Bwana Michuzi,
Naomba usome mail hii kisha ukiona inafaa uiweke kwenye blog yako wadau wanisaidie/wanishauri. Ila kama utaona haistahili, basi achana nayo, ila tafadhali usiweke e-mail yangu hadharani.
Mimi ni Mama nimeolewa na nina watoto watatu, ninaishi hapa Tanzania ninafanya kazi shirika lisilo la Kiserikali. Nimeishi na mume wangu kwa miaka mingi sasa kwa raha na karaha pia. Mume wangu alikuwa akifanya kazi shirika fulani, lakini kwa bahati mbaya aliachishwa kazi miaka miwili nyuma kutokana na sababu flani flani.
Wakati mume wangu akifanya kazi, tulikuwa tukiishi nyumba ya shirika alilokuwa akifanyia kazi, na baada ya kuachishwa, nikaomba nyumba ya shirika na nikapewa ambayo tunaendelea kuishi mpaka sasa.
Let me cut the story short.
Ni kwamba miezi kama sita baada ya mume wangu kuachishwa kazi, mara siku moja jioni natoka kazini nakuta watoto wawili wameongezeka wakiwa na bag kabisa, nikamuuliza mwenzangu ugeni wa wapi huu, akadai ni habari ndefu japo baadae alikiri ni watoto wake/wetu mtu mzima nikajua haya ni matunda ya zile siku alikuwa akilala nje nikawapokea na kuwatambulisha kwa watoto wangu kwamba na hao ni ndugu zao.
Kama hiyo haikutosha, baada ya kama miezi miwili hivi akaletwa Mama wa watoto hao (mke mwenzangu)!, Nikauliza itakuwa vipi na sisi ni wakristo wa ndoa moja tu, tutaiambiaje jamii? Yule Mama akadai hapo haondoki kwani kaja kulea wanawe na hana imani na mimi kumlelea watoto wake. Nikabeba mzigo kwamba sawa na akae lakini kwa kivuli kwamba ni ndugu wa mume wangu (nakiri udhaifu kwa hili).
Siku zikaenda kificho nje lakini ndani inajulikana na yeye ni Mama kwani hakukuwa na kificho hicho hata kwa watoto! Tuliita wazazi wa pande zote mbili kusuluhisha, siwezi kuwalaumu kwa kufuata sheria za dini kwani walidai katika kiapo cha Ndoa tuliapa kutokuachana mpaka kifo kitapotutenganisha, na kwamba nivumilie ndio mitihani katika maisha.
Nikavumilia kwamba huu ni msalaba wangu niubebe mwenyewe. Kinachoniuma sasa ni kwamba ndani ya nyumba hakuna tena maelewano kati yangu na Mume wangu, na tumegeuka maadui mimi na mkwe mwenzangu, kiasi hata kile kificho kwamba ni ndugu wa mume wangu hakipo tena kwani mbali na watu kuhisi, yeye alikuwa mstari wa mbele kutamba kwamba na yeye ni mke kama nilivyo mimi, hivyo ana haki na mamlaka ndani ya nyumba, kuwekeana nyimbo za vijembe na kuvaliana kanga za mafumbo zinazonunuliwa kwa hela yangu! Kero ni nyingi ndani ya ndoa yangu nyingine hata aibu kuzisema hadharani, na nikisema tuachane Mume wangu anakuja na visingizio kwamba ninamnyanyasa vile hana kazi na mimi nina kazi, wazazi nao wanadai sio vizuri watoto kulelewa upande mmoja, Jamani nimeshindwa na sina raha ya maisha tena nifanyeje?
Mke mwenzangu nikampa ushauri walau apange chumba nje ya nyumba yetu tutamlipia hataki, anadai atakuwa pale mume wake na watoto wake watakapokuwepo! Sijui, labda mimi sio mvumilivu vya kutosha, lakini kweli niko njia panda naomebi uhsuri nifanyeje jamani.
Sina raha tena na ndoa yangu, na maisha nayaona machungu. Ieleweke, sio kwamba vile hana kazi ndio maana nafanya hivi, hapana ila manyanyaso na vituko ndani ya nyumba nimechoka.
Samahani kwa kuwapotezea muda kuwaelezea shida zangu, naomebi msaada wenu Watanzania wenzangu.
Kwa Mume wangu, najua ukisoma ujumbe huu utajua ni wewe na familia yetu naiongelea, nisamehe kwa kuchukua uamuzi huu ni kwa sababu sina pa kukimbilia tena, acha tusikie wanajamii wengine wanasemaje then we can act on the advise.
natanguliza shukrani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 80 mpaka sasa

  1. Dada yangu pole yaliyokufika. Mfukuze akaishi na watoto wake huko katika nyumba atakayotafuta. Mume 1 mke mmoja unamkaribisha nyoka ndani ya nyumba yako unataka akungate ndio uelewe kosa lako siyo? Ukewenza? Nobody want to share! Ni kina Sangoma waliokufanya hivyo au kitu gani hicho!

    ReplyDelete
  2. Pole sana dada! kwa vyovyote ni lazima uchukue hatua...

    mimi ningekushauri uchukue watoto wako uanze maisha mapya...

    hiyo sio ndoa ya kwanza kuvunjika, na pia ndoa haimaanishi mateso na kifo... maana huko ndio naona unaelekea.

    Pole sana na chukua uamuzi wa busara.

    ReplyDelete
  3. HAPO NDIO HUA NAPATA KIGUGUMIZI NA UKIRISTO. SHERIA YENU INA KATAZA WAKE WENGI, LAKINI NI WACHACHE WANATEKELEZA HIVYO JAPO WAKIRISTO WAMEKUA MSITARI WA MBELE KUKASHFU NDOA YA WAKE WENGI YA WAISLAM. NI BORA HATA KUO UISLAM AMBAO UMEANGALIA HALI HALISI KWAMBA KUNA BAADHI YA WANAUME HAWAWEZI KUTOSHEKA NA MKE MMOJA NDIO MAANA UKATOA RUKSA KWA MWENYE UWEZO, UADILIFU VINGINEVYO UONE MMOJA TU. NDOA NYINGI ZA WAKRISTO ZIMENGIWA NA LUBA, KWA MATATIZO KAMA YANAYO MKUMBA DADA ETU NA WENGINE WAMISHI KILA MTU CHUMBA CHAKE HATA KUKUTANA KINDOA HAKUNA LAKINI NJE WANAZUGA KWAMBA WAO NI MKE NA MME ETI KILICHOUNGANISHWA NA MUNGU BINADAM HAKITENGANISHI!!!! ILIHALI TAYARI WAKO SEPARATE. WENGINE WAMEKUA NA VIMADA WANAO WAPENDA SANA LAKINI HAWAWEZI KUWAOA KWA SABABU HIYOHIYO. WANAZITESHA NAFSI ZAO, NA BAYA ZAIDI WANAFANYA UNAFIKI WA HALI YA JUU KWA JAMII NA MOLA WAO.

    KUHUSU SHIDA YA DADAETU. KWA KWELI HAIWEZEKANI HATA SIKU MOJA UKACHANGANYA HALALI NA HARAMU PAMOJA. YULE SI MKE, NA NI DHAMBI HATA KUMUITA MKE "MWENZANGU" NI HARAM SANA. NI BORA KUMUITA MZINZI WA MMEWANGU" AU MZINZI MWENZAKE NA MUME WANGU" ONDOKA NDANI YA NYUMBA HIYO AU LA MMEO AMFUKUZILIE MBALI HUYO MALAYA MZINZI, ILA WATOTO WABAKI KWA MAANA WAO HAWANA MAKOSA YOYOTE NA WALA HAFAI KUITWA WATOTO WA HARAM MAANA HARAMU SI WAO ILA NI WAZAZI WAO. WAPENDE SANA WATOTO ILI MOLA WAKO AKUSAIDIE KUONDOA LUBA HILO KWENYE MAISHA YAKO.

    MZEE WA BUNJU

    ReplyDelete
  4. unajua siamini!whats wrong with you?huwezi kusimama na miguu yako mwenyewe?gal, you have o live your life the way you want sio kusingizia ndugu wa mume,hellloooo!unaletewa mwenzio mpaka ndani bado upo?unataka uambiweje?
    sijuagi kama wanawake wa dizaini yako karne hii ya 21 bado wapo!sikuonei huruma hata kidogo, uko so weak,hujiamini,na unawatesa wanao!usidhani wewe ndio wa kwanza kuvunjikiwa ndoa,wapo wengi na going strong vilevile!au unasubiri maradhi dada?
    please,please unatudhalilisha wenzio!kha!

    ReplyDelete
  5. achana na hao kupe...waache solemba..kaanze maisha yako somewhere else.....Huyo mumeo hana adabu, haya wala shukrani....wakibaki wenyewe watalijua jiji na mataa yake...

    ReplyDelete
  6. Sijawahi kusikia hamu ya kuweka comments zangu kwenye blog hata siku moja lakini leo wewe mama umenigusa nikahisi unahitaji kusoma hizi zangu.

    Huyo anayekushauri kuwa uliahidi kanisani kuwa hamtaachana na mume wako mpaka kifo kiwatenganishe yeye si mshauri mzuri kwani anatumia sehemu baadhi za sheria ya dini kukukandamiza, mbona haoni kuwa mume wako anakatazwa na sheria hiyohiyo kuwa na mke mwingine? Kwanza huyo mama wa hao watoto wawili yeye sio mke ni mvamizi wa ndoa yenu.

    Kwa hali yoyote ile hukutakiwa kumkubalia kuingia kwenye nyumba yako na kama anataka kulea watoto, mpe aka kae nao anakojua yeye, alikuwa wapi kabla ya mume wako kupoteza kazi?

    Dada nahisi utakuwa umelogwa maana hayo maamuzi unayofanya hayawezi kufanywa na binadamu mwenye akili timamu hata siku mmoja. Na kama hujalogwa basi ndio unachanganyikiwa sasa, wahi hospitali.

    Kifupi, WAFUKUZE HUYO MAMA WA WATOTO WAWILI NA MWANAUME WAKE NA WATOTO WAO.

    ReplyDelete
  7. NDOA IMEGEUKA NDOANA.ANGALIA SANA
    HATARI INAKUFUATA.HATARI YA KUJERUHIWA AMA KUUWAWA KABISA.SASA
    CHUKUA MAAMUZI YA BUSARA.NAJUA BADO
    UNAMPENDA SANA MUMEO.ILA KWA STAILI
    HII NI KWAMBA HANA AKILI NZURI.
    FANYA HIVI.NAOMBA UONDOKE KATIKA
    NYUMBA HIYO,PANGA NYUMBA NYINGINE NA KAMA UTAKUWA NA PESA KIDOGO
    ENDELEA KUMSAIDIA KIASI KIDOGO AJUE
    KUWA BADO UNAMPENDA ILA TABIA ZAKE
    ZA KISHENZI NDIO ZIMELETA YOTE HAYA
    WEWE NI MVUMILIVU SANA.KAMA ISSUE
    NI KIAPO MBONA YEYE KAVUNJA KIAPO
    HICHO.ACHA MAMBO YA KIAPO FOR THE TIME BEING YANAWEZA KUKULETEA MADHARA USIOTARAJIA.UAMUZI NI WAKO
    USHAURI NI WETU.AHSANTE

    ReplyDelete
  8. Mama pole sana na matatizo.
    Leo humu humu niliandika kwa kirefu isivyo kawaida juu ya suala la ndoa(soma Videti 1: 1) juu ya ile mada iliyoletwa ya ndoa za kimataifa huko marekani ya Videti.
    Soma hapo!
    Mimi sielewi kama ni kwa uhuru wako kuwa katika ndoa ya mitala na kama unampenda mmeo na pia unaona anakupenda basi endelea kuishi naye ili iwe sehemu ya maisha yako. Vinginevyo endapo umegundua kuwa hakupendi maana angewezaje hata kumleta mke mwingine na watoto bila kuwasiliana nawe? basi muachane. Mimi huwahuria sana dada zangu wanaendelea kunyanyaswa maisha yao yote in the name of fake marriages ambapo wanapigwa na kudhurumiwa na kudhalilishwa kila siku! Je hiyo ndiyo maana ya Ndoa?

    NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO

    ReplyDelete
  9. Mh! kasheshee!
    Mimi ni mwana dini na naheshimu saana Mungu na dini yangu! Lakini haitaningia akilini pale dini inapotutaka mume na mme kuishi pamoja katika RAHA NA SHIDA! Katika neno RAHA hakuna anayebishi kwani ndo maana ya kuoana, lakini kwa neno SHIDA, naamini kuna limitations! zipo shida ambazo kweli tutavumiliana lakini si manyanyaso ya KUJILETEA NA KUJITAKIA!

    Ziko mila na yapo mafundisho ambayo sitakubali na siwezi kuyatetea! Kwanini unaniambia nikae na nivumilie SHIDA ZA mme au mke ambazo yeye ndo analazimisha?

    Umekubali kubeba watoto wa yule mama, haya ukavumilia tena kumaribisha mme mwenza ndani kwenye NYUMBA YAKO, then SHUKRANI ZINAZOTOKA NI KUTUKANWA NA KUNYANYASWA, SIYO?

    Wewe sasa ndo una matatizo, we ni mjinga, au umelambishwa sangoma kama mchangiaji wa mwanzo hapo juu alivyosema..!!!!

    Kazi ufanye wewe, chakula uwanunulie wewe, sijuhi bills n.k ufanye wewe alafu bila aibu unakuja kwenye hii blog kulalamika unanyanyaswa, fikiria mara mbili!
    Ukiwafukuza ndani utalala njaa, utalala nje, utafukuzwa kazi?

    Wewe ni kama hao wanaotunza mafisadi wa nchi na kuja tena kulalamika maisha magumu, nyamanfuu!!

    Unamtunza mwizi ndani, unaibiwa then unapiga kelele polisi kuwa mtaani tuna majambazi, nyamanfuu!!

    Dada pole saaana, naongea hapa kwa machungu na ninakutukana ni kwasababu kero hizi uwa zinanichafua ubongo wangu!! Mimi ni mwanaume lakini nachukia saana tabia hizi ziwe upande wa mme au mke...

    Nifupishe: FUKUZA HAO MAJAMBAZI NDANI, FUKUZA HAYO MAFISADI YA MSHAHARA WAKO, YATIMUE YAKAJIFUNZE KUSEMA ASANTE, FUKUZA FUKUZA, FUKUUZA YOTE NJE....

    Kwanza wewe una huruma, lakini sidhani hiyo huruma ndo Mungu anatwambia!!!

    ReplyDelete
  10. kwa kweli nakupa pole sana kwa mkasa uliokupata, jamani mwanamke mwenzangu hivi umepewa limbwata au vipi? Ulifanya makosa makubwa sana kumkaribisha mke mwenza ndani, umeiona wapi hiyo? jamani unaishia na nyoka ndani? Du, una roho ya ajabu sijawahi kuiona hapa duniani, au unaogopa kuachwa? jamani kama kubembeleza ndoa kiasi hicho it is too much!!!
    Pole mtu wangu lakini take care, chukua watoto wako ukapange mwisho watoto wako watapewa sumu bure!

    ReplyDelete
  11. Pole sana dada kwa yaliyokupata. Kosa kubwa ulilolifanya na ambalo wanawake wengi huwa wanalifanya ni kumkaribisha huyo mwanamke na watoto wake ndani kwako. Sijui ulifikiri ndio utaonekana mstaarabu, na baada ya kukupata yote hayo unamwangalia tu? kwani mwanao huyo?? wanawake wengine mmpoje lakini? Na hata hao ndugu wa mwanaume hawajakutendea haki kabisa. Sasa ushauri wangu, Mfukuze huyo mwanamke na wanae pamoja na mumeo kama anampenda kweli akamjengee nyumba yake. Na mwisho dada ukumbuke kuwa hizi ni zama za UKIMWI bado unakubali tu kushare unahalalisha tu. yatakupata makubwa ukiachia hii hali iendelee.

    ReplyDelete
  12. Dada yangu nakupa pole sana. USHAURI:-
    1).Uamuzi wa jambo usikae muda mrefu, maumivu ni makubwa ukiendelea kugugumia.
    2).Kosa ni la msingi ni Mumeo, wewe wema umekuponza tuu.
    3).Waende wakaishi nje ya hapo nyumbani.
    4).Ikishindikana, tafuta uwezekano wa wewe kuwaacha ukaishi pengine.
    KUMBUKA:-Mungu hakutuumba tuishi kwa kuteseka, ila mateso, kama hayo uyapatayo tunajitakia. Kwani siku zote kuna njia mbadala ya kila jambo tuamualo kufanya. FIKIRIA na CHUKUA hatua. HURUMA isizidi uwezo Dada yangu.

    ReplyDelete
  13. mmmm! wakubwa!! jamani.
    Anti pole sana nemesoma email yako kwa haraka, kwanza nimeshindwa kuamini kwamba hili jambo limetokea na umelibeba kiasi hicho. kwanza nikupe hongera kwa uvumilivu mkubwa uliouonyesha kwa swala la watoto nadhani ni upendo mkuu ulouonyesha kuwakubali maanake ungefanyaje watoto hawana kosa. ila UJINGA- na UBWEGE uloufanya kumuingiza huyo kimada ndani kwako, mtu kashakuibia mume kakuongezea mzigo wa watu ambao hawakuwa kwenye budget yako afu ibilisi huyo huyo unamuingiza ndani aendelee kukuchukulia mumeo mbele ya macho yako ivi anti una moyo wa jiwe au nyama? angalia labda umerogwa!! ivi unajua thamani ya mumeo na familia yako kweli? afu huyo mumeo naye hana lolote ni wazi wamelisuka na huyo kimada maana angekuwa anakuheshimu na kukupenda asingethubutu kumleta huyo kimada nyumbani kwako. mama funga kanga zikaze nyumba hujengwa na mke!! na kama wewe ni mkrisho biblia inasema Mungu ameumba Jambo jipya ya kwamba Mwanamke atamlinda Mumewe!! andiko hili mi huwa naliangalia kwa upana sana!! wewe ni mlinzi gani unayeleta mwizi ndani??Ndoa na Iheshimiwe anti hujui? unadhani nani wa kuiheshemu kama si wenye ndoa wenyewe?? plz sababu isiwe kazi wala ajira. katika mazingira yoyote usimwache mumeo. nikwambie kitu?? mchawi na mzizi wa tatizo hapa ni mumeo. kaa chini na mumeo muwekane sawa. funga na kuomba pia.... maana hawala hana talaka. unaweza kufanikiwa kumtoa hapo hm lakini pia akaendlea kuendesha nyumba yako... vita vyetu si juu ya damu na nyamba....fahamu.

    ReplyDelete
  14. WOMAN U ARE SICK. YOU MAKE ME SICK. WHAT KIND OF A WOMAN U ARE? UNAONA UKIMWACHA HUYO MUME NDIO MWISHO WA MAISHA? ELEWE UNAFANYA KAZI UNAKIPATO CHAKO NA UNAWEZA KULEA WATOTO WAKO SIO WATOTO WA MKE MWEZIO HUYO MUMEO KAMA AMEACHISHWA KAZI AENDE KUTAFUTA KAZI MAANA ANAJUA TOSHA ANAFAMILIA YA KUTUNZA. KAKULETA WATOTO HALAFU MKE WAKE HALAFU UKIMWI WHAT NEXT UTAACHA WATOTO WAKO KWA SABABU YA UJINGA WAKO. NA KAMA NDOA YENU MMEFUNGIA KANISANI NA WEWE UMESEMA KUWA NI YA KIKRISTO HAPO NINA WASIWASI MAANA SIDHANI KAMA ANGEWEZA KUFANYA HIVYO NA WEWE KUKUBALI UJINGA HUU.
    JAMANI NDIO MAANA NAPENDA USA DIVORCE NJE NJE. MUME AU MKE HAKULETEI MCHEZO KAMA HUU. MWISHO NDUGU YANGU NADHANI UNAKASORA KUBWA SANA NDIO MAANA UMEKUBALI BULLSHIT KAMA HII.

    ReplyDelete
  15. Pole dada,
    Kama uvumilivu, uvumilivu ndio huo,
    kama ni Utii kwa mume, utii ndio huo, na kama ni wema, wema ndio huo. lakini imepita mpaka, sasa utadhurika wewe mwenyewe. Kadiri ulivyotuelezea huyo mke mwezio (mwizi wa mume) ni kiumbe mbaya kuliko hata shetani. Tafadhali chukua hatua ya kufukuza haraka sana yeye na watoto wake, na hata huyo mumeo kama atakuwa upande wake nae aondoke. Dada huyo fisadi atakuwekea hata sumu ufe na wanao atawanyanyasa. Kama wema umeshamuonyesha yeye na wanae. Huna haja ya kuchanganyikiwa wewe ndio baba ndio mama sasa kwa vile mumeo hana msimamo ndio maana akakusaliti. Ondoa kabisa huo ugeni japo hao watoto wake hawana hatia lakini mama yao ndio anawatumia kama ngao. Fanya haraka kwa usalama wa wako na wanao, kabla huyo ibilisi hajakuangamiza. Pole sana.

    ReplyDelete
  16. Mpendwa,
    Kosa la kwanza kabisa ulilofanya ni kumkaribisha huyo mwanamke wa mumeo ndani ya nyumba yako.lakini kwa sasa hiyo sio issue tuangalie mbele. what are you supposed to do? Mimi nadhani wewe ni mvumilivu na unaheshima sana, na mumeo anajua hilo ndio maana he is taking you for granted. Kukubali watoto wake nyumbani kwako ilikuwa ni heshima kubwa sana lakini kukuletea mwanamke wake ndani ni dharau isiyopimika.sasa kama kakudharau hivyo wewe huna haja ya kumng'ang'ania ...huwezi kuishi maisha ya masononeko kila kukicha...utakufa utawaacha wakifurahia na inavyoelekea wala hawatawajali watoto wako.wao nia yao sasa hivi ni KUKUCHUNA tu kwasababu wewe ndio bread winner, na ndugu wanajua wanafaidika ndio maana wako upande wao. I suggest you gather courage na Mwenyenzi Mungu akusaidie utafute nyumba upange ukae na watoto wako...YOU NEED TO MOVE AND DO IT VERY VERY FAST. unahitaji sana afya yako kwa ajili yako mwenyewe na watoto wako...ukiwa nje utaona jinsi umepoteza muda mwingi na pia utakuwa huru kufikiria mambo yako vizuri zaidi. right now you cannot think clearly ukiwa katikati ya vijembe. Halafu huyo mumeo for 2 years hajaweza ku-earn a living ana tatizo gani? I can smell more problems in him than what you are telling us. Najua unampenda sana mumeo lakini kwa anayokufanyia ni wazi kuwa yeye hana mapenzi tena na wewe.RUN FAST BABY FOR YOUR OWN YOUR OWN SAKE NA WATOTO WAKO.

    ReplyDelete
  17. Kweli makubwa!
    Ni biblia gani unasoma dada angu? labda unasoma biblia B, mana biblia me ninayoisoma inaniambia mke au mume anaruhusiwa kuachwa kama atafanya uasherati au uzinzi ila kwa sharti tu kwamba hutaolewa tena hd huyo mumeo afe.
    Hebu acha huo upuuzi na ujinga toa hawo wa2 nyumbani kwako wote hd mumeo.

