Kwa miaka nenda rudi, tangu miaka ya sabini,jina la Freddy Macha (pichani) sio geni miongoni mwa wasomaji mbalimbali wa magazeti, vitabu vya hadithi fupifupi,wapenzi wa muziki na pia sanaa ya ushairi nchini Tanzania. Iwe unamfahamu Freddy kupitia muziki wake,makala zake au mashairi yake, utakubaliana nasi kwamba Freddy ni mojawapo ya hazina tulizonazo linapokuja suala zima la usanii. Wengi miongoni mwa wasomaji wa makala zake katika magazeti ya The Guardian na Mwananchi nchini Tanzania, wanakiri kwamba makala za Freddy huwa ni mojawapo ya sababu zinazowafanya wakati mwingine wadamke. nenda www.bongocelebrity.com upaate uhondo zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. KWENZETU ULAYA NI KITABU CHAKE NILICHOWAHI KUKISOMA :NASIKITIKA KWAMBA KWA SASA SIKIONI MADUKANI>>>HAPA BONGO.MUZIKI WAKE SIJAWAHI KUSIKIA ILA MAKALA ZAKE NASOMA SANA>AMANI KWAKE KAKA

    ReplyDelete
  2. kwakeli fredi namkubali sana hasa kwa makala zake za kusisimua kila wiki ktk magazeti ya mwananchi, kinachonipendeza hasa anapotupa story za ughaibuni. yaani some time ukisoma unakubali kumbe maisha si ulaya kama tunavyofikiria vijana wengi kuna gharama zake kuishi ughaibuni.
    Namtakia maisha marefu yenye furaha na amani na azidi kutuletea makala motomoto

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...