WADAU KUNRADHI. HIVI SASA TUNAJONGELEA KWA MDAU ATAYEKUWA WA MILIONI 3 KUINGIA KWENYE GLOBU HII YA JAMII, AMBAPO KAMA MAMBO YAKIENDA VYEMA NA MFADHILI WETU, MDAU HUYO ATAJISHINDIA ZAWADI YA DOLA 500.
MASHARTI YATAKUWA NI YALE YALE TU; ATAKAYETHIBITISHA KWA KUTUMA POSTI YAKE KUWA NDIO YA MILIONI 3 KWA WAKATI MUAFAKA NDIYE MSHINDI.
AIDHA, BAADA YA KAMATI YA UFUNDI YA GLOBU HII YA JAMII KUKETI NA KUTAFAKARI KWA KINA, IMEONEKANA KWAMBA SI AALI KUANGALIA KAMA MDAU HUYO WA MILIONI 3 ATATOKA WAPI - UGHAIBUNI AMA BONGO - KWANI DHANA YA BAHATI NASIBU HAINA MUAMANA.
KWA MAANA HIYO MDAU YEYOTE POPOTE ALIPO DUNIANI AKITHIBITISHA KWAMBA YEYE NDIYE WA MILIONI 3 ATALAMBA DOLA 500 NA UAMUZI WA KAMATI YA UFUNDI WA GLOBU HII NDIO WA MWISHO.
NAOMBA KUWASILISHA...
MICHUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. habari ndugu michuzi, mm naomba kujitokeza na kusema kuwa zawadi hiyo naiomba mm kwani nafikiri mm ndiye mfunga dimba hapa.george mavura.Philadelphia, USA.

    ReplyDelete
  2. grmavura@yahoo.com
    7022terminal sq
    19082
    PA.
    mm nahisi ndiye mshindi.

    ReplyDelete
  3. kutuma post?? lazima ujiandikishe? wengine mara yetu ya kwanza kuingia hii blog boss, msaada

    ReplyDelete
  4. Mie sio mtalaam wa mtandao lakini huwa kuna kafundi kanafanyika kwenye web, hako ka technologia ukifika namba uliyoset inaonekana kwa mambwembwe kuna ka pop up kanasema kuwa wewe ni mtu wa hiyo namba iliyosetiwa kama kwa hii blogu ni wa milion 3. Hivyo inakuwa rahisi huyo mtu wa milion 3 kujijua kuwa yeye ni wa milion tatu na nyie wenye web blogu yenu munajua kuwa mtu wa milion tatu kapatikana, na hiyo njia inakuwa haina ulalamishi. Hebu fanyeni hako ka ufundi kuondoa malalamiko.

    ReplyDelete
  5. Michuzi mimi nikishinda hiyo pesa nitadonate popote pale ambapo kunasaidia watoto yatima,na ukumbuke ni mimi mdau wako mbeba box

    ReplyDelete
  6. Braza Michuzi,

    mwaka 2010 nakuja kugombea Ubunge ndani ya Bongo, naomba endorsement yako braza ili tujenge nchi.

    itabidi nikutafute tupate lunch ya usiku nikija vekesheni ila simpeti mai waifu wangu mpaka na wewe umelete mai waifu wako manake brother Michuzi wewe kwa Mokonooz hatari!!!

    ReplyDelete
  7. Mbona wengine hatuelewi, tutathibitishaje kuwa ni wa ml 3? Maana kila comment inakuja annon
    Tafdhali fafanua tuweze kuelewa maana mimi ni mmoja wa wadau wakuu wa hii blog

    Nikipata zawadi au hapana, sijali, la msingi mchezo uwe fair! Siyo kubebana kama inavyotaka kutokea hapa~

    ReplyDelete
  8. kaka michu usitake kuleta kamchezo kako ka kifisadi,zingatia;wewe ni m-bana comments,pili hata ulaya phone in competitions mshindi alikuwa anachaguliwa kabla na wengine kuzungwa sasa suprising mshindi wako ambaye atakuwa mdau wa mil 3 atakuwa mwanamke cos utajidai kubalance gender sasa usituzuge ,tuache tuenjoy blog sio ahadi hewa,mbongo ni mbongo tu

    ReplyDelete
  9. POST HII NDIO YA MILIONI TATU NA NIMEITUMA WAKATI MUAFAKA.

    SASA NASUBIRI KAMATI YA UFUNDI IWEZE KUFIKIA UAMUZI WA MWISHO.

    ASANTE

    hot4life@hotmail.com

    ReplyDelete
  10. nadhani mi ndo mshindi, sababu sielewi mcezo unavyochezwa, no maelezoz

    ReplyDelete
  11. okay michuzi na mimi nimo...
    sthugs4j@gmail.com

    ReplyDelete
  12. Braza Michuzi najua mimi ninashinda, isipokuwa hivyo nitakujumuisha katika listi ya mafisadi!!

    ReplyDelete
  13. Hi Bro Michuzi,
    I Know am the one,p'se send me the money.
    Upendo Kunda.

    ReplyDelete
  14. Mambo. Mimi nimefungua blog yako na kujikuta ni wa MILLIONI TATU, lakini nimeshindwa jinsi ya kuweka ushahidi maana hapa nilipo sina KAMERA. Inasikitisha, lakini ndiyo imetoka. Tayarisha utaratibu wa kisayansi ambapo yule anayefungua uweze kumtambua haki itendeke. Shindano lako naona hujaliwekea vigezo vya kisayansi vinavyowapa haki sawa washiriki, walioko UGHAIBUNI, Tanzania bongo, Tanzania mikoani na Tanzania Wilayani/vijijini. Nawasilisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...