezwavyo huko ni bora kuliko vitengenezwavyo na Issa michuzi. Tuache kasumba za kutukuza vya magharibi. Suti kutoka Tanzania au Ghana au Nigeria inaweza kuuzwa New York kwa dala 5000 kutegemea na umaridadi wake hata kama label ya suti itaitwa Masai. Tuko nyuma sana kibiashara ndio maana lable zito hatuwezi kuzipromote na kuzifanya ziwe na quality ya kimataifa. Kuna ukiritimba wa kuzionea nchi maskini ndio maana sio rahisi ukute bidhaa za IPP ndani ya Supa Market ya Mzungu iliyo London au New York.Tujikwamue kiucumi na kupigana mambo ya biashara na utamaduni. Suti ya kitenge inaweza kuwa mali kuliko suti ya wool kutegemea na namna ilivyoshonwa na kukatwa na finishing na packaging. Mpo hapo wazee?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...