Msaada kwenye tuta,

Kuna mada ulitoa kuhusu suti zenye lebo,ile mada ilikuwa fine sana nimejifunza mengi sana.
Sasa nataka kuuliza wadau je upi ni uvaaji sahihi wa tai kati ya
1) Tai iwe ndefu mpaka kwenye kiuno i mean kwenye mkanda or
2) Tai iwe ndefu mpaka kwenye maeneo ya kitovu juu kidogo.
Pili Tai inavaliwa kulingana na color zinavyo fanana na nguo ulizo vaa au Tai ni tai hata kama color yake haifanani na nguo yoyote uliyo vaa.


Mdau Brayan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. hiyo mbona simple...gentleman anatakiwa kuvaa tai ifike kwenye maeneo kitovu..izungushwe mara mbili ili-kisambusa kitoke pina sio kiduchu na vile vile chini ya sambusa unakipiga ki-dimple...colour zina tegemea rangi na pattern ya shati na trouser..ikija ku-coordinate hapo inatiakiwa rangi zisi-clash na pattern na visa versa...

    ReplyDelete
  2. Mchango wangu ni kuwa hakuna standard maalumu ya uvaaji wa tai. Kama utaiweka ndefu ni jinsi mwenyewe upendavyo, na ukitaka fupi ni chaguo lako.

    Hata hivo, mimi nijuavyo mtu anayevaa tai katika vazi kwa shughuli rasmi, anavaa tai fupi kuishia kwenye kitovu. Hata hivo, kwasababu tai si utamaduni wa Wabongo, imekuwa kawaida mtu kuvaa tai kwa namna apendayo, iwe ndefu au fupi, hiyo mosi. Lakini pili, wabongo wengi (si wote) hawajui taiinavaliwa wakati gani. Kimsingi watu wanavaa tai, hasa nchi za Ulaya na Marekani kwenye tukio maalumu kama unapohudhuria mkutano, kikao, harusi, kwenda ofisini, au unapofanyiwa usaili (interview) ya kazi, au unaomba kuchukua tenda fulani, nk. Pia inavaliwa sana na maprofesa, tena wale waliobobea katika taaluma 'distinguished' ones. Acha mambo ya sasa hivi unakuta kuna baadhi PhD zimewapata wataaluma badala ya wao kuzipata. Nina maana kuwa ukishakuwa profesa kwa mfano, no excuse ya kwenda kwenye mikutano au vikao rasmi na ukajifaya unakwenda na wakati kwa kuvaa T-shirt. Wapo wa namna hiyo, na unakuta wanashabikiwa eti wapo 'simple' na 'poa'. What is poa? Kila field au taaluma ina maadili yake bwana.
    Bongo nionavyo mimi hakuna anayefungwa kuvaa tai kwa namna fulani, iwe fupi au ndefu, kwani kimsingi kila mtu anavaa, hata mpiga debe, hata kama hajaoga wala kuchana nywele. Na unakuta kavaa ndala na kaptura na kwenye shati kaning'iniza tai. Hizo irregularities huwezi kuzionanchi za watu huku, hata USA ambako sometimes wako 'laid back'.

    NAWASILISHA.

    ReplyDelete
  3. Tie should just reach your belt buckle. Try not to match it with your shirt as Tie is supposed to stand out on its own but if you cant try to wear a tie with subtle lines that matches your shirt I know some people will disagree with my comment, you dont want to match tie with a shirt.
    To anony 917pm.
    FYI:You dont have to be a distinguished prof. to wear a tie and also I dont think going to work/office is "tukio maalum"

    ReplyDelete
  4. Please if you don't know how just wear suit without tie and you will look just fine.Because some people just make us dezzy.

    ReplyDelete
  5. Eeh kwa utaalam nilionao wa designing and decoration tai huvaliwa hadi chini ya magoti kwa sisi mapededjee,na tai nzuri ni zile zilizoshoneshwa kwa kitenge au kaniki,historia inaonyesha vazi la tai lilikua ni sehemu ya utumwa kwani kama vile dogs wanavyofungwa na mnyororo ili wasikimbie ndivyo na tai ilitumika kuwadhibiti watumwa,kuhusu rangi ni simpo mfano ukivaa suruali nyekundu yenye mistari ya kijivu na shati la njano lenye maua ya bluu chini umepigilia mokasini za kijani na soksi za rangi ya ukili basi hapo tai inayomatch ni rangi ya zambarau iliyonakshiwa na maua ya rangi nyeusi...Warning : Hakikisha hukatizi eneo lenye nyuki wengi for emergence!

