Jina la Dr.Willibrod Peter Slaa (pichani akiwa wima akiteta na mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe na Mbunge machachari Mh. Zitto Kabwe), Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Karatu, hivi sasa linaweza kuwa jina ambalo linatajwa zaidi kushinda lingine lolote katika anga za kisiasa nchini Tanzania. Pata habari zake kamili kwa kubofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Nimesoma CV yake lakini sioni wapi na lini alitunukiwa PhD na kujinyakulia title ya Dr. au ndo ule u-Dr wa kujizoelesha???

    ReplyDelete
  2. safi sana michuzi kwa kuniwekea picha ya hawa wazalendo wenye uchungu na tanzania, i wish viongozi wetu wote wa serikalini wangekuwa kama hawa jamaa, basi tungefika mbali sana..

    ReplyDelete
  3. mtu yeyote anayeweza kusimama kidete dhidi ya ufisadi kama huyu bwana ni Dr kuliko mbongo yeyote mwenye PhD za MIT, Makerere, Cambrisdger n.k.

    ReplyDelete
  4. huyu Mbowe amebondwa..jicho la kushoto hapo ..

    ReplyDelete
  5. Vichwa hivyo balaa!! bila ya hao wazalendo tusingejua chochote kuhusu ufisadi unaoendelea nchini (Buzwagi, BoT,n.k) we need them. Na kile chama kilichotuma wajumbe nchi nzima kusafisha hali ya hali hewa naona kimyaaa kabisa. Kitume tena wajumbe kikawaambie ukweli. SIASA BWANA UZUSHI MTUPU. Tutamshtaki... nani wa kumshtaki. Na sasa nasikia wamejigawia mikataba ya muda mwingi kuendesha shughuli za makontena bandarini hata kabla mkataba wa awali haujaisha. Hao hao wanaodai ndege inapaa, maisha bora kwa kila mtanzania na kugawana sote 'kanyama ka sungura'.

    ReplyDelete
  6. Hii mtu tatu safi sanaaaaa!!!fichua siri kaka zetu..LAKINI NANI KANIBONDEA RAISI WANGU MBOWE JAMANI?

    ReplyDelete
  7. Nipeni mwanafunzi wa sekondari Bungeni mwenye uchungu wa nchi kuliko mr PHDr' au luba anayenyonya damu za binadamu, au kwa vingine phd anayekula pesa za watoa jasho bila kujali. watu wanakufa kwa ajili yakukosa matibabu hospitalini tanzania na hapo hapo pesa hizo hizo za serikali zinaliwa na mtu mmoja, Daud hata Mungu hutamuona, kama kweli Mungu yupo.

    ReplyDelete
  8. hawa ndo wapinzani wa kweli, sio kina bwana mrema wanatuchanganya tu, na ndo wanaomaliza upinzani wanaonakana ni warpokaji tu kwa ishu hata ambazo hawana vithibitisho! lakini hawa jamaa tunaona siri wanazozitoa na vikiambatana na detailz, sio hawa wengine longolongo tu

    ReplyDelete
  9. kazeni buti wapinzani, kwani hamna leo hii mtu aliyekuwa anategemea kuwa mtu mweusi anaweza akasimama mbele ya kadamnasi ya wazungu wamsikiliza na akaeleweka anachokiongea, lakini tunameona yanayoendelea marekani nikiwa namaanisha obama, kwahiyo kama kweli mna uchungu na hii nchi yetu, basi ipo siku wananchi wahata sita kuwapa dhamana ktk nchi yetu inayonuka uovu! 'yes we can'

    ReplyDelete
  10. Tunahitaji wabunge kama hawa both from CCM and vyama vya upinzani ili kuweza kudhibiti serikali inayotawala kama hamna katiba na sheri Tanzania. Tumechoka na rubber stamps za CCM na serikali bungeni.

    ReplyDelete
  11. Dr. Slaa ni vile aliwahi kuwa Padre na ubongo wake unahekima za kutosha hivyo uamuzi wa kuhamahama vyama ovyo kama akina naniniii hana lakini kuna tabia mbaya sana CHADEMA, tena sana haswa kwa hao wenye vijipesa na walikuwa "founder members wa CHADEMA" kwanza wanarithishana madaraka kiukoo kama si ki-wakwe pili wanapeana ubunge kifamilia.

    Slaa hapendi mambo hayo lakini alishajitosa kwenye hicho chama kutetea nchi yake na hataki kuonekana anatamaa yoyote kwa kuhamahama.

    WITO kwa CHADEMA msiwe na tabia za ajabu ajabu kupeana madaraka kiukoo/kikabila.

    Heshimuni Katiba! Acheni Ubabe,

    Kwa maneno mengine mafisadi wa BoT wapo CHADEMA pia, tena hao hao wanaojiita "founder members" chunguzeni taratibu.

    ReplyDelete
  12. Ehhh bwana ehh.... hawa hawaaminiki hapo wanatafuta wapate madaraka then baadaye hawatakuwa na tofauti na hao waliokuwa madarakani kwa sasa
    Pesa ina-change mtu nakusahau ulikotoka
    Embu michuzi tuulizie na ile kesi yake Dr na rafiki yake wa karibu huko Karatu (tuone kama kweli wanafuata haki kwa mengine) kitanda usichokilalia hujui ......

    ReplyDelete
  13. hawa hawana lolote wanatafuta mishen tu wameona sasa hivi mpango wa hela siasa wakipata habari zitakuwa mbaya kuliko ccm wangeendelea kupiga disco watu wacheze wasilete mazabe

    ReplyDelete
  14. From the Church to the State House(Slaa),From a DJ to a Vice President(Mbowe),From a commonner to a Prime Minister(Kabwe), Ohh! what a dream ticket that is!! Wanawane,remember the trio in 2010.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...