    ReplyDelete
  18. pole mama kwa yaliyokusibu,
    lakini unalea ugonjwa!!! mumeo ndo chanzo cha yote haya!! hao watoto ni baadhi ya waliojitokeza na mamayao, je wakija wengine na mama zao utavumilia!! Mungu ameona juhudi zako, sasa ni wakati wa kuangalia mbele. kwa sababu hio ni nyumba ya ofisi kwenu, waambie kuwa wakutafutie nyengine, hiyo huitaki, wape ukweli, then we hama, wape notice hao wapangaji wa kujitakia, na we anza mbele na wanao, Mungu atakupa nguvu, na kama mumeo ataona kosa lake ataachaana na huyo hawara na kukufuata, but dont give a damn about him.
    nana

    ReplyDelete
  19. Dada una moyo wa chuma na kwa mtindo huo usitegemee MUNGU akupe tafu ni wewe mwenyewe! MUNGU YUPO BUSY sana kwa sasa na mambo ya Kenya huko, Darfur n.k sio issue kama hizo ambazo zipo kwenye uwezo wako. Pole sana dada yangu mie nakwambiaje huyo mama hawezi kutoka humo ndani wala huyo mume. Kama nyumba umepewa na ofisi wewe irudishe kwa wenyewe baada ya kutafuta nyumba nyingine somewhere ukaishi na wanao. Maisha yamebadilika hakuna kitu kama hicho hivi sasa, badala ya kufikiri habari za maendeleo ya familia yako unapoteza muda kulea mijizi na mijitu isiyo na shukrani soo hiyo. Chimba mara moja mwachie vumbi mheshimiwa ale jeuri yake KUDADADEKI, acha hizo. Unachelewa wahi!

    ReplyDelete
  20. Dada pole sana ulifanya vibaya na dhambi kubwa kusema uongo kwa majirani na marafiki zako,unaona sasa shetani kakuumbua iwekuwa sio siri tena,nakushauri uende kwenye maombezi omba kwa imani kabisa kama ni ndumba Mungu atamuumbua huyo mumeo na mzinzi wake mchana kweupe.jesus is able
    by mwinjilisti

    ReplyDelete
  21. Mimi niko tofauti, naona huyu dada ni mkorofi kwa kuwa anauwezo ndani ya nyumba. Kwa kawaida mwanaume ndio mkuu wa familia ila wewe unataka umuendeshe. Ugomvi wako uendeleze na mke mwenza wako usimnyanyase mumeo. Alafu unaweza ukakuta wewe ni sababu ya hata huyo mumeo kwenda nje. Ungekuwa mpole na umempa mapenzi tosha asingeenda nje. Haya ni makosa yako nashangaa kuona watu wote wanamlaumu huyo mumeo.

    Fikiria kama ungekuwa kama zamani na unakaa kwenye nyumba ya mumeo na mumeo ana kazi yake je wewe ungefanya vile unavyotaka kufanya sasa? Sidhani. Mumeo masikini sasa inaonekana hana thamani kwako tena.

    Kumbuka wakati mumeo anauwezo alikuwa anaweza kukutelekeza wewe na watoto wako na kwenda kuishi na huyo mama lakini hakufanya hivyo kwa upendo wake sasa iweje wewe leo unataka kumtelekeza mumeo na watoto wake kwa kuwa umepata?

    Umasikini umewagombanisha. Kutatuta ni kuwa mkae chini, mjadiri jinsi ya kutafuta ajira na mzunguke mjini kila siku mpaka wote watatu mrudi makazini. Iwapo yule mama mtamsaidia atafute kazi na apate basi ataishi kwake na watoto wake. Hili suala litaisha nila ndoa kuvunjika.

    ReplyDelete
  22. We dada! we dada! helooooo. GET OUT FROM SHELL. unahabari kuna waume wengine wana vijitabia vya nzi? jaani yupo, mezani yupo sasa ukimshiriki atakuletea mardhi bure. mambo muhimu ni matatu kwenye ndoa 1. akupende, 2. akujali, 3. akuheshimu. sasa wewe kwa huyo mumeo unapata nini ? furaha huna ulinzi huna ni kudhalilishwa na kuungua na ulsers na pressure. Achana nae huyo akili yake imeshaharibiwa hasikii chochote hapo wanakutumia tuuuu na furaha unayoitafuta huipati,
    waambie watoke wakatafute mahali, na kama sababu ni hao watoto waambie waondoke nao pia isiwe tabu.
    si wakwanza wewe kuachwa kama hiyo ndoa itoe sadaka kwa bwana kisha atakurudishia kwa upya kama mmepangiwa kuishi nae atarudi ila akili mu kichwa.

    ReplyDelete
  23. Kwanza nakupa pole sana.

    Pili ningependa tu kukuambia kwa kifupi tu kuwa pamoja na viapo vyote mnavyotoa kanisani lakini biblia iko wazi sana kwa swala ulilolielezea. Mimi ni mkristo na napenda tu kukushauri usome mafngu yafutuayo katika biblia yako kama unayo: Mathew 10:9-12 na 1 Corinthians 7:10-15.

    Mafungu hayo niliyokupa yanafafanua wazi kabisa ni kwa jinsi gani Mungu anatoa mibaraka ya kuachana na mume ambaye ameishafanya kitu kinaitwa 'Fornication'. Mambo yote yanavumilika kwenye ndoa lakini hilo la kuzini halina nafasi kwenye ukristo!

    Kwa hiyo mama hakuna jinsi ya kuvumilia maisha kama hayo maana na wewe unaanguka kwenye dhambi ya mumeo na ukumbuke kuwa hakuna mtu yeyote atakayekuokoa - si mumeo, si watoto wako, si ndugu zako wala si wazazi wako. You have to deal with the issue yourself and diligently!

    Stay blessed, I will be praying for you!

    ReplyDelete
  24. Kwanza napenda kukupa pole kwa yaliyokusibu.Na pili siamini kama mpaka kipindi hiki kuna wanawake ambao hawajiamini kiasi kama cha kwako.Kwa mtazamo wangu ninafikiri sababu kubwa iliyokufanya uamue hivyo ni either bado unampenda sana mume wako au hujiamini Kuwa mwanamke ana uwezo wa kujisimamia mwenyewe na familia yake na kufanya maamuzi yake.lazima ujue kuwa umefanya kosa kubwa sana pengine zaidi ya wao kwa kumkaribisha huyo mwanamke(nyoka mwenye sumu kali) katika nyumba yako.kwa sababu kuna uwezekano mwenzio akakutilia hata sumu kwenye chakula ili mradi tu akuondoe.Hata hivyo bado hujachelewa.Kama wewe ni mmiliki wa hiyo nyumba mpaka sasa una uwezo wa kuwaondoa haraka sana wakatafute maisha yao ila nisingekushauri uendelee na huyo mwanaume kwanza hakupendi na wala hakueshimu vilevile huwezi jua pengine mungu atakuepushia magonjwa kupitia kwake.Hizo gharama unazotumia kuwahudumia wao au familia nzima ungeshafanya mambo mengi makubwa na mazuri kwa ajili yako na wanao.Napenda kumalizia maoni yangu kwa kumwambia huyu dada kuwa Life is how you make it, unatakiwa uamke sasa kama ulikuwa usingizini,tengeneza maisha yako ukiwa na watoto wako,jijenge ili watoto waweze kuwa na maisha bora,usipoteze muda achana na huyo mwanaume pia muombe mungu aweze kukupa ujasiri wa kusimama mwenyewe bila kutegemea fimbo ya mwanaume.

    ReplyDelete
  25. Dada pole.
    Mimi nakuelewa sana kuwa wewe ni mwema sana, lakini WEMA wako usizidi uwezo na usiwe karaha kwako. Mumeo hana ADABU kabisa anakuelewa ulivyo ndio maana anakufanyia yote hayo. AMKA SASA DADA, huwezi kuishi namna hiyo. Ondoka na watoto wako, uwaache mumeo na mke mdogo waenjoy zaidi. Kwa sababu sidhani kama mumeo anajali feelings zako kwa sasa, atakuua huyo kwa stress na magonjwa mengine, TIMUA NOWWWWWW.

    ReplyDelete
  26. Pole sana Sis!
    Lakini inaonekana haya mambo umeyataka mwenyewe ama akili yako inachelewa kutambua mambo na athari zake!samahani anyway but i thought niko sahihi,coz nyumba umepewa wewe na shirika,then unashindwa kuisimamia!unakaribisha watu au mtu"watoto hawana kosa"anakusumbua!!
    fukuza mume na mkewe,baki na watoto wako maisha yanaendelea wake up!!!
    then unaweza kuitwa fisadi kwa kutumia vibaya mali ya shilika!anyway pole sana tena sana!
    frm Salim H Simba.

    ReplyDelete
  27. Bahati mbaya mambo haya yapo sana bongo. Ushauri wangu: Aliambiwa asizini, akafanya hivyo mara kibao na kutotoa watoto wawili. MFUKUZE NA KIMADA NA WATOTO WAKE. Je! una hakika huo ndo mwisho? Ataleta wengine tena. Kesho akipata kazi, wote na mizigo yake hawatasema hata asante.
    Mfano mzuri: Supu alitoa juzi juzi picha ya Dj mmoja mzuri hapa Dar. Hata Bongocelebrity wanamsifia: Kwa taarifa yenu, mama yake alikuwa house girl aliyempindua mke wa ndoa baada ya kupata mimba kwa baba mwenye nyumba. Wataalam wanadai kuwa hata JK yule mtoto yatima anayemlea, ni mtoto wa nyumba ndogo......
    Kalaga bao

    ReplyDelete
  28. DADA MI NADHANI JAMAA KESHAFANYA DHAMBI KUBWA HATA HUKO KANISANI WAKIJUA WATASHANGAA. ULE WAKATI WA KUAMINI KUWA ATABADILIKA UMEPITWA NA WAKATI... MEN NEVER CHANGE WAKISHAANZA HAKO KAMCHEZO, HIVYO DADA JUST COUNT THAT NDOA NI HISTORY, GET THEM OUT OF YOUR HOUSE/LIFE, ENDELEA NA MAISHA NA WATOTO WAKO - CAUSE THAT IS NOT HEALTHY TO ANY OF YOU ESPECIALLY KIDS THEY DONT DESERVE KUSIKILIZA TAARABU ZA MISUTO NK. DONT YOU EVER FEEL GUILTY KUWA ETI KWA SABABU HANA KAZI NDIO ATAONA UNAMNYANYASA.. IF HE LIVED HIS LIFE CLEAN HAYO YOTE YASINGEKUWEPO SO HE MUST NOW PAY THE PRICE OF LIVING DIRTY LIFE (NYUMBA NDOGO...HUKU UNA NDOA YA KIKRISTU) AND YOU GIRL.... START YOUR NEW LIFE WITHOUT HIM. AISEE MIMI NINA ROHO MBAYA SANA WHEN IT COMES TO THINGS LIKE THOSE MANAKE DADANGU MPAKA KAISHIA KUFA KWA UKIMWI KWA MAMBO KAMA HAYO NA MUME NA MTOTO MMOJA SO WE ARE LEFT WITH ONE MTOTO KUMKUZA!! USIFUMBIE MACHO WALA KUWA NA ROHO YA HURUMA KATIKA SITUATION KAMA HIZO.. YOU DONT DESERVE THAT GIRL

    ReplyDelete
  29. Wake up Sister!!
    Duh siamini kua kuna watu wana roho kama yako na akilizao zinafanya kazi taratibu hivyo, dada hayo sio maisha na wala usiseme unamuachia mungu manake hayo mambo yako ndani na uwezo wako, inaonekana unampenda sana huyo mumeo sasa mimi naomba nikuambie kitu kimoja huyo mwanaume umekutana nae ukiwa mtu mzima, sasa iweje now ushindwe kufanya maumivu yako kisa ndoa?? hiyo ndoa au madharau??huyo mwanaume anakudharau sana dada yangu hana heshima kabisa kwako,as u said hiyo nyumba ni ya shirika unalofanyia kazi wewe yaani kama ingekua mimi ningekua nimeshawatimua zamaniiii or kama kuna uwezekano basi hama wewe tafuta nyumba ingine halafu mumeo na huyo mzinzi mwenzie uwaache hapo pamoja na watoto wao wewe ukaanze maisha mapya na wanao mahali pengine yatakayotokeea kwenye nyumba ya shirika wew hayakuhusu tena.....sio kama unamnyanyasa ila mumeo hana heshima kabisa.AMKA MWANAMKE MWENZETU

    ReplyDelete
  30. Huyu anon 12:13:00 PM EAT,ni mzushi na usimchuuze dada wa watu haiwezekani ukawa'against'watu woooote na lazima uelewe mtizamo wako umekufa na hauna nafasi dunia ya leo. Huenda nyie ndo mnaotafutiwa wake au waume! Huo ni unywanywa. Dada lazima uelewe kila kitu kipo mikononi mwako usipoteze muda na maisha yenyewe ndo hayo yanakwenda mijitu imepoa tu inakula na kunywa na uroda mna'shea' wapi na wapi bwana. Changamka, komaa, funga mkanda angalia mbele. Tazama familia yako dadaa. To be a single parent is not an issue nowadays at all. Kwanza unaweza kuona ndo kwanza MUNGU anakufungulia milango mingine ya NEEMA na maisha yanakwenda mswano. Hapo unacholazimisha wewe ni mapenzi na sio MAPENDO. DADA SIMAMA FANYA MAAMUZI SASA!!!!