    ReplyDelete
  6. WAJAMENI HII MADA NIMEPENDA KWASABABU KUNA BAADHI YAWATU WANAKERA NA MUONEKANO WAO. VAZI LA TAI ASILI YAKE ULAYA LAKINI UFUNGAJI TAI NI MMOJA KWAMAANA NAJUA SIO WATU WOTE WANAJUA KUFUNGA TAI, WANAUME BAADHI TAI WANAOMBWA KUFUNGIWA ILA UAMUZI WA KUWA NDEFU AU FUPI NI MAPENDEKEZO YAKO ILA NACHOJUA TAI FUPI ASILI YAKE NI SPECIAL KWA WAITERS UKIACHILIA MBALI ZIKE BALLTAI TAI INAKUWA FUPI SANA ILI ISIINGIE KWENYE MCHUZI NA SIO "MICHUZI" USININUKUU VIBAYA, TAI INAKUWA MODIFIED KUTOKANA NA WAKATI KWASABABU ZAMANI TAI HAIPITWI NA WAKATI ILA UFUNGAJI NA DESIGN NDIO ZINABALIKA UNAFUNGA NDEFU MPAKA TUMBONI SASA HIVI WANAFUNGA FUPI KIASI USAWA WA KITOVU SABABU ATA MAKOTI YA THREE PIECE YAMETOKA KWENYE WAKATI, ZAMANI TAI NYEMBAMBA NDEFU NA VIFUNGIO KIBAO KM VIBATIBATI KIBAO. RANGI NI MUHIMU KUFANANA JAPO NA SHATI, CHRISTMASS TREE NI ZAMANI. KUNA MASHATI HAYAENDANI NA TAI MFANO YA KUCHOMEKEA NA KOLA ZINAMATA KWENYE TAI NA MASHATI YA MAUA SI YAKUFUNGIA TAI.

    ReplyDelete
  7. Mijitu mingine bwana, mtu anatoa mada kwa kiswahili yenyewe inajidai kuchangia kwa kiengereza, kwan mmesikia watu hawajui hicho kiengereza chenu kibovu, na kama mnajidai kiswahili hakipandi, sasa mada mmeielewa vipi kama sio unafiki huo??

    ReplyDelete
  8. wadau mimi nafikiri au niseme kwa uzoefu wangu tai inapendeza ikiwa ndefu mpaka maeneo ya kitovu and pili iwe imefungwa vizuri kwasababu siku hizi watu wanavaa tai zimefungwa hovyohovyo nikimaanisha lile fundo la shingoni imezeleka kwa jina kisambusa linatakiwa liwe kubwa kidogo na limekazwa vizuri kwa ajili ya muonekano mzuri zaidi.na tai isiwe nyembamba sana kwenye ulimi wake.

    ReplyDelete
  9. Anony wa 1: 52am umenikosoa kuwa si lazima uwe distinguished profesa, nashukuru. Lakini una matatizo ya kutafsiri Kiswahili. Narudia, nimesema;

    "Pia inavaliwa sana na maprofesa, tena wale waliobobea katika taaluma 'distinguished' ones."

    Kama Kiswahili umeelewa, basi hapo nilikuwa naonyesha msisitizo kuwa tabaka moja linalojitokeza sana kwa umuhimu wa tai hi hili. Neno "PIA" lina maana ya nyongeza, baada ya kutaja vitu mwanzo. Nami niishawataja wengine au mahali unapoweza kuivaa tai. Neno dogo sana limebeba maana nzima ya sentensi. Linaweza kumfunga mtu au kumweka huru kwa jinsi lilivotumika.

    POLE.

    ReplyDelete
  10. we jamaa, we unaonyesha kingereza hakipandi, unajua kusema "saa ngapi sasa hivi" kwa kiingereza?

    ReplyDelete
  11. Jibu "how many watches now"

    ReplyDelete
  12. Duuu! hii kali, huu ni mjadala wa Tai au lugha?!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...