Ndugu Michuzi na Wadau wote,
Naomba kutoa mapendekezo kuhusiana na mchango wa mtoto Samwel Ndkya. Kwanza kabisa ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa ndugu, jamaa wa mtoto kwa kuweza kufanikisha kutoa michango yao ikiwa ya fedha, mawazo, taratibu, muongozo au wa service kwa ujumla. Yote hii ni kujaribu kumuwezesha Samwel katika safari ndefu ya kuweza kujikomboa kutokana na maradhi haya. Mungu ampe unafuu.
Tukiongelea kwa ufupi tu, mimi binafsi na nafikiri na mapendekezo ya wengi wanablog humu ndani, wanayo haja ya kuweza kumsaidia mtoto huyu, lakini sasa kuna mambo machache yanayokwamisha mchango huu.
Kwanza kabisa, tungependekeza Michuzi na wanablog wengine, wangependelea kama wewe binafsi uwe ni muweka hazina ya msaada huu. Sababu moja kubwa kuu ya kukupendekeza Michuzi, ni nia yako ambayo umeionyesha ya kuwezesha kutufikishia habari hizi, na itakua wepesi sisi wasomaji na watembeleaji wa blog hii, kuweza kupata habari za Samwel kwa urahisi na haraka, ikiwa kiwango cha michango ilipofikia, matibabu na maendeleo ya Ndkya kwa ujumla.
Jengine, ambalo tunalifikiria sisi, ni jinsi gani ya kuweza kufikisha msaada wetu ili uwafikie, katika mfuko wa hazina wa mchango wa Ndkya, Mapendekezo yetu tungeomba kufunguliwa kwa account maalum ambayo wakazi wa nje au nchini Tanzania kuwawezesha kuingiza pesa za mchango moja kwa moja kwenye account husika, ikiwa kwa kupitia Credit Card au njia yoyote ile rahisi ambayo itawaruhusu walio wengi nje ya nchi, kufanikisha kwa urahisi ku-deposit hizo fedha. Hili swala tutakuachia wewe Michuzi kuweza kulikamilisha, kama utafungua account kwa ajili ya hili itakua vyema zaidi. Na utupe na uelezee taratibu nzima kabisa ya jinsi gani ya kufikisha huu msaada wa fedha kwenye account hiyo, kwa walio nje.
Jengine zaidi ni kuwajulisha na kuwaomba wanablog waweze kumchangia mtoto wetu, ndugu yetu Ndkya, kuanzia Dollar 5 au Euro 5 au Shilling 5000. Ni mategemeo yetu makubwa kwa tarakimu za upesi upesi, wakipatikana watu 1000, tu basi itakua mchango mzima umekamilika. Na hili litawawekea wepesi watu wengi kuhamasika kutoa mchango wao.
Tumpeni Samwel mategemeo ya maisha bora hapo baadae, Ajue watanzania wameonyesha moyo mzuri wa kuweza kufanikisha maisha yake, tukifanya hili kwa pamoja tunajipa utajiri wa mshikamano hapo baadae au kwa sasa, ikiwa sisi na ndugu zetu, sisi na rafiki zetu, sisi na majirani zetu, sisi na watanzania wote kwa ujumla.
UMOJA NI NGUVU.
au munaonaje wadau?
By Mchangiaji
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...