    ReplyDelete
  31. Ahha, fix tupu hiyo story. Ukisoma between lines, hakuna kitu ya namna anayoelezea huyu dada. Anataka kutunga kitabu tu, sasa ameweka hapa asikie tunasemaje.

    Mme hana kazi, halafu akuletee watoto wa mke mwingine uwalishe wewe?!!

    ReplyDelete
  32. Uuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuwi!!!!!!!! Damn!!!! Michu naomba namba ya huyu dada nimsaidie. I got the Gun and the bullets! dada show me the Bastards i will show you the graves!Huyo jamaa anatakiwa kupewa ratirati!!!

    ReplyDelete
  33. Ngoja nijaribu tena, manake mwanzoni asubuhi na mapema nilituma maoni yangu yakatiwa kapuni. Sawa sio mbaya.

    Mimi kwa ushauri wangu, kwanza kabisa angalia watoto wako. kwasababu una uwezo wa kuwasomesha, jibidishe kwa hilo. nasema hivi kwasababu hali ya kitoto ina kusononeka, na anavyokuwa na msononeko moyoni, hali hii humuathiri mtoto katika maisha yake ya baadaye. Kwanini mimi sina baba, kwanini mimi sina mama...haya maswali ni nyeti katika maisha na makuzi ya mtoto.

    Lakini upo umri wa kuelewa nini kinachoendelea, hapo unaweza kuchukua hatua ambazo unaona ni sahihi.
    Najua wengi wetu tunakimbilia kuachana, `achana naye, muache huyo...'! Ni sawa kwanza kwasababu jamaa kazini, hii ni red card, hilo muelewe waheshimiwa. Mukiwa mumeona na mko ndani ya ndoa mmoja akazini, ina maana gani, si ina maana kuwa ndoa hapo, je hiyo kutokuachana mpaka kifo inatoka wapi? Hapo wamezungumziwa wacha Mungu....

    La pili wakati ukiwa katika kuvumilia, na huku unawaendeleza watoto wako, jijenge, jitengenezee maisha yako ya baadaye. Na wakati huohuo geuka kuwa mchungaji, jaribu kuwaelimisha hasa mumeo
    pale inapobidi, nini ubaya wa hayo wayayoyatenda, huenda nyoyo zao zikalainika. Kwani wanavyoishi wanazini, wanazidi kumkosea muumba, wanazidi kuwazaa watoto ambao watakuja kuwahukumu, wanajenga mgongano ambao utawaathiri watoto....

    Ingekuwa vizuri tungesikia na upande wa huyo mumeo anasemaje kuhusu hili, huenda naye akabahatika kuipitia hizi hoja.
    Natashukuru.

    ReplyDelete
  34. "Nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,Nami na warehemu wenye kunipenda na kuzishika amri zangu"USIZINI.....nakadhalika nakadhilika...Kwa mungu hao watoto pia wanamakosa waliyorithi toka kwa wazinzi hao Baba na kimada wake.We dada yangu anza mbele achana na bwana huyo kwani kuvuja kwa pakacha siyo mwisho wa uchukuzi.

    ReplyDelete
  35. KWELI INANIUMA SANA KUSIKIA DADA UNAPATA MATESO KIASI HICHO.
    KWELI USIPOANGALIA STRESS ITAKUUA.
    WATOTO WAKE HAWANA MAKOSA KABISA.RUDISHA NYUMBA YA OFISI,HAMA WEWE NA WATOTO WAKO.WALE WENGINE KWA SABABU KUNA MGOGORO NA WAZAZI WAKE WAACHE.
    PIA VEMA SWALA HILI UKALIFIKISHA KANISANI KWA MCHUNGAJI WENU.KIMSINGI MUMEO AMESHATENGWA NA KANISA.KUKAA HAPO NA KUMWACHA MWANAMKE HUYO KWENYE NYUMBA YAKO JIANDAE KUPATIWA MTOTO WA TATU WA NJE.KWELI WEWE UNA MATATIZO YA AKILI.MWAJIRI WAKO USIMWAMBIE ATAKUFUKUZA KAZI KWANI ATAJUA ANANFANYAKAZI MWENYE ULEMAVU WA AKILI.HAKUNA MTU MWENYE TABIA KAMA YAKO SIJAWAHI SIKIA.POLE SANA ILA UJINGA WAKO NA UPUMBAVU WAKO UMECHANGIA UOZO HUO.KAMA UNASHINDWA KUMFUKUZA TUAMBIE.NJIA ZA KUMFUKUZA.

    ReplyDelete
  36. Pole sana dada kwa yaliyokukuta, laikini kumbuka wema wako umekuponza nyumba haikai nyumba kwako kwako tu!!!!!watimulie mbalini watakuua hao!
    Mwanaume asiye na adabu wala upendo wanini? hakukupa nafasi yako kama mke bado anakuletea kimada ndani hakupendi huyo!kunamchangiaji hapo juu amesema eti inawezekana wewe ni mkorofi unayetaka kumtawala mmeo no!!!mimi nasema hivi mwanaume ni tabia hata akipewa penzi la aina gani kama hajatulia ujue atatoka nje tu!
    DADA FUNGA KIBWEBWE LEO LEO WATIMUE HAO WAJINGA KAMA HAWATAKI ONDOKA NA WANAO ONLY WAACHIE NYUMBA USITETEREKE MUNGU ATAKUSAIDIA, IKIWA MWANAMKE NDO ANAYEJENGA NYUMBA NA KUIBOMOA MWENYEWE, SASA ISHAPATA UFA WAKIJA WATOTO NA MWANAMKE MWINGINE UJUE INABOMOKA.

    ReplyDelete
  37. pole sana Dada yangu kwa yaliyokukuta. Wewe Kama ni mkristo umefwata Dini Ungefuata bible inasemaje, the bible says Mungu apendi kuachana isipokua kama mwenzio kazini unaweza kutengana neye, sasa wewe inafikia mme anakuletea watoto wa nje we kimya, anakuja mke mwenzako we bado kimya tena kwenye nyumba uliyopewa wewe na shirikia WHAT IS WRONG WITH YOU WOMAN!!!!!!!!!!!! GET HIM OUT. SOMETHING IS WRONG SOMEWHERE IN YOUR HEAD.

    ReplyDelete
  38. Hebu ondoka hapo haraka sana kabla hawajakuua! Chukua hatua zifuatazo:
    1. Kwanza ripoti polisi na ueleze una wasiwasi na maisha yako, uombe ulinzi, au hata kwa rekodi ili mtu asijisikie huru kukufanyia lolote.
    2. Pili, tafuta nyumba nyingine haraka sana, upange.
    3. Kodisha lori, rudi nyumbani mchana kweupe beba kila kilicho chako, hakikisha una escort ya polisi (hata ikibidi kuwapa rushwa polisi wape tu, hii ni kwa usalama wako). Ondoka na watoto wako, nenda kwenye nyumba yako. Hapo mwache huyo mzinzi, kimada wake na wanae, watajua wenyewe wataishije, haikuhusu.

    Natarajia kuona unatuma email nyingine kutueleza umetekeleza haya, vinginevyo usitutake ushauri mwingine maana kinyume cha hapo nitakuona unatuchezea!

    ReplyDelete
  39. No comments fuata moyo wako bibie

    ReplyDelete
  40. Ni vizuri tumwuulize mke wa kwanza wa Michuzi alijisikiaje na alichukua hatua gani alipoona Michuzi anaoa mke wa mwingine wa Kiganda na kumleta ndani ili wachangie kutumia mchi mmoja wa kutwangia vinu tofauti.

    ReplyDelete
  41. Baada ya comment zote hizo ulizozipata sasa dada umeamua vipi maana watu wengi wamejaribu kukupa ushauri.

    ReplyDelete
  42. 1.kisheria una haki ya kusikilizwa hivyo nenda Mahakamani ama baraza la usululishi wa ndoa na utoe shida yako na kama utaomba talaka utapewa.Kama utapenda kuishi na hao watu kwa masharti pia yawezekana. Usiwasikilize wasemao Watimue hao Mafisadi kama wewe roho yako inaona tofauti. Kila mtu kaumbwa na roho tofauti na nikuonavyo wewe upo tofauti na walo wengi.

    2.

    ReplyDelete
  43. Mmmh mwanamke mwenzangu pole na mimi nimepita katika hali hiyo. Lakini mimi sikukubali huyo mwizi aingie ndani ila kosa nililofanya ni kumwona rafiki yang ila baada ya vituko nikagundua hakuna urafiki hata siku moja na mke mwenza. Sasa dada yangu nakushauri huyo mwanaume mpe muda na wewe endelea na maisha yako na kama ni wa kwako atarudi ila kama si wa kwako basi Mungu atakuonesha aliye wa kwako baadaye. Hata kama unafikiria huyo jamaa ni mzuri kwa mambo ya mapenzi kiasi amekuteka unafikiri huwezi kupata kama yeye, achana nae wanaume wako wengi na utampata atakayekuthamini na kukupenda kwa dhati ambaye hatapenda uumie. Ukiendelea kukaa hapo unawaumiza watoto wako maana wanaona mambo ambayo yanaweza kuwaafect kisaikologia, sasa dada acha kuwa mbinafsi na angalia maisha ya wanao. Hao wanaharamu wawili achana nao na ikiwezekana hama kabisa hapo.

    ReplyDelete
  44. Hizi ndio zile hadithi za Abunuasi. Dada hongera kwa kutunga story tamu na ya kufikirika. Lakini story yako imekuwa too extreme hakuna kitu kama hicho kwa mwanamke yeyote. Jitahidi kutunga zaidi baadae utakuwa mtunzi mzuri sana. Biblia ipo wazi juu ya ndoa, na inasema wazi ni mazingira yapi yanapelekea kuvunjika kwa ndoa. wewe hautokuwa wa kwanza kuvunja ndoa.

    ReplyDelete
  45. Bado haijaniingia akilini hadithi yako naona kuna anoy mmoja amediriki kusema ukisoma btn ze lines utagundua kuna fix tupu hapa..nami naungana nae..Maelezo yako bado hayaoneshi ka ukweli katika life hii ya sasa!! unless unakasoro kubwa za kibinadamu..Maana hata ukilogwa huwakuna matatibu wakusaidia ila kama kweli hilo ndo tatizo na ukaja kuomba ushauri kwetu ukijiona ni mzima kabisa basi nadhan utakuwa na matatizo makubwa zaidi..Its not accepted in my mind!

