hello kaka michuzi,
heri ya mwaka mpya !!!kaka michuzi nahangaika kutafutanusery school in dar hamna website with properinformation.my daughter is moving to tanzania and im really struggling to get a school.its unbelivable how we don even have a website for schools jamani.naomba kama kuna mtu anayejua shule yeyote nzuri with agood standard(a good class school apart from IST) plz to send me some information, fees structures, contact, starting of terms n stuff.
i will appreciate

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. sasa wewe mbona kama bwege. kwani kila kitu lazima kiwe na website!
    nafikiri ist ni gharama ndo maana unakwepa, unapenda vizuri ila unaogopa gharama sio, mpeleke tu ist ambao umeona website yake!

    ReplyDelete
  2. Kama budget yako iko kwenye medium level..Jaribu kumpeleka Laurete International School.. Sijui kama wana web site..Binti yangu alianza Nursery na sasa yuko Grd 1..Kila nikirudi home naona uwezo wake wa kuelewa ni sawa na mabinti wa rika yake huku tunakoangaika..Lakini kama unavyojua Bongo..msaada wa mzazi kwa elimu ya mtoto ni muhimu sana lazima wazazi wawe karibu kufuatilia maendeleo ya binti kutokana na mazingira, uchumi na mambo fulani ya nchi yetu..Anyway..Kuna shule nyingine niliambiwa Best of the Best in Dar..Jina nimesahau..ila iko barabara ya Bagamoyo..baada ya Mbezi beach na njia panda ya kawe..kama unaendea wazo...All the best!

    ReplyDelete
  3. Laurete International School is good a friend of mine is teaching there and she is a very dedicated teacher.
    There is also another nursery school in Mikocheni my son was attending when we were there on a long holiday- fees $400 per term they have 3 terms per year,i dont remember the name but its alog a straight forward road from 2nd right turn from morocco junction towards science, there is a hospital agency office at the beginning of that road, the school is owned by 2 south african ladies its very easy to find when u ask around si unajua home tena we kind of know everyone.
    All the best.

    ReplyDelete
  4. http://www.almuntazir.org/amuns.asp

    ReplyDelete
  5. Nursery school Dar ni nyingi na pia ni nzuri ila inategemea unataka eneo lipi kutegemea na eneo unaloishi. Kama ni Masaki ziko Nursery schools, mpaka ambazo zinazofuata system ya kimarekani. Kama ni city center ziko mpaka zinazofuata system ya kihindi.

    Pia kuna Almuntazir Seminary, nao wana nursery school nzuri tu karibu na hiyo ya IST watu wanapeleka watoto wao bila kujali itikadi za dini ingawa ni ya kiislam. Vile vile kuna Aghakhan iko karibu na Zanaki sec school. Na Upanga nursery school karibu na Maktaba ya Taifa.

    Chang'ombe pia kuna shule nzuri ya Mama Kubaga ambayo iko jirani na TCC Club.

    Vile vile kuna nursery Mikocheni kama Academy, Lauriate, na nyinginezo. Kwa Dar inabidi mtu afanye kibarua cha kwenda huko shule ili aangalie na mazingira pia. Kwa watoto wadogo ni vizuri wakasoma jirani na wanakoishi. Mie watoto wangu wamesoma shule zilizo jirani ninapoishi wakiwa nursery na sasa wanasoma shule za primary maeneo ya jirani ambako wanaweza kwenda kwa gari au hata kutembea.

    Ushauri, tafuta shule yenye primary school hapo hapo ili kukuondolea usumbufu wa kuingia primary. Maana huwa wanachukua watoto wa nursery zao kabla ya watoto waliosoma nursery za nje ya shule yao.

    Pole na mchakato wa kutafuta shule ni ngumu kwa kweli.

    ReplyDelete
  6. Mtoa maoni wa kwanza anaonesha ni kwa jinsi gani ufahamu na uwezo wake wa kufikiri ulivyo mdogo. Kama alikuwa hana majibu angekaa kimya tu. Yaani kwa zama hizi kama mtu hajui faida ya kuwa na website kwaajili ya kujitangaza na kukuza biashara basi tuna safari ndefu sana mpaka tufike huko tunakotaka kwenda. Kwa ujumla Tanzania tupo nyuma sana katika swala zima la kutumia teknolojia kukuza biashara.

    ReplyDelete
  7. Nashauri..Laurete International School in Nursery, Primary hadi Secondary School..

    ReplyDelete
  8. mimi sishauri mtu hapa kuhusu shule wala chekechea,

    wa tz kwa kujidai ndio wenyewe, wewe sijui ni dada au kaka unaemtafutia mtoto wako shule umeniudhi sana, hapa nilikuwa nasoma komments tu wala nilikuwa sina shida ya kukomenti ila imenibidi,

    yani wewe ndugu hivi huna ndugu kabisa hapa nyumbani hata mmoja wa kuweza kukutafutia shule, au ni makiadai tu tukuone eti unarudi home kutoka majuu,

    halafu unaponda eti tunashindwa hata kuwa na website,kama huna ndugu home ninakusamehe ila kama unao nakuona huna maana unataka kupotezea wtu muda wao tuu, nakusikia wanasema nini,

    na wewe dada sijui baba unasema eti mtoto wako alisoma shule moja ulivyokuwa kwenye long holiday, ila hata jina hukumbiki, siniuongo jamani, wewe mbumbu kiasi gani mtoto wako alisoma hapo ikiwa holodai na unasema long one but hata hujui jina iti unasema sijui iko barabra gani sijui,
    na wewe mwingine unaaelekeza sijui barabara gani kata kushoto karibu na wapi sijui kata kulia wote huo uongo,

    watu nimewashtukia hapa nikujionyesha tuu, japo hata majina yenu na sura zenu hatuzioni, kujidai tu mko majuu basi, kwani watu wangapi wako majuu na wanaishi kama watu wengine,

    huu ni ujinga ujinga kabisa, tena aibu zako,
    lione kwanza mimi nimekasirika sana,mpuuzi wee, yani unaonekana huna cha mtoto wa kusoma wala nini.

