jk juzi na jana alipokea ujumbe toka kwa watani wetu wa jadi ukimwakilisha rais mwai kibaki ulioletwa na mh. uhuru kenyatta (juu) na mwingine toka kwa mpinzani mkuu mh. raila odinga wa odm ulioletwa na katibu wake mkuu profesa peter anyang'nyong'o (chini) katika haraakati za kutafuta muafaka baada ya songombingo lilofuatia kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuu. wadau hii imakaaje?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. SIFA ZA KIJINGA!!!!!!....


    Papa Upanga

    ReplyDelete
  2. Huyo Uhuru Kenyata kaleta umbeya tu anajua Kibaki alichafanya hana lolote zaidi ya kusubiri kupewa uwaziri tu.Siasa za Afrika bwana ovyo sana sasa anajua fika wamesababisha mauaji makubwa ya raia wasio na makosa afu analeta ujumbe kwa JK wa Kibaki sasa JK afanye nini?Au ndo kale kausemi ka Kibaki kushangaa why JK mpaka leo kakaa kimya bila kumpa Pongezi?Uhuru Kenyata kwa mtaji huu ndo kakiua kabisa chama cha KANU ambacho Mhasisi wake ni baba yake mara kumi angilishirikiana na ODM.

    ReplyDelete
  3. INAPENDEZA KUONA SERIKARI YETU IKO MAKINI KIASI GANI,NA HASA KUTOKURUPUKA MKUNTAMBUA MTEULE WA MASHAKA KAMA ALIVYO FANYA RAIS MTARAJIWA WA SHIRIKISHO LA AFRIKA MASHARIKI.

    ReplyDelete
  4. Ndio mnataka waje kwenye Federation hao na ukabila wao sisi Bongo (Home)hatuna ujinga huo waambieni kabisa hata hao wachache waliopo hapo na kuinsult watanzania sijui chiriku sijui white elephant wapi nyingi Bongo ndio NY Yenu na tunaleta undergraound kama ya hapa London soon. Amani Tz amani Dar jiji la maraha nalimiss kinoma
    Peace ya'll

    ReplyDelete
  5. Kesi ya Nyani unapelaka kwa Tumbili.Unategemea nini???

    ReplyDelete
  6. Mimi watu wakimponda nyerere huwa nawashangaa sana.Tanzania tunajivuna sasa,hatuna ukabila kama wenzetu sabau ya Nyerere.Huu ni wema usiopimika aliotuachia Nyerere.Wenzetu sasa wanahangaika kwa vile walimkosa mtu kama nyerere,ambaye angewajengea upendo,umoja na mshikamano miongoni mwao bila kujali rangi,kabila,udini,ujimbo....
    Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Mwalimu.Tutakukumbuka daima.

    ReplyDelete
  7. Wakenya kweli wanaamini kwamba Tanzania tunaweza kusuluhisha mgogoro wao.Mimi binafsi nadhani hilo haliwezekani kwani hata sisi wenyewe mgogoro wetu wa Zanzibar hatuja usuluhisha sasa iweje tuweza kusuluhisha balaa kubwa la wizi wa kura uliofanywa na Watani wa jadi wetu.
    mambo ya wizi wa kura sio mageni hata Nyumbani kwetu na hiyo yote inatokana na Serikali nyingi za Afrika kukataa kuwepo na Tume Huru za Uchaguzi.Wewe uliona wapi simba ikicheza mechi na watani wao wa jadi yanga, mwenyekiti wa Simba ndio achague refa wa kuchezesha mechi hiyo.......unategemea Yanga itashinda.Sasa Rais ambaye yupo madarakani ndio anachagua Tume nzima ya Uchaguzi nini unategemea kitatokea...................hahahahaha ni wizi tu wa kura na machafuko baadaye

    ReplyDelete
  8. Lakini jamani wakenya wanapenda mademu wetu wa kitanzania wacha tu mimi hawa watani wakija inabidi tufungie mademu wetu kabla mapepa hayajatoka.Maana naona huu ujirani umefika jikoni na mademu wetu walivyo bomba basi ipo kazi.Any way naona jamaa wanatutaka tuwashauri na hiyo ni sifa kubwa.Karibuni watani maana tuna mengi ya kuwaambia kuhusu ukabila.

    ReplyDelete
  9. Kenya we hope for the best but tribal conflicts have to stop.there is no magic like one love watani.Don't have your head up too high because western countries mention Kenya everyday,be wise.You will always be African on face of the earth.Violence never solve anything look at Iraq today with no solution on the table.Be wise people.UMOJA NI NGUVU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...