    ReplyDelete
  46. Michuzi mimi ndo mume wa huyo mama aliyeandika kulalama kuhusu mke mwenza. Mbona hatoi upande mwingine wa habari? Mbona hasemi katika watoto watatu aliozaa mmoja si wangu; alimpata nilipokuwa masomoni? Anatafuta public sypathy isiyo na justification! After all si kwamba sina kazi; I am a consultant. Nimejiajiri. I take care of my family. Muulizeni alikuwa akifanya nini hadi nikajikuta naenda nje? Anyway, haya yalikuwa ya ndani ya familia. Sikutarajia atayaleta huku. Sasa tutaona kama ana jeuri aliyotamba katika waraka wake kwamba anayo, nyo!

    ReplyDelete
  47. OOh jamani siamini kama una moyo mgumu kiasi hicho au ndo limbwata.mimi ushauri wangu kama watoto wako ni wakubwa umri wa kwenda shule peleke boarding wote kama uwezo upo alafu wewe wala usiondoke kwenye hiyo nyumba maana ni dhamana umepewa kazini kwako,we hama chumba kabisa na usikubali kufanya nae ngono huyo mumeo mzinifu,atakuletea ngoma aka Ukimwi.kwa kuwa una kazi uwe unakula restaurant ukirudi home uchune hamna kupika wala nini siutakuwa umeshiba na usiwape hela yoyote watajijua wenyewe watakula wapi wa vifaranga wao.dada be careful vinginevyo utajuta maana unaweza wekewa sumu ukafa na watoto wako.
    kuna mfano halisi mwl wangu wa primary mumewe alikuwa anamletea wanawake nyumbani alichofanya yeye hakuondoka nyumbani bali alihama chumba akawa anafanya mambo yake kivyake na ngono ikawa hamna tena yeye na mumewe,at the end of the day mume wake akapata UKIMWI akafa ila huyo mwl mzima hadi kesho anadunda na afya yake njema.kwa kuwa alikuwa jasiri na mwenye msimamo.
    by mgogo asilia

    ReplyDelete
  48. Dada uko karibu sana na ukamilifu.
    Dhamira yako yakuelekeza vema ila haipaswi kuwa ilivyo.
    Mpe mume choice ya kuondoa wanawe na nyumba ndogo yake ama urudishe nyumba kwa wenyewe kisha wewe na wanao watatu muende mkujuako na mume na wanawe atajiju.
    ANAPASWA KUWAONDOA,AWAPANGIE CHUMBA KIMOJA KISHA MUWE MNAWASAPOTI KIAINA.
    Ila dada mapenzi yako nimeyakubali

    ReplyDelete
  49. Mh pole sana dada yangu. Yaliyokukuta yamenigusa na nina kuonea huruma sana. Huruma huwa inazaa dhambi na pili hata Biblia inasema kuwe na kiasi. Mimi mwenyewe ni mwanaume lakini ya mume wako yamezidi, kaa naye mwambie achague wewe au ya yule mwanamke. Wakati ana wazaa hao watoto alikuwa anafikiria atawatunza vipi? Hiyo nyumba ni umepewa na shirika lenu, usitoke humo ndani ila wafukuze kwa njia yoyote ile.
    Na wewe mwanaume kama unasoma hii, huna adabu na heshima kwa mke wako na kwa watu wote, unafanyia huyo mama vituko kwa sababu ni mpole na anakupenda? Ukitaka kuwa successful katika life lazima umuheshimu mke wako na hata Mungu mwenyewe atawamwagia baraka, usimpe huyo mwanamke stress zisizo na maana.

    ReplyDelete
  50. Saa zingine ni sisi wanaume are to blame for all these matatizo kwenye ndoa zetu! Na saa zingine nasi tunakuwa tumeshalishwa limbwata maanake hatuelewi wala hatusikii! Ni kama vile kumpigia mbuzi gitaa, au kumpiga kinyago makonzi!!!

    Nashindwa kuelewa wapi tunapopata wazo eti mke wangu aanze kulea watoto wa mwanamke mwingine - why? Kwa nini? Kila mwanamke alee watoto wake unless mama yao kafariki ambapo napo pia kuna taratibu zake za kufuata ili kuchukua watoto. It may sound apologetic being with a nyumba ndogo with kids but damn this tabia sio nzuri na tunaendekeza sisi wanaume.

    Haijanitokea mimi kuwepo na nyumba ndogo yenye watoto (and God forbid, I beg, I beg!!) and I shouldn't be saying anything condemning us men.

    Huyu dada hapa namsifu sana because I know some women who will throw such a fit and even cut of their husbands reproductive organs, just for starters! Pack your bags and call it a day in that relationship, especially if you are the bread winner in that "household". We in western America cowboy land would say; Get out of Dodge, pronto!!

    ReplyDelete
  51. Kwanza pole sana kwa yaliyokukuta dada yangu,yaani mimi sioni nini unaangaika kutafuta msaada wa ushauri wakati njia ni nyepesi wewe kutenda tu moyo wako unavyokutuma,Hakuna Ndoa ya kikristo ya wake 2 ! sasa kama mumeo alifikia kuoa mke 2 na wazazi watatetea dhambi ya uzinzi na ujinga wa memuo na wewe usiwe mjinga,ili mradi unafanya kazi tafuta nyumba ya kupanga ukapange huko hata vyumba viwili tosha na watoto wako,hiyo nyumba ya shirika rudisha yeye na familia yake ya pili watajua jinsi ya kuhishi na kuendeleza maisha yao ,hasa wazazi watamsaidia maana wamemkubali mke wapili,huyo si mwaminifu tena kwako wala ana mapenzi nawe hata kidogo ,maana anhekuwa anakupenda na kukusamini angekujulisha kama hana mke mwingine na ana watoto 2 kabla ya haya yote kutokea,nakutakia kila la kheri kumbuka pia maombi katika yote haya yaliyombele yako.

    ReplyDelete
  52. anon wa jan 28, 4:08 Hizo si hadithi za abunuasi wala alinacha kama unavyofikiria,ukiona kwako kunaungua ujue kwa mwenzio kunateketea mi nina mfano hai wa maisha ya namna hiyo ya mume wangu wa kwanza thanks god mimi dhehebu langu linaruhusu talaka ingawa haipendelewi na nilikua siitaki ila mwanamme alinipa nikitaka nisitake, sipendi kukumbuka kwani baadhi ya niliyokuwa natukanwa na kudharauliwa, inaniuma mno, inataka kufanana na huyo ila mimi hakuwaingiza ndani kwangu ila alinisahau kiasi kikubwa si kwa chakula si kusomesha watoto si sabuni ya kuoga yeye aje ale atoke hata kwenye kipindi cha muda sita kwa sita siku akinikumbuka anasema ehee nafkiri leo unawashwa ngoja nikukune kidogo.au ananambia sikutaki hebu nenda katafute mwanamme mwengine wala sitakufanya kitu nenda kasimame barabarani utafute bwana, siku nyengine ananiamsha akirudi saa 7 anakutukana hadi majogoo yanawika sbh,au kunipiga ananilazimishia kesi hata si yangu anakusema kwa watu mambo mengi ya uongo ili kujiosha na anayofanya nilijiona hata paka nilimuona anathamani kuliko nilivyokua naaibika.mpaka alipooa mwanamke wa pili kwa vile alinipa talaka dada mmoja sitamsahau, ingawa aliongea kishangingi ila alinifunua macho baadae. alisema kwa kukaripia hivui wewe ushakutana na wanaume wangapi nikamjibu ni yule mme wangu tu akanambia si ujaribu mwengine uone hawafanani hao kuna wengine wazuri. nami nikapata mume mwengine na tunaishi nae kwa raha nikaona kumbe kunawanaume wazuri pia mpaka nikaona nilikua napoteza mda wangu, sasa cha ajabu tangu aniache keshaoa na kuacha wanawake watatu sasa mpaka ameamua kuishi pekeyake anaokoteza okoteza mitaani

    Hivyo naelewa fika kwa nini huyo mwanamke mwenzetu anasitasita si hofu ya mungu wala sio huyo bwana ni mjuzi sana ila amampeda sana bado huyo jamaa yake ndo maana anaweza kuvumilia hayo yote, nilipata kujua kwa nini wanawake wengine wanawaume bado wanatoka nje, nilielewa kwanini wanawake wengine wanakazi nzuri wana waume wazuri bado wanatoka nje,nilipata kujua jinsi mwanamke anavyolazimika juu ya asiyoyapenda kwa ajili ya watoto, luck enough nilikua na kazi yangu other wise ningefikia hatua ya kutoka nje kutafutia watoto mkate na ada labda?

    ReplyDelete
  53. Pole sana dada yangu kwa mkasa huo mkubwa, napenda kukufahamisha kwamba sio wewe peke yako uliyepatwa na balaa hilo, wako wengi kama wewe wenye mikasa kama hiyo, na tumeshuhudia wengi wameumia kwa wema wao. nakuomba dada yangu mpenzi, kama kuna uwezekano wa wewe kuondoka katika nyumba hiyo, fanya hivyo haraka sana, maana huyo mke mwenzio anaonekana sio mtu mzuri kabisa na hana nia njema na wewe, kwanza hashukuru kwa kusitiriwa nani uliyemuona akakubali kukaa na mke mwenzie nyumba moja? yeye hana hata shukurani, sasa wewe ondoka mwache akae na mumewe, atakuua huyo dada yangu uache watoto wako wateseke bure. pia mshauri huyo mumeo atafute kazi, ili aweze kujikwamua kimaisha, sio kila kitu kukutegemea wewe. pole sana dada yangu kwa mtihani huo, usiache kumuomba mungu kila wakati, na iko siku yatakwisha tu, mungu atakusaidia dada yangu. UKEWENZA NI JAMBO BAYA SANA KATIKA DUNIA HII, HIVYO DADA YANGU KUWA MAKINI SANA NA HUYO MKE MWENZIO. HII MICHEZO YA KINIGERIA TUNAYOANGALIA INATUFUNDISHA MENGI SANA. KILA LA KHERI DADA YANGU. mdogo wako Nus.

    ReplyDelete
  54. mimi kama mkristu mwenye hofu ya Mungu, namshauri huyo dada asali sana, haijalishi yeye ni wa dini gani lakini biblia imesema majaribu hayana budi kutupata WOTE na kila yanapotokea lazima kuna mlango wa kutokea... soma
    1wakorintho10:23
    labda huu ndio wakati wako wa kuwa karibu na Mungu, hao umeshawaona hawawezi kukusaidia, ongea na Mungu kuhusiana na hao, mueleze Mungu maumivu yako yako wapi..
    pole sana jamani.
    usihau kuwa kila jaribu ambalo Mungu mwenyewe ameliruhusu katika maisha yetu ni kwa mpango wake mwenyewe. pole sana dada.
    sali sana na ukiweza funga ukiomba.

    ReplyDelete
  55. DADA HAKUNA DINI YOYOTE INAYOKUBALI HUO UZINZI TENA KAMA UNGEKUWA MWISLAM HAWEZI MWANAUME KULETA HAWARA YAKE AKASEMA MKEWE. KWA SHERIA ZA KIISLAM HUYO MUMUEO ANGEPIGWA MAWE MPAKA AFE KWA SABABU HANA KISINGIZIO CHA KUTOKA NJE YA NDOA. HALI KADHALIKA SHERIA ZA KIKRISTO PIA HAZIMRUHUSU KUZINI. KWA HIYO AMEMKOSEA MUNGU NA AMEKUKOSEA WEWE NA WATOTO WAKO PIA.