    ReplyDelete
  9. Kama hao waliotangulia walivyosema, ni muhimu kujua wapi watakaa sababu ya usafiri. Chekechea zipo nzuri kila mahali.

    Bagamoyo Road karibu kabisa na nyumba ya Kambona kuna shule inaitwa DIS ni nzuri sana, Masaki kuna shule inaitwa Dar Academy ni mpya ina kama miaka miwili au mitatu hivi. Hizo zinafuata system za UK. Haven of Peace ipo barabara panda ya Kunduchi kwenye shamba la Mantheakis, hii ni system ya US. Kuna chekechea ya Kifaransa karibu kabisa na Oysterbay Hotel, pia najua kuna shule ya wa-swede, sasa sijui familia yako inatoka wapi na lugha gani unapendelea. Kuna Kwanza nursery ipo opposite na Kwa Nyerere, Mikocheni A ile njia ya Cocacola kuna shule pia ila nimesahau jina lake pia yenyewe ni nzuri tu. Sunrise ipo Chato str. pale Regent.

    Ukitaka boarding jaribu St. Constantine Arusha, Iringa pia kuna shule nzuri tu na ni ya watoto wa wafanya kazi wa kiwanda cha karatasi.

    Cha muhimu ni kutafuta shule ambayo iko kinyume na foleni za magari, vinginevyo ukitaka kutumia usafiri wa shule hawakawii kukuambia ya kwamba maeneo yako mtoto lazima awe tayari saa 12 asubuhi na watamrudisha kwenye saa 11 jioni baada ya watoto wenzake kushushwa. Hii itamfanya mtoto achoke sana (kumbuka barabara za Bongo ni mashimo matupu) na hatimaye kuichukia shule. Vinginevyo ni muhimu kuwa na usafiri kwa ajili ya watoto tu.

    Nakuombea mafanikio,

    Ubarikiwe.

    ReplyDelete
  10. We mtoa maoni hapo juu mbona una roho ya korosho namna hiyo?? You sound so EVIL...kwani kuna kosa gani kuuliza swali kama hilo?? ehh comment zako zila dalili za wivu wa maendeleo ya wengine. Sijaona kuna shida gani kwa mtu kuuliza shule wether ana ndugu home au la, na kama hujisikiii kujibu shut the hell up..instead of talking like that. Wivu haujengi badala yake unakuumiza bure..

    ReplyDelete
  11. Mtoa maoni wa kwanza na wa 7:54 unajua ni kwa vile sijui mpo bongo hivi mtu akiuliza shule ni makidai...kwani kuishi nje ya nchi ni jambo la kujivunia sanaaaa...Sisi wengine tunaona sio jambo la ajabu na kuuliza ni kusaidiana kama angekua huko akimtafutia mtoto wake angeambiwa ni makidai pia???? hapa watu wengi wanajua na ameona wengine wanelewa mimi mama yangu mzee hajui hata nursery nzuri sasa kama ni kuuliza ushauri hata mimi ningeweka hapa tu...

    Mbona watu wakiulizia shule nzuri nje ya nchi hamna mtu anayesema ni makigai ....


    I wish ningekua na uwezo wakuwaleta wabongo wote nje ya nchi japo kwa siku moja tu ili muelewe....Watu wako so normal huku na kila wanalofanya n i normal life huko kwenu ni makidai...Nilienda bongo nataka kufanya something mama anasema watu watasema....INABIDI TUBADILIKE KIDOGO

    ReplyDelete
  12. mie sielewi mnavyoandika na kuponda hapa wakati huyo muhusika ametoa anuani yake..
    kaka au dada uliyeuliza ni kwamba kwa experience yangu mie sijapeleka mtoto shule wala binam ni mie mwenyewe niliyesoma hiyo shule.ipo kimara upande wa kushoto kutopka ubungo shule inaitwa filbert bay na ina secondary yake kibaha.mie nimesoma hapo na mpaka sasa nipo huku USA nakumbuka malezi yao bila wao mie ningekuwa sijiwezi kabisa.ina boarding kuanzia pre unit na ina day,

    ReplyDelete
  13. mtoa maoni wa 7.54....why do u have to be so ignorant?????? kama wewe unaona ujiko kukaa nje basi ni wewe mimi sioni ndio maana natafuta shule na narudi kwetu ,nafanya kitu chenye faida kwangu na wengine wengi wasiojua pakutafuta shule jee kama ndugu zangu wanaishi kijijini ?????hapa ni sehemu ya watu wenye experience ,upeo tofauti mbona wengi wamejitole kunisaidia kutafuat information na waliokuw wanajua wamenitumia personal emails kunisaidia ushauri !!!wewe nakusamehe bureee sina cha kukujibu theres no need kubishana namtu kama wewe ignorant to an extreme ,bisha kitu chenye umaana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...