Hi! Bro michuzi,
napenda niwadunge wadau wa blog hii walioko juasun musoma(jeff,peter,mjarifu,kahenaki,justine na dugu ) picha hii ya adha za usafiri huku kigoma,hivyo wakiona nimekwenda likizo wajue ninapopita,hii ni siku ya tatu sasa kukiwa na mvua zisizokoma na hali ya barabara ndiyo hiyo mnayoiona katika picha. sasa pamegeuka kisiwa kwani hakuna kutoka. hapo ni njiani ukitokea wilaya ya kibondo kwenda kasulu na kigoma mjini katika kijiji cha Nyakitonto eneo la Galaganza karibu na redcross compound ila mimi niko salama naendeleza libeneke.

Mdau Gebo

everything happen for a reason

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Huku nako ni Tanzania? Kwa nini Kigoma msiombe mkahamishiwa Burundi mkawa tu mojawapo wa majimbo ya Burundi? Tanzania ni kubwa mno hatuwezi kuwafikia huko. We fikiria kukatiza pori lote lililopo kutoka Dar mpaka huko, tuna mambo mengine mengi ya kufikiria ati.

    ReplyDelete
  2. KAKA MICHUZI;

    KAMA UNAKUMBUKA NI SEHEMU ILE ILE NILIYOKUTUMIA NILIYOKUTUMIA PICH MOJA MWEZI WA NOVEMBA 2007.KUNA NYINGINE HAPA NIMEPIGA JUZI NITAKUTUMIA....HALI NI BADO TETE.

    ReplyDelete
  3. Wakati wa Kampeni za Uchaguzi walisema eti na barabara hizi za Kigoma zitatengenezwa ziwe kama za mikoa mingine. Ahadi hii imedumu kwa miaka kama 20. Leo wananchi wa mkoa huu wako hoi, miundo mbinu ndiyo kama hii. Mzee, hii ni Tanzania, mbunge wa Kasulu yuko busy anashughulikia michezo kwa sana. Hana muda wa kuangalia mambo haya.

    ReplyDelete
  4. Hao ni njian ukitokea wilaya ya kibondo kwenda kasulu na kigoma mjini katika kijiji cha nyakitondo eneo la galaganza karibu na redcross compound..pembeni ya mwembe ukitazama bondeni utaona mbuyu,kata kushoto kuna nyumba ya kalumanzira maarufu kama braza k ambapo kuna magenge wanauza mchicha,maembe,karanga nk"sijawahi kupata maelekezo kama haya.nina uhakika hakuna mtu yeyote atakayeweza kupotea.ha hahahahahaha

    ReplyDelete
  5. NA KUNA MTU AMECHOTA BILLIONI 133 NA SERIKALI INAMWANGALIA!!! MNASHANGAA HIZO BARABARA HATA DAR ITAKUWA HIVYO MUDA SI MREFU KWA MTINDO WA WIZI WA HELA YA SERIKALI (WANANCHI) UNAOENDELEA HAPO BONGO!

    ReplyDelete
  6. Kweli Kigoma iko kisogoni

    ReplyDelete
  7. Shikamoo kaka muchuzi!

    Mi kwetu ni KIGOMA, sasa roho imeniuma saana na nakwambia hadi machozi yamenitoka, MUNGU IBARIKI TANZANIA YA KINA MKAPA NA BALALI NA SASA KINA RICHMOND!

    Hadi sasa Sielewi kama KIGOMA kuna wabunge au wabwege!! Sasa huyu kaka yangu Zitto yuko busy na issue za kitaifa, analalamikia BUZWAGI, inamana haya hayaoni?? Afadhali hata Sanzugwanko kaamua kujikita na michezo, mana naona kishaona huu ni ujinga.

    Nakuomba vitu kama hivi weka katika magazeti na TV zinazoweza kusomwa na kuonwa na watu walio wengi. Sasa wakati ukifika tukiamua kujigawa kama mjumbe wa kwanza alivyoshauri, watanzania wasitushangae!!

    Inauma saana, naomba nisiendeele zaidi

    ReplyDelete
  8. Si bora tulete ngamia na punda jamani...at least bidhaa zetu zitafika on time bila kukwamakwama na hayo matope!!!

    ReplyDelete
  9. I want to criticise all the things that have been said above na kuhusu maisha kwa ujumla ya eneo husika si kweli kabisa yote yaliyosemwa hapo juu mimi naongea kwa experiance kubwa sana maana nimekaa eneo husika kwa mda mrefu na najua nini kinasemwa sio kweli kabisa
    Kwanza ukitaka kujua hayo si kweli ni neema na baraka ilizonazo mkoa wa Kigoma kitu kinachotokea hapo juu ni propanganda ambayo ipo miak nenda rudi juu ya mkoa wa Kigoma
    Kusema ukweli kati ya mikoa yenye neema na maisha ya kawaida ya kitanzania ni Kigoma kwa nini nasema hilo
    mfano kati ya mikoa ambayo haijawahi kutangazwa kupata baa la njaa hapa Tanzania ni Kigoma peke yake ukiacha ile inayoeleweka kwamba ina nafuu!!Pili Kigoma ndiko unakoweza pata vitu vizuri kuliko sehemu yoyote Tanzania mkumbuke tunapakana na nchi tatu Burundi,Zambia na Congo kitu kinachosababisha kuwepo na nafuu kubwa kwani kuna easy acess ya kutoka au kuingia ukitumia mipaka ya nchi hizi!! anyway kuna mengi ila kwa vile mtu anakuwa hafahamu basi huwezi kusema lolote
    Pia kila kinachotokea hapo kina Historia ndefu sana mengine hayaandikwi kwa vile watu hawafatilii historia ya yaliyotokea siku za nyuma
    ninaloweza sema ni kwamba Watanzania tunaishi kwa fashion na hili linasababisha mengi yanayotokea yasiwe na umuhimu kwao watu wanasema bora liende wasahau bila kujari effect ya jambo lenyewe na impact kwa mfano yote yanayotokea sasa na uhakika kabisa soon watu watasahau na itakuwa ile story ahh!! mwaka furani ilikuwa hivi!!tunaongelea utawala wa sheria tusizozifata nini maana ya utawala bora kama mtu hajari kwa nini anafanya ayafanyayo kwa vile anajua hata likitokea lolote hakuna atakayefanya kitu mbona yuko na hao watoa adhabu!!mbaya sana!!ukiuliza kwa nini inakuwa hivyo jibu kila mtu analo hapa@!!! kwa nini kwa sababu fashio yake imekwisha na itabaki kuwa kama ilivyo. ANYWAY NIISHIE HAPA LAKINI KUHUSU HIYO PICHA HAPO NI ENEO DOGO SANA LILIONGELEWA NA HALIWEZI KUWAKILISHA KWA UJUMLA HEBU MJARIBU KUANGALIA upande wa pili wa Kigoma nendwa kwa link hii
    http://video.google.com/videoplay?docid=-661780702001269646&q=kigoma&total=52&start=0&num=10&so=0&type=search&plindex=9
    Na useme sio kuzuri you just sit there unasubiri maisha yaje kwako maisha yako Kigoma huyo jamaa aliyeweka picha hiyo wala hajui nini kinafanyika napenda niishie hapo lakini usitoe maoni fikili kwanza la kusema!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...