    TURUDI KWENYE MADA YAKO, HIVI DADA KABLA YA KUKUPA POLE UNAJUA KUWA UKO ABUSED? UNAVYOSIKIA KUWA ABUSED SIO LAZIMA UWE UNALAMBA MAGUMI NA MATEKE HAPO UKO KWENYE PSYCHOLOGICAL ABUSE AMBAYO NI MBAYA NA INAUA HARAKA.

    SASA KAMA UNAWAPENDA WANAO (SIULIZI KUHUSU HUYO MUME MAANA HUO NI UNDUGU WA KITANDANI!) TAKE ACTION AND RUN AWAY FROM THOSE TWO PEOPLE WHO ARE ABUSING YOU AS FAST AS YOUR FEET CAN TAKE YOU. HALAFU UKISHAZOEA KUWA ABUSED UNAKUWA ADDICTED, MIE SICHANGAI STORY YAKO NA WEWE SIO WA KWANZA KUKUTWA NA HAYO ILA YOU HAVE TO GET HELP AND RUN AWAY FROM THEM FOR THE SAKE OF YOUR LIFE AND YOUR KIDS LIFE.

    HUYO ABUSER WAKO USIFIKIRI KUWA ATAPONA HUO UGONJWA WAKE MAANA ANAONA RAHA KUKUTESA KISAIKOLOJIA, NA UKISHOTOKA NDANI YA MAKUCHA YAKE ATAKUFUATA NA KUKULILIA MACHOZI YA MAMBA. YOU KNOW WHAT, NOT BECAUSE HE LOVE YOU BUT BECAUSE HE WILL BE MISSING ABUSING YOU AND ENJOYING YOUR SUFFERING. THAT MAN IS SICK! ALL ABUSERS ARE SICK! REALLY SICK.

    SISTER YOU ARE NOT ALONE! ALOT OF WOMEN OUT THERE ARE BEING ABUSED IN ONE WAY OR ANOTHER BUT YOU NEED TO TAKE ACTION, NOW, NOT EVEN TOMMORROW, JUST TAKE YOU KIDS DONT EVEN PACK YOUR BAGS SOMEONE WILL COLLECT THEM FOR YOU! RUN DEAR! RUN AS FAR AWAY FROM THEM AS YOU CAN!!!
    BUT YOU KNOW WHAT THERE ARE PEOPLE OUT THERE WHO MIGHT HAVE TOLD YOU THE SAME BUT YOU ARE CLINGING TO HIM THINKING THAT HE WILL CHANGE. NO HE WONT BECAUSE HE IS SICK AND HE IS GONNA DO THE SAME TO HUYO HAWARA YAKE AFTER YOU HAVE MOVED OUT!

    TAKE CARE OF YOURSELF AND YOUR KIDS THEY ARE TOO YOUNG TO DIE FOR YOUR COWARDICE!

    ReplyDelete
  56. Unaejiita Kithuku umenichekesha.Ila shoga pole,umeomba msaada kwa watanzania wenzio,maoni umepewa nafikiri yote yanaoana kasoro lunatic mmoja.Mie dada ni mwisilamu miaka yote nilifikiri dini yangu ngumu kumbe ukristo nao manati.Uishi na mume mpaka kufa endapo umeamua kuachwa huna ruhusa kuolewa mpaka afe mume.Itikadi hii si kifo jamani.Kuna baadhi ya wadau wame doubt hii story lakini kwa mimi cha ajabu sikioni,ziko familia nyingi tuu ziko kwenye situation kama hii,tofauti ni kwamba hii ni story ya mkristo,ukewenza haukubaliki,kwa waisilamu ni jambo ambalo mwanamke hana jinsi ila kukubali.Mimi uke wenza siukubali au niseme siutaki bora aende zake nitasononeka lakini hakubananwi na mtu.Sasa hasira nilizo nazo kwako dada yangu ni huko kujitia "I STAND BY MY MAN IN SICKNESS AND IN HEALTH FOR RICHER FOR POORER TIL DEATH DO US PART"nionavyo mimi ni "FOR POORER FOR MADNESS TIL DEATH DO YOU PART".Maisha bongo magumu mumeo kaona akuletee watoto wengine,hiyo haikutosha kakuletea kichangudoa,na alivyo hana adabu kafadhiliwa bado analeta upana kama pazia la sinema.Mfungie virago vyake muekee nje,mumeo mpe choice to stay if he really loves or to go na kimada chake.Upande wako sijui ni ku define vipi?naona una kazi yako,niki guess pia umesoma,why do you put up with it?au ndo mambo ya msondo babu anayaweza,kaza roho dada mwanzo ni mgumu baadae utazoea na kama utaona mawazo yanakuzidi tafuta kitu cha kufanya take an evening class or join a gym itakusaidia kutoa stress,jaribu kufikiria watoto wanapata picha gani ya mama wawili ndani ya nyumba moja,ukizingatia huyo mama mwingine hajaolewa,tuko kwenye karne ya hatari maradhi nje nje,nchi inajitahidi kutangaza safe sex halafu wewe unafuga uzinzi.Wake up sister,umekufa na haya mambo peke yako kwa muda umeomba watanzania wakusaidie kimawazo tumechangia kwa makundi ni wakati wako sasa wakuonyesha muamko,amka you are not in a healthy relationship,madada wengi humu wamechangia kujaribu kukushtua usiendelee kutumiwa kwa kisingizio bwana hana kazi ataona namnyanyasa,tofauti na mada iliyowekwa jana ya VIDETI kaka zetu wengi wametuchambua kama mchele,leo hii story yako itawapa jibu kwanini wanawake wengi wakipata mzungu wanaona wameukata.Wanaume wakiafrika wengi ngono mmeifanya swala tano Mungu hamumuogopi.

    ReplyDelete
  57. we anon wa 4:54 tutajuaje kama kweli wewe ndio mume wake,hata kama ndie ukweli uko palepale huwezi ukawaweka wanawake wawili kwenye nyumba moja,and two wrongs dont make a right.Ikiwa ulilea mtoto wake wa nje ina maana ulimsamehe lakini na wewe kwenda kuzini ni uchafu wa hali ya juu mnaleta na watoto ndani ya uchafu wenu hamja sikia kitu kinaitwa contraception.Vile mmeyaweka mambo yenu kwenye public domain hebu twambieni KILICHO KUFANYA UKAENDA NJE YA NDOA YAKO NI NINI? kama si kushindwa kufunga zipu yako.Watu wana work panapo kua na mvutano lakini wanaume wetu hukimbilia sketi nje,nimetumia sketi kustahi jamii nilikusudia kukupa tusi la nguoni.
    ASANTE.

    ReplyDelete
  58. NDIO UZURI WA KUOA MZUNGU, MAANA YEYE MKISHA KOROFISHANA HAKUNA BIBLIA WALA MANENO MUREEEEEEFU!

    ReplyDelete
  59. Pole sana dada yangu kwa yaliyokukuta,nimesoma barua yako mpaka mwisho,nikajaribu kusoma maoni nikashindwa kuyamaliza kwani moyo wangu unaniuma sana kuona wanawake wenzangu bado wananyanyasika na wanaume.Kwa kweli ushauri wangu ni hivi:CHUKUA KILICHO CHAKO NA WANAO KAANZE MAISHA YAKO UPYA.Huyo mwanaume anayedai unamnyanyasa muulize kama yeye HAONI HAYO MANYANYASO UNAYOYAPATA TOKA KWA HUYO HAWARA YAKE aliyemleta ndani?Kwa hivyo yamekufika shingoni,aamue kusuka au kunyoa,abaki na wewe na amuondoe huyo hawara au uondoke umwache na mwanamke wake.Wamekugeuza mjinga hujajua.Nachukia kuona wanawake tunashindwa kusimama kwa miguu yetu wenyewe,na istoshe Mungu kakujalia kazi hutakufa njaa ndugu yangu wala wanao hawatatangatanga,Mungu yupo na anaiona kero yako atakutoa na atakua mtetezi wako,hivyo jikaze ukaanze maisha yako.Sina mengi zaidi,ukiendelea kukaa nao,kwa jinsi ulivyoelezea wanaweza kukuua ili wabaki wanaponda raha na mali zako ulizozisotea siku zote na uache watoto wako wanateseka,kisa uliapa mpaka kifo kiwatenganishe.Mimi ni Mkristo ninaekwambia hivi.Akili kichwani mwako.
    Kila la heri na Mungu akusaidie.

    ReplyDelete
  60. AMA KWELI NDO MAANA UKIMWI AHUSHI BONGO.SUBIRI KIDO ATAKULETEA MKE MUME SASA.

    ReplyDelete
  61. We mume unataka kutuambia nini? kuzaa mtoto mmoja ambae sio wako ndo ukaona umletee kabisa mke ndani? Kwani yeye alikuletea mume ndani mkaishi waume wawili?? Tafadhali bwn.... usijitetee hapa. Tunajua siku zote wanaume mlio wengi hamna roho za utu. Mnawaona wanawake kama sijui kitu gani. Nyie mnatenda mangapi bwn... acheni hizo...

    ReplyDelete
  62. MICHUZI,

    SIJUI KAMA WASOMAJI WAKO WAMEGUNDUA KUWA MUME WA HUYO DADA AMEJIBU TUHUMA HIZO ALIZOTOA MKEWE? HAYA NIMEWEZA KU-COPY NA NINA-PASTE KAMA IFUATAVYO, MAJIBU YANGU YATAFUATA KWA CHINI:

    "Michuzi mimi ndo mume wa huyo mama aliyeandika kulalama kuhusu mke mwenza. Mbona hatoi upande mwingine wa habari? Mbona hasemi katika watoto watatu aliozaa mmoja si wangu; alimpata nilipokuwa masomoni? Anatafuta public sypathy isiyo na justification! After all si kwamba sina kazi; I am a consultant. Nimejiajiri. I take care of my family. Muulizeni alikuwa akifanya nini hadi nikajikuta naenda nje? Anyway, haya yalikuwa ya ndani ya familia. Sikutarajia atayaleta huku. Sasa tutaona kama ana jeuri aliyotamba katika waraka wake kwamba anayo, nyo!""

    WAHESHIMIWA HAYO NI MAJIBU YA HUYO BWANA LIYAJIBU KAMA ANON 4 54PM.

    1. SIKUTAKA KUANDIKA CHOCHOTE HUMU KUHUSIANA NA HILI SUALA LA HUYU MAMA MAANA KIDOGO HAKUWEZA KUTOA MWANGAZA MZIMA WA MATATIZO YAKE KWETU ILI TUMSAIDIE KIMAWAZO ILA KWA KUPATIKANA JIBU LA HUYU BWANA TENA ILIYOJAA DHARAU NDIO IMENIFANYA NIANDIKE JAPO CHOCHOTE.

    2. MIMI NI MKE KATIKA NDOA ILIYODUMU MIAKA 12 NA NINAELEWA FIKA HAYO ANAYOPITIA HUYU DADA JAPOKUWA SIWEZI NIKAJILINGANISHA NAYE MAANA YA KWAKE NI MAZITO MNO ILA KWA UPEO WANGU NATAKA NIMUULIZE HUYO MUMEWE AMBAYE ANADAI MKEWE ANATAFUTA PUBLIC SYMPATHY, YEYE ALITAKA AIPATE SYMPATHY KUTOKA KWA NANI?? MBONA FAMILIA YAKO HAIKO SUPPORTIVE?

    3. INAELEKEA MWANAUME HUYO AMEAMUA KUMKOMOA MKEWE BAADA YA MKEWE KUZAA NJE YA NDOA ILA SWALI KWA MUMEWE, JE ULIPOKUWA NJE UKISOMA ULIKUWA UNAMJALI MWENZIO? UMEWAHI KUJIULIZA NI KWANINI AKATOKA NJE YA NDOA NA KUZAA MTOTO? KAMA ULIKUWA UNAONA KUWA AMEKUTENDEA KOSA BASI NA WEWE UNGEMUACHA KIPINDI KILE. NA INAVYOONEKANA WEWE MWANAUME UNATUMIA KISINGIZIO CHA HUYO MTOTO KUPATA CHOCHOTE UNACHOTAKA KWA KUWA MKEO KESHAKUBALI KOSA LAKE LA MWANZO BASI UMEBAKI KUMFANYA AWE MKOSAJI KIASI CHA KUMLETEA MWANAMKE NA WATOTO WAKO WA NJE. HIYO SASA SI NDOA BALI KUMKOMOA HUYU MAMA. HAVE YOU EVER HEARD OF FORGIVENESS??

    3.INAONEKANA WEWE KUJIITA "CONSULTANT" NI EUPHEMISM YA KUSEMA WEWE NI MISHENI TAUNI! KAMA NI CONSULTANT SI BASI MNGEKUWA KWENYE NYUMBA YENU?? AU ULIYOJENGA KWA NGUVU ZAKO NA UPATE MWANYA WA KUMSHURUTISHA MWENZIO VIZURI ZAIDI?? KWA TAARIFA YAKO HUYU MKEO HAKUJA KWENYE HII BLOG KUONYESHA UJEURI WAKE BALI ALIKUJA KUOMBA MAWAZO SASA KWA KUWA WENGI WAMEMSHAURI AKUACHE UMEAMUA KUMTUKANA WAZIWAZI.

    IF I WERE YOU, NINGEENDA KUKAA NA MKE WANGU NA KUMWAMBIA AMEKOSEA ALICHOFANYA MAANA NDIVYO UNAVYOLICHUKULIA HILI SUALA NA KUTAKA TUELEWANE.

    KUWA CONSULTANT INA MAANA UNA UWEZO WA KUMWEKA HUYO MWANAMKE WAKO MWINGINE KTK NYUMBA NYINGINE NA SIYO HIYO.

    REMEMBER WHAT GOES AROUND COMES AROUND................. SASA WENGI TUMEJUA MATATIZO YAKO NA WEWE UMEZIDI KUYAWEKA WAZI TUMEJUA WHAT TYPE OF MAN YOU REALLY ARE!

    A MEASURE OF A MAN IS NOT BY HOW MANY WOMEN HE SLEEPS WITH BUT BY WHAT HE CAN DO FOR THE ONE WOMAN HE LOVES!! SORRY TO SAY YOU DO NOT QUALIFY. YOU SHOULD HAVE REALLY THOUGHT ABOUT FORGIVING YOUR WIFE IN THE TRUE SENSE OF FORGIVENESS MAANA HAYA YASINGEFIKA HAPO

    ReplyDelete
  63. Kwanza nianza kwa kukupa pole dada yangu.
    Kwa kweli huwa nasoma tu hii blog lakini wewe umenigusa hata mimi kutoa comment kwa mara ya kwanza ndani ya chombo hiki.Comments zilizotolewa humu ni nyingi hata sijamaliza kuzisoma maana nitaacha kiporo kazini,kwahiyo inawezekana ushauri huu nitakaokupa umeshaupata.Nakubaliana na wale walioshauri uachan na huyo bwana,maana kuishi naye ni kujitafutia kifo,kuanzia ukimwi mpaka mengine youte. Sasa ushauri wangu ni huu. KUACHANA NA MTU ULIYEISHI MUDA MREFU NI NGUMU SANA,TENA KAMA UNAMPENDA,NA PIA KAMA UNA WATOTO,HUWEZI FANYA PEKE YAKO UTAHITAJI MSAADA WA KIJAMII NA KISHERIA.NAKUSHAURI UENDE UKAONE VYOMBO HUSIKA VYA KUSAIDIA JAMII KAMA TAMWA NA TAUWLA.HAWA HUWA WANATOA MSAADA BURE KWA JAMII.NADHANI UNAWAHITAJI SANA HASA KWASABABU NDOA YAKO NI YA KIKRISTO NA PIA MASLAHI YA WATOTO.UKIZINGATIA WEWE NI BREAD WINNER.MWISHO BE STRONG AND SOLDIER ON WATOTO WAKO WANAKUTEGEMEA.Y

    ReplyDelete
  64. Tatizo letu la bongo ni lile lile hatuko straight foward na kuendeleza mambo ya umwenzangu na kushindwa kufanya decision zako mwenyewe mpaka ukamuulize fulani au wazazi.Sasa jamani kesi kama hii ni ndigo na simple kabisa,kwa sababu
    1.wakati unaona watoto wawili wanakuja nyumbani kwako hapo ulishafind out kabisa kwamba wakati mume wako ana kzi alikuwa malaya.
    2.umeshaona mume wako si muadilifu na wala si mkweli katika ndoa.Kwa hiyo hapo ianjulikana kabisa kama wewe una kazi nyumba unayoishi umepewa na shirika under your name unachoogopa kumfukuza mume wako nini mpaka uite wazazi wasuluhishe?
    Sasa ushauri ni huu mfukuze huyo mumeo ambaye ni malaya na mmalaya mwenzake waambie waondoke na hao watoto wawili nafikiri wakikosa pa kuishi watatia akili maana hata biashara ya maandazi watafanya wapate kuishi lakini kuwaelea ni kuwaitia ujinga na kuwanyima haki wanao.
    BK from Pa

    ReplyDelete
  65. We dada annon Jan 28: 6:49 una mantiki katika maneno yako.

    Kumbuka kuwa kuwa na hela nyingi au kazi nzuri hakuleti furaha katika ndoa. Na pia wengi huwa tukioana tunategemea furaha. Lakini kadri muda uendavyo, ndivyo mambo yanabadilika. Kuna sababu nyingi sana sana. Kuna ndoa zina furaha sana na kuna ndoa zina matatioz sana. Sababu ya moja kuwa na furaha au matatizo hazifanani kabisa. Huwezi ukaangalia ndo ya mwenzako ukalinganisha na yako. Haipo hiyo kitu.

    Lakini mambo mengu huwa ni creation ya mwanamke. Angalia jinsi scandinavian zilivyo na highest rate ya divorce duniani. Sababu watalaamu wanasema ni uhuru na kiwango cha juu za haki sawa kisheria ziliko nchi hizi. Pia fanansiha stability za ndoa za watu wa Asia.

    Kwa Scandinavia issue ni haki sawa na usawa. Lakini hamna kitu kama usawa kati ya mwanamke na mwanamme! Haipo popote kwenye dini wala kwenye midheaval stories.

    Ingawaje huyu mwanamke kesi yake ni ya kufikirika, lakini mambo mengi kwa Watanzania yanaletwa na modern life. Wanawake waangalia TV au kusoma stories za RISASI/KIU/IJUMAA, wanahamishia ndani ya nyumba. Haiwezi kuwa nyumba hiyo. Mimi nategemea mwanamke awe yule yule niliyemwona kabla na siku ya ndoa. Asiote pembe baada ya miaka mitatu ya ndoa.

    Kwa kumalizia, wewe dada Jan 28:6:49 PM EAT unamalizia kwa kuseuma ungetoka nje, mimi sidhani kama ni solution. Kwani ukitoka nje unatembea na mwanamme au mwanamke?! Ni sisi wenyewe wale wale ambao nyumbani kwako umeshindwa!!?? Sana sana unajiongezea upungufu wa furaha kwenye life kwa kuwa na watoto kibao wasio na consistency katika fathering. Watoto wakikua huwa wanaumia sana kujikuta wako baba tofauti. Kwani inatoa picha kuwa mama hajatulia. Na ni kweli, lazima ulikuwa hujatulia!

    Wanawake ndoa ni kazi sana. Inahitaji uvumilivu na subira. Usione baba na mama yako wanacheka wako pamoja. Wamepita hatua kibao za utatanishi mpaka leo ambamo mama yako alivumilia sana. Naposema kuvumilia siyo kwa maumivu, ila kwa fikra. Nanyi Vumilieni tu mjenge familia.

    ReplyDelete
  66. Annon Jan 28 10:08 hiyo ngono unayosema wanaume tumeifanya swala tano tunaifanya na nani?! Si na wanawake? Au una maanisha nini? Kataeni muone kama tutafanya hiyo kitu

    ReplyDelete
  67. Mr Michuzi, am not pleased the way you handled my comments. For some reason you didnt publish the comments that i made concern this particular issue.

    I feel so discriminate because i offered what i believe the best judgement concern this matter. I don't know you didnt post response because i used foreign language, or because it is personal attack concern certain people.

    Thanks
    US

    ReplyDelete
  68. Michuzi mimi ndo mume wa huyo mama aliyeandika kulalama kuhusu mke mwenza. Mbona hatoi upande mwingine wa habari? Mbona hasemi katika watoto watatu aliozaa mmoja si wangu; alimpata nilipokuwa masomoni? Anatafuta public sypathy isiyo na justification! After all si kwamba sina kazi; I am a consultant. Nimejiajiri. I take care of my family. Muulizeni alikuwa akifanya nini hadi nikajikuta naenda nje? Anyway, haya yalikuwa ya ndani ya familia. Sikutarajia atayaleta huku. Sasa tutaona kama ana jeuri aliyotamba katika waraka wake kwamba anayo, nyo!

    HA HA HA HAH HA HAA.. WEWE UNAYEJIITA MUME WA MAMA ANAYELALAMIKA, HAUONI AIBU HATA KUJITOA HUMU GLOBUNI TENA KWA VI COMMENT VYAKO VYAKISHENZI? WEWE KWELI AKILI HUNA NA HUJAELIMIKA HATA KIDOGO KWANI HAKUNA MTU ALIYESOMA NA AKAELIMIKA AKAFANYA UPUMBAVU KAMA WAKO.. UNALETA HABARI ZA PAYBACK KITANDANI? TEH TEH TEH.. I WISH U WERE MY MAN. KAMA WEWE NI CONSULTANT AS U HAVE CLAIMED, BASI DO SOME CONSULTATION NA HAUZ YAKO NYAMA WE.. CHAGUA MOJA KUSUKA AU KUNYOA, SIO KUMFANYIA MTOTO WA MWENZIO VITUKO, USIJIFANYE KAMA WEWE HUNA WATOTO! HUJUI KUWA MUNGU ANAWAPATILIZA WANA MAOVU YA BABA ZAO? SASA WAZA KAMA MWANAO NDIO ANAFANYIWA HUU USHENZI, UTA REACT VIPI? WEWE SI KIDUME? BASI TOKA HUMO NDANI UMUACHE NA WANAE WEWE UENDE UKAENDELEZE MAISHA NA HUYO KISALATA WAKO(SMALL HAUZ), SI UNADAI UNAKAZI BWANA? KWANINI UNAMNYONYA MAMA WA WATU? HAMA,ONYESHA UANAUME WAKO IF U HAVE GUTS. NYIE NDIO WALE LADY JAY DEE ANAOWAIMBA WANAUME KAMA MABINTI, KUTEGEMEA MIGINGO YA WENZENU KUISHI NA VITUKO JUU.. NYOOOOO..

    ReplyDelete
  69. MICHUZI NA WADAU WENGINE KAMA NI HUYU MAMA NINAYEMFAHAMU MIMI NINAWASHAURI MSIPOTEZE MUDA WENU KUMSHAURI, HUYU MAMA HAYUPO SERIOUS, ANAMPENDA MUME WAKE SIJUI ALIAMBIWA HIYO YA MUME WAKE INA NINI? ILA KAMA SIO YULE NINAYEMJUA MIMI NISAMEHE, ILA KWA HABARI HII HATA WEWE NI WALE WALE TU, SIKUONEI HURUMA NG’O.
    NINAISHI NAO JIRANI HII FAMILIA, HAKUNA ANAYEMUELEWA HUYU MAMA MPAKA TUNAHISI ANA KASORO. ANAONDOKAGA NYUMBANI CHA AJABU ANAACHAGA WATOTO, SASA SIJUI NI KUONDOKA GANI HUKO, HATUJAKAA SAWA TUNAMUONA HUYO NA VIRAGO VYAKE ANARUDI KWA KISINGIZIO CHA WATOTO, KAMA KWELI ANATAKA KUONDOKA, KWA NINI HUWA ANAWAACHA WATOTO ASIONDOKE NAO?
    KWANZA ANA KERO KUTUGONGEA MAJIRANI KUOMBA HIFADHI NA KUDANGANYA KACHOKA KUMBE KANOGEWA. ACHA ATIE ADABU YAKE. BINAFSI SIMUONEI HURUMA WALA NINI, LABDA ANAKERA KULIKO FISADI, KILA SIKU HODI MAJUMBANI MWA WATU, HATA NINGEKUWA MIMI HUYO MWANAMME NINGEMCHEZEA AKILI HIVYO HIVYO. KALAGABAHO, ETI MARA UTAWAONA HAO WAMETOKA OUT NA MUME WANAKUNYWA BIA NA NYAMA CHOMA HADHARANI ETI KUWAONYESHEA WATU, ANAONA KAUCHINJA SISI TUNAMCHORA TU, SIKU MBILI HUYO HODI NAOMBA HIFADHI MWE!
    HATA KAMA NI UMRI MAMA, KWANI LAZIMA KUNANILII JAMANI SABABU HATUONI UNACHOPATA KWA HUYU BABA ZAIDI YA HILO ATI. MWE KAMA NDOA NDIO HIZI MIMI AKU, ACHA NISIOLEWE ATI KWA RAHA ZANGU.
    MAMIE, ELEWA HATA MAJIRANI WAMECHOKA KUKUHIFADHI ATI, SI UNAJUA NYUMBA ZETU TUNAKUWA TUMESHAJIBAJETI SASA KUHIFADHIANA KWA KWELI DUH.NI HAYO TU.

    ReplyDelete
  70. Michuzi wewe ni mtu mzima na pia una familia, hakuna mtu anakuingilia wewe na familia yako katika mambo yenu. Kuna mambo na mambo ya kuweka kwenye blog yako, hata kama unatafuta umaarufu sio kwa njia ya kuandika mambo ama siri za ndani za watu. Kwanza wewe ni nani hata uandike siri za watu za ndani, kwa kibali kutoka wapi na una uhakika gani kwamba unayoambiwa ni ya ukweli? au unataka kupata umaarufu kupitia migongo ya watu kwa kuchafulia watu majina? Hizo ndoa unazotaka kuzivunja kwenye ukurasa wako, hao wanawake utawaoa wewe?
    Kuwa mstaarabu kuingilia mambo yasiyokuhusu huna mamlaka yoyote na hutakuwa nayo itabaki kuwa ndoto tu. Umaarufu na sifa hazitafutwi kwa nguvu Kaka.
    Hata usipoiweka comment yangu, ujumbe huu ni wako wewe, uzuri ni kwamba umeusoma kama ulivyokusudiwa.

    ReplyDelete
  71. Wewe unayemlaumu Michuzi kwa kuweka mambo ya watu nafikiri una matatizo, na hujui hasa sheria zinasemaje kuhusu suala, hilo. Hivi wewe uandike mwenyewe habari zako gazetini ukiomba watu wakushauri halafu eti uwe umeingiliwa mambo yako ya ndani?

    Huyo dada aliyeamua kuomba kurudishwa UNYAGONI na kufundwa MSONDO upya ndiye alieamua kwa matakwa yake binafsi kuanika mambo yake hadharani. Sasa kama Michuzi angekuwa amesikia hizi habari kama za udaku wa kina Shingongo akaziweka kwenye blogu yake ndio ungekuwa na haki ya kusema haya yote unayosema lakini si katika hali hii hizi habari zilivyoletwa humu. Na kama yamekukera ungemshauri huyo dada na wengineo wasianike mambo yao hadharani sio kulaumu watu wasiohusika na sakata hili. Anyway kama hata majirani wanajua hii kesi there is no privacy na even before that mume aliamua kutokuwa na privacy ya nyumba yake kwa kutembea na mwanamke mwingine huko barabarani so I dont understand hiyo privacy unayoizungumzia.

    Dada uliomba UNYAGO, makungwi na manyakanga wamekupa ulichokitaka ni vizuri ukafunga huu mjadala. Kama kufuzu ushafuzu kwa lectures zoote hizo hapo juu.

    ReplyDelete
  72. ha ha haaaaa...Wee anon wa Tuesday, January 29, 2008 2:46:00 una uhakika uko sawa? Mara ya mwisho kuchekiwa kichwani ilikuwa lini? nahisi kale kaugonjwa kako kamerudi, wahi mirembe kabla mambo hayajachanganyia!! uko nje ya mada!! kwikwikwikwiiiiiiiiiii.....

    Dada Pole mwaya, kama jiti unalipenda vumilia, au jimuvuzishe out halafu uwe unalikamua ukiwa out!! na nakuhakikishia huko utakokuwa utayapata ya kumwaga, si unajua yalivyo mengi? unachagua kama nyanya vile...wenzio twala kwa ulaiiiini!!! nitafute nikupe kianzio, ndoa ndoa ndoa ndo nini??? ndoa zilikuwa kwa mama zetu huko sio leo, achana na ndoa..kula raha..LIFE IS TOO SHORT MAMA!!

    ReplyDelete
  73. WEWE ANON January 29, 2008 2:46:00, NAHISI KAMA UNAKURUPUKA, MICHUZI KAKOSA NINI? UTAKUWA WEWE NDO MUME WA HUYO MAMA..TULIZA MZUKA WEWEEEE...NENDA KWA MAI WAIFU WAKO WOTE WAWILI WAKUTANISHE SEHEMU UWAPE KAZI WOTE KWA PAMOJA, UKIWATOA NDANI YA CHUMBA HICHO WOTE WATAKUWA WAMEPATANA NA WATAHESHIMIANA...TRY IT WORKS KWA WAKE WENZA WANAOGOMBANA..

    ReplyDelete
  74. Anon wa hapo juu,usiigeuze hii story kosa la Michuzi,Michuzi katumiwa hii message ili ai publish hakuitunga yeye,sasa kosa lake liko wapi mtukane huyo mama kwa kujianika,ama wewe ndie huyo mume mwenye kuongeza chumvi kwenye kidonda.It's clear this lady is psychologically abused,she said she need our advice but really she need psychological help no woman in her right mind would live like that.

    ReplyDelete
  75. We annon Jan 29 2:46 ni balaa! Na wewe yanakuhusu nini? Mhh!

    Kwa Michuzi ni sawa sawa tu kwani anaposti anavyoletewa. Ndo maana ya hii blog au globu. Lakini issue ni mwanamke mwenyewe. Nilijua ana matatizo. Ni kweli kumbe. Kwani mwanamke aliyetulia si rahisi akatoka ndani na kuanina uchafu wake na mmewe nje ya nyumba!

    Wanawake mjifunze na acheni ujizi wa jumla (collective crazness), kama kawaida yenu.

    ReplyDelete
  76. naona dada kama ni ushauri umeshapata sana sasa fanya maamuzi zeni utujulishe wana blog ya jamii hatua kwa kwa hatua utayo chukua

    ReplyDelete
  77. aiseee i dont know what to comment but all that i can say is dada all these people have said what is ought to be said therefore the decision is yours. but one thing i can comment which not so many people have commented is that.

    wewe na mume wako hamuwafanyii justise watoto wenu its just that hapa sisi watanzania hatuna culture ya kufanya therapy session ila ukiwaangalia vizuri watoto wenu wutagundua they are very much traumatised by your actions. na unaweza kuta watoto wenu wana so much potential ya kudevelope maybe shuleni but they are not doing so well because ya matatizo ya baba na mama . na this will affect them hata katika makuzi yao and when they became adults.

    sometime we women tend to think that we are doing things for our children but in reality its for our own sake because hapa i dont see the best interest of the children if dad and mum are not ok.

    so i advise you to consider the best interest of your children (not that mistress children) because you may think by remaining with your husby unawatendea jema watoto.these hussles in the house realy affects them big time , mimi nakumbuka tu zamani ukiona wazazi wanashoutiana tulikuwa tunalia kichizi na hapo ni once in a while sasa kwa hali yenu it really hurts your children more than you can think. hata kama watoto wako ni wadogo but you should know and experts will support me on this kwamba watoto at the age of three years wanashika vitu sana so events kama hizi hazitawatoka kabisa maishani mwao.

    so please i know you love your husband so much na its not about morals au watoto no i disagree with you there its because you still love your husband and unaogopa kutry life alone because umezoea kuishi na mume wako kwa muda mrefu so unaona kama ukiachana nae utashindwa kumake it on your own. but believe me you will have a better life ukiwa peke yako than this life unayoishi sasa na watoto wako watakuwa very happy and they will support and encourage you. just try it and utafanikiwa sana.

    i wish you all the best in the begining of your new life.

    please follow the majority advise.

    some times you never know if you take the courage to leave your husby utashangaa baadae atabadilisha conduct yake( kuachana na mistress) na atakuja kukuomba msamaha and you never know mtakuja kuishi a happy life like normal husby and wife just show him that you can dare.

    ReplyDelete
  78. Wewe anynymous 2.46 naona issue imekuchoma sana....kama ni wewe pole sana. Hakuna majina yametajwa hapa na hata wewe hujataja jina lako sasa kwanini michuzi asiitoe issue wakati mtu anaomba ushauri? kuna mambo mangapi watu wa humu ndani wameomba na wamepewa ushauri? wewe unadhani ni siri tena? kuwa na mke na kimada kwenye nyumba moja? inaonyesha jinsi ambavyo huna ustaarabu na nadhani wewe unahitaji msaada zaidi kwasababu umesha athirika kisaikolojia...wasiwasi wako ni kuwa akiondoka huyu mama utahenya sana kwasababu umezoea kumchuna. wewe kwa akili yako finyu unadhani kuna ndoa tena hapo? ndoa umeivunja mwenyewe una mlaani michuzi...what a shame...!!!!!

    ReplyDelete
  79. MPENDWA POLE SANA SANA MZIGO NI MREFU NA ANAYEJUA ZAIDI UZITO NA UCHUNGU NI MUNGU TU, WEMA WAKO NDO UMEKUPONZA UNAFUGA NYOKA WADOGO(HAO WATOTO WA NJE) HUYO MAMA YAO NI CHATU TENA MWENYE NJAAA HUKUPASWA HATA KUMWANGALIA USONI KINACHOKUTESA NI UNAISHI NA MANYOKA WATATU MAMA NA WANAWE WAWILI, CHA MSINGI WE TOKA ZAKO NA WANAO MANA HUWEZI WAACHA WANAO WALELEWE NA NYOKA MWENYE NJAA,TAFUTA NYUMBA AMA CHUMBA KAPANGE KAA NA WANAO WAACHE HAO BILA HURUMA, MAANA HAWANA ADABU KABISAAAA POLE SANA KAKA WEWE NI MKRISTO THEHEBU LA ROMAN CATHOLIC TAFUTA SALA YA MT YUDA THADE SALI BILA KUKOMA ANAJIBU MAOMBI YA AKINA MAMA WENGI KAMA WEWE NA WALIO NA MIZIGO TOFAUTI NA MAGUMU ZAIDI.

    ReplyDelete
  80. Hivi ulikubali yote hayo kwa ajili ya kumpenda mume au hujielewi?, nashindwa hata kukunea huruma maana wewe hujajihurumia. Usipojua thamani yako usitegemee kuna mtu ataiona.yote umeyataka mwenyewe, and you deserve it. So amua kuondoka au kuendelea kubaki, mi naona hata ushauri haukufai labda maombi tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...